Sokoine was not a hero, Salim was...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,118
115,947
Nimejikuta namkumbuka Sokoine na siasa za Tanzania miaka ile na kwa jinsi ambavyo watu huwa wanam refer kama 'a big hero' au best PM ever..

Tanzania yetu hii ni nadra sana watu hajadiliwa katika 'fairness inayostahili'wapo ambao wanakuzwa kupita hali halisi na wapo ambao wanapondwa kuliko hali halisi..

Mmoja wa watu ambae mimi binafsi nimefuatilia kidogo tu siasa zake za enzi hizo ni Edward Sokoine aliwahi kuwa waziri mkuu mara mbili....wakati wa Nyerere....kiukweli tukiwa kama watu ambao tunataka kujifunza from our past ni sahihi sana tuwe tunajadili vitu kama why Sokoine alioneka 'a hero' kwa baadhi ya watu? Na nini hasa alikifanya kustahili sifa hiyo? Na kama aliyoyafanya yanastahili kumuita shujaa na mfano wa viongozi wengine wa baadae wa Taifa hili.. na kama hakuwa a big a hero then.. je wanaojaribu kumfuata wana kipi cha kujifunza?

Kuna vitu viwili vilijitokeza ambavyo binafsi naona ni mfano tosha wa kwa nini Sokoine hakuwa 'role model ya viongozi bora' Tanzania.....na Salim A Salim kwangu namuona a hero sababu alifanya yale ambayo Sokoine alishindwa kwa muda mfupi tu....bila kutafuta sana ujiko wala kujipa credit ...ilikuwa kimya kimya lakini wanaojua historia wanakiri....

La kwanza ni lazima pia kujua mazingira ya Tanzania kipindi kile;

Kufuatia vita ya Iddi Amini na Nyerere kukataa masharti mbalimbali ya World Bank na IMF nchi iliingia kwenye shida kubwa mno ya bidhaa za msingi za matumizi vitu kama sigara,sukari,unga mchele vilikuwa adimu kupatkana, watu walikuwa wanapanga foleni hasa mijini kama Dar kwa ajili ya kupata tu sukari au sigara.....sasa wafanyabiashara wengi wakawa wana take advantages kwa kulangua bidhaa na wengine kuzificha ili zizidi kupanda bei..

Hapa ndo umaarufu wa Sokoine ulipojitokeza.... Sokoine aliiongoza kamata kamata ya 'walanguzi' na 'wahujumu wa uchumi' na aliifanya hiyo kazi na kusaidia 'kupunguza' hiyo shida ya bidhaa madukani..

Alionekana shujaa wakati ule lakini kiukweli tatizo halikuisha.....lakini alikuwa anaogopwa kupita maelezo 'alionekana mzalendo na anaejali' kwa kuwakamata 'walanguzi' lakini mwisho wake tatizo liliendelea.

Nchi ilikuwa na matatizo tele mfano nguo za kuvaa tu ilikuwa hakuna.... usafiri wa mijini kampuni kama KAMATA ilishakufa na kadhalika...matatizo haya yaliendelea kuwepo moja ya sababu ilikuwa KUKOSA ' mtu wa kumwambia Nyerere UKWELI wa hali halisi na makosa ya sera na mbinu mpya inahitajika kuondoka na matatizo hayo na sio kuendelea kukamata kamata tu watu...

Baada ya Sokoine kufariki kwa ajali mwaka 1984 Nyerere alimteua Salim kuwa Waziri mkuu na Salim bila woga alienda kum face Nyerere na kumwambia lazima baadhi ya sera zibadilishwe hata kwa dharura tu, baada ya tukio maarufu Mtwara ambapo wananchi walijifunga viroba kumkaribisha waziri mkuu na wengine wanasema 'walivua nguo' kuonesha kero yao ya kukosa nguo za kuvaa.

Salim alim face Nyerere na ndio 'mitumba ikaruhusiwa Tanzania' kama 'sera ya dharura' baada ya viwanda vyote kufa.....Salim alipoona watu wanahangaika na kusubiri mabasi ya KAMATA kwa masaa kadhaa akaja tena kuruhusu 'daladala' kama mbinu ya dharura kutatua tatizo hilo.

Nyerere alikuwa hataki kabisa hizi sera za kuruhusu watu binafsi wafanye biashara hata kama wananchi wanateseka, 'ujasiri wa Salim' kumface na kumshawishi Nyerere akubali japo kwa 'dharura' ili wananchi wasiteseke hadi hapo nchi uchumi utakapotengemaa..

Nyerere alikuwa anaogopwa... Ndio maana Mtei alijiuzulu alikuwa hashauriki.......lakini Salim mbele ya mateso ya wananchi aliweza kum face na kumbadili msimamo.

Sokoine kwangu naona alikuwa 'mtiifu' na waziri mzalendo na mchapakazi akitekeleza 'vizuri' maagizo ya Nyerere lakini kama 'ushujaa' mimi namuona Salim alikuwa 'shujaa mkubwa'.

Aliweka maslahi ya wananchi mbele, sera za kukamata kamata na kufukuza fukuza zinaweza mfanya kiongozi awe maarufu sana na avuume mno lakini je zinatatua tatizo kiasi gani? Je, sera zinabadilishwa? Je, unafuu unaohitajika unapatikana?

Kiongozi anaweza kupata 'cult followers' huku 'matatizo' yale yale bado yapo vilevile unafuu wa msimu tu lakini sio kuondoka kabisa...

Salim alifanya kile Sokoine alipaswa kukifanya siku nyingi....lakini hakukifanya ingawa Sokoine ana 'cult followers' na Salim hana mashabiki die hard...lakini still ukitazama historia unbiased..utakubaliana na mimi.

Nakaribisha mjadala, ambao mnaamini Sokoine was a hero nini mnaamini alikifanya cha kustahili kuitwa a hero?

Kumbuka ninachokisema, Sokoine alikuwa mzalendo na mchapakazi lakini siamini kama alikuwa mfano bora wa viongozi... Salim was better......
 
The Boss

Salim alikataa kuwa Rais akaona bora kuwa katibu mkuu wa umoja wa afrika, hilo tu lilimchafua.
 
Last edited by a moderator:
The Boss na urushaji wa jiwe gizani...!
=====================================
Nikirudi kwenye mada kibunuasi na kikarumekenge....:Nasema hivi

Salim yawezekana 'alifanya ukorofi' labda ndiyo maana akaondoshwa kiana kwenda OAU. Mwalimu (R.I.P) yawezekana aliamini kuwa necessity is the mother of creativity na subira inavuta heri. Salim yawezekana hakulisoma hilo kwa Mwalimu(R.I.P). Salim yawezekana hakuamini katika kujitegemea, Salim labda hakuamini katika ujamaa,undugu,umoja na mshikamano...eeh tumuulize!Pia nadhani ushawishi wa Salim yawezekana ndiyo uliolitumbukiza taifa hili katika 'Ombaomba' ya kupigiwa mfano...!
Vilevile nadhani Salim akiulizwa sasa kama unazungumziaje huo ushawishi kwa Mwalimu(R.I.P) yawezekana 'akabubujikwa machozi na kuanza kuomba msamaa watanzania bila kikomo kwa muda wa siku sita(6)' juu ya ushawishi alioufanya...!
===========================================
Kwa hiyo: Kwangu mimi Edward Sokoine (R.I.P) ni kiongozi shujaa 'hero' kama mzalendo namba mbili baada ya Mwalimu (R.I.P). Hivyo Salim ataaendelea 'kuzisoma namba za viongozi wazalendo wengine wengi wa taifa lile lile' la Tanzania.
 
Nikiri toka mwanzo mimi ni mshabiki mkubwa wa Sokoine. I have very fond memories. Sitapenda kufanya comparison na watu wengine au mawaziri wakuu wengine. Lakini nikiangalia anecdotes fulani, ninashuhudia kwamba Sokoine alikuwa mfano bora wa kiongozi. Si lazima watu wahusike na mambo yale yale ili tukubali nafasi zao katika historia.

Wakati wa Nyerere huo, usafiri Dar es Salaam ulikuwa umehodhiwa na serikali hasa kwa kutumia UDA, na pengine kidogo COCABS. Kama mleta uzi alivyosema, biashara kubwa za binafsi na hata ndogo sehemu nyingine zilipigwa vita. Jiji la Dar liliendelea kupanuka wakati mabasi ya UDA yakipungua. Sokoine, Waziri Mkuu wakati huo, alishuhudia hilo siku moja alipenda Ubungo pale Maji wakati huo ndiyo kituo, akaona saa 4 asubuhi pamesheheni watu wakisubiri UDA zinazokuja zimeshajaa toka Magomeni. Pale zinageuza tu.

Kwa mbali kule watu walikuwa wanakimbilia mabasi ya watu binafsi yaliyokuwa yakisomba watu kuwapeleka makazini kinyume cha sheria kwa nauli ghali sana wakati huo ya Dala (lile gwala la Sh. 5 lilivyoitwa wakati huo). Ndivyo zilivyoanza daladala. Nauli ya UDA wakati huo ilikuwa Sh 1.50. Alipouliza kilichokuwa kinaendelea, akapata stori kamili. Haraka sana kwa maagizo ya Sokoine ukaundwa utaratibu wa kuhalalisha daladala, ambazo wakati huo walipaswa kuilipa UDA. Nafikiri alifanya kitu kikubwa ambacho siamini kama kilikuwa katika ratiba za Mwalimu.

Nilikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wakati huo. Maji yalikuwa yanakatika ovyo kwa wiki kadha pale. Na tulikuwa na viongozi wa serikali ya wanafunzi ambao wengine sasa hivi wana nyadhifa za juu sana hapa TZ. Viongozi hao hawakushinikiza utawala wa chuo kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo. Utawala wa chuo, nadiriki kusema, haukuwa na interest yoyote ya kulitatua pia. Maghorofani kule, hebu fikiria hakuna maji kwa mwezi.

Sokoine alianza masomo ya uzamili pale chuoni. Siku moja akaomba aoneshwe maliwato. Ilikuwa kasheshe. Hatimaye akaoneshwa hali halisi. Akawaita wahusika wa chuo, wizara ya elimu na wizara ya maji. Mara moja tukaona matanki ya maji yamemwagwa pale mlimani. Haraka sana kazi ikaanza ya kujenga tanki lile lililo nyuma ya Hall 4. Mabomba yakajengwa kuunganisha na Ruvu Chini.

Ukweli ni kwamba alikuwa mtu ambaye alikuwa tayari kufanya kazi kutatua matatizo ya wananchi. Wengine tuliguswa moja kwa moja na utendaji wake. Doa katika utendaji wake hasa linatokana na kampeni ya wahujumu uchumi ambayo kwa maoni yangu ni kwamba iliendeshwa vibaya na watu nchini kote na pia hakupata kuungwa mkono ipasavyo katika serikali ya Mwalimu. He was like a lone ranger. There were other people whose performance in that office was mediocre, but most certainly Sokoine was not one of them.
 
Tu put the record straight, aliyeruhusu daladala kufanya kazi ni Sokoine sio Salim Ahmed Salim. Sio daladala tu, hata pickups.

Credit lazima iende kwa anayestahili. Daladala na pickups zilikuwa ni major reforms kwa Tanzania ya wakati ule. Watu walikuwa wanaibaiba lakini Sokoine akazifanya ziwe halali.
 
Sokoine shall remain a hero. No amount of misinformation can change that.
Niishie tu hapo.
 
@The Boss

Mkuu wewe humfahamu marehemu Sokoine na umeongea maneno mengi ya uongo. My hunch unampigia chapio SAS ambaye amefeli kwenye maeneo mengi. SAS alikuwa hawezi kumwambia Mwalimu kitu chochote. Wacha kupotosha members wa hii Forum.

FYI Sokoine ndiye aliyefanya mpaka wa Tanzania na Kenya ufunguliwe. Je, unafahamu kwa nini ulifungwa? Leave Sokoine to rest in peace and do not write something which you do not know.
 


Mkuu wewe humfahamu marehemu Sokoine na umeongea maneno mengi ya uongo. My hunch unampigia chapio SAS ambaye amefeli kwenye maeneo mengi. SAS alikuwa hawezi kumwambia Mwalimu kitu chochote. Wacha kupotosha members wa hii Forum.

FYI Sokoine ndiye aliyefanya mpaka wa Tanzania na Kenya ufunguliwe. Je, unafahamu kwa nini ulifungwa? Leave Sokoine to rest in peace and do not write something which you do not know.

Kuna kitu kimejificha kwenye kumpaka matope Sokoine na kumpa credit SAS. Kwa leo tuishie hapo.
 
The Boss

Leave SOKOINE alone,Let him rest peacefull he was a Hero, he was the one who stood up against Mwalimu(RIP) in diferent issues and views
 
Last edited by a moderator:
Umeandika kishabiki sana na mjadala wako haujabalance hata kidogo ukizingatia hawa watu unaowasifia na kuwaponda hawakutawala kipindi kimoja ambapo mwingie alikuwa kwenye post war crisis na mwingine akaja baadaye kitu ambacho hali za uchumi katika nyakati hizi mbili zilikuwa tofauti.

Unashadadia importation of goods and services huku unaua local production.

Unaongelea Dar as if ndiyo Tanzanai nzima walikuwa na shida za usafiri Dar ambazo hadi leo hazijawahi kuisha.l

Husemi habari ya ubaya wa kitu alichokuwa anapambana nacho sokoine cha kuzuia watu wachache kukusanay bidhaa ili wa create scarcity na kuwafanya Watanzania waliotoka vitani wazidi kudhoofika, na kama salimu alimaliza tatizo la ulanguzi wa bidhaa bila kuathri uzalishaji wa ndani na mgawanyo wa raslimali.

Wwe ni shabiki tu wala huna facts sahihi na huwezi kujalidi fairly.
 
..tatizo kampeni ya uhujumu uchumi ilifanyika kwa uonevu.

..pia ilikuwa inakiuka misingi ya sheria na utawala bora.

..watuhumiwa walikamatwa, wakatiwa kizuizini, baada ya hapo bunge likapitisha sheria ya kuwashtaki.

..kuna watuhumiwa waliotiwa kizuizini na baadaye kushtakiwa lakini mahakama ziliwaachia huru. wananchi hao baadaye walikuja kuidai serikali na kufidiwa. lakini maisha yao yalishaharibiwa kabisa.

..kwasababu hizo ndiyo maana Raisi Mwinyi alipoingia madarakani aliachana na kamata-kamata pamoja na mahakama za wahujumu uchumi.

..pia kile kipindi cha redio cha MIKINGAMO nacho kikafutwa, kwasababu kilikuwa kimejaa majungu kwa kiwango kikubwa.

NB: Kulikuwa na uhaba wa bidhaa nchini. uhaba huo ulitokana na viwanda vyetu kutokuzalisha bidhaa za kutosha. kilichopaswa kufanyika ni kuchukua hatua za dharura kuruhusu wafanyabiashara kuagiza bidhaa toka nje, siyo kukamata wafanyabiashara waliokuwa wakihodhi bidhaa.
 
Mkuu The Boss ,unaweza kuwa sahihi kwa hoja lakiniukakosea ulinganifu

Sokoine alikuwa administrator
Salim alikuwa Diplomat
Kuwaweka katika kapu moja, ni sawa na kulinganisha nanasi naembe

 
Last edited by a moderator:
Tu put the record straight, aliyeruhusu daladala kufanya kazi ni Sokoine sio Salim Ahmed Salim. Sio daladala tu, hata pickups.

Credit lazima iende kwa anayestahili. Daladala na pickups zilikuwa ni major reforms kwa Tanzania ya wakati ule. Watu walikuwa wanaibaiba lakini Sokoine akazifanya ziwe halali.

Ahsante kwa hili somo mkuu...
 
Nikiri toka mwanzo mimi ni mshabiki mkubwa wa Sokoine. I have very fond memories. Sitapenda kufanya comparison na watu wengine au mawaziri wakuu wengine. Lakini nikiangalia anecdotes fulani, ninashuhudia kwamba Sokoine alikuwa mfano bora wa kiongozi. Si lazima watu wahusike na mambo yale yale ili tukubali nafasi zao katika historia.
Wakati wa Nyerere huo, usafiri Dar es Salaam ulikuwa umehodhiwa na serikali hasa kwa kutumia UDA, na pengine kidogo COCABS. Kama mleta uzi alivyosema, biashara kubwa za binafsi na hata ndogo sehemu nyingine zilipigwa vita. Jiji la Dar liliendelea kupanuka wakati mabasi ya UDA yakipungua. Sokoine, Waziri Mkuu wakati huo, alishuhudia hilo siku moja alipenda Ubungo pale Maji wakati huo ndiyo kituo, akaona saa 4 asubuhi pamesheheni watu wakisubiri UDA zinazokuja zimeshajaa toka Magomeni. Pale zinageuza tu. Kwa mbali kule watu walikuwa wanakimbilia mabasi ya watu binafsi yaliyokuwa yakisomba watu kuwapeleka makazini kinyume cha sheria kwa nauli ghali sana wakati huo ya Dala (lile gwala la Sh. 5 lilivyoitwa wakati huo). Ndivyo zilivyoanza daladala. Nauli ya UDA wakati huo ilikuwa Sh 1.50. Alipouliza kilichokuwa kinaendelea, akapata stori kamili. Haraka sana kwa maagizo ya Sokoine ukaundwa utaratibu wa kuhalalisha daladala, ambazo wakati huo walipaswa kuilipa UDA. Nafikiri alifanya kitu kikubwa ambacho siamini kama kilikuwa katika ratiba za Mwalimu.
Nilikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wakati huo. Maji yalikuwa yanakatika ovyo kwa wiki kadha pale. Na tulikuwa na viongozi wa serikali ya wanafunzi ambao wengine sasa hivi wana nyadhifa za juu sana hapa TZ. Viongozi hao hawakushinikiza utawala wa chuo kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo. Utawala wa chuo, nadiriki kusema, haukuwa na interest yoyote ya kulitatua pia. Maghorofani kule, hebu fikiria hakuna maji kwa mwezi. Sokoine alianza masomo ya uzamili pale chuoni. Siku moja akaomba aoneshwe maliwato. Ilikuwa kasheshe. Hatimaye akaoneshwa hali halisi. Akawaita wahusika wa chuo, wizara ya elimu na wizara ya maji. Mara moja tukaona matanki ya maji yamemwagwa pale mlimani. Haraka sana kazi ikaanza ya kujenga tanki lile lililo nyuma ya Hall 4. Mabomba yakajengwa kuunganisha na Ruvu Chini.
Ukweli ni kwamba alikuwa mtu ambaye alikuwa tayari kufanya kazi kutatua matatizo ya wananchi. Wengine tuliguswa moja kwa moja na utendaji wake. Doa katika utendaji wake hasa linatokana na kampeni ya wahujumu uchumi ambayo kwa maoni yangu ni kwamba iliendeshwa vibaya na watu nchini kote na pia hakupata kuungwa mkono ipasavyo katika serikali ya Mwalimu. He was like a lone ranger. There were other people whose performance in that office was mediocre, but most certainly Sokoine was not one of them.

Mkuu, nakiri kujifunza mengi kwenye hii post yako.

Shukran.
 
The Boss hapa ni sawa na kumlinganisha Zenedin Zidane na Ronaldinho Gaucho. Kila MTU mtamu kwa flava yake. Mwingine chunvi mwingine sukari.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom