Wasafiri wa ndege kuweni makini na wizi kwenye ndege

ZINDAGI

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
1,117
1,424
Huu ni mkasa uliotokea leo kwa abiria mmoja aliesafiri kwa ndege ya Oman Air iliyowasili leo alfajiri.

Kwa kuwa ndege ilikua haikujaa, abiria mmoja aliamua kulala ktk siti 3, baada ya kuwa hewani kwa masaa kadhaa huku amelala akasikia abiria wa nyuma yake analalamika begi yake ya mkononi (hand luggage) imefunguliwa na kwa bahati nzuri hakuna kilichoibiwa, ndipo yule abiria wangu na yeye akaamka na kuangalia begi yake ipo katika hali gani, alivyoangalia begi yake akakuta imefunguliwa na pesa na saa yake vyote vimeibiwa.

Wafanyakazi wa ndege wakatangaza kuna abiria ameibiwa hivyo ndege hii ilikua ishushe abiria Zanzibar na itaelekea moja kwa moja Dar ili abiria wote wachekiwe.

Baada ya tangazo hili, abiria mmoja wa ki-China akaanza kuwa na wasiwasi, akawa restless anataka kwenda chooni, akazuiliwa na vyoo vote vikawa locked.

Wakati wote huo wafanyakazi wa ndegeni walikua wanamfuatilia yule mchina.

Ndege ilipofika Dar, askari wa uwanja wa ndege wakaitwa na kuingia ktk ndege, wakati watu wamesimama wakamuona yule mchina anahamisha zile pesa na saa ktk begi la dada mmoja alilovaa mgongoni, basi wale wafanyakazi wakawaambia wale askari suspect wetu ni huyu na hizo pesa na saa kaziweka ktk begi la huyu dada.

Maskini ya Mungu dada wa watu alistuka sana, yule mwenye pesa zake a saa akaambiwa ataje kiasi na aina ya saa vilivyoibiwa, maelezo yaliyotolewa yakawa 100% sawa na vitu vilivyokutwa. Mchina akachukuliwa na abiria mwenzake wapo Airport Police.

Hii ni mara ya pili nashuhudia wizi wa namna hii kutoka kwa waChina, niwaombe mchukue tahadhari mnaposafiri.

Siku njema
 
Huu ni mkasa uliotokea leo kwa abiria mmoja aliesafiri kwa ndege ya Oman Air iliyowasili leo alfajiri.
Kwa kuwa ndege ilikua haikujaa, abiria mmoja aliamua kulala ktk siti 3, baada ya kuwa hewani kwa masaa kadhaa huku amelala akasikia abiria wa nyuma yake analalamika begi yake ya mkononi (hand luggage) imefunguliwa na kwa bahati nzuri hakuna kilichoibiwa, ndipo yule abiria wangu na yeye akaamka na kuangalia begi yake ipo katika hali gani, alivyoangalia begi yake akakuta imefunguliwa na pesa na saa yake vyote vimeibiwa.

Wafanyakazi wa ndege wakatangaza kuna abiria ameibiwa hivyo ndege hii ilikua ishushe abiria Zanzibar na itaelekea moja kwa moja Dar ili abiria wote wachekiwe.
Baada ya tangazo hili, abiria mmoja wa ki-China akaanza kuwa na wasiwasi, akawa restless anataka kwenda chooni, akazuiliwa na vyoo vote vikawa locked.

Wakati wote huo wafanyakazi wa ndegeni walikua wanamfuatilia yule mchina.
Ndege ilipofika Dar, askari wa uwanja wa ndege wakaitwa na kuingia ktk ndege, wakati watu wamesimama wakamuona yule mchina anahamisha zile pesa na saa ktk begi la dada mmoja alilovaa mgongoni, basi wale wafanyakazi wakawaambia wale askari suspect wetu ni huyu na hizo pesa na saa kaziweka ktk begi la huyu dada.

Maskini ya Mungu dada wa watu alistuka sana, yule mwenye pesa zake a saa akaambiwa ataje kiasi na aina ya saa vilivyoibiwa, maelezo yaliyotolewa yakawa 100% sawa na vitu vilivyokutwa.
Mchina akachukuliwa na abiria mwenzake wapo Airport Police.

Hii ni mara ya pili nashuhudia wizi wa namna hii kutoka kwa waChina, niwaombe mchukue tahadhari mnaposafiri.

Siku njema
Namuonea huruma yule dada, kwanza anyone kana ni mgeni wa kusfiri, kama vile dada wa kazi anarudi nyumbani, vupi kama wale afanyakazi a ndege wasingemuona yule Mchina akimchomekea vile vitu
 
Back
Top Bottom