Slaa, Lissu na wafuasi wao wafikishwa mahakamani Arusha

Acha vyombo vya dola vifanye kazi yake, hawawezi kutuharibia Tanzania yetu kwa uchu wa madaraka

siyo uchu wa madaraka wanapigania haki japo mlioko madarakani hamuwezi kuona kinachoendelea kwa sababu mmepofushwa.
 
Ngoja Prince Charles aje aone jinsi misaada yao inavyotumika kununulia mabomu ya machozi na pilipili badala ya dawa na madawati shuleni.
Kweli CCM ni janga la kujitakia. AR tunawapa support tulio mbali,msirudi nyuma mashujaa na historia itawakumbuka
 
Wanaoililia amani ya Tanzania ni kwa kuwa wanahofia amani ya MAHEKALU yao na mihela na sio kweli kuwa wanaihitaji. Hii amani haina maana yoyote kwetu sisi machokoraa tunaoishi mitaani.

Tutalianzisha kisha tuone nani mwenye hasara.
 
Magamba waje na strategy nyingine, hii ya kamata kamata haiwasaidii kabisa!
 
Dawa yake Lema ni ile ya Chacha wangwe tu. Kijana Deus uko wapi? Hfi wewe Slaa na Mbo....mnajiona nyinnyi nidyo wakombozi? Wapiuuizi wakubwa nyie.

Harakati nyingi sana duniani zimekumbana na changamoto, ni hii ni mojawapo ya hizo changamoto, mwishowe ukweli utashinda, amka Mkuu njoo ungana na wanaharakati.
 
Harakati nyingi sana duniani zimekumbana na changamoto, ni hii ni mojawapo ya hizo changamoto, mwishowe ukweli utashinda, amka Mkuu njoo ungana na wanaharakati.
kweli mkuu huwezi kupingana na haki ya mtu, tatizo hawasomi alama za nyakati.
 
Katika mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa wa Arusha leo mpaka muda huu ambao ni majira ya saa 10:29 (kumi na dk 29 jioni) Dr.Slaa na Lissu na wananchi wengine 27 wamesomewa mashtaka na yako kama ifuatavyo;

1. Kukusanyika kinyume cha sheria .
2. Kukataa kutii amri halali ya polisi

Ila Slaa kasomewa shitaka la tatu peke yake nalo ni la uchochezi, ila maneno yaliyosemwa na polisi kjuwa yalitamkwa sijui yatakuwa yalitamkwa wapi ila sio kwenye mkutano wa hadhara wa jana kama ambavyo mwendesha mashitaka anataka kuiaminisha mahakama .

Taratibu za dhamana zinaendelea kwenye mahakama hiyo , ila ntawajulisha nini kiuitatokea kwani taarifa ni kuwa Lissu na Dr.Slaa wao wataenda Kisongo kuonana na LEMA na kupafanya kuwa ni makazi ya kudumu kama ambavyo polisi na serikali wanataka .
 
Ngoja Prince Charles aje aone jinsi misaada yao inavyotumika kununulia mabomu ya machozi na pilipili badala ya dawa na madawati shuleni.
Kweli CCM ni janga la kujitakia. AR tunawapa support tulio mbali,msirudi nyuma mashujaa na historia itawakumbuka

Mkuu hv unadhani hata hilo gamba likiona litafanya nini ukifuatilia sana utakuta labda naye anamchongo wake huku wala si hivi-hivi.
 
Hivi magamba wana akili kweli? Jambo dogo wanalifanya kubwa, kubwa likanakuwa dogo bullshi magamba!. Polisi wanagekuwa sharp kukamata mafisadi, nchi hii tungekuwa mbali sana, hata camerun asingethibutu kusema ule upuuzi wake. Lakini mafisadi wanalindwa kwa hali na mali tena kwa kodi zetu, wale wanaowafichua wanawekwa ndani, tena bila makosa.

Tazama siku zinakuja, ambapo haya yote yatawekwa wazi, hivi mafisadi mtakimbilia wapi?

Siku zinakuja ambapo dhuluma haitakuwepo katika nchi hii, haki itatawala. ee Mungu tupe uvumilivu.
 
Jamani kwani asiwatupe lupango iwe fundisho kwa mamluki wote wa siasa kwamba hakuna serikale legelege duniani
 
Hivi Slaa na wenzake walikutwa na silaha? Polisi wa magamba!!!!!!! ni vibaraka wa CCM sijapata kuona. Waliufyata kumkamata yule Shabab Rage alipopanda jukwaani mbele ya wananchi huku amening'niza basota kiunoni mithili ya John Wayne

Polisi wetu kwa kufuata haki ni ZERO kabisa, wanaendeshwa na wanasiasa wa CCM kwa pua.
 
kuwakamata na kuwaweka ndani(mahabusu) viongozi wa CDM si suluhisho la wananchi kuacha kudai katiba mpya na kuendelea kupinda ufisadi waziwazi.
 
Mkuu Daffi,umenifanya nicheke kidogo japo tangu jana sina amani moyoni na nimelala usingizi wa mang'amunga'mu usiku kucha.nimejikongoja kibaruani lakini nipo physical mentall niko Arusha na kuwafikiria hawa magamba na vitendo vyao,na hata mimi naona nitoke niende kugonga safari bia yangu niliyojifunzia nitarudi jukwaani kusikia habari mpya kama zipo,maana akili haindi kabisa...( ulichonifanya nicheke kicheko cha uchungu ni ili ulivyosema ukapate tasker baridi)

Lakini twende mbele turudi nyuma hii hali itaishia wapi?maana hawa watu wanazidi kutukandamiza na kutunyonya bila woga,mfano ni juzi wakati kamati za bunge zinafanya mapitio,kila mahali ufisadi na wizi,inaonekana watu wamegawiana maeneo ya kuchota fedha za umma kwa sababu hakuna wa kumkemea,angalia TCRA watu 2/3 wanasomeshwa kwa bilioni mbili,jamani walikuwa wanasomea kurudisha uhai wa mtu alokwisha kufa?

Angalia bodi wanalipana mishara in terms of US $,na sehemu zingine ni yale yale,sasa hawa wanaonekana wana nafasi ya kukemea na wakasikika kwa umma dili imekuwa ni kuwatia ndani na kuwapiga mabomu na risasi.wanyonge kama wale wa njedenga pale dodoma walivamiwa alfajiri na kuanza kuvunjiwa nyumba kana kwamba hakukuwa na njia mbadala ya kuwatoa pale.hivi kungelikuwa na mjomba ake Pinda au Kikwete ama Malecela pangevunjwa kwa style hiyo? No bwana.

Ngoja nitoke nitakuja kusoma kama kuna update za AR
 
Jamani we mbundi wa balaa kwanini hautui mikoa yote uonyeshe kila kilichokuwa kinatafutwa na CCM muda mrefu?itakuwa ni vema na haki likinuka nchi nzima maana hapa ni ubabe unatumika sasa kama kweli serikali hii inawekwa na watu na watu wenyewe ni pamoja walioko Arusha basi kuna haja ya kukataa uonevu.

Tupeni habari kama wameshampeleka gerezani hao viongozi na wanachadema wengi

Ila kama hawatatumia akili na busara wajiulize ni kwa nini mshabiki wa mpira alijinyonga Kenya baada ya Arsenal kufungwa?ni kwa nini kuna watu wanajilipua,ni kwa nini Libya na kwingineko?ni kwanini mkaburu kule Afrika kusini aling'olewa?

Haya bwana dola mnayo ninyi lakini panueni Magereza,hayatoshi kabisa.
Acheni kudanganyana, Tanzania haijawa kama hizo Libya wala huko mnakotaja. Tatizo mnalazimisha machafuko wakati hali haijafikia huko. Mmeshindwa Igunga mmekimbilia Arusha kama kawaida yenu watu wa kaskazini
 
Time ya mahakama mwisho saa 9.00 imekaaje hii?
Na mimi nlikuwa najaribu kujiuliza swali hili. Ama walijua kuwalaza mahabusu leo kituo kingechomwa moto?
Inamaana viongozi wa cdm ni powerfull kuliko majeshi yetu ya ulinzi na usalama??? AIBU
 
Jamani kwani asiwatupe lupango iwe fundisho kwa mamluki wote wa siasa kwamba hakuna serikale legelege duniani


Swala la kwenda au kutokwenda ni uamuzi wao maana hayo makosa yana dhamana. Na kuhusu serikali legelege, ukweli ni kwamba hapa duniani ipo Tz. That is beyond any reasonable doubt!
 
Back
Top Bottom