Wana jamvi nimekuwa nikijiuliza swali bila kupata jibu....kesho Mh jakaya mrisho kikwete atahutubia bunge...swali langu, je, wabunge wa chadema watatoka bungeni kama kawaida yao au itakuwaje? nawasilisha!
Sababu ya kutoka mara ya kwanza ilikuwa nini?...Huwa hawatoki bila sababu.Nadhani huwa inakuwapo sababu ya msingi kufanya hivo.
Wana jamvi nimekuwa nikijiuliza swali bila kupata jibu....kesho Mh jakaya mrisho kikwete atahutubia bunge...swali langu, je, wabunge wa chadema watatoka bungeni kama kawaida yao au itakuwaje? nawasilisha!
Mimi namuunga mkono, mtoa mada, ameuliza swali zuri sana, ila majibu aliyoyapata sio ya kistarabu hata kidogo, kutakana na majibu ya wachangiaji walionitangulia hapo juu, nimejifunza ama kulielewa na kugundua jambo, kwamba mjinga mwelimishe, mpumbavu mwache na upumbavu wake, asiyejua mjulishe, na asiyeelewa mweleweshe. Nami natarajia kesho kwa umakini na makisio makubwa kwamba wabunge wote wa chadema watatoka nnje na kama sivyo watakuwa hawana tofauti na john shibuda na jose selasini wa huko rombo, maisha na mfumuko wa bei, madaktari kugoma n.k, haviwezi kuwaruhusu wabunge makini kukaa kimya kusikiliza upupu wa kikwete. Naunga mkono mtoa hoja 50 kwa 100, na baadae kadri tunavyoendelea kuijadili nitaiunga mkono 100 kwa 200.
Unaonekan kusumbuliwa na mchecheto na umbeya kuliko mgando wa busara. Ungekuwa na akili ungekumbuka kuwa wabunge wa Chadema walitoka wakati wa hotuba ya Kikwete wakati ule kuonyesha kuwa hawakuridhika na mchezo uliofanywa na tume ya uchaguzi katika kura za urais. Hawakusema kwamba hawatambui uwepo wa rais katika nchi, jambo ambalo hata Kikwete mwenyewe alishindwa kuligundua akaishia kutoa mistari ya taarabu.
Kwa akili zako wewe na mleta mada mnaweza kutaja sababu ya msingi ya wabunge wa Chadema kutotaka kuhudhuria hotuba Kikwete atakayoitoa?
Halafu je, unafahamu hotuba yake itazungumzia nini?