Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Sumaye agoma kumchafua Slaa
Na Ezekiel Kamwaga
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ameingia katika kampeni za mgombea urais wa chama chake kwa sharti la kutomchafua Dr Willbrod Slaa.
Taarifa zilizofikia gazeti hili kutoka Moshi zinamnukuu Sumaye akisema, hatamchafua mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa vile kufanya hivyo kutamvunjia hadhi.
Sumaye ameingia kwenye kampeni kufuatia mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, kuwaomba msaada viongozi wastaafu wanaodaiwa kukacha kampeni zake.
Naweza kukuthibitishia pasipo shaka kwamba, Kikwete amewaangukia baadhi ya wazee wetu kumsaidia katika mikoa ambako CCM ina hali mbaya, ameeleza mtoa taarifa.
Chanzo hicho cha habari kimesema awali ilionekana Kikwete angeweza kushinda bila msaada wa wastaafu, lakini sasa ameona upepo umegeuka.
Taarifa zinasema Kikwete alimwomba Sumaye kumsaidia hasa katika mikoa ya kanda ya Kaskazini ambako imeelezwa kuna upinzani mkubwa.
Awali, Sumaye alisita kukubali ombi hilo la rais, lakini baadayeakakubali kwa kutoa masharti ya mahala hasa anapoweza kwenda, kimeeleza chanzo chetu cha habari.
Hata hivyo, alimwambia kikwete kwamba atakwenda tu katika maeneo ambayo anadhani anaweza kuroa msaada mzuri, kimeeleza chanzo hicho.
Ofisa mmoja wa ofisi ndogo ya makao makuu, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam ameliambia gazeti hili kuwa awali Sumaye alielekezwa kwenda majimbo ya Moshi Mjini, Hai, Rombo, Moshi Vijijini na Vunjo.
MwanaHALISI lina taarifa kuwa Sumaye amekataa kufanya kampeni katika majimbo hayo, kwa maelezo kwamba anaamini wagombea ubunge wa Chadema huko hawana matatizo.
Haikufafanuliwa iwapo kwa hawana matatizo Sumaye alikuwa na maana ya kusema hawashikiki au wana uwezo wa kuwakilisha majimbo yao ..
..Kuna taarifa kwama ilibidi Sumaye awasiliane na Kikwete moja kwa moja kumweleza uamuzi wake huo. Imeripotiwa kuwa Kikwete amekubalkiana naye.
Taarifa zilizopatikana juzi Jumatatau zimesema Sumaye amekubali kufanya kampeni katika majimbo ya Vunjo na Hanang.
Aidha, imefahamika kuwa Sumaye amekubali kuingia katika kampeni kwa sharti la kutoshiriki katika kumkashifu mgombea wa urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, jambo ambalo amenukuliwa akisema linaweza kumuondolea hadhi.
Taarifa zaidi zinasema Sumaye amegoma kumfanyia kampeni mgombea ubunge wa jimbo la Rombo kupitia CCM, Basil Mramba, kwa vile ana wasiwasi ataonekana ni mtetetezi wa watuhumiwa wa ufisadi na anaweza kuanza kuandamwa baadaye .
Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo.