Slaa, Mbowe wamkaanga JK

Naona Chadema wameishiwa na sera, hawana kipya ila majungu, fitina na hoja zisizo na maana hata chembe.

Kuwepo au kutokuwepo nchini Rais si hoja ya msingi, kwani huko alikokwenda alienda kucheza?

Wanatubowa na vijineno neno vya ufataani na siasa za kuwabagua wananchi, halafu wanaongelea udini? Wamesahau kuwa kanisa liliwakataa waumini kwa kuwa wameipigia kura CCM? wamesahau Slaa alipoifananisha CCM na Taliban? Sasa hapo nani ni mdini?
Na utaboeka sana safari hii. Movie ndo inaanza.
 
Waberoya,

Tunashukuru kwa ushauri. Najiuliza, je tukifanikiwa katika hilo utajiunga Chadema? Ni nini ambacho kinakuzuia kujiunga Chadema sasa hivi ili tujenge wote chama?

Kikubwa zaidi kwenye hoja yako ni kushift focus kutoka kwa Kikwete kwenda kwenye mfumo tunaoupinga. JK tayari ni Raisi na inawezekana akabaki mpaka 2015. Hatagombea tena. Kwa hiyo kama amefeli ndio amefeli na hatakuwepo tena. Atasimamishwa mwingine halafu tutaanza nae. Wananchi wataona 'afadhali labda huyu'. Atashinda. Lazima tuzuie hilo. Tujijenge sisi kama chama na wananchi watuamini na watuelewe. Tujenge personalities...watu huchagua watu mara nyingi. Lazima wakuamini.

Ninapata mashaka na habari hii ilivyoripotiwa. Kuna kila uwezekano imekosewa.

Dr Slaa hawezi kusema JK alikataa kutoa hela mara mbili mabomu yaharibiwe halafu amwambie Waziri na Mkuu wa Jeshi wajiuzulu kwa uzembe. Kama Raisi amewanyima fedha wamezembeaje sasa? Nadhani habari hiyo haijakamilika.

Tuendelee kutafakari
 
Daaah habari ya kushindwa kuteketeza mabomu kwa kukosa fedha imeshaanza kuwekwa wazi kwa wananchi basi JK yuko hatarini! Ni kweli bomu likitua nila square metre zake ambazo linaweza kuleta madhara, ukiangalia yale ya Gongo la Mboto yalikuwa yakitua either hayalipuki au madhara yake yalikuwa makubwa baada ya kugonga kuta na kuua watu.
Kama mabomu yale yangekuwa hayapitwa na muda wake basi leo hii Gongo la Mboto isingekuwepo!
 
Waberoya,

.......ninapata mashaka na habari hii ilivyoripotiwa. Kuna kila uwezekano imekosewa.

Dr Slaa hawezi kusema JK alikataa kutoa hela mara mbili mabomu yaharibiwe halafu amwambie Waziri na Mkuu wa Jeshi wajiuzulu kwa uzembe. Kama Raisi amewanyima fedha wamezembeaje sasa? Nadhani habari hiyo haijakamilika.

Tuendelee kutafakari

Ni kweli kama taarifa mkuu wa nchi anayo ila kwa uzembe wake au kwa sababu anazojua yeye ameshindwa kutoa fedha basi itakuwa ameshindwa kutimiza wajibu wake, hivyo yeye binafsi ndiyo anatakiwa ajiuzuru na siyo waziri Mwinyi wala Mwamnyange.

Naye Dk. Slaa, alisema kuwa amesikitishwa na milipuko ya mabomu iliyotokea Gongo la Mboto ambayo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na uzembe wa serikali ambayo iligoma kutoa fedha kwa ajili ya kuyaharibu mabomu hayo.

Alibainisha kuwa anazo taarifa kuwa Rais Kikwete alilinyima jeshi hilo fedha za kuharibu mabomu hayo ambayo yalionekana kwisha muda wake miaka miwili iyopita.

[SIZE=4[B]]"Ninayo taarifa kwamba serikali ya Rais Kikwete iliombwa fedha mara mbili za kuharibu mabomu lakini ilishindwa kufanya hivyo...hali hiyo ndiyo iliyosababisha vifo vya Watanzania Mbagala na sasa Gongo la Mboto[/B]," alisema Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa, kutokana na uzembe huo, anamtaka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, pamoja na Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Davis Mwamnyange, kujiuzulu mara moja nyadhifa zao na iwapo watashindwa, basi Rais Kikwete awafukuze.

Hapa Dr. Slaa anatukanganya.

.....Dr. Slaa anasema jeshi linaloongozwa na Mwamunyange liliiomba Serikali fedha ili liyaharibu mabovu yaliyokwisha muda wake ili kuzuia milipuko ambayo ingeleta madhara kwa jeshi na wananchi walio maeneno ya karibu.

.....Dr. Slaa anasema Serikali ya Kikwete ilikataa kulipa Jeshi fedha za kutekeleza kazi hiyo na hivyo kupelekea jeshi kushindwa kutekeleza mpango wao wa kuteketeza mabomu hayo na mwishowe kupelekea kulipuka kwa mabomu hayo.

.....Dr. Slaa anasema Mwamunyange na Mwinyi wawajibike kwa uzembe wao uliopelekea mabomu hayo kulipuka.

.....Dr. Slaa anasema wasipojiuzulu wenyewe basi Rais Kikwete aliyekataa kuwapa pesa ya kutekeleza mpango wa kuyaharibu mabomu hayo na hivyo kupelea yalipuke na kusababisha madhara yaliyojitokeza awafukuze kazi.

Hivi kama Dr. Slaa anajua anayoyasema atamuombaje tena Kikwete amtimue kazi Mwamunyange na Mwinyi kwa kosa ambalo Dr. Slaa mwenyewe amesema ni la Kikwete?
 
Ndivyo ninavyofikiri pia Mzee wa Rula. Ni vizuri pia 'vyanzo vya taarifa' vikatoa taarifa kamili. Aliombwa lini na alikataa lini. Hii itasaidia kumnyoosha yeyote ambaye amezembea hata kama ni Raisi.

Ikibaki kuwa taarifa ya kuaminika lakini hatuna cha kufanya zaidi ya kunung'unika haitatusaidia. Itabaki kuwa siasa.
 
Hapa Dr. Slaa anatukanganya.

.....Yeye mwenyewe anasema jeshi linaloongozwa na Mwamunyange liliiomba Serikali fedha ili liyaharibu mabovu yaliyokwisha muda wake ili kuzuia milipuko ambayo ingeleta madhara kwa jeshi na wananchi walio maeneno ya karibu.

.....Yeye mwenywe anasema Serikali ya Kikwete ilikataa kulipa Jeshi fedha za kutekeleza kazi hiyo na hivyo kupelekea jeshi kushindwa kutekeleza mpango wao wa kuteketeza mabomu hayo na mwishowe kupelekea kulipuka kwa mabomu hayo.

.....Sasa kama kesi ipo hivyo Dr. Slaa atamuombaje tena Kikwete amtimue kazi Mwamunyange na Mwinyi kwa kosa ambalo Dr. Slaa mwenyewe anasema ni la Kikwete?

Nadhani kuna kitu mnakosea kidogo ktk muktadha wa kujiuzulu.

Iwapo waziri na jeshi waliomba fedha za kuteketeza mabomu na wakanyimwa basi:

1. Mkuu wa majeshi (CDF) ataachia ngazi kwa sababu anafanya kazi na serikali isiyomwamini hivyo kuonekana ni mzembe machoni mwa wananchi. Ataachia ngazi kwa msingi kwamba maafa yametokea kwa jambo ambalo lingeweza kuzuilika.

2. Waziri aachie ngazi kwa sababu yeye ndiye mwakilishi wa rais mahali pale na alitakiwa ajenge hoja na kumwonyesha rais kwamba mahitaji mengine yanaweza kusubiri ili kuokoa janga. Pengine hoja ilikuwa nyepesi na kiasi kwamba rais aliona inaweza kusubiri au hata kwamba rais aliwaomba wasubiri bajeti zinazokuja nao wakakubali.
Ukiwa safari haitoshi mkeo kusema tu "mtoto anaumwa" anapaswa kusema "mtoto anaumwa kiasi gani" ili ujue uchukue hatua gani coz hayewezekana aumwa mafua tu.

3. Rais hawezi kujiuzulu kwa hili kwa sababu yeye si mtaalam wa mabomu na kama kuna uzembe basi unatokana na wateule wake hivyo ana wajibu wa kuwataka waachie ngazi kwa heshima ama awafukuze. Urais ni taasisi kwa hiyo hatuwezi kukurupuka asubuhi na kutaka rais atoke madarakani..akitoka nini kinafuata??

Kama kuna waliofuatilia hotuba ya Mbowe Mwanza aliuza umati ule "Mnataka Kikwete ajiuzuluuuuuuuu.....??", lile wingu la watu likalipuka "ajiuzuluuuuuuuu...!!!!". Mbowe akasema "Kikwete mwacheni kwanza tunampa muda"!

Anaposhindwa kuwawajibisha watendaji wake hapo ndipo wana Upinzani wanaweza kuja kwa wananchi kushitakia ili wananchi waamue kuvumilia hadi 2015 au wampige chini immediately.

Na wakati mwingi when we talk of Kikwete haimaanishi an individual bali anawakilisha utawala.
 
Ni saa ya ukombozi,wanachofanya chadema ndio hasa wajibu wa chama cha siasa,,huwa nashindwa kuelewa baadhi ya watanzania wanaposhindwa kuuona ukweli wa maisha ya watanzania.Serikali ya ccm chini ya JK imeshindwa kuboresha maisha ya watanzania,wanaposimama mashujaa wachache kama kina Dr Slaa,Mbowe,na wengine kuelimisha umma,wengine mnaanza kuwabeza,huu si uungwana,lazima kama taifa tujifunze kusema na kuutetea ukweli,,,to dare is to do....
 
Waberoya,

Tunashukuru kwa ushauri. Najiuliza, je tukifanikiwa katika hilo utajiunga Chadema? Ni nini ambacho kinakuzuia kujiunga Chadema sasa hivi ili tujenge wote chama?

Kikubwa zaidi kwenye hoja yako ni kushift focus kutoka kwa Kikwete kwenda kwenye mfumo tunaoupinga. JK tayari ni Raisi na inawezekana akabaki mpaka 2015. Hatagombea tena. Kwa hiyo kama amefeli ndio amefeli na hatakuwepo tena. Atasimamishwa mwingine halafu tutaanza nae. Wananchi wataona 'afadhali labda huyu'. Atashinda. Lazima tuzuie hilo. Tujijenge sisi kama chama na wananchi watuamini na watuelewe. Tujenge personalities...watu huchagua watu mara nyingi. Lazima wakuamini.

Ninapata mashaka na habari hii ilivyoripotiwa. Kuna kila uwezekano imekosewa.

Dr Slaa hawezi kusema JK alikataa kutoa hela mara mbili mabomu yaharibiwe halafu amwambie Waziri na Mkuu wa Jeshi wajiuzulu kwa uzembe. Kama Raisi amewanyima fedha wamezembeaje sasa? Nadhani habari hiyo haijakamilika.

Tuendelee kutafakari

Mh. Msando salaam!

Asante kwa swali lako la mtego! mimi ni mpenzi wa mageuzi, napenda kila zuri la chadema na ninachukia kila baya la chadema na vyama vingine, recently nimekuwa niki-pose challenge nyingi kwa chadema kwa sababu wana uhai, wanarekebishika tofauti na mawazo ya wengine kuwa unapotoa challenge basi unakichukia hicho chama. Nikiangalia CDM kama iko siku wanaweza kushika dola, basi nakuwa mwangalifu kisije kuwa kama CCM !

Unataka nijiunge? bado kuna mambo ya kurekebisha ndani ya chadema, je nikijiunga na siku nikataka ku-aspire uenyekiti wa chama nitagombea na kupigiwa kura na watakaokuwa wapenzi wangu (mfano), je watoto leo wanaipenda CDM kiasi gani hata kuota kugombea urais kupitia CDM??. Sio siri mtu wangu I was greatly confused kwenye zile chaguzi zenu za uenyekiti wa chama na vijana.... that made me to think beyond, in future vinahatarisha demokrasia zetu kwa sisi tunaopenda ukweli. Sijisifu mh. ila naona ndivyo nilivyo kumlipua mtu kulingana na alichokosea ndiyo sera zangu na ndivyo nilivyo, nafanya hivyo makanisani, nafanya hivyo kwenye ukoo nafanya hivyo kazini, na nitafanya hivyo nikiwa ndani ya chadema, swali je chadema wako tayari kiasi gani kukubali challenge za wanachama wake wenyewe??

nikukumbishe, je CDM inaweza ikavumilia moto wa upinzani ndani ya chama kama ule wa H.Clinton na Obama? kama hatujafikia evel hiyo then we have serious job ahead us ambayo si tu kuwa ndani ya chama kunasaidia bali kugeuza fikra za watu ndiyo challenge kubwa sana, vyama vingi sana vinaharibiwa na wanachama wao wenyewe ambao wengi wamelelewa kwenye mbeleko na tabia za ki-CCM.

However, I like CDM nimekuwa na Mdee kwenye kampeni kawe kwa sababu naishi huko, na nilikuwa na myika kipindi kile ambacho kura zake hazikutosha. ukweli CCM siwapendi

Ukinipa jibu la uhakika kesho nachukua kadi!
 
Hivi ndio kikubwa kinachoongelewa huko? JK ameoza na hafai hata kuongelewa , kuacha misiba si mara ya kwanza, CDM waste time kupata wanachama wapya, kuuza sera zenu na kuwapa hope watanzania! jengeni ubalozi wa nyumba tano tano, tumieni style za Halima mdee kipindi cha uchaguzi, tumieni style ya mihadhara ya waislamu au mikutano ya injili....... SPREAD GOSPEL OF REVOLUTIN AND CHANGE kumsema Kikwete is wastage of time..

I wish you could attend personay
 
Mh. Msando salaam!

......................... Sio siri mtu wangu I was greatly confused kwenye zile chaguzi zenu za uenyekiti wa chama na vijana.... that made me to think beyond, in future vinahatarisha demokrasia zetu kwa sisi tunaopenda ukweli. .............................. swali je chadema wako tayari kiasi gani kukubali challenge za wanachama wake wenyewe??..........................Ukinipa jibu la uhakika kesho nachukua kadi!

Safi sana Mkuu Webby.............

Hivi ilikuwaje wakati wa Mh Kafulila akiwa Chadema................ilikuwaje mpaka akatoka CDM?
 
Slaa, Mbowe wamkaanga JK

• Wamshangaa kwenda nje wakati wa matatizo

na Mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wamemrushia kombora Rais Jakaya Kikwete kuwa analea nyufa za udini, ukabila pamoja na kukataa kutoa fedha za kuharibu mabomu yaliyozua balaa kwa wakazi wa Gongo la Mboto.

Viongozi hao walisema Rais Kikwete anashindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila kwa sababu ni mkakati wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuidhoofisha CHADEMA ambayo hivi sasa imejizolea sifa na wanachama wengi, kwa sababu ya uimara wake wa kukiwajibisha chama tawala na serikali yake.

Wakizungumza kwa wakati tofauti katika viwanja wa Shule ya Mkendo mjini Musoma jana, viongozi hao walisema kwa hali ilivyo, Rais Kikwete, amekosa sifa za kuwa kiongozi imara.

Mbowe alisema Rais Kikwete ameshindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila ambao umeonekana dhahiri kuanza kuota mizizi hapa nchini, hivyo zinahitajika juhudi za haraka na makusudi kuuwajibisha utawala wake ili kuinusuru nchi.

"Taifa limeingia kwenye udini na ukabila ambao rais wa nchi ameshindwa kuudhibiti...sisi tunafahamu ajenda ya udini na ukabila ni mkakati wa CCM wa kutaka kuimaliza CHADEMA, jambo ambalo kamwe hatulikubali," alisema.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Waziri Mkuu Kivuli, aliwataka Watanzania kuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kulikomboa taifa hasa katika kipindi hiki ambacho umasikini unazidi kushamiri siku hadi siku.

"Tukiwaachia hawa CCM waendelee kututawala kama wanavyotaka kamwe umaskini hauwezi kutoweka miongoni mwetu, uwezo wa kubadilisha uongozi na hali zetu za kimaisha tunao, kwanini tunashindwa kuutumia?" alihoji.

Kuhusu uundwaji wa Katiba, Mbowe aliionya serikali kuwa ni vema isifanye hila mara baada ya wananchi kutoa maoni yao, kwani mchezo wowote utakaofanywa kwa lengo la kupinga maamuzi ya umma hukumu yake itakuwa kubwa kama ile inayoonekana hivi sasa nchini Libya au ile iliyotokea Misri.

Naye Dk. Slaa, alisema kuwa amesikitishwa na milipuko ya mabomu iliyotokea Gongo la Mboto ambayo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na uzembe wa serikali ambayo iligoma kutoa fedha kwa ajili ya kuyaharibu mabomu hayo.

Alibainisha kuwa anazo taarifa kuwa Rais Kikwete alilinyima jeshi hilo fedha za kuharibu mabomu hayo ambayo yalionekana kwisha muda wake miaka miwili iyopita.

"Ninayo taarifa kwamba serikali ya Rais Kikwete iliombwa fedha mara mbili za kuharibu mabomu lakini ilishindwa kufanya hivyo...hali hiyo ndiyo iliyosababisha vifo vya Watanzania Mbagala na sasa Gongo la Mboto," alisema Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa, kutokana na uzembe huo, anamtaka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, pamoja na Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Davis Mwamnyange, kujiuzulu mara moja nyadhifa zao na iwapo watashindwa, basi Rais Kikwete awafukuze.

Alisema Watanzania hawawezi kuendelea kuvumilia viongozi kama hao wazembe wa kazi na kwamba ni vema Waziri Mwinyi akaiga mfano wa baba yake, Ali Hassan Mwinyi, aliyeachia ngazi kutokana na mauaji yaliyotokea wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

"Tunamtaka Waziri Mwinyi ajiuzulu, na akishindwa basi Rais Kikwete amfukuze kazi huyu mtu pamoja na Mkuu wa Majeshi...wananchi wameshachoka kuona usanii wa uongozi," alisema.

Mbowe na Slaa waliongeza kuwa wamemshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kuacha msiba wa Watanzania waliokufa kwa mabomu ya Gongo la Mboto, kisha kwenda nchini Mauritania kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast.

Walisema ni aibu kwa kiongozi wa wananchi kuacha msiba mkubwa nchini kwake na kukimbilia nje ya nchi kwenda kusuluhisha mambo ya nchi nyingine.
"Kwenda Mauritania kwa Rais kikwete ni kuwadhalilisha Watanzania ...ni sawasawa na baba mwenye familia kuacha watoto wake wanakufa njaa, yeye anakwenda kutoa chakula nyumba ya jirani," alisema Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Katika hotuba yake, Dk. Slaa alisema kamwe Watanzania hawawezi kuvumilia kuona usaliti wa namna hiyo unafanywa na mtu mkubwa kama Rais Kikwete, ambaye ndiye Amiri Jeshi Muu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Katika hatua nyingine, alimtaka Rais Kikwete na serikali yake kuitaifisha mitambo ya Dowans, kwani mitambo hiyo imeingizwa nchini kwa njia za kitapeli na ujanja ujanja, kinyume cha sheria za nchi.

Hapo kwenye red!.Je, hii inamaanisha CDM offially inamtambua JK kana rais wa URT au ni mwandishi kakosea? maana kuna sehemu anawa quote viongozi wote wawili wa CDM, Dr. WS na FAM wa kimuita Rais Kikwete!!! naomba mungozo tafadhali.
 
Naona Chadema wameishiwa na sera, hawana kipya ila majungu, fitina na hoja zisizo na maana hata chembe.

Kuwepo au kutokuwepo nchini Rais si hoja ya msingi, kwani huko alikokwenda alienda kucheza?

Wanatubowa na vijineno neno vya ufataani na siasa za kuwabagua wananchi, halafu wanaongelea udini? Wamesahau kuwa kanisa liliwakataa waumini kwa kuwa wameipigia kura CCM? wamesahau Slaa alipoifananisha CCM na Taliban? Sasa hapo nani ni mdini?

KWA KUWA KIKWETE NDIYE RAIS, ANATAKIWA ASHUGHULIKIE KUUONDOA UDINI. Hata ukiwa unasababishwa CDM au kwa maaskofu. Kama hahangaiki kuundoa, sisi tunaamini Kikwete ndiye chanzo cha udini.
 
Naona Chadema wameishiwa na sera, hawana kipya ila majungu, fitina na hoja zisizo na maana hata chembe.

Kuwepo au kutokuwepo nchini Rais si hoja ya msingi, kwani huko alikokwenda alienda kucheza?

Wanatubowa na vijineno neno vya ufataani na siasa za kuwabagua wananchi, halafu wanaongelea udini? Wamesahau kuwa kanisa liliwakataa waumini kwa kuwa wameipigia kura CCM? wamesahau Slaa alipoifananisha CCM na Taliban? Sasa hapo nani ni mdini?

Utakuwa ni M/Kiti wa UWT au mmoja wa wale comfort girls walioingizwa bungeni na shanga miguuni.
 
Hapo kwenye red!.Je, hii inamaanisha CDM offially inamtambua JK kana rais wa URT au ni mwandishi kakosea? maana kuna sehemu anawa quote viongozi wote wawili wa CDM, Dr. WS na FAM wa kimuita Rais Kikwete!!! naomba mungozo tafadhali.

Mbona TBC inamuita Dr Kikwete? Si anapenda? Bado kitambo atakuwa profesa.
Kwani Idd Amin hakuwa Rais na tena Field Marshal? Mtu akijiita basi huitwa.
 
Safi sana Mkuu Webby.............

Hivi ilikuwaje wakati wa Mh Kafulila akiwa Chadema................ilikuwaje mpaka akatoka CDM?

Hakuna chama Duniani ambacho kitamuruhusu kila anayetaka kugombea afanye hivyo bila kuchujwa. Kafulila unavyomuona ni mtu wa kuachiwa chama! Hata huyo Zitto! Na huwezi kusema waache eti demokrasia itawaondoa.

Unaweza kujikuta unakuwa na chama chenye m/kiti kama Kikwete na katibu mkuu kama Makamba. Bado CCM wanajiita chama kikongwe.

Hao ni watu ambao ukiwaonyesha cheki, wanahamisha mawazo ya chama kabla hata hawajafika benki.
 
Nitamaduni zetu ambazo kila Mtanzania anazijua ukiwa na Msiba uruhusiwi kutoka nje ya eneo unaloishi na hata ukiwa mbali na eneo la msiba inakulazimu ukaribie eneo la msiba. Mkwere sio mzalendo
 
Nduguzanguni,
Hii inaanza kutia kinyaa kwamba kila kukicha CDM lawama ni kwa JK tu. Inafika mahali mtu usipoona thread ya kumtukana na kumdhalilisha JK unashangaa kwamba hawa jamaa wako wapi leo?
Tulishaongea na wengi wamesema vyema kwamba Urais si mtu binafsi, bali ni taasisi. Kwa hiyo Rais kwenda kuhudhuria mkutano nje haimaanishi kwamba amewadharau watu, la hasha. Kwanza kabla hajaenda nje, alifika eneo la tukio na kujionea. Makamu wa Rais na viongozi wengi wengine walitembea waathirika wa tukio lile, sasa mulitaka kila kitu afanye JK tu? Maana mwisho mtasema hata kwenye mazishi hakwenda, angehudhiria mazishi ya wangapi?
Kwenye hali zetu za kawaida, tunapopata misiba, ina maana baba huwa hata nje hatoki? maana akitoka hana unchungu huyo? Asiende hata kununua au kutafuta mlo kwa wanawe na waombolezaji? Kuweni realistic na si kuongea kwa chuki na fitina. Hizi roho za namna hii zinaanza kuleta shaka kama ni za jamii hii hii ya watanzania wenye upendo.
 
Back
Top Bottom