Sokoine was not a hero, Salim was...

Mmenikumbusha ile sheria ;maarufu ya human resource deployment act,,,au NGUVU KAZI,ilikua maarufuku kuonekana kuonekana mitaani mda wa kazi,,watu walilima kwenye mashamba ya kijiji kwa lazima,,,
licha ya vita vya uhujumu kupamba moto:biashara ya vitu vya magendo toka kenya nayo ilikua imeshika hatamu,
mi nakumbuka SAS ndo alifungua mpaka wa kenya:kwani kipindi anaanza kazi ndo vitu vya kenya vikaanza kupatikana na kuuzwa bila kificho
 
Wengi hawakuwepo wakati huo wanafata wanayoyasoma au kuyasikia ambayo mengi yamebadilishwa uhalisia wake.

A question to you, why now?

Anazunguka sana!! Hamu yake wala siyo kumzungumzia WM bora hapo...
 
Well said mkuu, Ukiangalia kuangamia kwa uchumi wa Tanzania, Salim ana mchango mkubwa sana katika kuuangusha. Sera zake ndio chanzo kikuu cha kuua viwanda vyetu ambavyo ndo vilikuwa vinachipuka kila kona ya nchi. Focus ya Sokoine ilikuwa ya mbali, kujenga uchumi imara kwa siku za usoni, uchumi wa kujitegemea kama nchi. Focus ya Salim ilikuwa ya kutatua kero za wananchi zilizokuwepo kwa wakati huo lakini ziliua uchumi wetu. Kwa mifano hiyo mitumba anayosema The Boss iliua viwanda vyetu completly.

Wakati Salim anateuliwa U pm Hapakuwa na Mitumba lakini nchi nzima watu walikuwa wanavaa Viraka na Malapulapu japo pesa za kununulia nguo wanazo sasa hivyo Viwanda vya nguo vilikuwa vinazalisha nguo kwa ajili ya watu gani?
 
Last edited by a moderator:
Salim hakua Rais kutokana na siasa za Zanzibar za Upemba na Uunguja,hicho ndicho kilimwathiri sio utendaji wake
 
The Boss

Salim alikataa kuwa Rais akaona bora kuwa katibu mkuu wa umoja wa afrika, hilo tu lilimchafua.

Wapi! Katika uchaguzi huo wa OAU, Salimu alikwisha kwama na dakika za mwisho ilibidi Nyerere kuingia safarini kwenda kumuokoa. Kwa hiyo hata huko OAU nyota yake haikuwa nzuri kama unavyojaribu kueleza.
 
Kwenye Mkutano wa Chama Tawala Salim alipendekezwa agombee Urais wa Jamhuri,Wahafidhina kutoka Unguja walimkataa kwa ajili ya Upemba wake
 
Ni kweli mkuu wangu Sokoine alikuwa waziri mkuu mfuatiliaji wa karibu kila sekta.Watu wakizazi cha sasa si rahisi kujua nchi ilikotoka hasa baada ya vita ya Uganda hali ya uchumi ilikuwa mbaya sana.

Tu put the record straight, aliyeruhusu daladala kufanya kazi ni Sokoine sio Salim Ahmed Salim. Sio daladala tu, hata pickups.

Credit lazima iende kwa anayestahili. Daladala na pickups zilikuwa ni major reforms kwa Tanzania ya wakati ule. Watu walikuwa wanaibaiba lakini Sokoine akazifanya ziwe halali.
 
The boss
kama arguments zako ni hizi basi uko sawa.
Lakini kama mimi mpaka sahivi sijampata wa kumlinganisha na Sokoine......!

Sokoine Mtu Wa Watu
 
I stand to be corrected. Reading between the lines,thread inaponda utendaji wa JPM. Ana viashilia vya utendaji wa Sokoine.
Maana yake, bora angekuwa Lowassa.

Kuna angle nyingine kwenye kumlinganisha Sokoine na SAS. A topic for another day.

Chuo Kikuu cha kilimo kuitwa Sokoine University of Agriculture sio bure. Kumuenzi kule haikuwa bahati mbaya.

Ha ha haaaa... Asante kwa ufafanuzi hebu ngoja niendelee kusoma watu humu
 
Mmenikumbusha ile sheria ;maarufu ya human resource deployment act,,,au NGUVU KAZI,ilikua maarufuku kuonekana kuonekana mitaani mda wa kazi,,watu walilima kwenye mashamba ya kijiji kwa lazima,,,
licha ya vita vya uhujumu kupamba moto:biashara ya vitu vya magendo toka kenya nayo ilikua imeshika hatamu,
mi nakumbuka SAS ndo alifungua mpaka wa kenya:kwani kipindi anaanza kazi ndo vitu vya kenya vikaanza kupatikana na kuuzwa bila kificho

Mkuu hivi unajua wakati wa uhaba wa Bidhaa ndio kipindi watu walibuni kufua nguo kwa Majani ya mPAPAI unadhani tungeendelea na zile dhiki mpaka leo tungekuwa wapi au hujui shida inamfanya MTU aongeze kiwango chakufikiri.... manake kutokana na shida ubunifu ungekuwa mkubwa Unajivunia kuagiza bidhaa za Kenya huoni kwamba akili zimegandia hapo Inafikia hatua Rais wa NCH anaamini ktk kuomba...ili kuongoza Taifs..lake...ni UJINGA...Hapa ndipo tulipokwamia......
 
hukumundo

Ni kweli aliyeruhusu daladala na pickups kumilikiwa na watu binafsi alikuwa Sokoine.

Ni kweli Salim Ahmed Salim aliruhusu mitumba kuingizwa nchini baada ya lile sakata la Mtwara. Kwa wakti ule kwa kweli ilikuwa ni aibu sana kwa Watanzania.

Aliyetatua tatizo la maji Chuo Kikuu cha DSM (Mlimani) alikuwa ni Rais Mwinyi. Lile tangi la maji pale Hall 4 lilijengwa wakitegemea kupata maji kutoka Ruvu chini pale Survey. Chuo Kikuu kiliomba litobolewe lakini Idara ya Maji ikakataa kuwa pressure itapungua. Rais Nyerere aliafiki hilo baada ya kuingilia kati. Kwa hiyo lile tangi la Chuo Kikuu likabakia halina maji. Chuo Kikuu mlimani wakashauriwa wachimbe vyoo vya mashimo. Na kweli walichimba, mpaka leo vingine ndhani bado vinaonekana.

Baada ya kuingia Rais Mwinyi alielezwa hilo tatizo na akaafiki lile bomba pale Survey litobolewe. Bahati nzuri wakati huohuo DANIDA walijitolea kukarabatai Chuo kikuu kwa kurudhisha vioo vyote vilivyopasuka, kurudisha vyoo vilivyoibiwa kama pale Nkrumah Hall, kutrace upya na kuchora ramani ya mabomba ya Chuo Kikuu (Ramani ilikuwa imepotea), kutoboa bomba kuu pale Survey na kuweka pump ya kupeleka maji kwenye Tank pale Hall 4.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hivi unajua wakati wa uhaba wa Bidhaa ndio kipindi watu walibuni kufua nguo kwa Majani ya mPAPAI unadhani tungeendelea na zile dhiki mpaka leo tungekuwa wapi au hujui shida inamfanya MTU aongeze kiwango chakufikiri.... manake kutokana na shida ubunifu ungekuwa mkubwa Unajivunia kuagiza bidhaa za Kenya huoni kwamba akili zimegandia hapo Inafikia hatua Rais wa NCH anaamini ktk kuomba...ili kuongoza Taifs..lake...ni UJINGA...Hapa ndipo tulipokwamia......

Watu walishaanza kutembea uchi. Leo labda tungekuwa tuanaishi mapangoni.
 
The Boss, nenda tu moja kwa moja kwenye hoja yako," Magufuli ni Sokoine, hatatoa suluhu ya matatizo ya Tz".Sikutegemea tu hizi propaganda kwa mtu kama wewe, it's too low kwako.. Wa Tz ni watu wa ajabu sana.
 
Sibonike na mtanzania1989 sielewi ni kwa nini mnadhani lengo la The Boss ni kumsema Magufuli. Mimi simtetei the boss lakini kwa nini watu mnakuwa kama vile kila wakati mnawaza Magufuli anaonewa na anatakiwa kupewa ulinzi wa ziada?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,boss mimi nakupinga kwa 100% kila mtu alifanya kulingana na anavyo amini sokoine na nyerere waliamini ktk sera ya ujamaa,hvyo kutokana na ile vita kuathiri uchumi wa nchi waliona kukubali sera za ubepari ni sawa na kujiwekea kitanzi waliamini wananchi ni lazima wavumilie hali iliyokuwepo huku serikali ikiwa inatafuta suruhisho mojo wapo ni kubana matumizi ya serikali.

Kumbuka sera za IMF na WB tulizo zikubali ndo zinatutesa mpaka sasa. Emu nikuulize,unahisi deni tulilo nalo sasa la zaidi ya Trillion 36 litakuja kuisha lini?

Sera za ubepari zinaua uchumi wa nchi nyingi duniani sasa leo utasemaje zilikuwa nzuri.nyerere aliliona hilo na ni kweli ndivyo inatokea.hatutakuja kupata uchumi unaojitegemea hata kidogo..
 
The Boss na urushaji wa jiwe gizani...!
=====================================
Nikirudi kwenye mada kibunuasi na kikarumekenge....:Nasema hivi

Salim yawezekana 'alifanya ukorofi' labda ndiyo maana akaondoshwa kiana kwenda OAU. Mwalimu (R.I.P) yawezekana aliamini kuwa necessity is the mother of creativity na subira inavuta heri. Salim yawezekana hakulisoma hilo kwa Mwalimu(R.I.P). Salim yawezekana hakuamini katika kujitegemea, Salim labda hakuamini katika ujamaa,undugu,umoja na mshikamano...eeh tumuulize!Pia nadhani ushawishi wa Salim yawezekana ndiyo uliolitumbukiza taifa hili katika 'Ombaomba' ya kupigiwa mfano...!
Vilevile nadhani Salim akiulizwa sasa kama unazungumziaje huo ushawishi kwa Mwalimu(R.I.P) yawezekana 'akabubujikwa machozi na kuanza kuomba msamaa watanzania bila kikomo kwa muda wa siku sita(6)' juu ya ushawishi alioufanya...!
===========================================
Kwa hiyo: Kwangu mimi Edward Sokoine (R.I.P) ni kiongozi shujaa 'hero' kama mzalendo namba mbili baada ya Mwalimu (R.I.P). Hivyo Salim ataaendelea 'kuzisoma namba za viongozi wazalendo wengine wengi wa taifa lile lile' la Tanzania.

na hiki ndicho nimwambia mtoa mada,kama kuna watu wangetakiwa hata kunyongwa na huyu salimu alitumika vibaya na westn countries,haya matatizo tulio nayo sasa yametokana na hiki alicho kishauri,nyerere aliona mbali sana.hatuta kuja kupata uchumi unao jitegemea mpaka dunia inazizima
 
Ni kweli kuna upotoshaji. Sokoine ndiye aliyeruhusu daladala, Salim aliruhusu mitumba, Nyerere alitaka Salim amrithi ila wakina kingunge wakaleta fitina wakiogopa mabadiliko ingawa leo wanajifanya vinara wa mabadiliko ndio maana Nyerere akampeleka afanye kazi kimataifa ili kumweka mbali na wakina kingunge na hata aliporudi ni hao hao waliompinga tena kwa kumzushia uongo.

Kwa kifupi kila mmoja aliitendea haki nafasi yake.
 
Mmmh !! na madeni waliyolimbikizwa... hadi leo waTanzania tunadaiwa !! deni lisilokwisha kutokana na nini?)
 
Kaka inawezekana kweli hakuwepo sina uhakika sana, lakini mtoa mada anaonekana ameandika histohisia zake kwa kufuata maneno ya vijiweni kwa misingi na itikadi zake,
inawezekana vipi uandike habari yenye uongo mwanzo mpaka Mwisho? Hivi kweli mtu aliyukuwa zama hizo hajui tofauti ya UDA na KAMATA?, hapo la ukweli ni hilo la nguo za mitumba tu,


Huyu mtu ana agenda yake ambayo wala si ya kisiasa na haina maslahi kwa taifa. Ukiangalia wanaomuunga mkono wana common elements ambazo ndizo zna wamfanya abebe zigo la kufuta uzuri wa Sokoine kama wale wamekuwa wakijitahidi kuponda mazuri ya Julius Kambarage.

Na usishangae muda mfupi ujao wakafuta kabisa mazuri ya baadhi ya watawala kwa agenda zao hizo hizo wakaja na slogan Ccm ya Jakaya ndiyo ilikuwa mfano wa kuigwa.

Inahitaji kumwelewa mwandishi kabla hujatumia nguvu nyingi kuelewa anachotaka kuiaminisha dunia na hasa vizazi ambavyo havijui historia.
 
Back
Top Bottom