Spika Ndugai: Asiyetaka tozo ya kizalendo atupe njia mbadala ya kupata fedha

Spika Ndugai amesema wabunge wameshapitisha tozo ya kizalendo kwenye miamala ya simu na sasa ni sheria hivyo asiyeitaka atupe njia mbadala ya kutufikisha 2025

Roho wa Bwana akamshukia mtumishi wake Jerry Slaa mbunge wa Ukonga naye akajibu; Wabunge tuanze kulipa kodi.

Labda kama Spika ana swali lingine....lakini sidhani.

Ijumaa kareem?

---
Baada ya mijadala mingi kuhusiana na tozo ya miamala ya simu hususani kwenye mitandao ya kijamii ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameibuka na kudai kuwa tozo hizo ni halali na kwamba fedha hizo zitachagiza masuala ya maendeleo ikiwemo huduma za kijamii kama vile shule,hospitali na maji.

Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kwamba kumekuwa na tozo kubwa katika miamala ya simu huku akipigilia msumari kwenye tozo hizo kwa kudai kuwa Bunge ndio limepitisha na kwamba wanaopinga wanatakiwa kutoa mawazo mbadala nini kifanyike huku akisisitiza lengo ni ifikapo 2025 Tanzania iwe Taifa tofauti katika suala la Maendeleo.

Akizungumza mapema leo Julai 23,2021,katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,Spika Ndugai amesema "Sisi kama Bunge tulikaa kwa pamoja na kujadiliana kisha tukaamua kuwa na tozo katika miamala ya simu kwa sababu fedha zitakazopatikana zitaenda katika mfuko Maalum ambao utawasaidia wananchi,"amesema na kuongeza;

"Tumepitisha na tukatunga sheria , tunataka kuliona hilo,sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofaut,CCM hoyee,nimemaliza,"amesema Spika huyo.

Chanzo: Malunde
Huo ni mkakati wa ndugai na mwigulu kumuhujumu mama

Aisee mheshimiwa rais suala la tozo unahujumiwa!!!


Mama nataka nikuambia mwigulu na ndugai wanafanya kusudi na kutoa matamko mabaya kuhusu tozo kwa maksudi tu ili wakuhujumu

Mama umesahau kuwa mwigulu na ndugai ni lile genge la S?

Mama naskia hata kukamatwa kwa mbowe ni maagizo ya ndugai....mama haya yanafanyika kupitia mgongo fulani ili kukuchezea shere yaani wanakuhujumu kupitia haya

Lengo lao ni hili ushindwe mapema wamuingize mtu wao madarakani

Mama naamini huwezi kuamuru mbowe afanyiwe vile mama najua hukuamuru tozo mama shtuka mapema....mama hao mawaziri wa mwendazake uliowarithi ni hatari sana.......

Unapaswa ung'amue hili mapema......unahujumiwa kwa maksudi kwa kutumia akili kubwa ili uchukiwe na wananchi huku wao wakijua wanaucheza mchezo kukuharibia

..
 
Back
Top Bottom