Spika akalia kuti kavu

Naogopa ku comment ntapigwa ban..ngoja nikae kimya tu ila mungu yupo
 
Spika kung’olewa?

Baadhi ya wabunge wameanza kuwahamasisha wenzao kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge.
Wabunge hao walifikia hatua hiyo kwenye kikao cha dharura walichokifanya jana katika Ukumbi wa Pius Msekwa kwa lengo la kufanya maandalizi ya kwenda Zanzibar kuhudhuria msiba wa wenzao waliozama katika ajali meli ya Skagit.

Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahimu Sanya (CUF), alisema Spika Makinda hana utu ndiyo maana aligoma kuahirisha shughuli za Bunge ili kutoa nafasi ya watu kushiriki kwenye jambo hilo.

“Huyu Spika hatufai, yaani vifo vikitokea kwa watu wa Bara yeye ndiyo ataona kuna uzito…hapa alikufa Amina Chifupa tukaahirisha Bunge, sasa iweje wenzetu wamekufa kule Zanzibar yeye akatae kuahirisha shughuli za Bunge? Jamani tujipange kupiga kura za kutokuwa na imani naye, ameonyesha kushindwa kulihimili Bunge,” alisema.

Mbunge mwingine kutoka Zanzibar alisema hawaoni sababu ya kuendelea na mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa sababu wapiga kura wao ndio waliofariki dunia.

“Tuna raha gani ya kuendelea kujadili hotuba ya bajeti, huyu Spika tumedhihirisha hana uwezo wa kutuongoza, hatufai, waliokufa kule ni binadamu si paka wala wanyama,” alisema.

Chanzo:Tanzania daima

makinda ya kuku
 
Mnataka awe na uchungu kwani ameshawai kujifungua au kuwa na mtoto?

Kwa kauli yake ya jana inaonyesha jinsi alivyokuwa na roho mbaya, roho iliyokosa utu.

Pia, hata akalie ncha ya hilo 'kuti kavu', kwa mfumo wa kimagamba huyu Spika hawawezi kumng'oa uspika, tuhesaba tumeshalamba garasa, tusubiri 2015...

Hata kama amekosea tuseme amekosea tu. Haina haja ya kwenda "personal". Her private life is off limits as much as you would like yours to be. This is misguided thinking, please restrain yourself
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Atamuomba Kova amsaidie kukamata mtui yeyote hata wa sumatra na kumfikisha mahakamani ili hilo suala lisizungumzike tena na yeye aponee hapo!!ni upepo tu utapita!liwalo na liwe na Bunge siahirishi!!
 
Wabunge wa CCM wasipokuwa makini huyo Spika atawaingiza kaburini. She has nothing to loose, hagombei tena, na tayari ana pension ya uhakika kama Spika mstaafu, kwa hiyo sasa hivi atapeleka mambo ili mradi yanafurahisha mtandao wake (ambao nao wataingia kwenye pension) shida ni kwa CCM kama chama na hasa wagombea nafasi za ubunge kwa kupitia CCM!
 
Makinda alipopewa Uspika kwa mbinu na CCM walifikiri wamepata kumbe wamepatikana!

Tuliwaambia CCM tangu mwanzo kabisa kwenye ukumbi huu kwamba,MWANAMKE HATA SIKU MOJA HAWEZI KUONGOZA WANAUME(KAYA/FAMILIA) KWA MAANA MUNGU AMEKATAZA HILO JAMBO. BIBLIA INASEMA,"SIMPI RUHUSA YA MWANAMKE KUMTAWALA MWANAMME".Full Stop!

KILE TUNACHOSHUHUDIA KWA SASA BUNGENI NI LAANA YA KUTAWALIWA AU KUONGOZWA NA MWANAMKE ANNA MAKINDA. WATAZNANIA MTAJUTA KUKUBALI UPUUZI NA UJINGA HUU WA CCM!
 
kuendelea kuwa na watwala wanaowaza maslahi yao kuliko ya umma tutaendelea kupoteza maisha kama hivi..poleni sana mliokumbwa na ajali hii na wale waliopotelewa na ndg zao kupitia ajali hiyo
 
Haya sasa limehairishwa! je wote wameenda huko Zenji au ndo wengine wameenda kuendeleza ufuska wao mtaaani?
 
Circus man hajui hata kuowanisha mambo. Kanumba na Chifupa walikuwa maelfu ya watu. Halafu unawezaje kufananisha ajali ya watu 280 kati ya watu wa Zanzibar 1,500,000 na idadi ya watu karibu 40,000,000. Waswahili husema maji yako kiombeni ni ziwa kwa chungu!
Sijui lakini kama unaweza kufahamu , naona akili yako si ya kawaida!

Ungekuwa na akili timamu wala usingetoa mapovu kama hivi! Katika hali ya kawaida serikali inapotangaza msiba wa kitaifa shughuli huendelea kama kawaida! Timu ya mafunzo kutoka Zanzibar jana iliendelea na mashindano ya Kagame lakini kuonyesha kuwa kuna msiba wa taifa walifunga vitambaa vyeusi.

Acha kutoa kilio cha mchawi!
 
Hahahah... Wameanza uchadema, wakaingia udini , wakaenda ukabila, wamekwenda u zanzibar na ubara, wataenda uccm magamba --- uccm safi, then uccm vijana na uccm wazee... Kwa majumlisho ... Mfa maji haishi kutapatapa.
 
Mnataka awe na uchungu kwani ameshawai kujifungua au kuwa na mtoto?

Kwa kauli yake ya jana inaonyesha jinsi alivyokuwa na roho mbaya, roho iliyokosa utu.

Pia, hata akalie ncha ya hilo 'kuti kavu', kwa mfumo wa kimagamba huyu Spika hawawezi kumng'oa uspika, tuhesaba tumeshalamba garasa, tusubiri 2015...

ana mtoto wa kike tena huyo binti (sio spika)alizaa na msanii mmoja wa jijini Mwanza wakiwa shule..akakimbizwa Ulaya kusoma
 
Ungekuwa na akili timamu wala usingetoa mapovu kama hivi! Katika hali ya kawaida serikali inapotangaza msiba wa kitaifa shughuli huendelea kama kawaida! Timu ya mafunzo kutoka Zanzibar jana iliendelea na mashindano ya Kagame lakini kuonyesha kuwa kuna msiba wa taifa walifunga vitambaa vyeusi.

Acha kutoa kilio cha mchawi!

Nakubali kuwa sina akili timamu ya kuweza kukuelewa mtu usiejuwa kufananisha vitu! Sawa hivyo ulitaka na wabunge nao wavae vitambaa vyeusi au sio ? Kwa bahati mbaya hawakuvaa sasa ina maana kuwa wao msiba haukuwahusu.
Iwapo akili yenyewe ndio hiyo uliyonayo wewe basi bado naridhika kkuwa sina akili lakini siko tayari kuwa na akili za aina yako!
 
Sioni kosa kabisa la Makinda kama meli inge zama ziwa victoria hao wanafiki wa zanzibar hata wasingefikiria kutoka bungeni!
 
Nakubali kuwa sina akili timamu ya kuweza kukuelewa mtu usiejuwa kufananisha vitu! Sawa hivyo ulitaka na wabunge nao wavae vitambaa vyeusi au sio ? Kwa bahati mbaya hawakuvaa sasa ina maana kuwa wao msiba haukuwahusu.
Iwapo akili yenyewe ndio hiyo uliyonayo wewe basi bado naridhika kkuwa sina akili lakini siko tayari kuwa na akili za aina yako!

Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake!
 
Back
Top Bottom