Slaa, Lissu na wafuasi wao wafikishwa mahakamani Arusha

Ngoja Prince Charles aje aone jinsi misaada yao inavyotumika kununulia mabomu ya machozi na pilipili badala ya dawa na madawati shuleni.
Kweli CCM ni janga la kujitakia. AR tunawapa support tulio mbali,msirudi nyuma mashujaa na historia itawakumbuka

Watamkwepesha magamba wajanja sana unaweza kuta tayari wamesha andaa miradi bandia akazungushwa uzunguni na kupelekwa kwenye hotel ya kitalii wakamdanganya hapa ndo tunalelea watoto yatima hawa magamba sio watu
 
Zaburi 58
1 ni kweli enyi wakuu mnanena haki? Enyi wanadamu mnahukumu kwa adili?
2 Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu; katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.
3*Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
4 Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka; mfano wao ni **** kiziwi azibaye sikio lake.
5 Asiye sikiliza sauti ya waganga, ijapo wafanya uganga kwa ustadi.
6 Ee Mungu uyavunje meno yao vinywani mwao; ee Mungu uyavunje magego ya wana-simba.
7 Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi; Akiielekeza mishale ya yake, iwe imetiwa ubutu.
8 Kama konokono ayeyukae na kutoweka; kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua.
9 Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba; ataipeperusha kama chamchela, iliyo mbichi na iliyo moto.
10 Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi; ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.
11 Na mwanadamu atasema, hakika iko thawabu yake mwenye haki. Hakika yupo Mungu anaehukumu katika dunia.

My take:

Maneno haya ya zaburi hii ni mahsusi kwa serikali dhalimu kama ya ccm na nyinginezo katili. Basi watanzania tunaweza elewa kile serikali ya kisanii ya ccm ilichowaahidi wananchi wake hasa kupitia Jk. Aliahidi mambo yasyotekelezeka kwani alifahamu wazi serikali yake iliyokwisha filisika kwa sababu ya matanuzi yaliyonayo haiwezi kubeba hizo ahadi. Tunafahamu pia jinsi ambavyo ni mshirika kamili wa mafisadi wanaoiibia nchi hii hata kufikia kuvunja katiba ya nchi kuwasamehe wazi nae akiwa miongoni mwao.

Nchi haizalishi kwa sababu ya kuendekeza cheap politics na hivyo bidhaa hasa za muhimu katika maisha ya kila siku zimepanda kwa kiwango cha asilimia 200 na 500 kulingana na eneo. Sasa hivi anaficha udhaifu wake kwa kushughulika na watu kama kina Lema. Ni usanii mwingine wa kufichia madhaifu waya huyu rais legelege tuliewahi kuwa nae. Angalia mawaziri wake wanavyojibu maswali bungeni, hasa juu ya ahadi alizotoa rais wao, ni usanii juu ya usanii huku wakiwa hawana hata haya ya uso. Hii ni kwa sababu wanajua wanatetea uongo wa aliyewateua hivyo hawatakuwa na madhara ya kufukuzwa kazi.

Popote mlipo wapenda amani kote nchini, wapenda ukweli na uwazi, wenye kuamini imani ya uadilifu na uwajibikaji kwa adili. Kesheni katika kuiombeya serikali hii kwa kusoma zaburi ya 58 kila siku. Huenda Mungu wa mbinguni akatusikia na kuamua kumtuma malaika wake kuithibitisha kila nucta ya neno lake katika zaburi hii kwa serikali yetu tukutu!
 
Mkuu Daffi,umenifanya nicheke kidogo japo tangu jana sina amani moyoni na nimelala usingizi wa mang'amunga'mu usiku kucha.nimejikongoja kibaruani lakini nipo physical mentall niko Arusha na kuwafikiria hawa magamba na vitendo vyao,na hata mimi naona nitoke niende kugonga safari bia yangu niliyojifunzia nitarudi jukwaani kusikia habari mpya kama zipo,maana akili haindi kabisa...( ulichonifanya nicheke kicheko cha uchungu ni ili ulivyosema ukapate tasker baridi)

Lakini twende mbele turudi nyuma hii hali itaishia wapi?maana hawa watu wanazidi kutukandamiza na kutunyonya bila woga,mfano ni juzi wakati kamati za bunge zinafanya mapitio,kila mahali ufisadi na wizi,inaonekana watu wamegawiana maeneo ya kuchota fedha za umma kwa sababu hakuna wa kumkemea,angalia TCRA watu 2/3 wanasomeshwa kwa bilioni mbili,jamani walikuwa wanasomea kurudisha uhai wa mtu alokwisha kufa?

Angalia bodi wanalipana mishara in terms of US $,na sehemu zingine ni yale yale,sasa hawa wanaonekana wana nafasi ya kukemea na wakasikika kwa umma dili imekuwa ni kuwatia ndani na kuwapiga mabomu na risasi.wanyonge kama wale wa njedenga pale dodoma walivamiwa alfajiri na kuanza kuvunjiwa nyumba kana kwamba hakukuwa na njia mbadala ya kuwatoa pale.hivi kungelikuwa na mjomba ake Pinda au Kikwete ama Malecela pangevunjwa kwa style hiyo? No bwana.

Ngoja nitoke nitakuja kusoma kama kuna update za AR
Mkuu kwenye kupinga ufisadi tuko pamoja ila la kuacha shughuli zetu na kumfuatilia mtu aliyegoma mwenyewe asipewe dhamana,mnaweza mkadhikiri usiku kucha hatutokuwa pamoja.

Pamoja against UFISADI. Nalog off
 
Na mimi nlikuwa najaribu kujiuliza swali hili. Ama walijua kuwalaza mahabusu leo kituo kingechomwa moto?
Inamaana viongozi wa cdm ni powerfull kuliko majeshi yetu ya ulinzi na usalama??? AIBU
Wangekuwa powerful hadi saivi wangekuwa NMC
 
Zaburi 58
1 ni kweli enyi wakuu mnanena haki? Enyi wanadamu mnahukumu kwa adili?
2 Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu; katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.
3*Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao; tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
4 Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka; mfano wao ni **** kiziwi azibaye sikio lake.
5 Asiye sikiliza sauti ya waganga, ijapo wafanya uganga kwa ustadi.
6 Ee Mungu uyavunje meno yao vinywani mwao; ee Mungu uyavunje magego ya wana-simba.
7 Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi; Akiielekeza mishale ya yake, iwe imetiwa ubutu.
8 Kama konokono ayeyukae na kutoweka; kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua.
9 Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba; ataipeperusha kama chamchela, iliyo mbichi na iliyo moto.
10 Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi; ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.
11 Na mwanadamu atasema, hakika iko thawabu yake mwenye haki. Hakika yupo Mungu anaehukumu katika dunia.
My take: maneno haya ya zaburi hii ni mahsusi kwa serikali dhalimu kama ya ccm na nyinginezo katili. Basi watanzania tunaweza elewa kile serikali ya kisanii ya ccm ilichowaahidi wananchi wake hasa kupitia Jk. Aliahidi mambo yasyotekelezeka kwani alifahamu wazi serikali yake iliyokwisha filisika kwa sababu ya matanuzi yaliyonayo haiwezi kubeba hizo ahadi. Tunafahamu pia jinsi ambavyo ni mshirika kamili wa mafisadi wanaoiibia nchi hii hata kufikia kuvunja katiba ya nchi kuwasamehe wazi nae akiwa miongoni mwao. Nchi haizalishi kwa sababu ya kuendekeza cheap politics na hivyo bidhaa hasa za muhimu katika maisha ya kila siku zimepanda kwa kiwango cha asilimia 200 na 500 kulingana na eneo. Sasa hivi anaficha udhaifu wake kwa kushughulika na watu kama kina Lema. Ni usanii mwingine wa kufichia madhaifu waya huyu rais legelege tuliewahi kuwa nae. Angalia mawaziri wake wanavyojibu maswali bungeni, hasa juu ya ahadi alizotoa rais wao, ni usanii juu ya usanii huku wakiwa hawana hata haya ya uso. Hii ni kwa sababu wanajua wanatetea uongo wa aliyewateua hivyo hawatakuwa na madhara ya kufukuzwa kazi.
Popote mlipo wapenda amani kote nchini, wapenda ukweli na uwazi, wenye kuamini imani ya uadilifu na uwajibikaji kwa adili. Kesheni katika kuiombeya serikali hii kwa kusoma zaburi ya 58 kila siku. Huenda Mungu wa mbinguni akatusikia na kuamua kumtuma malaika wake kuithibitisha kila nucta ya neno lake katika zaburi hii kwa serikali yetu tukutu!!
.
Ni kumkosea Mungu kuingiza Zaburi kwenye mambo ya siasa za kijinga za akina Lema. Utangulie kutubu kabla hiyo Zaburi haijakugeukia
 
Hawa jamaa inabidi kabla ya kupelekwa kisongo wakapimwe akili. Haiwezekani kuhamasisha watu wakeshe uwanjani kulazimisha Lema atoke wakati anayapenda maisha ya jela.
 
Taratibu za dhamana zinaendelea , ila ni nje ya muda wa mahakama , sasa sijui hapo utaratibu ni kuwa hakimu atalipwa overtime ama itakuwaje .
 
Hawa jamaa inabidi kabla ya kupelekwa kisongo wakapimwe akili. Haiwezekani kuhamasisha watu wakeshe uwanjani kulazimisha Lema atoke wakati anayapenda maisha ya jela.
Watasumbua vipimo bure kupima watu ambao kuna uhakika asilima 100 hawana akili
 
Yaani leo kama wataenda mahabusu na wale jamaa waliotoka ukonga selo watawatia nizamu kwani viagara wapewa amini usiamini hunipi msosi
 
Kwa hili, serikali inalazimika kukopa busara ili kulitatua!

Swala hili lilikuwa dogo sana kwa serikali kuruhusu Lema atoke gerezani na jana wamalize mkutano wao lakini serikali kwa kukosa busara zao kwa kuhofia kuwa eti wataipa CDM umaarufu wameamua kukalia busara zao kwenye masaburi na kusababisha matatizo haya kwa wakazi wa Arusha.

Tumieni busara tu, hivi mkiwaacha wakaandamana na mkaimarisha ulinzi mnakuwa mmepungukiwa na nn nyie vikosi vya lntelejinsia?

If the Action is Wrong .. how do you REACT with IT, expecting to gate the RIGHT outcome? Simply don't react with reaction ... to be in a safe place!! ... Guys stop reacting with what is happening ...Do simple manure things ..you missed it Yesterday .. you should have let HIM out?! ... and do the surveillance... and the others you want send them at the same point? ... ..avoid to make a grouping.. dont miss it again...!! Please MAKE A DEAL WITH THEM ... ! ... CREATE A WIN WIN DEAL ...!! It will make the boys in the street relax go to sleep and grow up as a dissent Citizens ..stop chasing them around!!
 
Back
Top Bottom