Siri ya chupi!

chupi za watoto zenyewe hazina tatizo...Hapo ndio utajua jinsi MAWAZO yanavyoumba. Wengine wametangulia mbele zaidi...nywele,miguu navyo vimewekwa kundi hili la chupi,yaani visionekane wazi kwani vitakufanya uwe na matamanio. Mimi naenda mbele hatua kumi:hata Mungu unayemfahamu alitengenezwa mawazoni kama chupi...usihamaki hebu rudia kusoma. Mungu ambaye ana kiberiti na petroli, ambaye hata kama ulikufa kwa ajali ya moto lazima akupe mwili upya ili akuchome yeye afurahi...

Tatizo nini hasa!?
 
Na kwa bahati mbaya ikaanguka halafu akaiokota yule mtoto wako mtukutu na kuanza kuzunguka nayo mtaani!?

Ndiyo maana kuna vya kushikilia kwenye kamba isidondoke!! Ila kwa hilo ni vizuri ikaanikwa mahali ambpo watoto hawafiki. Na sijui kama wote tunaweza hilo.
 
Hili vazi linashangaza kweli!
Dukani linauzwa hadharani.
Wakati wa kununuliwa linanunuliwa kwa siri.
Wakati wa kuvaliwa linavaliwa kwa siri na linavaliwa sirini.
Linaficha siri.
Linafuliwa na kuanikwa kwa siri.
Linapochakaa linatupwa kwa siri.

Kwa nini limekuwa la siri kiasi hiki?

Hiyo nyekundu:
Labda hizi zenu za siku hizi. Sisi tuliokuwa tunavaa VIP hapakuwa na siri yoyote, tulihakikisha kwamba vazi hilo linaonekana na kila mmoja pindi unapolivaa...na kwamba lazima ile mistari yote ionekane. Kikamba cha kati kinapokatika sasa ndo balaa.
 
Kuna taarabu moja ya zamani kidogo nimesahau mwimbaji wake kwa jina aliimba akiuliza nini kazi ya kufuli, kwake yeye anaona heri anunue kofia ili imsitiri jua ila haoni kazi ya "PAZIA" maana wala hailindi chochote, mtu akitaka kuingia anaingia tu........ndio yule mwimbaji alieimba wimbo wa Njiwa peleka salamu
 
Mpwa hii kali!
Wewe waungana na huyo mwimbaji?
 
Je wale wanaovaa nguo nyembamba mpaka chupi unaiona, huwa hawaelewi kuwa chupi ni siri?
Chupi sio siri, siri ni kilichofunikwa, tena katika mazingira maalumu tu.
 
Cha kushangaza sasa:
Kama vazi hili linavaliwa maeneo ya siri kwa nini linawekwa marembo (hasa kwa wenzetu)/ya nini kuvaa za thamani kubwa.....kwa faida ya nani?
 
Cha kushangaza sasa:
Kama vazi hili linavaliwa maeneo ya siri kwa nini linawekwa marembo (hasa kwa wenzetu)/ya nini kuvaa za thamani kubwa.....kwa faida ya nani?

kuonekana sexy babu eh, nashanga hata mwasema ni siri.
 
Hili vazi linashangaza kweli!
Dukani linauzwa hadharani.
Wakati wa kununuliwa linanunuliwa kwa siri.
Wakati wa kuvaliwa linavaliwa kwa siri na linavaliwa sirini.
Linaficha siri.
Linafuliwa na kuanikwa kwa siri.
Linapochakaa linatupwa kwa siri.

Kwa nini limekuwa la siri kiasi hiki?

HUWA SIRI KWA WALE WALIO WACHAFU KUPINDUKIA. Otherwise kwangu mie ninaeitizama chupi kama sehemu ya mavazi, nainunua hadharani tena naipanua kwa bidii kabisa kucheki kama itaweza kunitosha, naifua pamoja na nguo zangu zote, naianika kwenye jua kali nje kwenye kamba, naikunja na kuiweka kabatini pamoja na nguo zingine na hata kuichoma inapochakaa naichoma nje mahali pa wazi. ila kwe wale wanaovaa chupi hadi inaota ukoko katikati ndio wanaanika chini ya magodoro
 
Back
Top Bottom