Sokoine was not a hero, Salim was...

Kama hujui histori nyamaza, ulegezaji wa kuingiza bidhaa toka nje ulianzishwa na Sokoine 1984 baada ya bunge la januari, wengine tulikuwa sekondari na tunajua, Baada ya bidhaa kuadimika 1980- 1983 ni Sokoine aliyemface JK kulegeza msimamamo ili wananchi wapate bidhaa. Salim aliendeleza tu alichoanzisha Sokoine, Sokoine hakuvumilia hata kidogo kuona wananchi wanapata shida. Ni aibu leo ukisema was not a hero.
Nadhani kuna kitu kinakusumbua kichwani..
 
Kama anavyosema Sibonike, kuna kitu kimejificha kwenye kumchukulia Sokoine sio shujaa wa Taifa. Nakumbuka, mwaka 1995(kama sikosei) katika kongamano la kumbukumbu ya marehemu Sokoine iliyofanyika pale IFM. Alisimama Mbowe akasema maneno haya haya kua hakuna ushujaa ndani ya Sokoine. Na ndio hapo niligundua kua, kuna kijitabaka fulani kilichojeruhiwa na harakati za marehemu Sokoine ambacho pengine kilihusika kwenye kuutoa uhai wake kina ugomvi usioisha.
 
Anaandika mapokeo wakati wa sokoine alikuwa hajazaliwa
Kaka inawezekana kweli hakuwepo sina uhakika sana, lakini mtoa mada anaonekana ameandika histohisia zake kwa kufuata maneno ya vijiweni kwa misingi na itikadi zake,
inawezekana vipi uandike habari yenye uongo mwanzo mpaka Mwisho? Hivi kweli mtu aliyukuwa zama hizo hajui tofauti ya UDA na KAMATA?, hapo la ukweli ni hilo la nguo za mitumba tu,
 
Kama anavyosema Sibonike, kuna kitu kimejificha kwenye kumchukulia Sokoine sio shujaa wa Taifa. Nakumbuka, mwaka 1995(kama sikosei) katika kongamano la kumbukumbu ya marehemu Sokoine iliyofanyika pale IFM. Alisimama Mbowe akasema maneno haya haya kua hakuna ushujaa ndani ya Sokoine. Na ndio hapo niligundua kua, kuna kijitabaka fulani kilichojeruhiwa na harakati za marehemu Sokoine ambacho pengine kilihusika kwenye kuutoa uhai wake kina ugomvi usioisha.

mkuu umeongea kwa ufupi sana, embu maliziaa
 
Salim is a strategist, a very good one at that. Salim can visualize the big picture and say sir here is our problem and this is the solution. Sokoine was tactician at the best of time.
 
Nikiri toka mwanzo mimi ni mshabiki mkubwa wa Sokoine. I have very fond memories. Sitapenda kufanya comparison na watu wengine au mawaziri wakuu wengine. Lakini nikiangalia anecdotes fulani, ninashuhudia kwamba Sokoine alikuwa mfano bora wa kiongozi. Si lazima watu wahusike na mambo yale yale ili tukubali nafasi zao katika historia.
Wakati wa Nyerere huo, usafiri Dar es Salaam ulikuwa umehodhiwa na serikali hasa kwa kutumia UDA, na pengine kidogo COCABS. Kama mleta uzi alivyosema, biashara kubwa za binafsi na hata ndogo sehemu nyingine zilipigwa vita. Jiji la Dar liliendelea kupanuka wakati mabasi ya UDA yakipungua. Sokoine, Waziri Mkuu wakati huo, alishuhudia hilo siku moja alipenda Ubungo pale Maji wakati huo ndiyo kituo, akaona saa 4 asubuhi pamesheheni watu wakisubiri UDA zinazokuja zimeshajaa toka Magomeni. Pale zinageuza tu. Kwa mbali kule watu walikuwa wanakimbilia mabasi ya watu binafsi yaliyokuwa yakisomba watu kuwapeleka makazini kinyume cha sheria kwa nauli ghali sana wakati huo ya Dala (lile gwala la Sh. 5 lilivyoitwa wakati huo). Ndivyo zilivyoanza daladala. Nauli ya UDA wakati huo ilikuwa Sh 1.50. Alipouliza kilichokuwa kinaendelea, akapata stori kamili. Haraka sana kwa maagizo ya Sokoine ukaundwa utaratibu wa kuhalalisha daladala, ambazo wakati huo walipaswa kuilipa UDA. Nafikiri alifanya kitu kikubwa ambacho siamini kama kilikuwa katika ratiba za Mwalimu.
Nilikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wakati huo. Maji yalikuwa yanakatika ovyo kwa wiki kadha pale. Na tulikuwa na viongozi wa serikali ya wanafunzi ambao wengine sasa hivi wana nyadhifa za juu sana hapa TZ. Viongozi hao hawakushinikiza utawala wa chuo kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo. Utawala wa chuo, nadiriki kusema, haukuwa na interest yoyote ya kulitatua pia. Maghorofani kule, hebu fikiria hakuna maji kwa mwezi. Sokoine alianza masomo ya uzamili pale chuoni. Siku moja akaomba aoneshwe maliwato. Ilikuwa kasheshe. Hatimaye akaoneshwa hali halisi. Akawaita wahusika wa chuo, wizara ya elimu na wizara ya maji. Mara moja tukaona matanki ya maji yamemwagwa pale mlimani. Haraka sana kazi ikaanza ya kujenga tanki lile lililo nyuma ya Hall 4. Mabomba yakajengwa kuunganisha na Ruvu Chini.
Ukweli ni kwamba alikuwa mtu ambaye alikuwa tayari kufanya kazi kutatua matatizo ya wananchi. Wengine tuliguswa moja kwa moja na utendaji wake. Doa katika utendaji wake hasa linatokana na kampeni ya wahujumu uchumi ambayo kwa maoni yangu ni kwamba iliendeshwa vibaya na watu nchini kote na pia hakupata kuungwa mkono ipasavyo katika serikali ya Mwalimu. He was like a lone ranger. There were other people whose performance in that office was mediocre, but most certainly Sokoine was not one of them.

Ndio maana ni bora historia ikaandikwa nakubaliana nawe sula la kuanzisha Daladala si la Salim Ahmed Salim bali ni Marehemu Sokoine kwani licha private sector ilikuwa inabanwa alimface Mwalimu na kumpa hiyo Idea mabayo wabnafik wengine wasingeweza na ndio inatoa huduma mpaka leo. Asante kwa kuweka historia sahihi. Na nisahihishe lingine Marehemu Sokoine wala hakujipa ujiko yeye ni wananchi walipotambua Corntribution yake. Watanzania ni watu makini sana ukifanya vizuri watajua na utapata tu credit ukiboronga as well watajua na mrejesho utaupata kwa namna fulani. Kwa wale wanmaopigiwa kura wanalielewa hili!!!
 
Nikiri toka mwanzo mimi ni mshabiki mkubwa wa Sokoine. I have very fond memories. Sitapenda kufanya comparison na watu wengine au mawaziri wakuu wengine. Lakini nikiangalia anecdotes fulani, ninashuhudia kwamba Sokoine alikuwa mfano bora wa kiongozi. Si lazima watu wahusike na mambo yale yale ili tukubali nafasi zao katika historia............................

Una data kamili mkuu, ni rahisi kwa watu waliokuwepo wakati ule kueleza kuliko waliosimuliwa. Na nakumbuka kwa hatua za muda mfupi magari yalianza kuleta maji mabwenini nyakati za jioni na wanafunzi tulijichotea maji na kuyahifadhi kitu ambacho kingeweza kufikiriwa na uongozi wa chuo/ Wizara ya elimu. Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu Sokoine, Amina.
 
kama hujui histori nyamaza, ulegezaji wa kuingiza bidhaa toka nje ulianzishwa na Sokoine 1984 baada ya bunge la januari, wengine tulikuwa sekondari na tunajua, Baada ya bidhaa kuadimika 1980- 1983 ni Sokoine aliyemface JK kulegeza msimamamo ili wananchi wapate bidhaa. Salim aliendeleza tu alichoanzisha Sokoine, Sokoine hakuvumilia hata kidogo kuona wananchi wanapata shida. Ni aibu leo ukisema was not a hero.
Nadhani kuna kitu kinakusumbua kichwani

Wacha kupotosha, mageuzi ya kiuchumi yalitokana na report ya tume ya Paul Bomani, report ile iliainisha mambo mengi ya kufanyia kazi, hii ilitokana na kufeli kwa sera za sokoine.
 
The Boss na urushaji wa jiwe gizani...!
=====================================
Nikirudi kwenye mada kibunuasi na kikarumekenge....:Nasema hivi

Salim yawezekana 'alifanya ukorofi' labda ndiyo maana akaondoshwa kiana kwenda OAU. Mwalimu (R.I.P) yawezekana aliamini kuwa necessity is the mother of creativity na subira inavuta heri. Salim yawezekana hakulisoma hilo kwa Mwalimu(R.I.P). Salim yawezekana hakuamini katika kujitegemea, Salim labda hakuamini katika ujamaa,undugu,umoja na mshikamano...eeh tumuulize!Pia nadhani ushawishi wa Salim yawezekana ndiyo uliolitumbukiza taifa hili katika 'Ombaomba' ya kupigiwa mfano...!
Vilevile nadhani Salim akiulizwa sasa kama unazungumziaje huo ushawishi kwa Mwalimu(R.I.P) yawezekana 'akabubujikwa machozi na kuanza kuomba msamaa watanzania bila kikomo kwa muda wa siku sita(6)' juu ya ushawishi alioufanya...!
===========================================
Kwa hiyo: Kwangu mimi Edward Sokoine (R.I.P) ni kiongozi shujaa 'hero' kama mzalendo namba mbili baada ya Mwalimu (R.I.P). Hivyo Salim ataaendelea 'kuzisoma namba za viongozi wazalendo wengine wengi wa taifa lile lile' la Tanzania.

Well said mkuu, Ukiangalia kuangamia kwa uchumi wa Tanzania, Salim ana mchango mkubwa sana katika kuuangusha. Sera zake ndio chanzo kikuu cha kuua viwanda vyetu ambavyo ndo vilikuwa vinachipuka kila kona ya nchi. Focus ya Sokoine ilikuwa ya mbali, kujenga uchumi imara kwa siku za usoni, uchumi wa kujitegemea kama nchi. Focus ya Salim ilikuwa ya kutatua kero za wananchi zilizokuwepo kwa wakati huo lakini ziliua uchumi wetu. Kwa mifano hiyo mitumba anayosema The Boss iliua viwanda vyetu completly.
 
Last edited by a moderator:
Sokoine is more than a hero, he is the National Icon. Just imagine nchi ndio imetoka vitani, rasilimali nyingi zimetumika, nguvuwatu nayo imepungua sana, yaani nchi ipo katika hali mbaya sana, Sokoine alijitokeza na kusaidiana na Mwalimu ku restore hali ya kiuchumi ya nchi. Salim aliikuta nchi imepiga hatua fulani ambayo kuendeleza haikuwa ngumu zaidi. Huwa nafikiria sana ni kwanini Salim Hakuwa Rais wa pili wa JMT, badala ya Mwinyi.... It means alikuwa short in something,.


The Spirit Of Sokoine Is Living.
 
Mkuu The Boss siku hizi chache umeonuenyesha uTURN nyingi hadi najiuliza imekuwaje ila siku sinyingi majibu yatapatikana humu
 
Last edited by a moderator:
Kwa Sikoine hata Mwl Nyerere anasubiri! Hakuwa na chembe ya unafiki hata kidogo.Lowassa anafanana na Sokoine vitu vitatu tu, Urefu, ubunge wa monduli na wote waliwahi kuwa Mawaziri wakuu.Kwny Uadilifu ni kama Mbingu na Ardhi au Magharibi na Mashariki
 
Hawa wote walikuwa watekelezaji wa sera mbovu za wakati ule. Mtu yoyote mwenye akili timamu asingejiingiza kutekeleza sera ambazo mpaka leo ndio zinatufanya kusuasua. Mwenzao alijiuzuru wao wakatekeleza sera ambazo baadae zilikufa kimya kimya. Watu wanasifia viwanda. Huu ni upotevu wa rasilimali. Km nyumbu kibaha na vifananavyo. Historia imetuonyesha hakuna nchi hata moja iliyofanikiwa kwa siasa ya ujamaa na kujitegemea.
 
Kwa Sikoine hata Mwl Nyerere anasubiri! Hakuwa na chembe ya unafiki hata kidogo.Lowassa anafanana na Sokoine vitu vitatu tu, Urefu, ubunge wa monduli na wote waliwahi kuwa Mawaziri wakuu.Kwny Uadilifu ni kama Mbingu na Ardhi au Magharibi na Mashariki

Mkuu kwa style hii huko nyumbani hujawahi kutaja jina la LOWASA kwa Sauti ya juu ukiwa usingizini kweli....!!! hapa anajadiliwa SAS na SOKOINE lowasa anaingiaje....!!!
 
The Boss kwan wote wawili hawawez kuwa heroes? Mi nadhan kinachompa edge Sokoine ni tragic and mysterious death.
 
Mkuu kwa style hii huko nyumbani hujawahi kutaja jina la LOWASA kwa Sauti ya juu ukiwa usingizini kweli....!!! hapa anajadiliwa SAS na SOKOINE lowasa anaingiaje....!!!

Ningejibalaguza kumfananisha Lowassa na Sokoine kwa uzalendo, ujasiri, uthubutu uchapakazi ungeandika uliyoandika?
 
Sikatai kuwa Salim A. Salim sio "hero", bali yafuatayo bado yananifanya niamini kuwa Edward Moringe Sokoine pia ni "hero";
  1. Ni kiongozi wa ngazi ya juu kabisa, ambaye amethubutu kusimama katika mstari wa mbele kwenye mapigano ya kivita (vita vya kagera), badala ya kutafuta pa kujificha kama ilivyo kawaida kwa viongozi wengine....!
  2. Ni kiongozi pekee alithubutu hadharani kuanza kupambana na uhalifu, kwa kuanzia kwa viongozi wenzake; mfano alipowatangazia viongozi wenzake wakiwemo mawaziri kuwa wahakikishe ni wasafi....! Hili alilifanya pale Dodoma siku aliyopatia ajali iliyosababisha kifo chake....! Ni nani leo mwenye kuthubutu hivyo?
 
Mkuu kwa style hii huko nyumbani hujawahi kutaja jina la LOWASA kwa Sauti ya juu ukiwa usingizini kweli....!!! hapa anajadiliwa SAS na SOKOINE lowasa anaingiaje....!!!

I stand to be corrected. Reading between the lines,thread inaponda utendaji wa JPM. Ana viashilia vya utendaji wa Sokoine.
Maana yake, bora angekuwa Lowassa.

Kuna angle nyingine kwenye kumlinganisha Sokoine na SAS. A topic for another day.

Chuo Kikuu cha kilimo kuitwa Sokoine University of Agriculture sio bure. Kumuenzi kule haikuwa bahati mbaya.
 
Kama ujasiri wa kiongozi ni kum-face mwalimu (R.I.P), je, wajua kwa nini Sokoine amekuwa waziri mkuu wa Nyerere kwa vipindi viwili tofauti? Wajua nini kilichomtoa katika kipindi cha kwanza?
 
Back
Top Bottom