Spika kungolewa?
Baadhi ya wabunge wameanza kuwahamasisha wenzao kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge.
Wabunge hao walifikia hatua hiyo kwenye kikao cha dharura walichokifanya jana katika Ukumbi wa Pius Msekwa kwa lengo la kufanya maandalizi ya kwenda Zanzibar kuhudhuria msiba wa wenzao waliozama katika ajali meli ya Skagit.
Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahimu Sanya (CUF), alisema Spika Makinda hana utu ndiyo maana aligoma kuahirisha shughuli za Bunge ili kutoa nafasi ya watu kushiriki kwenye jambo hilo.
Huyu Spika hatufai, yaani vifo vikitokea kwa watu wa Bara yeye ndiyo ataona kuna uzito hapa alikufa Amina Chifupa tukaahirisha Bunge, sasa iweje wenzetu wamekufa kule Zanzibar yeye akatae kuahirisha shughuli za Bunge? Jamani tujipange kupiga kura za kutokuwa na imani naye, ameonyesha kushindwa kulihimili Bunge, alisema.
Mbunge mwingine kutoka Zanzibar alisema hawaoni sababu ya kuendelea na mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa sababu wapiga kura wao ndio waliofariki dunia.
Tuna raha gani ya kuendelea kujadili hotuba ya bajeti, huyu Spika tumedhihirisha hana uwezo wa kutuongoza, hatufai, waliokufa kule ni binadamu si paka wala wanyama, alisema.
Chanzo:Tanzania daima
Mnataka awe na uchungu kwani ameshawai kujifungua au kuwa na mtoto?
Kwa kauli yake ya jana inaonyesha jinsi alivyokuwa na roho mbaya, roho iliyokosa utu.
Pia, hata akalie ncha ya hilo 'kuti kavu', kwa mfumo wa kimagamba huyu Spika hawawezi kumng'oa uspika, tuhesaba tumeshalamba garasa, tusubiri 2015...
Waspanish wana msemo huu, "Mdomo ulifumbwa hauingii nzi," kwa hivyo na mimi kwa hili bora nifumbe mdomo.Naogopa ku comment ntapigwa ban..ngoja nikae kimya tu ila mungu yupo
Circus man hajui hata kuowanisha mambo. Kanumba na Chifupa walikuwa maelfu ya watu. Halafu unawezaje kufananisha ajali ya watu 280 kati ya watu wa Zanzibar 1,500,000 na idadi ya watu karibu 40,000,000. Waswahili husema maji yako kiombeni ni ziwa kwa chungu!
Sijui lakini kama unaweza kufahamu , naona akili yako si ya kawaida!
Mnataka awe na uchungu kwani ameshawai kujifungua au kuwa na mtoto?
Kwa kauli yake ya jana inaonyesha jinsi alivyokuwa na roho mbaya, roho iliyokosa utu.
Pia, hata akalie ncha ya hilo 'kuti kavu', kwa mfumo wa kimagamba huyu Spika hawawezi kumng'oa uspika, tuhesaba tumeshalamba garasa, tusubiri 2015...
Ungekuwa na akili timamu wala usingetoa mapovu kama hivi! Katika hali ya kawaida serikali inapotangaza msiba wa kitaifa shughuli huendelea kama kawaida! Timu ya mafunzo kutoka Zanzibar jana iliendelea na mashindano ya Kagame lakini kuonyesha kuwa kuna msiba wa taifa walifunga vitambaa vyeusi.
Acha kutoa kilio cha mchawi!
Nakubali kuwa sina akili timamu ya kuweza kukuelewa mtu usiejuwa kufananisha vitu! Sawa hivyo ulitaka na wabunge nao wavae vitambaa vyeusi au sio ? Kwa bahati mbaya hawakuvaa sasa ina maana kuwa wao msiba haukuwahusu.
Iwapo akili yenyewe ndio hiyo uliyonayo wewe basi bado naridhika kkuwa sina akili lakini siko tayari kuwa na akili za aina yako!