Sio kila ombaomba anahitaji msaada- be careful

Hii stori ni nzito sana, inakuaje hatujasikia kuhusu ndugu wa huyo dada wakiongelea hili au kumtafuta? Na hii stori inasema kulikuwa na shuhuda ambaye ni trafiki,vipi hatujasikia lolote kutoka kwa huyu trafiki,manake hii si stori nyepesi nyepesi? Vipi hata magazeti ,especially ya udaku hayana hii stori mpaka sasa? Just curious
 
Conventional wisdom ninayofuata ni kuwa, kama tunavyopiga chenga kuwapa lifti tusiowafahamu au hata wake/mabinti wa majirani zetu, ndivyo hivyohivyo tunavyopaswa kutotoa nafasi ya kugusana na tusiowafamu au hata kusikiliza hadithi zisizoelekea. Si katika kuogopa ushirikina tu. It's becoming a crude world indeed.
 
Story hii inawezekana kuwa ya kweli, lakini naomba kufahamishwa kama kuna taarifa zozote za kipolisi kuhusiana na tukio hilo, taarifa za ndugu au majirani wa mhusika aliyepotea, ushahidi wa mwenye gari aliyekuwa nyuma yake, uhakika wa gari lenyewe isijekuwa hata gari lenyewe ni magumashi tu, je, TRA wana taarifa za hilo gari? n.k.
 
Hii habari ni kweli mimi nillipata habari hizi siku hiyo ilipotokea, Kimsingi ni kwamba hapa Tanzania kuna MILANGO SABA YA KWENDA KUZIMU.
Moja ya malango hayo lipo pale Salender umbali kidiogo kutoka kwenye daraja.
Biblia iliongelea haya malango MATAYO 16:18‘‘Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda.

Lango hilo linaitwa MUSTALA
Mustala lina aina 12 za walinzi wa kimajini, Yafuatayo ni majina ya hayo majini na kazi zao walizopewa kuwatesa wanadamu.Kimsingi huyo dada alichukuliwa na moja ya kati haya majini yafuatayo

1) KHATAFAR.
Majukumu ya jini hili ni

Linasimamia laana za ukoo.

2)MUZAPHAR

Linakwamisha kila kitu ambacho kinaweza kumletea mtu maendeleo kama likitumwa kwako

3)LADWIFU

Linasimamia
Mateso
Ufukara
Kupotea pesa bila kujua zilikokwenda

4)JAJUNI
Linawafanya wanawake kula udongo

5)JAKHARI
Hutorosha mali pia huzuia wateja wasije kwenye biashara yako

6)KHASINANI
Hili jini hutupiwa wanaume na linasimia mambo yafuatrayo
Sigara
Pombe
Madawa ya kulevya
Fujo
Mateso mbalimbali

7)JUBELI
Husababisha utasa kwa wanawake!!!!!!!!!!DSM ?

8)SIFAFINO
Linasimamia ukahaba both Male and F

9)SUBIANI

(a)Husababisha ajali. Linapenda damu na ndiyo chakula chake likitumwa lazima litengeneze ajali ili lipate kula.
(b)Husababisha wanawake wasione siku zao, linaivyonza hiyo damu.
(c)Husababisha maumivu sana siku za mwamke zikifika
(d)Some time husababisha mwanmke atokwe na damu kupita kiasi

10)SUMEL
Hili jini huangamiza mimba, mimba kutoka mara kwa mara.hata watoto wanao kufa wakati wa kuzaliwa huwa linawachukuwa.

11)MUNSAR
Linasababisha ushoga na usagaji

12)WAIDADAT
Hutumwa kwa wanume tu.

Husabaisha kuvaa hereni na kusuka rasta kwa wanaume.

Habari hii nimeiandika ili mtambua kuwa vita yetu si juu ya damu na nyama bali ni ya kiroho. Na VITA ili ushinde yafaa uzijue mbinu za adui yako ambaye ketu ni shetani

Malango sita yaliyobakia nayaifadhi ila ukitaka kujua yako wapi na aina za majini yanayomiliki na madhara yake kwa binadamu NITAFUTE KWA MUDA WAKO.

Hapo kwenye red fonts hapo.,BWABWA apaangalie sana.
 
Story hii inawezekana kuwa ya kweli, lakini naomba kufahamishwa kama kuna taarifa zozote za kipolisi kuhusiana na tukio hilo, taarifa za ndugu au majirani wa mhusika aliyepotea, ushahidi wa mwenye gari aliyekuwa nyuma yake, uhakika wa gari lenyewe isijekuwa hata gari lenyewe ni magumashi tu, je, TRA wana taarifa za hilo gari? n.k.

You are There Man!!
Yaani magezeti yote haya hata moja likose kuandika hii habari?
Binafsi sikubali. Hii habari kama Ndoto vile.
Lets just think again jamani.
Kwanza huyu dada lazima angushuka kwenye gari aanze kupiga mayowe mpaka walioko Ubungo wasikie.
pili huyu dada asingembusu jamaa
Hii story utafikiri movie za jack chan.. (The medalion)
 
kwa udaku wa town tena pale sal bridge weee mji mzima tungejua mda huo huo!!pia tungepata taarifa za dada aliepotea kimiujiza, aagh hii imetungwa kama kesi ya Jery Muro!!
 
Dada huyo kwa kumhurumia akamsaidia. Alipompa pesa tu mkono wa yule dada ukaota manyoya ya paka, akachanganyikiwa alipokuwa anaendelea kushangaa trafiki akawa anaruhusu magari ya upande wake yule dada akawa hawezi kuendesha gari, ndipo trafiki akamsogelea na kuuliza kulikoni?!

unatofautishaje manyoya ya paka na ya sungura, mbwa, kicheche, n.k. ulikuwa karibu kiasi gani hadi kujua ni ya paka?
 
Conventional wisdom ninayofuata ni kuwa, kama tunavyopiga chenga kuwapa lifti tusiowafahamu au hata wake/mabinti wa majirani zetu, - hapa sasa unataka kutuambia nini? kwamba ukiwapa lift wanawake hata kama ni mabinti na wake za majirai zako uta(&*&#%& sio?, yani huna self control hata kiduchu? ndivyo hivyohivyo tunavyopaswa kutotoa nafasi ya kugusana na tusiowafamu au hata kusikiliza hadithi zisizoelekea. Si katika kuogopa ushirikina tu. It's becoming a crude world indeed - Hapa nakubaliana na wewe.

check kwenye red na italics. strange people, strange world!
 
kama ni kweli basi usiombee ikukute au umkute mtu inamtokea, ni hatari sana
 
Usalama ni kuwa na Mwokozi ndani ya mioyo yetu, yeye yuko juu ya mashetani. Ukimwamini Kristo Yesu, shetani hawezi kukufanya chochote, na kama Mungu akiruhusu shetani akuguse basi ujue ni kwa ajili ya maepenzi yake, ila mwisho wa yote kuna uzima wa milele. Huyo dada kupotea, ni sawa na vile ambavyo watu wanaweza kupotelea angani baada ya ndege kupata ajali, swali ni kwamba, what next? Kama ulikuwa ndani ya Kristo, nakuhakikishia kuwa uzima wa milele una wewe.
 
Naona kuna watu humu wameshaingia kingi. Badala ya kuulizia originality ya habari nzima wao wanaitilizia zege kabisa na wengine kujaribu kuanzishia episode 2 ..lolz

Kaaz kwelikweli.
 
Hii habari ni kweli mimi nillipata habari hizi siku hiyo ilipotokea, Kimsingi ni kwamba hapa Tanzania kuna MILANGO SABA YA KWENDA KUZIMU.
Moja ya malango hayo lipo pale Salender umbali kidiogo kutoka kwenye daraja.
Biblia iliongelea haya malango MATAYO 16:18‘'Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda.

Lango hilo linaitwa MUSTALA
Mustala lina aina 12 za walinzi wa kimajini, Yafuatayo ni majina ya hayo majini na kazi zao walizopewa kuwatesa wanadamu.Kimsingi huyo dada alichukuliwa na moja ya kati haya majini yafuatayo

1) KHATAFAR.
Majukumu ya jini hili ni

Linasimamia laana za ukoo.

2)MUZAPHAR

Linakwamisha kila kitu ambacho kinaweza kumletea mtu maendeleo kama likitumwa kwako

3)LADWIFU

Linasimamia
Mateso
Ufukara
Kupotea pesa bila kujua zilikokwenda

4)JAJUNI
Linawafanya wanawake kula udongo

5)JAKHARI
Hutorosha mali pia huzuia wateja wasije kwenye biashara yako

6)KHASINANI
Hili jini hutupiwa wanaume na linasimia mambo yafuatrayo
Sigara
Pombe
Madawa ya kulevya
Fujo
Mateso mbalimbali

7)JUBELI
Husababisha utasa kwa wanawake!!!!!!!!!!DSM ?

SIFAFINO
Linasimamia ukahaba both Male and F

9)SUBIANI

(a)Husababisha ajali. Linapenda damu na ndiyo chakula chake likitumwa lazima litengeneze ajali ili lipate kula.
(b)Husababisha wanawake wasione siku zao, linaivyonza hiyo damu.
(c)Husababisha maumivu sana siku za mwamke zikifika
(d)Some time husababisha mwanmke atokwe na damu kupita kiasi

10)SUMEL
Hili jini huangamiza mimba, mimba kutoka mara kwa mara.hata watoto wanao kufa wakati wa kuzaliwa huwa linawachukuwa.

11)MUNSAR
Linasababisha ushoga na usagaji

12)WAIDADAT
Hutumwa kwa wanume tu.

Husabaisha kuvaa hereni na kusuka rasta kwa wanaume.

Habari hii nimeiandika ili mtambua kuwa vita yetu si juu ya damu na nyama bali ni ya kiroho. Na VITA ili ushinde yafaa uzijue mbinu za adui yako ambaye ketu ni shetani

Magnifico_Orallee!

Sasa hebu tupe reference ya uliyoongea ili tuende wenyewe tukasome hayo unayoyaongelea.

Malango sita yaliyobakia nayaifadhi ila ukitaka kujua yako wapi na aina za majini yanayomiliki na madhara yake kwa binadamu NITAFUTE KWA MUDA WAKO .

Mnapotangaza biashara zenu JF mjitahidi kidogo kutoa japo mrahaba kuwezesha jamvi kuendelea kudumu hewani.
 
Natumaini kwa uwezo wa Mungu mko wazima,

Leo kwenye misa ya asubuhi kanisani Azania Front mchungaji aliyekuwa anahubiri katufunulia siri nyingi sana za sheteni nakutupa shuhuda mbalimbali jinsi shetani anavyofanya kazi.

Moja ya ushuhuda wake ni kisa kilichotokea hivi karibuni hapa Dar es salaam. Napenda nikushirikishe ili uchukue hatua.

Pale salender Bridge ambapo anasimama trafiki akivuta magari, kuna mdada alikuwa ndani ya gari lake kwenye foleni akisubiri zamu yake ya kuruhusiwa na trafiki ifike apite. ndipo aliposogea kaka mmoja ombaomba, akasogea kwenye gari la yule dada na kuomba msaada.

Dada huyo kwa kumhurumia akamsaidia. Alipompa pesa tu mkono wa yule dada ukaota manyoya ya paka, akachanganyikiwa alipokuwa anaendelea kushangaa trafiki akawa anaruhusu magari ya upande wake yule dada akawa hawezi kuendesha gari, ndipo trafiki akamsogelea na kuuliza kulikoni?!

Yule dada akatoa mkono wake na kumuonyesha trafiki na kumsimulia kilichotokea na bahati nzuri yule kaka aliepewa pesa alikuwa mita chache pembeni anamuangalia yule dada. Ikabidi trafiki aende kumuuliza yule ombaomba kulikoni?

Ndipo yule ombaomba akamwambia trafiki kuwa yule dada akimbusu tu atapona mkono utarudi kawaida. Basi ikabidi yule dada atelemke aende kumbusu yule kaka, alivyombusu wakapotea wote palepale, gari ya yule dada ikabaki barabarani ndipo trafiki alipoita watu wakaanza kuisukuma ile gari na kuiweka pembeni.

Kuna dada mwingine alikuwepo leo kanisani baada ya ibada akawa anatusimulia, yeye alikuwa nyuma ya gari ya huyo dada alishuhudia hilo tukio anasema ni tukio la kweli kabisa ameshuhudia kwa macho yake.

Hivyo jamani nawatahadharisha ndugu zangu mlio na moyo wa huruma msipende kutoa pesa zenu hovyo sababu umekutana na maskini.

Biblia inasema maskini wapo na wataendelea kuwepo, mwombe Mungu kwanza kila unapotaka kutoa sadaka yako. Mwenye Masikio na Asikie
Baada ya mchungaji kumaliza misa,kwakuwa mimi ni mtu wa karibu sana na mchungaji alinipigia simu na kuanza kunihadithia kuwa,makusanyo ya sadaka kanisani hayaridhishi kwa sasa,na tatizo inaonyesha kuwa waumini wamekuwa wakitoa pesa sana kwa ombaomba kuliko kanisani,hivyo aliamua kubuni kisa kitakacho wakomesha tabia yao hiyo na kuendelea kutoa sadaka kama kawaida.Na kuhusu huyo dada aliyetoa ushahidi,mchungaji alinigusia kuwa huyo ni mtunza hazina msaidizi wa kanisa,hivyo hiyo ilikuwa ni njia tuu ya mchungaji kutengenezea ndama wake malisho!!Yapaswa ikumbukwe pia utaulizwa nilikuja pindi nlipokuwa na kiu,ukaninyima maji!!Mwisho yatupasa tujifunze kusaidiana hasa ktk nyakati hizi ngumu!!
 
MchajiKobe mh kachaji hayo mawazo upya bana, hii nilianza kuisoma kwa michuzi jana nadahni imekuja kama ilivyo huku. Haya mambo so mchezo. au ni ajenda za kuwabania riziki hawa omba omba?
 
Mbura wewe ni mganga wa kienyeji au jadi? Manake nasikia sikui hizi eti mnatofautisha hao watu. Na swali lingine nauliza kwa wote huyu dada kapotea au kafa?
 
Back
Top Bottom