Hii ni miaka 40 ya kumbukizi ya kifo cha Sokoine au ni kumbukizi ya miaka 40 ya usaliti na kujipendekeza?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
901
4,195
Ni jambo gani lililofanyika Monduli linaloashiria kulikuwepo na viongozi wa Kitaifa wanaomuenzi Mhe. Sokoine?

Nani amesimama kuzungumzia Sokoine kama ambavyo tunashuhudia ikifanyika kwa mwalimu Nyerere?

Kwanini kuanzia viongozi wa dini hadi wanasiasa wanamtisha Mhe. Rais kwa kuonyesha anao maadui? Mama Samia kwa nafsi na uvumilivu anapataje maadui? Amewafanyia nini hadi wawe maadui zake?

Kwanini viongozi wa dini wanataka kutafsiri kama hali siyo shwari wakati hakuna tishio lolote? Wao kukosekana kwa usalama hadi wasema tunakuombea usiku na mchana wanapataje habari?

Tulitegemea leo iwe kumbukizi ya Sokoine lakini tumeishia kuwa na kumbukizi ya wanafiki na wasaliti wanaopenda kukaa viti vya mbele wakihubiri na kutangaza mpasuko wa kisiasa na kiusalama waweze kuishi.

Sokoine alikuwa mchapa kazi na mwenye maono na msimamo, alijikita kusema kweli wakati wote. Leo kwanini tuombe taarabu kama ishara yakumuenzi.

Nilichokiona kinachoendana na Sokoine ni kuchoma nyama tu ambayo ni tamaduni ya Wamasai kama ishara ya upendo na shibe isiyobaghua .

Wazee na viongozi wa Kimasai, kimeru na kichaga wamenyimwa fursa wakapewa waheshimiwa wa kanda ya ziwa na pwani.....siyo poa tujisahihishe
 
Mimi naona ni majukwaa yanatengenezwa ili kuwasilisha propaganda zao, kuna aina fulani ya kushindwa ambao haijawekwa wazi na vile tulivyo wanafiki tunakaa kimya ili kulindana na kuenzi utamaduni.
wakati ilipaswa andaliwe anayepokea kijiti kutoka kwa huyu aliyepo ambae ni dhahiri kwa propaganda hizi ameshindwa ila wao wanazidi kumunadaa mshindwa akashinde.
 
Inasikitisha sana miaka 40 imepita bila ya sisi tuliokuwepo kuelezwa ni kwa nini Mwalimu alituomba sana Watanzania tukubali kuwa mpendwa wetu amekufa kwa ajali ya gari..
 
Back
Top Bottom