Katibu mkuu wa CHADEMA, Wilbrod Slaa na mkurugenzi wa sheria wa chama hicho Tundu Lissu na wafuasi wengine kumi wa chama hicho wanafikishwa mahakamani muda mfupi ujao jijini Arusha.
Kuna hatari ya kunyimwa dhamana kutokana na vurugu ambazo zinaendelea kwani vijana wa chama hicho wanavunja vioo vya magari na muda mfupi uliopita wamefanya hivyo katika mitaa ya Sabena iliyoko karibu na stand kuu ya Arusha
Katika mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa wa Arusha leo mpaka muda huu ambao ni majira ya saa 10:29 (kumi na dk 29 jioni) Dr.Slaa na Lissu na wananchi wengine 27 wamesomewa mashtaka na yako kama ifuatavyo;
1. Kukusanyika kinyume cha sheria .
2. Kukataa kutii amri halali ya polisi
Ila Slaa kasomewa shitaka la tatu peke yake nalo ni la uchochezi, ila maneno yaliyosemwa na polisi kjuwa yalitamkwa sijui yatakuwa yalitamkwa wapi ila sio kwenye mkutano wa hadhara wa jana kama ambavyo mwendesha mashitaka anataka kuiaminisha mahakama .
Taratibu za dhamana zinaendelea kwenye mahakama hiyo , ila ntawajulisha nini kiuitatokea kwani taarifa ni kuwa Lissu na Dr.Slaa wao wataenda Kisongo kuonana na LEMA na kupafanya kuwa ni makazi ya kudumu kama ambavyo polisi na serikali wanataka .
Last edited by a moderator: