Sugu, tulikuchagua ukashiriki kuwawanyanyasa mama zetu mbeya?

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
IMG-20120416-WA012.jpg

IMG-20120416-WA008.jpg

IMG-20120416-WA010.jpg

IMG-20120416-WA011.jpg

IMG-20120416-WA007.jpg
 
Nikiri tu kwamba unachofanya ni udhalilishaji wa huyo mama uliyemuweka hapo! maana heading yako na ulichokiweka havina uhusiano? au unataka kutuambia nini?
 
Rev Mzito K unahangaika sana kuharibu chadema ukijifanya umo kwa mema

Kwanza kabisa hizo picha ulizoweka hazionyeshi kabisa hoja yako na nafasi ya sugu, nani atathibitisha hizo picha ni za mbeya?
 
Rev Mzito K unahangaika sana kuharibu chadema ukijifanya umo kwa mema

Kwanza kabisa hizo picha ulizoweka hazionyeshi kabisa hoja yako na nafasi ya sugu, nani atathibitisha hizo picha ni za mbeya?

swali zuri kweli hilo.
 
Nikiri tu kwamba unachofanya ni udhalilishaji wa huyo mama uliyemuweka hapo! maana heading yako na ulichokiweka havina uhusiano? au unataka kutuambia nini?
Mkuu, ninamdhalilishaje huyo mama ambaye kila siku yuko barabarani jua lake mvua yake? Mimi na hao waliomwajiri nani ni mdhalilishaji?
 
Rev Mzito K unahangaika sana kuharibu chadema ukijifanya umo kwa mema

Kwanza kabisa hizo picha ulizoweka hazionyeshi kabisa hoja yako na nafasi ya sugu, nani atathibitisha hizo picha ni za mbeya?
Mkuu ungeshirikisha ubongo wako kwanza kabla hujapost hii post. Sugu ni mjumbe wa full council ya jiji la mbeya, Kwa lugha nyingine yeye ni diwani wa halmashauri ya jiji la Mbeya. Sugu anahusika katika kuhakikisha hao wamama wanafanya kazi wakiwa na vifaa na katika hali ya usalama wa afya zao.

Pili, uhusika wangu chadema au kutokuwa chadema haukuhusu. Hata kama naichafua Chadema kama unavyoona, ni sehemu ya uhuru wangu wa kikatiba kama ulivyo huru kuichafua CCM.

Tatu, Mimi siichafui Chadema. Chadema itajichafua yenyewe.

Nne. Mimi ni mwanachadema hai kuliko wewe shabiki wa Chadema mtandaoni
 
we unafikiri kwa masaburi nn kama unahuruma kwann usimweke kwenu..ndo tatizo la watanzania yumezidi kulalamika ulitaka awe ombaomba nn hapo ilibd kumsifia huyo mama kwa kujiajili
 
we unafikiri kwa masaburi nn kama unahuruma kwann usimweke kwenu..ndo tatizo la watanzania yumezidi kulalamika ulitaka awe ombaomba nn hapo ilibd kumsifia huyo mama kwa kujiajili
Soma post yangu kabla hii ya kwako uone wewe na mimi nani anafikiria kwa masaburi
 
Rev. Kama ulikuwa unajaribisha kamera, hiyo kamera ni nzuri, usingetumia mzunguko mrefu, mie nimeona hizi picha zimetoka poa. Kwa upande wa kunyanyasa mama zetu wewe unawazalilisha, kuwapiga picha bila mpango na kuwa leta Jf
Hizi picha nimezitoa Michuzi blog. Ni wamama wanaofanya usafi Halmashauri ya Mbeya. Kama ni kudhalilishwa wameshadhalilishwa na michuzi. Kikubwa ni kuwa Sugu anapokaa na wenzake halmashauri huwa hawazungumzi kuwapatia vifaa vya kazi hawa vikongwe?
 
Mkuu, ninamdhalilishaje huyo mama ambaye kila siku yuko barabarani jua lake mvua yake? Mimi na hao waliomwajiri nani ni mdhalilishaji?

Kwa akili yako unaridhika kwamba Sugu ndiye kamuajiri?
Acheni chuki binafsi ninyi watu dhidi ya wenzenu. Hujawahi kupita manzese uone akina mama wanavyokula vumbi barabarani? Bila shaka siku ukiwapiga picha utakuja hapa kumlalamikia Mnyika.

Mara nyingi hawa wamama wanaofanya usafi wameajiriwa na makampuni binafsi kwa mkataba na halmashauri ama halmashauri zenyewe ndo zinawaajiri moja kwa moja, mbunge anahusikaje katika kuwaajiri na kuwapatia vitendea kazi?
 
Huwezi mjua kichaa hadi uone matendo yake,hivi kati yako wewe mtoa mada na sugu swali linamlenga nani?maana sidhani kama umepata ridhaa ya kumpiga picha huyo mama,pia sidhani kama kwenye katiba inaruhusu kuingilia uhuru wa mtu kama unavyodai kwani kwa wewe kumweka hapa jf umeingilia uhuru wake,je,alilazimishwa kufanya hiyo kazi? La hasha ni kazi kama zingine, kuwa wazi unamwonea donge kwa yeye kuwa mchapakazi kwa ajili ya maisha yake tofauti na wewe utumiaye mabavu,ulaghai,dhuluma n.k

USIDHARAU KAZI YA MWENZAKO, WAAMBIE WAZAZI WAKO WAJITUME,TUACHIE WAZAZI WETU WAJITAFUTIE KIPATO CHA HALALI
 
Hizi picha nimezitoa Michuzi blog. Ni wamama wanaofanya usafi Halmashauri ya Mbeya. Kama ni kudhalilishwa wameshadhalilishwa na michuzi. Kikubwa ni kuwa Sugu anapokaa na wenzake halmashauri huwa hawazungumzi kuwapatia vifaa vya kazi hawa vikongwe?

Anayetakiwa kuulizwa hapa ni mkurugenzi wa jiji kwanini wafanya usafi wa jiji la mbeya hawana vitendea kazi.
Sugu sio mtendaji wa jiji la mbeya, ni muhimu ukalitambua hili.
 
Mkuu, ninamdhalilishaje huyo mama ambaye kila siku yuko barabarani jua lake mvua yake? Mimi na hao waliomwajiri nani ni mdhalilishaji?

sasa sugu ndio mwajiri wa watu wote wa MBeya???

Bible inasema asiyefanya kazi na asile, huyo mama anafanya kazi halali na analipwa kwa jasho lake, je wewe unayetumia muda wako kuchafua watu mitandaoni waweza kusimama na kusema unafanya kazi kweli???

we unadhani yupe anayeheshimika sasa, huyu mama anayefanya usafi wa jiji (vijana wengi wameishia kuvuta bange na kupiga debe, lakini mama ameonyesha kwamba waweza kufanya kazi na kuishi), au wewe unayetumia rasilimali zisizo zako kuchafua watu????

binafsi nasema kwamba nikiwekwa na huyu mama, ingawa mimi nafanya kazi ofisini na huyu barabarani, basi huyu mama anastahili heshima zaidi kwa kufanya kazi ya vijana

na kiujumla wake ameonyesha wanawake wanaweza

Kwa kuhitimisha tu, mimi nadhani wewe ndiye unayemdhalilisha huyu mama kwa kumuonyesha kama vile anafanya kazi isiyofaa, wakati huohuo unakua wa kwanza kulalama kwamba miji ni michafu

YOU ARE AN UTTER DISAPPOINTMENT AND I DONT WHO IS YOUR MASTER IN LIFE GOD OR DEVIL!!!
 
Mkuu ungeshirikisha ubongo wako kwanza kabla hujapost hii post. Sugu ni mjumbe wa full council ya jiji la mbeya, Kwa lugha nyingine yeye ni diwani wa halmashauri ya jiji la Mbeya. Sugu anahusika katika kuhakikisha hao wamama wanafanya kazi wakiwa na vifaa na katika hali ya usalama wa afya zao.

Pili, uhusika wangu chadema au kutokuwa chadema haukuhusu. Hata kama naichafua Chadema kama unavyoona, ni sehemu ya uhuru wangu wa kikatiba kama ulivyo huru kuichafua CCM.

Tatu, Mimi siichafui Chadema. Chadema itajichafua yenyewe.

Nne. Mimi ni mwanachadema hai kuliko wewe shabiki wa Chadema mtandaoni

Ok kama ulivyosema... je halmashauri ya mbeya ina mjumbe mmoja tu???
 
Anayetakiwa kuulizwa hapa ni mkurugenzi wa jiji kwanini wafanya usafi wa jiji la mbeya hawana vitendea kazi.
Sugu sio mtendaji wa jiji la mbeya, ni muhimu ukalitambua hili.

mkurugenzi wa jiji, mtenddaji wa eneo, kamati ya ulinzi na usalama wilaya na mkoa nk.

all in all, huyo mama needs to be proud maana mtaa ni msafi kweli, amefanya kazi nzuri sana, tungempa huyo rev. mzito K hata siku moja ungeona uchafu ambao ungebaki

Inasikitisha sana kuona mtu anakosa hoja na uelewa hata wa basics anaamua kuja kulalama... na siajabu hana kazi zaidi ya kuganga njaa kwenye siasa!!! Taifa haliwezi kuendelea kwa kuwa na watu type yake kwani wao huishia kulaumu tu bila kufanya kazi yoyote
 
Back
Top Bottom