Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 9,520
- 14,383
Dunia ina maajabu na hayajawahi kuisha maajabu hayo...kila unaposikia moja la kuajabisha jua kuna mambo elfu moja ya kuajabisha zaidi ya hilo lakini hujalijua..
Essie Dunbar.. mwanamke aliyekuwa na miaka 30 mwaka 1915 alikuwa anaugua ugonjwa kifafa (epilepsy attack).
Siku moja akadondoka ikawa hapumui ...familia ikawa haijui lakufanya......ikabidi ikamtafuta daktar aliyeitwa Dr. D.K. Briggs kutoka Blackville
Dr. D.K. Briggs alivyompima yule mgonjwa hakupata alama yoyote ya kuashiria kuwa mtu huyo alikuwa hai ...Essie Dunbar hakuwa anapumua na mapigo ya moyo yalikuwa yamesimama ...Dr. D.K. Briggs akaiambia familia kuwa mgonjwa amefariki
Baada ya kupata taarifa hiyo familia ikaamua kuanza mipango ya mazishi na mipango ya mazishi ikaenda haraka haraka.
Dada wa marehem alikuwa yupo nje ya mji ila kwa mujibu wa ratiba angewahi kutoa heshima kwa mdogo wake
Siku ya mazishi ikafika viongozi wa dini wakaongoza sala na taratibu zote zikawa zimekamilika lakini hadi muda huo dada wa marehemu alikuwa bado hajafika basi ikabidi azikwe
Muda mchache baada ya maziko dada wa marehem akawa amewasili, licha ya kuwa amechelewa na mdogo wake alikuwa ameshazikwa akaomba mwili ufukuliwe ili atoe heshima yake ya mwisho kwa mdogo wake
Hebu jiulize kwenye jamii yenu hilo lingewezekana?
Basi viongozi wa dini wakakubali ombi la dada mtu mwili ukafukuliwa na sanduku likafunguliwa kwa ajili ya dada mtu angalau atoe heshima zake za mwisho
La! Haula hakuna aliyeamini pale sanduku la mwili lilipofunguliwa na kukuta marehem ametoa smile kwa dada ake na kila mtu aliyekuwepo pale
Huwezi kuamini watu wengi waliokuwa pale walikimbia wakiamini kuwa Essie Dunbar alikuwa ni mzimu uliofufuka kutoka kuzimu
Hata viongozi wa watu dini nao walipata mawenge watatu wakadumbukia ndani ya kaburi ...na wawili walikanyagwa na watu
Lakin Essie Dunbar alikuwa hai tena ...na baada ya pale aliishi tena kwa miaka 47 mbele alikuja kufariki mwaka 1962 akiwa na miaka 77.........@bwana fact
Elewa hivi sio kila lenye kuwahi linakuwa sawa na sio kila lenye kuchelewa linakuwa baya ndio maana hadi leo waswahili bado wamechanganyikiwa juu ya kuwahi na kuchelewa...waliosema haraka haraka haina baraka ...ndio hao hao waliosema ngoja ngoja yaumiza matumbo