Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
- Thread starter
- #101
Anyways kwa sababu inajulikana wewe ni Rais wa wabeba boksi, sio mbaya kutoifahamu kivile...ipo karibu na chuo cha ustawi wa jamii...kijiwe maaruf cha totoz wa ustawi pale...
sasa turudi kwen topic ya Mbu bana....
Mi kitu kimoja kimenishangaza kidogo, ni kwa nini Mbu ameamua kuweka katika upande hasi (negative) peke yake...bila kuangalia pia upande positive? Inaweza kuwa uamuzi sahihi kabisa wa kwake, lakini nadhani ingekuwa more balanced kama angeuliza pia mchango wa hizi social networks katika:
Mengineyo tunaweza kuongeza...kwa hiyo si kweli moja kwa moja kuwa "na hii haikuanzia kwa Facebook pekee, Friends Reunited, myspace, WAYN, Hi5, Twitter na hata Google + mitandao yote hii kwa namna moja au nyingine imegeuka hatarishi kwa usalama wa mahusiano, mapenzi urafiki na ndoa!"
- "kustabilise" relationships
- Kuestablish new relationships, watu kibao wameo na kuolewa. sembuse Bf/GF
- Kupunguza 'real time' cheating, lol (hapo inategemea definition ya cheating...a 'new' topic altogether)
Huo ni mtizamo wangu. tuendeleee
...la la la,....
...binafsi Facebook na hii mitandao ya kijamii imeniwezesha kunikutanisha tena na watu weeengi niliokuwa nimesoma nao, nimeishi nao na hata wale ex-gelo frendz niliojirusha nao miaka hiyooooo....
...kimbembe ni jinsi gani ya ku handle hizo rekindled flames bana japo tayari wengi wetu tushakuwa na minyama uzembe, lakini si unajua tena....mnaanza na "..hivi nimekumisije?" au "...hivi kwanini ulinichunia!?"...kisha mnaendelea "...bado nakumbukia maujuzi yako, bado upo vile vile....?! " ----kufumba na kufumbua mshabadilishana namba za simu na na ahadi za kupeana 'what you've been missing all those years!"
Balaaa!