View attachment 2608230
Picha: Spika Dkt. Tulia Akson

Spika wa Bunge, Tulia Ackson ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.

Taarifa hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda.

Katika swali lake Mwakagenda ameuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.

“Mheshimiwa Tulia Ackson alishawasilisha kwenye mamlaka nia ya kuomba jimbo hilo ligawanywe, serikali inatafakari maombi hayo na wakati utakapofika vigezo vitatazamwa,” amesema Ummy.

Katika swali la msingi mbunge wa Kilindi Omari Kigua ameuliza ni lini Serikali italigawa Jimbo la Kilindi kutokana na jiografia yake.

Naibu Waziri amesema kwa sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi mbali mbali ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

“Hivyo kwa kuzingatia taratibu na vigezo ,muda wa kugawa majimbo utakapofika Tume itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa machakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao na hivyo kushughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kikatiba,”amesema Ummy.

Ummy amesema majimbo mengi yameomba kugawanywa lakini mambo yanayotazamwa ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa bunge, idadi ya wabunge wa viti maalumu na jiongrafia za maeneo yaliyoomba kugawanywa.

Chanzo: Mwananchi
Huyo Tulia anatafuta kukwepa kupambana na SUGU maana anajua hawezi kutoboa!
Waangalie gharama za kuwa na wabunge wengi
 
India ina watu 1.4 billon ina wabunge 788 wa upper house na lower house.Tanzania yenye watu 61M ina wabunge 360.
Africa aliye tuloga asha kufa.
 
Ili tuendelee tunahitaji wananchi wajiwakilishe kwa kujitolea zaidi kuliko mfumo wa sasa ambao muwakikishi analipwa zaidi ya mtaalamu.
Kwa utaratibu wa sasa;

Kwanza kabisa inadumaza maendeleo kwa wataalamu kukimbilia kwenye siasa.
Pili inaongeza rushwa kwa watu wenye tamaa kutumia gharama kubwa kushawishi.
Tatu inasababisha uwezekano wa watu wajinga kuwakilisha wengine kupitia rushwa.
 
Haya yalikuwepo enzi zile, Kongwa ilizaliwa baada ya Mchungaji kunena neno la Bwana, watu wakaanza kuelekea alipo, ili kuokoa jahazi Kongwa ikazaliawa!!!!
 
View attachment 2608230
Picha: Spika Dkt. Tulia Akson

Spika wa Bunge, Tulia Ackson ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.

Taarifa hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda.

Katika swali lake Mwakagenda ameuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.

“Mheshimiwa Tulia Ackson alishawasilisha kwenye mamlaka nia ya kuomba jimbo hilo ligawanywe, serikali inatafakari maombi hayo na wakati utakapofika vigezo vitatazamwa,” amesema Ummy.

Katika swali la msingi mbunge wa Kilindi Omari Kigua ameuliza ni lini Serikali italigawa Jimbo la Kilindi kutokana na jiografia yake.

Naibu Waziri amesema kwa sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika maandalizi mbali mbali ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

“Hivyo kwa kuzingatia taratibu na vigezo ,muda wa kugawa majimbo utakapofika Tume itatoa tangazo rasmi kwa wadau wote wa uchaguzi juu ya kuanza kwa machakato wa ugawaji wa majimbo ili wadau wawasilishe maoni na maombi yao na hivyo kushughulikiwa kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kikatiba,”amesema Ummy.

Ummy amesema majimbo mengi yameomba kugawanywa lakini mambo yanayotazamwa ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa bunge, idadi ya wabunge wa viti maalumu na jiongrafia za maeneo yaliyoomba kugawanywa.

Chanzo: Mwananchi
Anamkimbia Sugu na keshasema ulipo naye yupo mpaka uteme mbungo na bahati mbaya Samia sio Magufuri Free &fair election
 
Kinachonishangaza zaidi ni hivyo vigezo vya kugawa majimbo!

"Ummy amesema majimbo mengi yameomba kugawanywa lakini mambo yanayotazamwa ni pamoja na ukubwa wa ukumbi wa bunge, idadi ya wabunge wa viti maalumu na jiografia za maeneo yaliyoomba kugawanywa"
 
"the shit is real real"
from facebook(Livino Haule)

Enzi zetu darasani Sekondari unaulizwa "What are the major reasons for Tulia's suggestion to divide Mbeya Urban Constituency."

Majibu tungesema;

1. Lack of Legitimacy

2. Death of Mwendazake

3. Samia's ideology of Maridhiano (4-Rs)

4. Fear of 2025 General Elections

5. Strength of Mbilinyi the SUGU.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom