Siri ya chupi!

Umesomeka mtumishi,
Naamin km ww unainywa basi itakuwa ni nzuri,
Nikiwa huko nitaiulizia!

...lakini hajakwambia kama inatengenezwa kwa kutumia nini!
kwa mfano nikisikia supu ya utumbo najua inatengenezwa kwa kutumia utumbo, ya mbuzi...ya ng'ombe hali kadhalika..
 
Halafu sasa:
....zamani tulipokuwa tunataka kuona masaburi (ya Ke) ilitubidi kuhakikisha tunaliondoa vazi hili kwanza, siku hizi ni kinyume; vijana hamuwezi kuliona vazi hili hadi mmenye masaburi. Design ya hii kitu imebadilika mno!
 
Kitu kingine:
Hili vazi lina sifa kuu moja (ukiacha sifa nyingine ndogondogo):

.....Ni vazi la kwanza kuvaliwa na la mwisho kuvuliwa (tusibishane hapo!).

Sio kwa wavaa sketi na gagulo, huku hakuna utaratibu maana hakuna kikwazo.
 
Hahahhaaha....Huyu hataikiwa na matobo hatupi...ndo maana anakwambia anaianika uvunguni. Ana balaa huyu!!!!

Wala hana hasara hizo zenye matobo anazozihifadhi zikijafika 50 pc's anazifua na kuziungaunga na ku'make Chandurua hatokua na job ziada kutoboa matundu.
 
Mi nakataa! Hili vazi halinunuliwi kwa siri..otherwise lisingeuzwa hadharani.
Kwa anaeheshimu utupu wake hawezi akavaa chupi hadharani au kuivua hadharani...Hata nguo za kawaida sidhani unazivalia sebuleni au jikoni ndugu yangu...

Sehemu za siri (ni kiungo cha aibu)zinaheshimika..ndio maana huwezi ukapita mtupu mbele za watu unless ni mumeo/mkeo. Kuhusu kufuliwa,inaweza ikafuliwa kwa siri ila kuanikwa inatakiwa ianikwe kwenye jua..utatengeneza hata kamba ya kauanika nyuma ya nyumba.

Na kutupwa ni vizuri ikatupwa kwa siri tena huku ikichomwa moto ni vizuri zaidi..

Labda sehemu zako za siri ndo kiungo cha aibu, unajua maana ya aibu ni nini ? mimi nijuavyo kitu cha aibu ni kitu ambacho hustahili kuwa nacho na kama unacho hutaki watu wajue kama unacho. viungo vyetu vya uzazi sio sehemu za siri, kwa sababu teyari tunajua tunavyo na tunajua vilipo sasa siri iko wapi, sio viungo vya aibu kwa kuwa ni haki yetu kuwa navyo.

Kuficha viungo vya uzazi, haina maana kuwa ni siri au aibu, ila ni utamaduni wa kimaumbile, mwanamke au mwanaume anapotoka na mwenzake kwa mara ya kwanza hata kama wamejuana within a day, wanapovua nguo wala hawashangaani wala kuoneana aibu.
 
Vipi wale wamama wanaowapa mahausigeli wao wawafulie mavazi yao na mavazi wa wenza wao..!?
 
Hili vazi linashangaza kweli!
Dukani linauzwa hadharani.
Wakati wa kununuliwa linanunuliwa kwa siri.
Wakati wa kuvaliwa linavaliwa kwa siri na linavaliwa sirini.
Linaficha siri.
Linafuliwa na kuanikwa kwa siri.
Linapochakaa linatupwa kwa siri.

Kwa nini limekuwa la siri kiasi hiki?

Badidilika ndugu yangu. Hakuna siri juu ya chupi kwani watu wanajua kuwa mtu ni lazima avae chupi. Chupi ni vizuri ikaanikwa juani ili ikauke kwa jua. Hiyo ni nzuri kwa afya ya mtumiaji.
 
chupi za watoto zenyewe hazina tatizo...Hapo ndio utajua jinsi MAWAZO yanavyoumba. Wengine wametangulia mbele zaidi...nywele,miguu navyo vimewekwa kundi hili la chupi,yaani visionekane wazi kwani vitakufanya uwe na matamanio. Mimi naenda mbele hatua kumi:hata Mungu unayemfahamu alitengenezwa mawazoni kama chupi...usihamaki hebu rudia kusoma. Mungu ambaye ana kiberiti na petroli, ambaye hata kama ulikufa kwa ajali ya moto lazima akupe mwili upya ili akuchome yeye afurahi...
 
Badidilika ndugu yangu. Hakuna siri juu ya chupi kwani watu wanajua kuwa mtu ni lazima avae chupi. Chupi ni vizuri ikaanikwa juani ili ikauke kwa jua. Hiyo ni nzuri kwa afya ya mtumiaji.

Na kwa bahati mbaya ikaanguka halafu akaiokota yule mtoto wako mtukutu na kuanza kuzunguka nayo mtaani!?
 
Back
Top Bottom