MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,563
Mwanza kubwa Majimoto, ni sehemu gani?Malango saba ya kuzimu yalifungwa rasmi kwa moto mwezi uliopita, mashimoni walikuwepo maelfu ya watu walioenda huko kutafuta msaada wa kichawi kwa mungu wa dunia.
Maelfu ya majini ya kuzimu yalikuwa duniani yakifanya uchawi na yameshindwa kurudi baada ya malango yao kufungwa kwa moto.
Kisa cha huyu dada ni moja ya matokeo yasiyo ya kawaida ambayo yatatikisa Tanzania kuanzia sasa, huyu dada uwezekano wa kurudishwa upo.
Kwa sasa yapo magari mazuri sana kutoka kuzimu yanatembea barabarani, yakiendeshwa na majini, usikubali kutoa lift au kupewa lift kabisa kwa mtu usiyemjua.
Malango saba ya kuzimu yaliyofungwa ni haya:
1. Lango la kuzimu la salender bridge - Dar es Salaam, lipo kati ya daraja la salender na bomba la maji machafu, karibu na hospitali ya Ocean road. Mlinzi wa lango hili alikuwa akiitwa Mustara akisaidiwa na majini 12.
2. Lango la kuzimu la Tabora mjini. Lipo karibu na soko kuu la Tabora mjini. Mlinzi wa lango hili alikuwa akiitwa Swahirani akisaidiwa na majini 12.
3.Lango la kuzimu la Tanga, Pangani. Mlinzi wa lango hili aliitwa Rajuni akisaidiwa na majini 12.
4. Lango la kuzimu la Bagamoyo, lipo baharini. Mlinzi wa lango hili aliitwa Zazuni, akisaidiwa na majini 12.
5. Lango la kuzimu la Mwanza. Mlinzi wake aliitwa Gharik akisaidiwa na majini 12
6.Lango la kuzimu la Kigoma, lipo Kibirizi. Mlinzi wake aliitwa Jarafu akisaidiwa na majini 12.
7. Lango la kuzimu la Iringa, Njombe, lipo eneo la Igosi. Mlinzi wake aliitwa Twafifin, akisaidiwa na majini 12
Malango yote haya yamefungwa kabisa, wale wote waliokuwa ndani ya mashimo haya ya kuzimu wakitafuta uchawi wataendelea kubakia huko.
Mizimu iliyokuwa duniani yakakuta malango yamefungwa wameshindwa kuingia, na wana ghadhabu kubwa, lakini vyovyote iwavyo, moto wa Mungu unawawakia.