Sumaye kupasua bomu...

Status
Not open for further replies.
Hawa ndo aina ya viongozi nisopenda hata kuwasikia yaaani kawa waziri mkuu for ten good years bado anataka kuwa katika mashindano ya vitu kama hivi ili iwe nini sijui........alienda kusoma Havard sijui ........kwa nini wasianzishe miradi hata ya kuelimisha wananchi tuuu huko wilayani na kitaifa ili kusaidia jamii.......madawati hakuna na yeye ana links nyingi tu kutokana na wadhifa aliowahi kuubeba.......haoni Maajar's family atleast wanafanya kitu??????

Hivi hawaoni kina Bill Gates?????

Unapokuwa mtu mzima ni bora kurudi katika jamii utakozikwa kuliko kukomaa na era ambayo tayari haijali nani ulikuwa huko nyuma..........acha wajifunze in a hard way!!!!!!!

Huwa wanaishia kuumbuka tu!

Yeye alitakiwa afanye kama kaka yake BEN aanzisha ka NGO kake afanye mambo ya jamii.
 
Mzee mangula kaahidiwa na mwenyekiti ataingia nec kwa kuteuliwa,katiba inampa nafasi mwenyekiti,ndio mana hana wasiwasi,jk aliamua muda mrefu kurudisha uhusiano wake na mangula baada ya kugundua ni kina lowassa ndio walikua wanamchonganisha nae kwa kuwa walikua wanamuogopa kama ilivyokua kwa mwandosya,jk anamuhitaji sana mzee mangula kwa sasa

Huyo mzee si nasikia alikuwa hampendi JK!

Kila kukicha alikuwa anasuka mbinu za kumdondosha mwisho ikala kwake.
 
Itakuwa postmotam!expect nothin less than kauli tupu isiyo na mashiko!Sorry!
 
Nimefurahi Mama Nagu kushinda teh teh teh

Mangula nikiwa Rais nutahakikisha hupati nafasi yeyote ya uongozi kwenye Chama wala serikali na utaitwa babu kijijini hadi natoka madarakani- Jakaya Mrisho .Leo kumbukumbu za Mangula sijasema je kwamba hana bifu na wakubwa?CCM wanafiki sana
 
Mangula nikiwa Rais nutahakikisha hupati nafasi yeyote ya uongozi kwenye Chama wala serikali na utaitwa babu kijijini hadi natoka madarakani- Jakaya Mrisho .Leo kumbukumbu za Mangula sijasema je kwamba hana bifu na wakubwa?CCM wanafiki sana

Alifanya makosa kama aliyofanya Mashishanga kule Morogoro kwa ku declare interest mapema asubuhi kweupee!
 
bagwell waliambiwa asiyeridhika aondoke ccm, hawakuambiwa kwenda kwenye vyombo vya habari.

Na huo ndio mtihani wenyewe! Watakapohama/ watakapoondoka na kujiunga na chama kingine/chengine cha siasa watakuwa wameonesha uchu wao wa kupenda madaraka.

Sielewi vyama vinavyopokea hizi majeruhi za vita ya madaraka.

Sumaye hana bomu la kupasua, bomu limempasua yeye.

Nimekumbuka Dr. Slaa alivyotoa habari za unafiki wa Sitta na kujiengua CCM ili agombee Uspika/urais kupitia CHADEMA.
 
bagwell Mh. Simaye ana mgao wake wa keki inayomtosha maisha yake yote - 80% ya mshahara wa waziri aliye madarakani; aangalie mambo mengine ya kimaendeleo kama kutumia akiba zake kuibua miradi itakayoongeza ajira kwetu sisi walala hoi

Hata aanzishe ka-fund uchwara .i.e. Sumaye foundation hope angebaki anaheshimika zaidi,aangalie mwenzake Cleopa Msuya - is most respected person, nadhani angebaki na heshima ya kutosha kuliko haya ya kuita media kusutana, hivi atasema nini?uchaguzi haukuwa wa wazi? au anataka kujustify maneno yake kuwa "ukitaka mambo yakunyookee ingia CCM". kazi kwake yamemkuta
 
Last edited by a moderator:
Ukionja madaraka halafu ukataliwe nooooomaaaaaaa!
Ndiyo kama Kgalema Motlanthe. Alikaimu urais wakati ule Mbeki kajiuzulu urais

Sasa kaonja urais anaelekea kumsaliti Zuma. Motlanthe anataka kuchukua urais Zuma/Mbeki style. Na anakubalika na watu waishio mijini(urban dwellers survey)
 




Akizungumzia hatua hiyo, Waziri wa zamani wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Mbunge wa zamani Jimbo la Makete, Dk. Hassy Kitine, alisema kuangushwa kwa Sumaye katika nafasi ya NEC hakuwezi kumuathiri kisiasa kama atachukua uamuzi wa kuwania urais mwaka 2015 kupitia CCM.

"Katiba ya CCM haisemi kuwa kama unataka kuwania urais ni lazima uwe mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, kwa hiyo nasema kama Sumaye kweli anatafuta urais, bado ana nafasi ya kuwania," alisema Dk. Kitine ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alisema uchaguzi wa NEC ni wa ngazi ya wilaya tu kwa hiyo Sumaye anaweza akawa anakubalika kitaifa kuliko katika wilaya anayotoka.

"Kimsingi siwezi kumkadiria, sababu suala la urais ni kitu kingine, ni uamuzi wake binafsi sababu alipochukua fomu kugombea u-Nec alijua kuna kushinda na kushindwa, pia upo usemi kwamba nabii hakubaliki kwao," alisema Sitta.


Bwana mkubwa asikate tamaa mapema hivi....Shujaa wa kweli hupambana and for him has nothing to loose...Asikilize sauti ya wapenda taifa hili....There is always a second chance ila tu akikata tamaa nothing we can do to help him otherwise too early for him to surrender!....Hao chui ni wa makaratasi tu....We subiri mchaka mchaka uanze aone jinsi watakavyojikaanga kwa mafuta yao....Anaweza asiwe Rais kitu ambacho si lazima lakini role yake ni kubwa kukwamisha ufisadi ambao ndiyo adui yetu mkubwa...
 
[h=2][/h]JUMANNE, OCTOBA 02, 2012 05:08 NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

BAADA ya kushindwa katika nafasi ya kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupita Wilaya ya Hanang’, Mkoa wa Manyara, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema atazungumza na waandishi wa habari kueleza mchakato wa uchaguzi huo ulivyokuwa.

Sumaye alitoa taarifa hiyo jana kupitia ujumbe wa simu ya mkononi, baada ya kutakiwa na MTANZANIA, aeleze jinsi Mbunge wa Hanang’, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, alivyomgaragaza katika uchaguzi huo uliofanyika juzi.

Kabla Sumaye hajasema kwamba atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, awali mwandishi wetu alimwandikia ujumbe wa simu ya mkononi uliosema hivi.

“Mheshimiwa Sumaye, habari za mchana, mimi ni Mwandishi wa Gazeti la MTANZANIA, nimekupigia simu mara kadhaa lakini haikupokewa, shida yangu ni kutaka kujua hali halisi ilivyokuwa Hanang pamoja na msimamo wako baada ya Dk. Nagu kukushinda”.

Baada ya kuandikiwa ujumbe huo, Sumaye naye aliujibu baada ya muda mfupi akisema hivi. “Nimewaeleza waandishi wenzako wengi, kuwa nitawaita kwa pamoja mara nikirudi Dar es Salaam ndani ya siku tatu kuanzia leo,” alisema Sumaye kwa kifupi.

Kitendo cha Sumaye kupigwa mweleka katika uchaguzi wa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kupitia Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara, kiliwashangaza wengi, kwa kuwa alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda.

Uchaguzi huo uliokuwa ukifuatiliwa na wengi kutokana na kuibua makundi na mivutano ya wapambe, ulihitimishwa kwa wapiga kura 1,150 kushiriki uchaguzi huo.

Katika uchaguzi huo, Dk. Nagu aliibuka mshindi kwa kupata kura 648, huku Sumaye akiambulia kura 481. Kura 41 ziliharibika.

Hata hivyo, mgombea mwingine katika nafasi hiyo ya NEC kupitia Wilaya ya Hanang, Leons Marmo, aliamua kujitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa hiari yake.

Uchaguzi huo ulikuwa ukisimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo.

Baada ya Mbwiro kumtangaza Dk. Nagu kuwa ndiye mshindi, wafuasi wa Sumaye walijikuta wakiondoka eneo la tukio kwa hasira, wakionyesha kutoamini kilichotokea huku wakitishia kuihama CCM kwa madai kwamba, Dk. Nagu alitumia fedha nyingi kufanikisha ushindi huo.

Pamoja na wafuasi hao wa Sumaye kuonyesha kutoridhishwa na matokeo, pia Sumaye alipoona kuna kila dalili za yeye kugaragazwa, aliondoka ukumbini kimya kimya hata kabla ya matokeo kutangazwa.

 
Hata yule Dr. Vitumbua alisema hivi lakini mpaka leo hajaongea lolote.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ndiyo kama Kgalema Motlanthe. Alikaimu urais wakati ule Mbeki kajiuzulu urais

Sasa kaonja urais anaelekea kumsaliti Zuma. Motlanthe anataka kuchukua urais Zuma/Mbeki style. Na anakubalika na watu waishio mijini(urban dwellers survey)
Ebanaeeeh! Chacha huyu Chumaye wetu chijui kukubalika njini au shamba? Make alichachema kwa watu waichio njini achieweza kuchomecha ntoto chule kuzaa achizae.....akitaka mambo yanyokee atundike bendera ya chichiemu penye biachara yake hata kama ni chamaki nchanga au bange poa tu eti njomba? Na kijijini kazi yake kunyang'anya machamba ya watu tu. Bwana wewe acha tu, patamu hapo!
 
sumayi kwa ushauri wangu ni kuachana na siasa unapumzika nje ya hapo nikujidhalilisha. kwa unatafuta nini umaarufu au?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom