Special kwa wana CDM na wana Igunga tu

inshu ya Igunga ndo mahala CDM wanatakiwa kutulia na kuonyesha umakini wa hali ya juu sana. baada ya mgombea kupatikana, ilani za kuuza wakati wa kampeni,, ijadiliwe/ipatikane pia namna ya kulinda kura/kuhakikisha uchaguzi unafanyika fairly na kura zinasimamiwa vzuri. pressure itakuwa kubwa sana kwa mkurugenzi kuelekezwa kuchakachua matokeo incase mwelekeo unakuwa mbaya kwa CCM (binafsi nawaombea njaa ccm)

Kwa hali tunayoisikia Igunga kwa sasa, strategy ya cdm isiwe kuuza mgombea bali kuuza chama zaidi maana ndicho chenye mvuto kwa sasa kutokana na mvuto wa viongozi wake na wabunge wake vijana. CDM inamvuto zaidi kuliko chama chochote kwa sasa hivyo waitumie nafasi hii.

Mimi naamini zaidi katika vifuatavyo
1. Mgombea lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja wakati wa kampeni. Kama cdm watampata mtu mwenye uwezo wa kuwashawishi watu hasa vijana kwa nguvu ya hoja, Itakuwa ni mwanzo wa ushindi. Kumbuka vijana wote wa cdm walioko bungeni leo walishinda kwa kigezo hiki bila kujali ni sehemu gani ya nchi. Wasukuma wanapenda mtu mwenye uwezo wa kuongea na mwenye hoja, pia wanapenda mtu anayeweza kutumia mifano ya kwao unapoongelea issue za kuwaponda wapinzani wako.

2.Kuongelea zaidi issue zinazo wachoma wana igunga(watanzania) kama ugumu wa maisha uliotokana na ufisadi wa ccm, madeal ya kifisadi ya watumishi wa serikali ya ccm kama umeme,madini,na aridhi. Hapa ni kuchafua kila kitu kuhakikisha ccm hawafurukuti kwa hoja labda kwa kununua wapiga kura.

3. Kutumia kupendwa kwa viongozi wa cdm kwa sasa wakiwemo wabunge wake wote wennye mvuto kwenye hoja kama Dr. Slaa, Mbowe,zitto,Lema, mnyika,msigwa,wenje,Mdee, dogo wa mbozi etc. Kila mtu ajipange kuongelea hoja moja ambayo anauelewa mkubwa kama zitto anaweza kujikita kwenye ufisadi kwenye madini n, Mdee kwenye ufisadi kwenye Ardhi,Mnyika kwenye ufisadi kwenye project za umeme, Lema kwenye issue za haki za watu kupuuzwa na kupatikana kwa rushwa kama matibabu, mahakamani, ardhi na mengine mengi.

sasa kama hizi taarifa zinawahusu wana Igunga wa CDM kwanini umeileta Jamvini?

ushauri.

wape masunduku ya maoni jimboni.

Wewe ndo unamatatizo kwanini umesoma na kucomment post isiyokuhusu?

3. Kutumia kupendwa kwa viongozi wa cdm kwa sasa wakiwemo wabunge wake wote wennye mvuto kwenye hoja kama Dr. Slaa, Mbowe,zitto,Lema, mnyika,msigwa,wenje,Mdee, dogo wa mbozi etc. Kila mtu ajipange kuongelea hoja moja ambayo anauelewa mkubwa kama zitto anaweza kujikita kwenye ufisadi kwenye madini n, Mdee kwenye ufisadi kwenye Ardhi,Mnyika kwenye ufisadi kwenye project za umeme, Lema kwenye issue za haki za watu kupuuzwa na kupatikana kwa rushwa kama matibabu, mahakamani, ardhi na mengine mengi.
Bila kumsahau Sugu mzee wa vina.

wote naona mnaangaika bure! Maneno mengi mnawachambua wagombea feki.
Mnajifanya kama hamfahamu utaratibu wa chama chenu Mgombea ubunge jimbo la Igunga Mbowe na a loser Dr Slaa, wameishamchagua siku nyingi, kama vile ilivyokuwa BAVICHA na viti maalumu BAWACHA

Muhimu: Nani kati ya hawa unamwona anafaa kupeperusha bendera yetu Igunga toa pia sababu.

1. Kajua Sebastiani 2. Marco Amos 3. Kahema John, 4. Buzinza Magego, 5. Dickson Samsoni, 6. Anwari Luhumbi, 7. Erasto Tumbo, 8. Joseph Mwandu, 9. Juma Katigula, 10.Frank Matto, 11.Joseph Mapalala 12.Juma Chaha.

Pamoja Tutaweza, Nimerudi kuwashika............mapambano ndiyo yanaanza..... People's Power.
Erasto Tumbo lazima atapewa tuu..Si tumezoea kuona wanapeana..halafu huyu atakuwa mchaga ..subiri nizame google nicheki tumbo ni wapi.CCM oyeeeee

Mgombea wa kambi ya upinzani Igunga awe ni mmoja tu. Ni kivipi mgombea huyo apatikane; viongozi watusaidie kuratibu hilo.

Kambi ya upinzani Tz ni CDM peke yake. Ukiangalia CUF, akishinda mtu wa CUF au CCM ni sawa. May be CUF wakae na CCM watoe mtu mmoja wa kupambana na CDM

Muhimu: Nani kati ya hawa unamwona anafaa kupeperusha bendera yetu Igunga toa pia sababu.

1. Kajua Sebastiani 2. Marco Amos 3. Kahema John, 4. Buzinza Magego, 5. Dickson Samsoni, 6. Anwari Luhumbi, 7. Erasto Tumbo, 8. Joseph Mwandu, 9. Juma Katigula, 10.Frank Matto, 11.Joseph Mapalala 12.Juma Chaha.

Pamoja Tutaweza, Nimerudi kuwashika............mapambano ndiyo yanaanza..... People's Power.
yeyote atakayepitishwa na CDM ndiye mbunge

Wana Chadema nimeona niwatoe wasiwasi kuhusu matokeo yaliyopita ya jimbo la Igunga ieleweke Chadema hatukuweka mgombea wagombea walikuwa wawili tu RA wa CCM aliyepata kura 34,090 na Leopard Mahona wa CUF aliyepata kura 11,321 unaweza kuona kabisa ni kiasi gani kuna mtaji wa kura za upinzani huko, hiyo ni mbali na matokeo ya kura za urais.

Kwa taarifa yenu Chadema Igunga ina mizizi kuliko watu wanavyodhani, CCM imechokwa watu wanataka mabadiliko hizo kura za CUF zisiwababaishe wananchi walikuwa hawana alternative nyingine zaidi ya kukipigia chama hicho nafikiri Chadema ingeweka mgombea mambo yangekuwa tofauti, kura zinaonyesha mbali ya RA kugawa pesa kila kaya lakini bado watu walimkataa.

Ngoja niwakumbushe historia ya uchaguzi mdogo wa Busanda 2009, matokeo ya ubunge Busanda ya mwaka
2005: CCM= 61,868, CUF=13,094 na Chadema= 3,109 lakini kwenye uchaguzi mdogo uliofuata mambo yakabadilika...
2009: CCM= 29,242, CUF= 977 tu na Chadema ikapata kura 22,799 what happened to CUF?

Kilichoifanya Chadema iipiku CUF kwa kura nyingi kiasi hicho ndicho hicho hicho kitaifanya Chadema kuibuka kidedea kwenye uchaguzi huu. Kwa hilo sina wasiwasi kabisa kwasababu zifuatazo, kwanza Igunga tuna mtaji wa kura za upinzani pili tuna nyongeza kutoka CCM waliokatishwa tamaa na utawala wa CCM na tatu wapenzi wa mbunge wao kipenzi RA waliochukizwa na maamuzi ya kumfukuza mbunge wao tuko nao pamoja. Nne CCM imechoka haina mtu kitaifa wa kwenda Igunga na kukiuza chama Nape na Chiligati kwa hali ya kawaida hawawezi kukanyaga kule labda kama wanataka kuzomewa.

Pamoja na hayo Chadema ina kikosi kazi kilichokamili kuanzia mzee wa anga hadi askari wa miamvuli, NEC ikiacha haki itendeke kwenye uchaguzi huu na Chadema tukijipanga vizuri kuzilinda kura kwa sababu zipo tuna kila haja ya kutembea kifua mbele kuwa jimbo hilo ni letu.

Inatia faraja kuona wagombea kwa CDM ni wengi kuliko CCM au CUF na hiyo ina onyesha CDM wana nguvu na uhai mkubwa kuliko vyama vingine vyote na kila mtu angependa kuibuka mshindi kwa bendera ya CDM. Je CUF watakubali kujitoa na kuunga mkono CDM ili kura zisigawanyike?

Ushindi upo kwa kiasi kikubwa mpaka sasa ukizungumza na watu walioko igunga hakika inatia moyo sana

Viva CDM, viva wapiganajiiiiiiiiiiii

Ukiwasikia Magamba wanavyojitapa kuwa Jimbo la Igunga ni lao utakimbia, na hapa ukiangalia Makwanda wanavyosema unaona kabisa jimbo la kwao. CUF nao ndio usiseme wao wanasema wana mtaji wa mgombea wao! Tusubiri hiyo siku

Kama unawapigia debe,waite hapa jukwaani then kila mmoja atoe cv yake na malengo kwa wanaigunga.hapo nitacoment.

Kila la kheri CHADEMA na wote wana mtaji mkubwa sana katika siasa za usoni katika kuona wanaleta changamoto makini sana katika chama na hasa chadema!!

Wana Chadema nimeona niwatoe wasiwasi kuhusu matokeo yaliyopita ya jimbo la Igunga ieleweke Chadema hatukuweka mgombea wagombea walikuwa wawili tu RA wa CCM aliyepata kura 34,090 na Leopard Mahona wa CUF aliyepata kura 11,321 unaweza kuona kabisa ni kiasi gani kuna mtaji wa kura za upinzani huko, hiyo ni mbali na matokeo ya kura za urais.

Kwa taarifa yenu Chadema Igunga ina mizizi kuliko watu wanavyodhani, CCM imechokwa watu wanataka mabadiliko hizo kura za CUF zisiwababaishe wananchi walikuwa hawana alternative nyingine zaidi ya kukipigia chama hicho nafikiri Chadema ingeweka mgombea mambo yangekuwa tofauti, kura zinaonyesha mbali ya RA kugawa pesa kila kaya lakini bado watu walimkataa.

Ngoja niwakumbushe historia ya uchaguzi mdogo wa Busanda 2009, matokeo ya ubunge Busanda ya mwaka
2005: CCM= 61,868, CUF=13,094 na Chadema= 3,109 lakini kwenye uchaguzi mdogo uliofuata mambo yakabadilika...
2009: CCM= 29,242, CUF= 977 tu na Chadema ikapata kura 22,799 what happened to CUF?

Kilichoifanya Chadema iipiku CUF kwa kura nyingi kiasi hicho ndicho hicho hicho kitaifanya Chadema kuibuka kidedea kwenye uchaguzi huu. Kwa hilo sina wasiwasi kabisa kwasababu zifuatazo, kwanza Igunga tuna mtaji wa kura za upinzani pili tuna nyongeza kutoka CCM waliokatishwa tamaa na utawala wa CCM na tatu wapenzi wa mbunge wao kipenzi RA waliochukizwa na maamuzi ya kumfukuza mbunge wao tuko nao pamoja. Nne CCM imechoka haina mtu kitaifa wa kwenda Igunga na kukiuza chama Nape na Chiligati kwa hali ya kawaida hawawezi kukanyaga kule labda kama wanataka kuzomewa.

Pamoja na hayo Chadema ina kikosi kazi kilichokamili kuanzia mzee wa anga hadi askari wa miamvuli, NEC ikiacha haki itendeke kwenye uchaguzi huu na Chadema tukijipanga vizuri kuzilinda kura kwa sababu zipo tuna kila haja ya kutembea kifua mbele kuwa jimbo hilo ni letu.
Mkuu wangu, Chadema haishindani na CUF swala ni kuchukua Jimbo toka CCM. Mfano wa Busanda hautusaidii kitu kwa sababu jimbo lilibakia mikononi mwa CCM..
Sasa nadhani ni bora kutazama sababu ambazo zilipelekea Chadema ikashindwa Busanda na CCM kurudisha jimbo lake. Tumejifunza kitu gani na makosa gani yaliyofanyika kwa sababu hali ya kisiasa Busanda na Igunga sio sawa kabisa. Busanda tulikuwa na mgombea toka 2005 wakati Igunga hatuna wala hatukuwa na mtu hadi kujiuzulu kwa Rostam...

Hongera Joseph Kashindye Mwandu kupeperusha bendera ya wakombozi watumie vizuri walimu wenzako wakufanyie kampeni najua na wao wanajua walivyopigika.

Back
Top Bottom