Slaa awawakia wasioridhishwa na mgawo wa Viti Maalum

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Huyu jamaa kwa kweli ni dicteta na ni hatari ,kama unaweza kuisoma hii habari kwa kina basi utaiona rangi yake. Endelea...!

Dk. Slaa awawakia wasioridhishwa na mgawo viti maalum

By Thobias Mwanakatwe
21st December 2010

SlaaChadema%284%29.jpg

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa

[FONT=ArialMT, sans-serif]Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema njia ipo nyeupe kwa viongozi na wanachama wanaotaka kuondoka katika chama hicho kwa sababu ya kutoridhishwa na mgawo wa viti maalum vya wanawake katika Bunge. [/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza jana katika mkutano wa Baraza la Ushauri la Chadema jijini hapa, Dk. Slaa alisema tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, yamejitokeza malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama kwamba mikoa yao haijapata wabunge wa viti maalum licha ya kuwapo wabunge wa majimbo.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema miongoni mwa mikoa inayolalamika ni pamoja na Mbeya, ambao umepata wabunge wawili wa kuchaguliwa, lakini haukupata mbunge wa viti maalum.[/FONT]

“[FONT=ArialMT, sans-serif]Watu wa Mbeya mnalalamika sana kuhusu suala la viti maalum wakati Karatu tumeibeba Chadema toka mwaka 1995 hadi sasa, lakini hatujawahi kupewa viti maalum vya ubunge. Mbeya ni juzi tu ndiyo mmeanza kuibeba Chadema, halafu mnasema mnataka kuondoka kwenye chama. Tunasema ondokeni njia nyeupe kwa anayetaka kufanya hivyo,” alisema Dk. Slaa.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema viongozi wasioelewa kuhusu utaratibu wa utoaji wa viti maalum wanakuwa na ubinafsi wakati Chadema viti maalum havitolewi kama zawadi na wala siyo hisani kama wanavyodhani baadhi ya watu, bali vina malengo yake.[/FONT]

SOURCE: NIPASHE
 
Sioni udikteta wa Dr. Slaa; zaidi ya kusema ukweli. Labda kama kwenye chama chenu ukweli ni udikteta.
 
Huyu jamaa kwa kweli ni dicteta na ni hatari ,kama unaweza kuisoma hii habari kwa kina basi utaiona rangi yake. Endelea...!
Dk. Slaa awawakia wasioridhishwa na mgawo viti maalum
By Thobias Mwanakatwe
21st December 2010
SlaaChadema%284%29.jpg

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa

[FONT=ArialMT, sans-serif]Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema njia ipo nyeupe kwa viongozi na wanachama wanaotaka kuondoka katika chama hicho kwa sababu ya kutoridhishwa na mgawo wa viti maalum vya wanawake katika Bunge. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza jana katika mkutano wa Baraza la Ushauri la Chadema jijini hapa, Dk. Slaa alisema tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, yamejitokeza malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama kwamba mikoa yao haijapata wabunge wa viti maalum licha ya kuwapo wabunge wa majimbo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema miongoni mwa mikoa inayolalamika ni pamoja na Mbeya, ambao umepata wabunge wawili wa kuchaguliwa, lakini haukupata mbunge wa viti maalum.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Watu wa Mbeya mnalalamika sana kuhusu suala la viti maalum wakati Karatu tumeibeba Chadema toka mwaka 1995 hadi sasa, lakini hatujawahi kupewa viti maalum vya ubunge. Mbeya ni juzi tu ndiyo mmeanza kuibeba Chadema, halafu mnasema mnataka kuondoka kwenye chama. Tunasema ondokeni njia nyeupe kwa anayetaka kufanya hivyo," alisema Dk. Slaa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema viongozi wasioelewa kuhusu utaratibu wa utoaji wa viti maalum wanakuwa na ubinafsi wakati Chadema viti maalum havitolewi kama zawadi na wala siyo hisani kama wanavyodhani baadhi ya watu, bali vina malengo yake.[/FONT]

SOURCE: NIPASHE

Sasa undikteta uko wapi hapa?
 
We kweli ni mwiba, acha kupotosha ukweli wa mambo wewe una matatizo yako ya kiCCM ndio yanakusumdua, au hujui maana ya udikteta.

Ni lazima Slaa na Mbowe lazima CCM wawaone wabaya mno, maana wanaiumbua mno kwani hawahongeki. Ndio sababu mnawaandama lakini waTZ wanakubali kinoma except nyie mnaotumiwa na mafisadi.
 
"Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua; wasiuone ingawa walitokea mashahidi wa uongo wengi" Mathayo 26:59-60
 
Jamani mimi ndhani mtoa mada anajaribu kutufanya wote
hatuna akili kama za CCM, Dk. amewapasha ukweli na si
vinginevyo kama Chama Cha Majambazi (CCM) wamezoea
kulipana fadhila sio Chadema, lazima tuwe wawazi bila kuwa
na makunyanzi.
 
"Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua; wasiuone ingawa walitokea mashahidi wa uongo wengi" Mathayo 26:59-60

E-BWANA kweli wanasaka kwa udi uvumba na manemane ushuhuda wa uwongo wapate kumchafua DR.Slaa (PHD) na CDM yetu. washindwe na walegee...............
 
Unafiki hauwezi kutusogeza mbele kimaendeleo Tanzania. Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, sorry, vitano:
  1. Watu wakweli na wanaojituma kufanya kazi
  2. Siasa safi isiyo ya kulindana kiswahiba
  3. Uongozi bora usiowaonea aibu mafisadi kwa vijimsaada anuai
  4. Ardhi isiyouzika kwa wakoloni mamboleo kiholela
  5. Udikteta wa kadiri kwao wanaodhani kupiga domo kuna tija bila jasho
 
Huyu jamaa kwa kweli ni dicteta na ni hatari ,kama unaweza kuisoma hii habari kwa kina basi utaiona rangi yake. Endelea...!

Mkuu Labda kama una-definition nyingine ya neno Dictator... Lakini nilicho kiona kwenye hii habari ni kuwa wazi/mkweli....
 
Tafadhali Ndugu MWIBA rejea kauli hii kutoka kwa Dr.Slaa nanukuu! (Karatu tumeibeba Chadema toka mwaka 1995 hadi sasa, lakini hatujawahi kupewa viti maalum vya ubunge!) Natumaini tuko pamoja kwa hao wanaolalamika kuhusu kukosa viti maalum huko Mbeya!
 
Huwa nafurahishwa sana na watu wanaotamani utendaji wa Dakta Slaa ufanane na utendaji wa Luteni Mwalimu Makamba!
 
Yaani hii ya dr nimeipenda,wtz wanapenda mambo mepesi2,uongozi cio kitu cha kupeana bila malengo viva dr wa ukweli
 
...makamba si mwalimu ila aliwahi kuwa mwalimu. kwa nini hakuendelea na ualimu, malaria sugu, na mwiba wanajua!
 
Its no wonder you call yourself 'mwiba' May be your objective number one is to cause pain to true Tanzanians. Uimla wa Dr. Slaa hapo ni upi??? Sikushangai... kwa CCM.... ukweli ni kama pilpili machoni!!!!
 
Siku zote nilikua nahisi mwiba ana matatizo makubwa ya uelewa, leo nimeamini... kumwambia mtu aende ni the best democracy one can give

dah... kweli ficha upumbavu wako usifiche hekima zako... mwiba kajiani pwaaaaaaa
 
Mtoa mada, nashukuru kwa kuleta thread hii kwa namna ambayo inavutia wengi hasa wabaya wa Dr.
Nakushukuru zaidi kwa kuonesha Dr. Asivyopenda kubembelleza pale ambapo hakuna haja ya kufanya hivyo. Kwake kubembeleza si lazima bali kuwaeleza watu ukweli na watakao pata ukweli huo waamue baada ya kuuelewa.
Narudia tena, ahsante mleta mada kwa kunifanya nimuelewe Dr.vizuri katika mambo haya yanayohitaji msimamo thabiti usio tetereka.
 
Back
Top Bottom