Simulizi: Harakati za maisha

SEHEMU YA SABA

Gari ilisereka kidogo huku ikihama njia kabisa, Kisha nikatulia huku ng'ombe wengi sana wakipita, kulikuwa watu zaidi ya kumi na tano jamii ya wamang'ati wakiwa wanaume kwa wanawake huku wakionesha wanahama.

Sasa shemu Hawa watakuwa wanaenda wapi usiku huu, jamani tena wana watoto mgongoni, kwanini watembee usiku? yule mwanamke aliongea kwa mshangao sana.

Baada ya kuwa ng'ombe wamepita nilikanyaga mafuta huku nikiongeza speed tofauti na mwanzo, nafikiri yule mwanamke alikuwa ana hofu sana juu ya uendeshaji wangu lakini hakuwa na namna hangeweza kuniambia chochote.

Nadhani zile beer nne zilishachukua nafasi fulani kichwani nikakuta naanza kumtamani yule mwanamke, nikapanga lazima nitafute sababu yeyote ile ili tulale na najua naweza kufanya chochote na asinipinge nilijiamini sana.

Heeeeh shemu ina maana tushakaribia daraja la mkapa, umetembeaaaa, alisema yule mwanamke huku mwanga wa gari linalokuja mbele yetu likiwa Ukiwa unamtesa sana.

Yaani kuna watu sijui walisomea wapi udereva yaani anawasha taa namna hiyo tena tupo katikati ya daraja, namuashiria apunguze mwanga hataki,haya ni madhara ya kujulia gari mtaani kisha kupata leseni kwa njia ya magumashi hawa ndiyo wanaosababisha ajali kila kukicha. nililaumu .

Akili yangu juu ya yule mwanamke ilikuwa palepale lakini na ugumu nao ulikuwepo hivyo niliona siwezi kumuacha hivihivi ikabidi nianze kutafuta visingizio.

Yaani gari hili shemu silielewi kabisa , yaani breki inashika kwa mbali sana na muda mwingine nakanyaga hamna kitu kabisa na usiku huu tena sijui itakuwaje, afadhali ingekuwa mchana ningekokota hivihivi lakini usiku huu hapana. Yaani hizi gari za kupokezana mara aendeshe huyu mara yule ni shida sana. nilijifanya gari ni mbovu.

MUNGU wangu sasa itakuwaje shemu maana, mbona nitakuja kugawanywa vipande masikini mimi, shemu huwezi simama popote ili wakuangalizie nini tatizo?
alihoji yule mwanamke.

Hilo hakiwezekani shemu, kwanza kwenye vijiji hivi vya njiani hakuna mafundi wala gereji za kueleweka, hivyo unaweza Kuta unazidi kuipa matatizo zaidi gari ya watu. vyombo vya serikali hivi huwezi kubumba bumba ujuavyo wewe. nilizidi kujitengenezea mazingira.

Ndani ya muda mfupi tulikuwa Ikwiriri, nikapaki gari pembeni huku nikishuka,
Shemu twende tukapate chochote kitu basi, maana mimi naona tumbo halina kitu nilimsihi.

Shemu yaani acha tu hapa nilipo sina hata njaa, siisikii kabisaaa, naona kama nimechanganyikiwa tu, yaani hii siku ya leo nitasimulia jamani.
aliongea kwa uchungu huku akiwa kama vile kagundua Nia yangu ila akashuka kwenye gari na kuiegamia.

Niliingia bar ya pale njiani wanapaita Kivulini, nikaketi na kuulizia Chakula nikaletewa nikapiga huku nikimuona vizuri sana yule mwanamke ambapo simu ilikuwa sikioni akionekana anapiga huku na huko , alionekana mwenye haraka sana na hakupenda kitendo cha mimi kusimama pale ila hakuwa na namna.

Ubishani ulioendelea pale Kivulini bar kuhusu Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Rufiji ambaye alikuwa chama tawala huku wakidai hawamfahamu na si mzaliwa wa pale, ule mjadala ulinivutia sana nikatamani kujua japo A B C kadhaa, hivyo nikajisogeza kumsikiliza jamaa mmoja ambaye alikuwa anawashawishi wenzake kuwa wasije wakampa kura hata moja

Simu yangu iliita , kuangalia namba ni yule mwanamke ambaye tulipeana namba kwaniaba ya kwenda kumchekia mifugo yake,

Hello shemu, samahani lakini nilikuwa naomba uniruhusu niondoke kwasababu ninatakiwa nifike leo hii hii sitakiwi kulala njiani kabisa, naziona Coaster zinazofika mpaka Mbagala rangi tatu hivyo , nakushukuru kwa msaada wako . aliweka kituo akiwa ananipa nafasi labda niongee chochote lakini nilikata simu.

Huyu demu vipi naye, anawahi wapi?
Saa tatu hii si bora tulale tu ,
Nilimuita muhudumu nipewe bia yangu ili nishushie na Chakula nilichokula, huku nikisikia simu inaita kwa mara nyingine, kuangalia mpigaji ni yeye lakini sikupokea lengo nimcheleweshe ili tulale wote.nilijua asingeondoka kwani begi lake lilikuwa kwenye gari.

Nilimaliza bia kwenye glass Kisha nikaingia msalani, Kisha nikaenda kwenye gari huku nikiacha bia nyingine ikiwa haijafunguliwa nikakuta mwanamke kabadilika sana, uso wake haukuwa na masikhara hata kidogo.

Samahani kaka yangu naomba nipe begi langu siwezi kukaa kama vile yatima aliyefiwa na wazazi wote wawili naomba niondoke bwana, yaani unanifanyia visa kibao mara gari haina breki mara sijui kitu gani halafu unashuka unastarehe tu, wewe ni mwanaume unaweza kujiamulia mambo mengi, lakini Mimi ni mke wa mtu nipo kwenye himaya na miliki ya mtu hivyo naomba tuheshimiane. aliongea huku akiwa serious na sauti ya juu huku akionesha amechukia.

Hapana Shemu usiseme hivyo, lakini kwani Kuna ulazima wa wewe kufika leo, kesho alfajiri tutajihimu shemeji yangu, Mimi nipo na chombo Cha watu ambacho nina tahadhari nacho,nikipata ajali usiku huu itakuwaje? Vitu vingine vinazuilika shemu. hebu twende ukale kabisa shemu usijisikie vibaya bwana. nilimwambia lakini hakuwa tayari alikataa katakata huku akiomba nimpatie begi lake.

Nilikuja nikamalizia bia huku nikimuona, anaongea na wanaume watatu ambao sikujua wamefikaje pale labda kwakuwa nilikuwa tungi,

Kisha baada ya kumalizana na wale jamaa ambapo sikujua wameongea nini, akawa anakuja usawa nilipo akaingia , huku akikaa meza nyingine akionesha ana mawazo sana. wakati huo mimi moyo ulidunda kwa furaha maana dhamira yangu ilikuwa inakwenda kutimia , aliagiza chipsi kavu na soda tu, Kisha alipomaliza akaja kwangu kwa mwendo wa madaha kabisa , mwanamke mrefu sura isiyokuwa na makeup, huku akiwa kavaa tisheti nyeupe na suruali nyeusi iliyomkaa vyema sana huku akiwa kavaa raba fulani za kike nzuri sana, akiwa kajifunga kanga yake kiunoni.

Ahsante sana Kwa chakula shemu , aliongea huku akiwa kasimama pembeni yangu , huku nikimkung'uta vumbi vumbi lililonasa kwenye nguo zake, hakika nilienjoy maana nilimshika popote huku akiwa haoneshi kuchukia, alitabasamu tu, laiti ningejua mawazo yake.ama kweli mjinga hajijui.

Sasa vipi si tunalala shemu, niliuliza kwa sauti ya kilevi .

Hakuna shida shemu wewe si umesema si vizuri kutembea usiku, hivyo nimeridhia kulala, na pia nishaulizia na lodge nimeambia ipo ambako Kuna parking za magari na pia ni self hivyo nahisi ni pazuri twende huko.
Aliongea kwa kudeka huku akichochea hisia zangu, nilimaliza bia kwa pupa huku tamaa ya ngono ikishika nafasi yake.

Niliendesha gari huku nikiwa naulizia kwa watu ambalo walionesha kuwa ni paleeee kwenye taa za kuzunguka , baada ya kufika alishuka haraka sana kwenye gari.

Shemu paki gari vizuri, Mimi ngoja nikachukue chumba , aliongea Kisha nikamuona anaelekea mapokezi,
Mlinzi alinielekeza sehemu ya kupaki huku akiniuliza kama nitatoka asubuhi sana basi nipaki karibu na geti na gari iangalie nje.huku nikimshangaa yule mlinzi anavyonichelewesha kila napopark anasema siyo, hali ile ikafanya nichelewe kidogo,

Kisha kwa mbwembwe na tembea ya kilevi nikaenda mapokezi, huku nikivuta picha yule mwanamke ambavyo atakuwa kashabadilika huko chumbani.

Kuna mwanamke kaingia siyo muda hapa kavaa (nikiwaambia alivyovaa)

Ndiyo kaingia kwani unamuitaje, aliuliza yule dada wa mapokezi.

Ni mke wangu yule,. nilidanganya

Weee acha uongo yule siyo mkeo na katuambia Kila kitu na Kuna watu walikuja kumchukulia chumba hapa,
na anadai wewe unataka kulala naye wakati yeye hayupo tayari, hivyo uchukue chumba chako ulale au uondoke, na ukilala hapa hatutaki fujo , tutapiga simu polisi. aliongea yule dada wa mapokezi huku nikishangaa sana , Kisha nikapiga namba ya yule mwanamke ikawa haipatikani. nilichukia sana na pombe zikakata

Itaendelea.......................
 
Askari analinda ndoa yake,jamaa asipokuwa makini atapata mkong'oto hatari .
Heri awashe gari asepe
 
SEHEMU YA NANE

Oyaa bro naomba nifungulie geti nitoke . Nilimlazisha mlinzi.

Aaah kaka, huu usumbufu sasa, wapi unaenda, ila nimejua kumbe kweli ulitaka kumbaka yule mwanamkeee, we jamaa kumbe fala eeh, yaani wanawake wooote waliojaa miaka hii unalazimisha mapenzi halafu ulivyo na nilichosikia hata haviendani.
aliongea yule mlinzi huku akinimulika na tochi yake usoni.

Hebu usinimulike bwana, hebu fungua geti na aliyekwambia nilikuwa namfuata mwanamke hapa ni nani, fanya habari zako, wewe kazi yako ni kufungua na kufunga geti acha upuuzi. nilitoa gari huku mlinzi akiendelea kunirushia maneno.

Kwahiyo kupewa na kuendesha magari ya serikali unajiona nani sijui, unafikia hatua ya kudhani Kila mtu atakupenda kisa gari, wewe ni mjinga tu lione kwanza. alikuwa ni dada wa mapokezi akiungana na mlinzi wakinitukana. hakika ilikuwa ni fedheha ya aina yake.

Nilitafuta gesti nyingine huku nikiwaza alichonifanyia yule mwanamke, hakika alikuwa kaniweza sana na sikutegemea kabisa.

Asubuhi na mapema niliamka na kuoga vizuri kisha nikawasha chombo na kuingia njia kuu huku nikiwa high speed lengo niwahishe gari ofisini.
Nikiwa njiani niliwaza sana,

Dah kiufupi heshima yangu imeshuka kwa nilichokuwa nataka kufanya Jana Sasa kwanini nilifanya vile dah kweli shetani ana nguvu sana.

Hivi kwa mfano yule mwanamke akanisimulia mumewe kuwa nilikuwa nataka kulazimisha penzi yule jamaa atanionaje halafu wanadai wote ni maaskari na Wana namba yangu, loh najuta kutoa namba, lakiniiiiiiii si rahisi mwanamke kusimulia kwa mumewe hizi habari labda kama hana akili timamu. nilijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.

Halafu umri wangu, cheo changu wala sipaswi kufanya mambo haya yaani kifupi jana nimechemka.nilijilaumu Kisha nikachungulia pembeni yangu kwenye siti ya abiria nikaona mfuko wa samaki pia nikauona mtandio wa yule mwanamke kumbe wakati anashuka Jana kwa pupa alijikuta anasahau vitu vyake.

Loh afadhali nimeona hivi vitu Sasa ndiyo mke wangu anauona huu mtandio itakuwaje na vile alivyo mbona nyumba itaharibika. nilichukua simu nikapiga namba ya yule mwanamke ikaita sana tu bila kupokelewa. nikaamua kuachana nayo huyooo nazidi kusogea , nilijua ndani ya masaa mawili nitakuwa Dar es salaam, baadaye simu iliita alikuwa ni mke wangu.

Tukasalimiana,
Enhee vipi jana watu tumekesha tukikusubiri nikijua atarudi, lakini haikuwa hivyo vipi kuna shida gani mume wangu. aliuliza

Wee acha tu mke wangu gari liliharibika likaja kupona usiku sana, hivyo nikaona siwezi kuendesha chombo ambacho Sina uhakika nacho kama kimetengamaa nikaamua nilale ila ndani ya muda mfupi nitafika hapo. Nilimjibu.

Haya pole na matatizo na nakuombea ufike salama, lakini Mimi nitatoka kidogo naenda kukutana na akina mama wenzangu si unajua tena kampeni zimepamba moto. na pia Mimi ni mmoja wa viongozi hivyo sipaswi kukosa. alisema huku akisikiliza nitasemaje.

Lakini mke wangu si nimekuwa nikikukataza hayo mambo ya vyama, hizo mambo kwanza huwa zinajenga matabaka mnajikuta mnachukiana bila sababu na watu, na pili sitaki mtu yeyote aijue familia yangu ipo chama gani, Sasa wewe kwenda huko pia mkapeana na uongozi yaani unanishangaza mno. niliweka kituo.

Mume wangu huwa nakushangaa sana tena sana tu, Kuna misimamo mingine sidhani kama ina ulazima sana, nakujua kuwa wewe huna kipaji cha siasa na pia na ndiyo maana umeshindwa ndani ya muda mfupi, lakini kila mtu ana kile ambacho ana interest nacho, na pia ni sehemu ambako unapanua wigo wa kufahamiana na watu kwani unadhani muda wote tutajadili jambo moja , Kuna watu tunakutana nao wenye ujuzi wa vitu mbalimbali, kilimo, biashara Kuna ufugaji na mambo mengi. Sasa mtazamo wako Mume wangu unanitisha.

Unadai hutaki matabaka na watu wasijue kwamba wewe upo upande gani,lakini tambua kuwa familia yetu ni ya kikristo, je wewe huelewani na watu?

Si unafanya nao kazi na watu wa Dini na madhehebu mbalimbali, kwa mara ya kwanza ulikuwa unafanya kazi ya umakenika kwa waarabu, je wale wengi wao si unajua Dini yao.
Huko uliko Sasa kwenye ajira yako boss wako ni wa Dini yako?

Mbona wewe hapa nyumbani unapenda mpira kuliko kawaida na hakuna anayekughasi, ungependa kiushabiki nisingesema lakini ulitoa pesa nyingi sana kwenye timu ya hapa mtaani kwetu, je ulipata faida gani? ile pesa ungefanyia mambo mengine si ungekuwa mbali?
Je nilikulaumu? si nilikushauri tu kuwa ni vyema kufanya tafiti za kutosha kabla ya kuanzisha mambo yako.
Hela zenyewe huna, inafikia hatua unapaki gari lako kwa kukosekana hela ya matengenezo ambayo ni kiasi Cha kawaida tu. ila nisiongee mengi si unarudi ninachokuomba ni ruhusa yako tu sitaki kwenda sehemu Ukiwa haupo radhi. aliweka kituo akiwa kanisimanga .

Haya wewe nenda ila zingatia muda na pia naomba heshima iwepo, mambo ya kupeana lift na watu nisiowajua sipendi na yule shoga yako mnene naye sihitaji mazoea ya kujakuja kwangu hapo najua huyo ndiye kakuvuta uende huko Sasa sitaki awe anakuja hapo kwangu kama siku ile. nilitahadharisha nikakata simu.

Baada ya muda niliona sms kutoka kwa mwanamke niliyekuwa naye Jana, akitaka nimpigie.
Nikapiga huku nikiwa na hasira nikipanga nimchane.

Niliangalia mfuko wake wa samaki nikaangalia na ule mtandio Kisha nikaguna kidogo huku nikiwa namsifu mbinu aliyotumia kwani alianza kwa kujilegeza kumbe kashapanga ni namna gani atanikataa. Huyu mwanamke loh simuwezi.

Akapokea simu na kunieleza kuwa yupo kwenye gari la abiria Coaster na nimewapita muda si mrefu ndiyo maana akanipigia ili nimsubiri achukue mizigo yake.

Nikaweka Chuma pembeni kisha nikashuka, nikaangalia saa ni saa moja kasoro. Huku coaster fulani ikiwa inapaki karibu yangu akashuka yule mwanamke huku konda akija kwa pupa kwenye gari yangu.

Oyaa sorry bro huyu dada anasema ana mizigo yake humu kwenye gari lako hebu nipe tuondoke maana tunakimbizana Kuna mchawi anakuja sitaki anikute hapa.

Itaendelea...............................
 
Mkuu shukrani,Leta vitu mzee baba
 
SEHEMU YA TISA

Panda kwenye gari shemu wala usijisikie vibaya pia nisamehe sana kama Kuna mahali jana nilikuudhi , najua ni pombe si unajua tena shemu.niliongea kwa upole sana

Kishingo upande akapanda huku nikigundua dhahiri hajapenda, hiyo ilikuwa ni sehemu moja wanapaita kilimahewa kina Dispensary moja inamilikiwa na kanisa katoliki kama sikosei. niliendesha gari dakika zaidi ya kumi na tano tukiwa hatuongei. ni yeye tu alikuwa anaongea na simu huku nikigundua atakuwa ni mumewe kwa namna nilivyosikia

Baada ya muda kidogo akapiga simu hapa akiwa anaongea huku anafoka huku akiwa anatoa maagizo fulani akakata simu na kunigeukia mimi ,

Yaani shemu acha tu ni bora mtu kubaki kwenye Imani yako kuliko kujiingiza kwenye shirki zisizokuwa na mpango wowote na yote haya kayataka mume wangu. Kisha akatulia lakini mimi niliguna tu na sikuongea chochote Mimi nikawa macho mbele tu.

Hivi shemu kwa Imani yako unaamini katika Imani za waganga wa kienyeji? aliniuliza.

Mmmh sina imani hizo moja kwa moja ila naamini ukibanwa au kuwa kwenye matatizo makubwa sana unaweza kwenda huko kwa hiyari au lazima kutokana na nani anakuongoza kwa wakati huo. Unaweza kuumwa ugonjwa ambao hutakuwa na kauli ukaja kushangaa tu umepelekwa kwa mganga wa kienyeji hata kama wewe huwa hupendi. nilimjibu kwa uelewa wangu.

Ahaaa nimekuelewa sana shemu, iko hivi mimi nimefanya kazi TANAPA karibia miaka kumi lakini nilikuja kuachishwa kazi mwaka jana kwenye mazingira tatanishi sana, ni baada ya kutokea matatizo fulani kuwa tuliruhusu wawindaji kwa vibali vya kughushi ili tugawane hela , ndipo mamlaka zilipotusimamisha kazi ili tupishe uchunguzi. aliweka kituo.

Aisee pole sana lakini shemu kwanini na nyie mfanye hivyo hamkujua mnakiuka miiko ya kazi? niliuliza

Shemeji wewe acha tu huwezi amini wakati wawindaji wale wanapitishwa mimi sikuwepo kabisa, usiseme labda najitetea hapana, hiyo siku mimi nilikuwa kwenye patrol na watalii fulani na hata niliporudi wala sikujua chochote lakini baada ya siku nne nilipewa kiasi fulani cha pesa na wafanyakazi wenzangu, ikabidi niulize ni za nini ndipo nilipoambiwa Kuna mchongo waliutengeneza hivyo umeshatiki. lakini Mimi nilikataa zile pesa huku Ukiwa ni mwanzo wa chuki dhidi ya wafanyakazi wenzangu, nikakaa zaidi ya nusu mwaka nikapewa likizo kama ilivyo kawaida lakini nilishangaa kabla sijamaliza likizo yangu, nikaitwa makao makuu huku nikituhumiwa kuwa Mimi ni mmoja wa wafanyakazi wasio waaminifu tulishiriki kutoa vibali feki kwa wawindaji huku tukijua ni kosa kisheria kwa kuinyima serikali mapato na kujipatia pesa kwa njia isiyo halali. pingu zikanihusu muda huo huo. Nilikaa zaidi ya miezi mitatu nikiwa mahabusu pasipo kupelekwa hata mahakamani ndipo nilipotolewa wakidai wamefanya uchunguzi na kubaini Mimi sikuhusika. aliweka kituo.

Pole sana shemu kweli Dunia haiishi mitihani Sasa ilikuwaje, hata Mr hakukudhamini? maana mwanamke kukaa mahabusu siyo poa.niliuliza

Alihangaika sana tu, zaidi ya kuhangaika kwani kosa lile huwa halina dhamana kwa mujibu wa sheria, hivyo nikawa Sina namna nadhani kwakuwa sikushiriki kufanya kosa lile MUNGU alisikia kilio changu. alinijibu kiufasaha.

Kwani hizo pesa zilikuwa kiasi gani na kwanini uache wewe uliajiriwa upate pesa, upo kazini ukizipambania pesa ,ikawaje ukakataa shemu, niliongea kimtego.

Zilikuwa nyingi sana tu, ila kiapo nilichoapa kutumikia kazi yangu ndicho kilichofanya nikatae , ni neno moja tu UAMINIFU,halafu unajua baada ya uchunguzi kufanyika ni Mimi pekee nilifanikiwa kutoka shemu, wengine sitaki kujua habari zao ila umeshanielewa. na baada ya kutoka sijarudishwa kazini ila mwezi uliopita nilipewa taarifa kuwa nitarudi kazini na taratibu zote zimekamilika huku nikipangiwa sehemu nyingine.

Ndipo mume wangu alivyoshauri kuwa kabla sijarudi kazini napaswa kwenda kuosha nyota yangu, yasije kujirudia ya kujirudia lakini mpaka Sasa Fatma mimi nishakosea masharti kibao ya mganga yaani. ndiyo maana najikuta nipo njiapanda.alifafanua

Shemeji kwanza nikupe pole kwa mitihani yako, lakini nikupongeze kwa kusimamia kiapo chako maana Mimi Daniel nisingeacha hela napenda pesa kuliko neno kupenda,lakini yote kwa yote mshukuru MUNGU kwa yote yeye ndiye aliyeshikilia hatma ya kesho zetu. Kikubwa Imani tu, Ukiwa na Imani na subira yote yanawezekana. niliongea kwa kadri ya uelewa wangu.

Kwahiyo unanishauri nini shemu maana nawezaje kwenda kazini bila kujizatiti? aliuliza.

Naomba unijibu maswali yangu haya,

Je, kwa mara ya kwanza wakati unaanza Kazi ulitumia mganga?

Wakati upo mahabusu, labda ulisikia Ndugu zako walienda kwa mganga ili uachiliwe ili utoke)

Na baada ya kutoka ulienda kwa mganga ili urudishwe kazini?
niliuliza maswali matatu akajibu hajawahi kwenda kwa mganga ndiyo kwanza anaenda.

Kwakweli shemu umenifungua Kuna jambo nimegundua ubarikiwe sana, nimejifunza kitu kupitia maswali yako, hakika sipotezi muda kwenda tena kwa wataalamu na najikuta nipo huru maana nilikuwa nawaza masharti nimekosea Sasa nikawa sijui itakuwaje nikawa kama mtumwa.

MUNGU humbariki mja wake bila masharti kazi yako ni kuomba, kuwa na subira na uvumilivu huku Ukiwa na Imani iliyo thabiti, maana kudra za mwenyezi MUNGU hazipo karibu hivyo subira ya tunachoomba ni muhimu, tatizo letu tuna haraka ya kupata, hapo hapo hatutaki mitihani itupate, kwa mujibu wa biblia kwenye agano la kale, Ayubu alimlilia MUNGU akidai kwanini impate mitihani ile, ndipo MUNGU akamjibu Ayubu, ulitaka mitihani hiyo impate nani?kwahiyo ni vema tujifunze kukabiliana na changamoto zetu.niliweka kituo huku mwanamke yule akinisikiliza kwa umakini.

Ahsante sana Shemu , yaani siamini ni wewe ulikuwa unakunywa pombe huku unaendesha gari, ulinitisha ujue, aliongea huku alicheka.
nimependa sana Imani yako hakika upo vizuri.

Kwani Mr alienda Kilwa Masoko kufanya nini? niliuliza nikimtoa yule mwanamke kwenye reli.

Ameenda kuangalia fursa za biashara tumesikia Kuna mashamba ya chumvi huko hivyo kaamua kwenda ili kujua a b c kadhaa si unajua biashara zimekuwa nyingi Kila unachoanzisha tayari Kuna watu wanafanya. alijibu kiufupi

Ok sawa shemu una watoto wangapi . nilizidi kumchimba.

Nina mtoto mmoja tu, nilichelewa kidogo, ila mume wangu yeye ana watoto wengi kwa mkewe mkubwa.alijibu huku akitabasamu kwa aibu.

Ina maana wewe upo kwenye mitala shemeji yangu, maana..... niliuliza huku nikishindwa kumalizia sentensi yangu.

Ndiyo kwani ni ajabu, na huyu mume wangu ana mchango mkubwa sana tangu nasoma hadi napata kazi,lakini pia Dini yetu inaruhusu wala hakuna shida halafu huwezi amini hata mke mwenzangu tunaelewana sana tu. alijibu Kwa kujiamini.

Nilitabasamu kidogo huku nikiwaza watu ambao wanasomesha watu hadi kuja kuwaoa, hii ni kama kama kubeti tu mkeka ukichanika basi ukubali matokeo.kimya kikapita huku nikiikaribia Dar es salaam.

Itaendelea.....................
 
SEHEMU YA SABA

Gari ilisereka kidogo huku ikihama njia kabisa, Kisha nikatulia huku ng'ombe wengi sana wakipita, kulikuwa watu zaidi ya kumi na tano jamii ya wamang'ati wakiwa wanaume kwa wanawake huku wakionesha wanahama.

Sasa shemu Hawa watakuwa wanaenda wapi usiku huu, jamani tena wana watoto mgongoni, kwanini watembee usiku? yule mwanamke aliongea kwa mshangao sana.

Baada ya kuwa ng'ombe wamepita nilikanyaga mafuta huku nikiongeza speed tofauti na mwanzo, nafikiri yule mwanamke alikuwa ana hofu sana juu ya uendeshaji wangu lakini hakuwa na namna hangeweza kuniambia chochote.

Nadhani zile beer nne zilishachukua nafasi fulani kichwani nikakuta naanza kumtamani yule mwanamke, nikapanga lazima nitafute sababu yeyote ile ili tulale na najua naweza kufanya chochote na asinipinge nilijiamini sana.

Heeeeh shemu ina maana tushakaribia daraja la mkapa, umetembeaaaa, alisema yule mwanamke huku mwanga wa gari linalokuja mbele yetu likiwa Ukiwa unamtesa sana.

Yaani kuna watu sijui walisomea wapi udereva yaani anawasha taa namna hiyo tena tupo katikati ya daraja, namuashiria apunguze mwanga hataki,haya ni madhara ya kujulia gari mtaani kisha kupata leseni kwa njia ya magumashi hawa ndiyo wanaosababisha ajali kila kukicha. nililaumu .

Akili yangu juu ya yule mwanamke ilikuwa palepale lakini na ugumu nao ulikuwepo hivyo niliona siwezi kumuacha hivihivi ikabidi nianze kutafuta visingizio.

Yaani gari hili shemu silielewi kabisa , yaani breki inashika kwa mbali sana na muda mwingine nakanyaga hamna kitu kabisa na usiku huu tena sijui itakuwaje, afadhali ingekuwa mchana ningekokota hivihivi lakini usiku huu hapana. Yaani hizi gari za kupokezana mara aendeshe huyu mara yule ni shida sana. nilijifanya gari ni mbovu.

MUNGU wangu sasa itakuwaje shemu maana, mbona nitakuja kugawanywa vipande masikini mimi, shemu huwezi simama popote ili wakuangalizie nini tatizo?
alihoji yule mwanamke.

Hilo hakiwezekani shemu, kwanza kwenye vijiji hivi vya njiani hakuna mafundi wala gereji za kueleweka, hivyo unaweza Kuta unazidi kuipa matatizo zaidi gari ya watu. vyombo vya serikali hivi huwezi kubumba bumba ujuavyo wewe. nilizidi kujitengenezea mazingira.

Ndani ya muda mfupi tulikuwa Ikwiriri, nikapaki gari pembeni huku nikishuka,
Shemu twende tukapate chochote kitu basi, maana mimi naona tumbo halina kitu nilimsihi.

Shemu yaani acha tu hapa nilipo sina hata njaa, siisikii kabisaaa, naona kama nimechanganyikiwa tu, yaani hii siku ya leo nitasimulia jamani.
aliongea kwa uchungu huku akiwa kama vile kagundua Nia yangu ila akashuka kwenye gari na kuiegamia.

Niliingia bar ya pale njiani wanapaita Kivulini, nikaketi na kuulizia Chakula nikaletewa nikapiga huku nikimuona vizuri sana yule mwanamke ambapo simu ilikuwa sikioni akionekana anapiga huku na huko , alionekana mwenye haraka sana na hakupenda kitendo cha mimi kusimama pale ila hakuwa na namna.

Ubishani ulioendelea pale Kivulini bar kuhusu Mgombea wa ubunge wa Jimbo la Rufiji ambaye alikuwa chama tawala huku wakidai hawamfahamu na si mzaliwa wa pale, ule mjadala ulinivutia sana nikatamani kujua japo A B C kadhaa, hivyo nikajisogeza kumsikiliza jamaa mmoja ambaye alikuwa anawashawishi wenzake kuwa wasije wakampa kura hata moja

Simu yangu iliita , kuangalia namba ni yule mwanamke ambaye tulipeana namba kwaniaba ya kwenda kumchekia mifugo yake,

Hello shemu, samahani lakini nilikuwa naomba uniruhusu niondoke kwasababu ninatakiwa nifike leo hii hii sitakiwi kulala njiani kabisa, naziona Coaster zinazofika mpaka Mbagala rangi tatu hivyo , nakushukuru kwa msaada wako . aliweka kituo akiwa ananipa nafasi labda niongee chochote lakini nilikata simu.

Huyu demu vipi naye, anawahi wapi?
Saa tatu hii si bora tulale tu ,
Nilimuita muhudumu nipewe bia yangu ili nishushie na Chakula nilichokula, huku nikisikia simu inaita kwa mara nyingine, kuangalia mpigaji ni yeye lakini sikupokea lengo nimcheleweshe ili tulale wote.nilijua asingeondoka kwani begi lake lilikuwa kwenye gari.

Nilimaliza bia kwenye glass Kisha nikaingia msalani, Kisha nikaenda kwenye gari huku nikiacha bia nyingine ikiwa haijafunguliwa nikakuta mwanamke kabadilika sana, uso wake haukuwa na masikhara hata kidogo.

Samahani kaka yangu naomba nipe begi langu siwezi kukaa kama vile yatima aliyefiwa na wazazi wote wawili naomba niondoke bwana, yaani unanifanyia visa kibao mara gari haina breki mara sijui kitu gani halafu unashuka unastarehe tu, wewe ni mwanaume unaweza kujiamulia mambo mengi, lakini Mimi ni mke wa mtu nipo kwenye himaya na miliki ya mtu hivyo naomba tuheshimiane. aliongea huku akiwa serious na sauti ya juu huku akionesha amechukia.

Hapana Shemu usiseme hivyo, lakini kwani Kuna ulazima wa wewe kufika leo, kesho alfajiri tutajihimu shemeji yangu, Mimi nipo na chombo Cha watu ambacho nina tahadhari nacho,nikipata ajali usiku huu itakuwaje? Vitu vingine vinazuilika shemu. hebu twende ukale kabisa shemu usijisikie vibaya bwana. nilimwambia lakini hakuwa tayari alikataa katakata huku akiomba nimpatie begi lake.

Nilikuja nikamalizia bia huku nikimuona, anaongea na wanaume watatu ambao sikujua wamefikaje pale labda kwakuwa nilikuwa tungi,

Kisha baada ya kumalizana na wale jamaa ambapo sikujua wameongea nini, akawa anakuja usawa nilipo akaingia , huku akikaa meza nyingine akionesha ana mawazo sana. wakati huo mimi moyo ulidunda kwa furaha maana dhamira yangu ilikuwa inakwenda kutimia , aliagiza chipsi kavu na soda tu, Kisha alipomaliza akaja kwangu kwa mwendo wa madaha kabisa , mwanamke mrefu sura isiyokuwa na makeup, huku akiwa kavaa tisheti nyeupe na suruali nyeusi iliyomkaa vyema sana huku akiwa kavaa raba fulani za kike nzuri sana, akiwa kajifunga kanga yake kiunoni.

Ahsante sana Kwa chakula shemu , aliongea huku akiwa kasimama pembeni yangu , huku nikimkung'uta vumbi vumbi lililonasa kwenye nguo zake, hakika nilienjoy maana nilimshika popote huku akiwa haoneshi kuchukia, alitabasamu tu, laiti ningejua mawazo yake.ama kweli mjinga hajijui.

Sasa vipi si tunalala shemu, niliuliza kwa sauti ya kilevi .

Hakuna shida shemu wewe si umesema si vizuri kutembea usiku, hivyo nimeridhia kulala, na pia nishaulizia na lodge nimeambia ipo ambako Kuna parking za magari na pia ni self hivyo nahisi ni pazuri twende huko.
Aliongea kwa kudeka huku akichochea hisia zangu, nilimaliza bia kwa pupa huku tamaa ya ngono ikishika nafasi yake.

Niliendesha gari huku nikiwa naulizia kwa watu ambalo walionesha kuwa ni paleeee kwenye taa za kuzunguka , baada ya kufika alishuka haraka sana kwenye gari.

Shemu paki gari vizuri, Mimi ngoja nikachukue chumba , aliongea Kisha nikamuona anaelekea mapokezi,
Mlinzi alinielekeza sehemu ya kupaki huku akiniuliza kama nitatoka asubuhi sana basi nipaki karibu na geti na gari iangalie nje.huku nikimshangaa yule mlinzi anavyonichelewesha kila napopark anasema siyo, hali ile ikafanya nichelewe kidogo,

Kisha kwa mbwembwe na tembea ya kilevi nikaenda mapokezi, huku nikivuta picha yule mwanamke ambavyo atakuwa kashabadilika huko chumbani.

Kuna mwanamke kaingia siyo muda hapa kavaa (nikiwaambia alivyovaa)

Ndiyo kaingia kwani unamuitaje, aliuliza yule dada wa mapokezi.

Ni mke wangu yule,. nilidanganya

Weee acha uongo yule siyo mkeo na katuambia Kila kitu na Kuna watu walikuja kumchukulia chumba hapa,
na anadai wewe unataka kulala naye wakati yeye hayupo tayari, hivyo uchukue chumba chako ulale au uondoke, na ukilala hapa hatutaki fujo , tutapiga simu polisi. aliongea yule dada wa mapokezi huku nikishangaa sana , Kisha nikapiga namba ya yule mwanamke ikawa haipatikani. nilichukia sana na pombe zikakata

Itaendelea.......................
Unajitafutia kipigo tu kutoka kwa askari
 
SEHEMU YA KUMI

Kwanini kuna nini mbele mbona magari hayatembei? lakini sishangai sana asubuhi hii watu wanaenda makazini ni kawaida sana. yule mwanamke alijiuliza na kujijibu mwenyewe.

Miaka mitano nyuma ilikuwa ni ngumu kukuta foleni maeneo haya tofauti na city center hii inadhihirisha kuwa nchi inapiga hatua kimaendeleo sasa hivi watu wengi wanamiliki usafiri. wewe tazama kule juu magari mengi ni madogo. nilimuonesha.

Aaah wapi kuwa na magari mengi barabarani ndiyo maendeleo,si kweli nakataa kabisa nchi bado ina umasikini wa kutupwa, bado hakuna ule uwiano sahihi Kati ya population ya watu na ongezeko ya unavyosema, wewe mwenyewe umesema ni kawaida sana huwa unaenda maeneo ya vijijini hebu tizama maendeleo ya huko, na tunaweza sema huko ndiko waliko voters walio wengi. aliongea yule mwanamke akinipinga.

Hamna shemu bwanaa, wewe mwenyewe tu, sasa hivi mabus ya abiria ni ya kutosha hata vijijini pia watu wamepata muamko wanajenga nyumba za kisasa si mjini tu hata huko vijijini kuna watu wanajitahidi sana kutoka nyumba za tembe hata kuwa na nyumba zenye muonekano , najua una sababu zako kuhusu maendeleo ya mtu mmoja mmoja, lakini tambua hata hapa mjini Kuna watu wanaishi maisha mabaya sana Lakini si kwamba hawajitumi au hawataki kuwa na kitu fulani, bali ule mpangilio wa maisha ambao unaanzia mbali mtu anakuwa ameukosa. nilijibu kwa uelewa wangu.

Wee shemeji nishakuona mwanasiasa bwana achana na mambo yako, Jana tu tumeshindwa kufika kwa wakati kisa ukosefu wa magari, haya mamia ya magari unayoyaona si kwamba watu wengi wamepiga hatua hapana bali Mimi nalia na uwiano wa watu.
aliweka kituo

Nilifanikiwa kupenyapenya hadi nikapita huku mbele foleni ikipungua kutokana na kuwa nipo kwenye barabara za mjini,
vipi shemu Mimi hapa naelekea kwanza mjini Kisha ndiyo nitarudi nyumbani wewe utashukia wapi , niliuliza maana sikutaka tena kuwepo na mtu kwenye lile gari.

Mimi ni hapo tu nashuka na nyumbani kwangu si mbali, niache kwenye Bajaji hapo maana ndiyo usafiri wetu tunaomudu mjini. aliongea Kisha nikapaki gari pembeni akashuka.
akachukua mizigo yake yote , Kisha akaniaga

akiwa pale chini akawa anaonekana mwenye furaha sana tu, eeh niambie gari ilipona breki? na kama ni hivyo ulitengeneza saa ngapi, lilikuwa swali la kijinga nisilotarajia lakini lenye mantiki wakati nikibabaika kutaka kumjibu akaniwahi.

Wewe ni mtu unayeonekana ni mwelewa wa vitu vingi tena sana tu,pia ni mwenye heshima zako japo umeficha kazi yako, lakini jaribu kujiheshimu, wanawake poapoa wa mjini wanaharibu sana nyinyi wanaume, mnajikuta kila kitu kinawezekana tufanye na mimi nilikupenda ndiyo lakini Jana ileile tunafahamiana mara nishalala na wewe? mbaya zaidi mume wangu tulikuwa wote na umemfahamu, si ungeniona Malaya na mwanamke nisiyejitambua, Mimi sipo hivyo na pia na wewe usiwe hivyo kutaka mademu kirahisi utakuja kuibiwa ohoooo unashangaa asubuhi mwanamke hayupo na gari halipo na ulivyokuwa umelewa sasa , kuwa makini Mr Daniel. aliongea huku safari hii akinitaja jina tofauti na mwanzo alivyokuwa ananiita.

Kiukweli aliongea facts tupu, nilitamani niongee chochote lakini aliingia kwenye bajaj na kutokomea,
huku baadhi ya maneno yakiwa kama mwiba maana aliongea ukweli,
Ila potelea mbali kwanza nilikuwa najaribu bahati yangu tu si mbaya, wanawake wazuri halafu kuwanyamazia tu siyo sawa kabisa hata kama kakataa potelea mbali.

Nilikanyaga mafuta hadi ofisini kwetu kisha nikakutana na mwanamke mmoja ambaye anaitwa Veronica lakini tulikatisha kwa kumuita Vero au Vee.
ni mwanamke huwa tunaelewana na tunatembeleana anakuja kwetu, na mimi naenda kwao ni mtu ambaye hata kimaisha aliniacha mbali sana labda kwakuwa mumewe alikuwa sehemu nyeti .

Daniel, afadhali umerudi kaka yangu, yaani siku ambazo hukuwepo nilikuwa najisikia vibaya mno , ila hakika huwa napata amani sana ukiwepo . aliongea huku akiwa
anaandika vitu fulani kwa notebook yake.

Dada Vero punguza uongo, wiki nzima na siku kadhaa sipo hapa na hujawahi kupiga hata simu kweli halafu unadai ulinikumbuka. siwezi kuamini , niliongea Kisha tukacheka ,

Niliingia ofisi ya boss nikamkuta akiwa na wageni fulani lakini nikaingia Kisha tukasalimiana.

Aaah Dani vipi wewe safari ya kutoka Lindi tu hapo umetumia siku mbili, ungeenda mikoa ya mbali ingekuwaje?
ile nataka kujieleza akanizuia.

Achaacha najua misukosuko yako, nasikia gari lako liliharibika lakini nimeshatuma mafundi najua kesho wataleta. lakini pia Dani bado nipo na wewe kwa mara nyingine ,
Unawezaje kunikatalia ninachokutuma, wenzenu wote wapo huko wanatoa sapoti kwa mheshimiwa lakini wewe na yule mlevi mwenzio mkakataa , yaani sijui mambo ya kijinga mtaacha lini , halafu tukiongea tuonekane wenye majungu siyo.

Hapa penyewe tunabebana tu , hata hiki cheo ulichonacho si umependelewa tu, na sijui mchawi wewe maana CV zako na kuwa hapa hata hufanani yaani ila nidhamu ya kazi inakubeba. aliongea akiwa anakaribia kuharibu siku yangu.

Boss tuheshimiane si wewe umeniweka hapa, sijajikuta tu nikiwa hapa, nipo ngazi kwa ngazi , taaluma yangu ni X , huyo unayempigia debe ndiye aliyenishauri nikasome taaluma Y. ananijua na namjua. tangu naokota mizizi barabarani, nimechimba misingi ya majengo mbalimbali nikishika sululu huku vyeti nikifungia ndani. ilikuwa ngumu kipenya huku ndipo nikatumia zaidi ya miaka minne kuhamia taaluma Y kwa ushauri wa huyo ambaye sidhani kama unajua tumetoka wapi , wenzio huyo tunamuita baba. niliongea kwa jazba maana dharau za boss zilinitoa kwenye mudi.

Tatizo lako Dani ni hilo unapenda sana kuchukulia vitu serious, haya ni maneno wewe umekuwa incredible kwenye hii taasisi wala usijisikie vibaya bwana, halafu na Mimi pia ni boss wako , usinijibu kwa kujiamini hivyo.na Mimi nilikuwa nakushauri tu ungesapoti hili zoezi lakini wewe umekuwa na mtazamo tofauti. Aliweka kituo

Mimi si mwanasiasa boss na sijui chochote kuhusu siasa utanionea tu ndugu yangu. nilizidi kuweka msimamo wangu

Sawa naelewa tuachane na hayo, Mimi nasafiri leo hii natoka saa kumi na moja ili nikakale Mkoa XXX ambapo mheshimiwa atapita , Sasa nishtulie dereva wangu hapo nje nataka nimpe maagizo. lakini pia na wewe kwa siku hizi tatu pumzika tu ila kukiwa na tatizo site usisite kwenda. tukaagana nikatoka.

Niliwasha mkweche wangu baada ya kurudisha ndinga ya wenyewe nikaingia barabarani huku tumbo nalo likidai chochote, hapa naenda kula nyumbani tu sili popote .
kwakuwa ilikuwa mchana wa saa sita barabara haikuwa busy sana hivyo kuniwezesha kufika nyumbani mapema , licha ya mke wangu kutomkuta sikushangaa kwani alishaniambia wapi atakuwepo ,nilipumzika huku wasichana wa pale home wakitimiza majukumu yao.

Nikiwa nipo nyuma ya nyumba nikicheki bomba la maji linalovuja simu iliita namba ikiwa ngeni, sikusita kupokea,

Kisha tukasalimiana na yule jamaa huku mapema nikitambua sauti yake kavu yenye kukwaruza, alikuwa ni yule pot mume wa mwanamke niliyekuwa naye.

Nikaingiwa na hofu kidogo huyu naye anataka nini ? Pia namba yangu kaipataje mbona jana hatukupeana namba? ina maana mkewe kampa namba yangu? ili iweje?

Halloo, halloo! vipi bro mbona huongei, jamaa alizidi kuongea.

Nakusikia vizuri vipi Kwema kaka?
niliongea kwa tahadhari.

Kwema ila poleni na safari, maana Mimi Jana niliahirisha safari yangu nikaamua kurudi tu nikafanikiwa kupanda gari la mizigo, japo nimeingia mjini kunakucha maana ilikuwa ni saa kumi alfajiri. Sasa cha ajabu sikumkuta mke wangu wakati alitangulia.aliweka kituo.

Njaa ilipotea ghafla hata sijui Nini kilinipeleka kule nyuma ya nyumba yangu nikajikuta uoga umenikamata ghafla.

Itaendelea................
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Nashindwa kuelewa maelezo yako vizuri, sijui una maana gani. nilijifanya sijui chochote.

Aaaah nimestuka kidogo kaka kwasababu mimi nilitegemea utaingia jana, Dar es salaam lakini hata mke wangu alinihakikishia kuwa amefika ndiyo maana kanichanganya sana. aliongea kwa upole sana.

Mimi nadhani ni vema umuulize mkeo binafsi Sina majibu ya kukupa , ila nikuhakikishie tu kama mwanaume mwenzangu kuwa uwe na amani tu. nilimjibu huku simu ikiwa hewani bado na nikawa nasikia mabishano fulani, nikawa na hofu sana.

Watu wengine bwana wivu tu hadi lini ndiyo hawa huwa wanaishi maisha ya taabu kwa kuwaweka watu vifuani mwao, mtu mzima uliyekutana naye ukubwani unawezaje kumchunga , kama siyo uwendawazimu ni nini.
Maisha, ndoa na mahusiano ya sasa hayahitaji nguvu badala yake ni heshima baina ya watu wawili. Kila mtu atambue wajibu na nafasi yake katika familia, sasa kuna mijitu inaendekeza wivuuu, ah atakuwa mshamba tu yule.watu tuacha wake zetu miezi ,angekuwa yeye angeweza.niliwaza sana

Jioni sana mke wangu alirudi akiwa kapendeza sana akiwa ndani ya sare ya chama (jina kapuni) tulisalimiana juujuu huku akiwa na furaha fulani hivi nadhani yanayoendelea kwa wakati huo yalimpa hiyo hali haswa ukizingatia wanawake wengi huingia kwenye masuala mengi kwa miguu miwili.wakati sikutaka kwenda ndani mapema nilikuwa nje nikipunguza punguza majani huku akili yangu ikiwa si nzuri kutokana na jamaa alivyokuwa na hisia mbaya na ukweli alikuwa sahihi.

Hapa ipo siku nitapata matatizo na wanasema mwisho wa ubaya ni aibu, ukweli ni kama MUNGU anataka kunionesha ni njia ipi napaswa kuishika , hakukuwa na sababu ya kulala njiani jana, kwakweli nastahili kulaumiwa. nilijiwazia hiki nikiwa na panga kupunguza majani ya mti fulani ndani mwangu.

Naambiwa karudi lakini naingia ndani sikuoni kumbe upo huku, habari za siku mbili tatu na pole kwa matatizo ya hapa na pale. aliongea mke wangu huku akinisaidia kukusanya yale majani sehemu moja .

Mke wangu acha tu nilikoenda mazingira ni magumu sana kufanya kazi, pia gari likawa linasumbua
sana hivyo mambo yakawa magumu ili nilijitahidi kukamilisha kwa wakati, kimbembe wakati wa kurudi ilikuwa ni shida sana, hakuna usafiri wa uhakika uhakika ni hadi nilipoletewa
gari baada ya kufika barabara kuu. nilimjibu.

Poleee, ila ahsante kwa kutuletea samaki japo wanatoa harufu, sijui tunakulaje, sidanganyi nadhani wamekaa muda mrefu sana. aliongea huku akionesha hawataki wale samaki.

Hebu kama nyie hamtakula mnipikie mimi, ila msitupe nimenunua bei ghali sana tafadhalini bwana, niliongea kama utani lakini nikimaanisha.

Hakuna anayetupa na wote watakula ila mimi hapana, halafu mume wangu huwa unapenda sana kuvaa kapelo , zipo nimekuletea.niwaambie wakuletee uzijaribu? aliongea huku akitabasamu.

Zilete wewe mwenyewe unajua jinsi navyopenda , lakini baada ya kuziona tu kwa mbali nikamwambia dada wa kazi azirudishe ndani kwani huwa sivai vitu vile. niliongea huku tukicheka na mke wangu.

Unajua nini mke wangu hizo watu wengi huvaa kwenye matatizo, Ukiwa huna hela ya hospital unavaa hizo huku ukienda kuomba matibabu ya bure

Au mtaani kwenu kukiwa hakuna maji, umeme na miundombinu mingine unavaa hizo kofia au zile fulana mbele ya wenye mamlaka na mambo hayo ili tu kuwakumbusha madai yenu.lakini hivi hivi hapa licha ya kuwa ni shabiki wa timu X hapa nyumbani lakini ulishawahi kuona nina jezi yeyote? nipo radhi ninunue Kisha nimpe mtu lakini si kuvaa hadharani nilifafanua.

Yaani baba Jack kuna vitu vingine wala huwa kuweka misimamo sana tambua maisha ni hayahaya , usijibane sana utakuja kuugua magonjwa yasiyo yako kwani moyo unapotaka kitu na wewe akili yako inakataa basi kuna vitu unavitengeneza vinaweza kjkugharimu baadaye. alifafanua mke wangu Kisha simu yangu ikaita ni yule mke wa jamaa pot alipiga.

lakini mke wangu alitoka na kuingia ndani hivyo ikawa rahisi Mimi kuongea,

Nilitoka nje ya fence kwa tahadhari huku nikiangalia kulia na kushoto maana sometimes watu wanaweza kupeleleza wakapajua Hadi kwako teknolojia imekuwa juu sana.

Nilipokea Kisha nikawa naisikilizia ni sauti ya nani,
hello shemu samahani kwanza nikupongeze kwa jibu fupi ulilompa Mr, kuwa aniulize mwenyewe hapo angalau alishusha presha, nikushukuru sana. aliweka kituo

Sikuongea chochote ila nikamwambia asipige tena simu na ikiwezekana afute namba yangu kwakuwa hakuna umuhimu wa kuwasiliana na Mimi lakini pia niliona isije ikawa ni mtego saa nyingine wapo wote wananisikiliza.
nilitafuta sehemu ya block basi nikaipiga tofali ile namba ya yule mwanamke.

Maisha yaliendelea vizuri , siku zilikimbia huku serikali mpya ikiingia madarakani , malalamiko ya mtaani yaliongezeka lakini siye wengine hatukulalamika kwani hakuna kilichokuwa kimeongezeka wala kupungua kama ni maisha haya ya dollars kadhaa kwa siku basi ni Yale tunayoishi siku zote.wiki.

Siku zilikimbia huku nikiwaza mambo mengi maana nilihisi kadri siku zinavyokwenda mambo mengi yanaongezeka huku nikihisi napitwa na vitu vingi na siendani na muda.

Basi katika harakati za kutafuta maisha na kujiongezea kipato Kuna jamaa yangu alinishauri kuwa kuna biashara ya madini, ambapo soko lake lipo na mtu anayenunua yupo hapa hapa mjini.

Niliona ni dili zuri hasa ukizingatia nishapiga madili kibao na nilifanikiwa kwa kadri ya nilichowekeza. hivyo nikaona ni muda wa kukutana naye huyu jamaa , kesho nilitoka kazini Kisha tukaonana kama tulivyopanga.

Dani hii ishu inalipa , na hii ishu si kwamba wewe unaenda kuchimba au nini maana ile ni kama kamari kuweka vijana kuwahudumia, Chakula, na mambo kibao mwisho wa siku unakuta umetumia gharama nyingi kuliko unachopata , au usipate
Kabisa, kuna jamaa yangu alienda mwaka fulani kwenye machimbo ya dhahabu, alitumia zaidi ya million hamsini lakini hakupata kitu yaani Kila akichimba hakuupata ule mwamba jike. aliokusudia hapo gold mine ditector ilikuwa inasoma lakini mwamba ulikuwa dume.

Sasa nilichokuitia ni kwamba sisi tutakuwa tunanunua kwa wachimbaji wadogo Kisha tunampelekea tajiri ambaye yupo hapa hapa mjini. alifafanua mshikaji wangu aliyeitwa Jastini au Jax kama alivyopenda kuitwa.

Lakini Jax eeh, hii ishu kwanza nimeipenda na ningependa kujua, vibali vyake vikoje na unavipataje, pia unaweza kuanza na mtaji wa bei gani, lakini pia mimi si mtaalamu wa mambo ya madini, na huwa nasikia kuwa Kuna fake na original japo kwa jicho la kawaida unaweza kuona yanafanana. lakini pia wewe nakujua a_z kazi yako na mengine mengi, hizi mambo wewe umeziuaje?maana Sina uhakika kama wewe ni mtaalamu wa masuala haya
niliuliza.

Na ndiyo maana tupo hapa, akaingia kwenye gari yake na kutoa makaratasi fulani Kisha akaleta pale tulipo huku nikiyapitiapitia.kujiridhisha

Itaendelea...........................
 
Shughuli inaanza,jamaa angalia usijeitwa mhujumu uchumi,kesi nzito na Yule polisi uliyetaka kumhujumu ,mhhhhhhh!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom