Simulizi: Harakati za maisha

SEHEMU YA KUMI NA SITA

Madini yalipimwa na kuonekana yapo safi angalau moyo wangu ulipata tumaini jipya, huku hata akili ya kuweza kupepesa mle ndani kujua kulivyo ikija maana mwanzo nilikuwa kama nipo kituo cha polisi nikikabiliwa na kesi nzito.

Tunaweza kufanya biashara nipe kwanza documents ili nijue uhalali wake, aliongea yule mzungu ambaye muda wote alivuta sigara kama vile ni oksigeni.

Hapa kiukweli sina na niwe mkweli , hivi vitu Kuna jamaa aliniazima pesa yangu siku nyingi sana akaacha kama dhamana hivyo nimekaa navyo muda mrefu sana hadi pale watu walivyonielekeza hapa, ila sina chochote sina lolote ninalolijua. nilijitetea.

Unanijaribu? au unanipeleleza ili ujue mimi nanunua vitu halali au visivyo halali? aliuliza huku uso wake ukibadilika.

Hapana , mimi kama nilivyokwambia kuwa naomba unitue tu huu mzigo ambao umenitesa siku nyingi sana maana kukaa na kitu ambacho hujui soko lake wala taratibu zake ni shida kwakweli.nilizidi kujitetea.

Yule mwanamke ambaye alitufungulia geti pindi tunakuja, alimshauri Yule mzungu anunue tu , sijui saikolojia yake ilisomaje ila akawa anamkonyeza kuwa alipe hela.

Ok ok Mr Dani, ila hakikisha ukitoka hurudi tena hapa kwa stori tofauti hapa siyo club wala sehemu ya kupiga stori hapa ukija njoo na madini ila kumbuka kununua kwa njia halali na hapa nimekusaidia tu.

Nilipewa hela ambapo kwanza sikuamini , kama vile vitakataka vinaweza kuleta faida mara mbili ya hela niliyotoa pindi nanunua hakika, Kuna moyo wa tamaa ulianza kuniingia , na hapa ni Grams 48 vipi zingekuwa mia. jamani nilingia mtaani huku nikitaka nimalizane na dereva mwenye bajaji.

Enhee sasa mdogo wangu, hapa tuweke hesabu zetu sawa ili tuachane tu maana Sina haja ya kuendelea kuzunguka hapa mjini.
niliongea huku nikitoa hela iliyokuwa imebaki na kumpa.

Cha ajabu akaanza kukataa huku roho ya tamaa ikimuingia,

Bro niongeze hela hiyo umepiga pesa mbele yangu pale halafu unataka kunikadiria tu , kwanza tumeingia sehemu mbaya nimepigishwa magoti , na adhabu zisizonihusu, we jiongeze bro.
aliongea akiwa serious huku akitoa kitambaa na kujifuta usoni.

Wewe tulikubaliana kuwa tutafanya mizunguko yangu kutwa nzima Yaani Hadi jioni, na pia nilikupa hela nusu baada ya wewe kuomba hela ya mafuta, na jioni haijafika ndiyo kwanza saa nane hii unataka kusemaje, wewe uache tamaa. nilimwambia.

Oyaa bro wewe ndiye mwenye tamaa vitu vyenyewe umeokota tu hata hujui vinapatikana vipi, umepiga hela nzuri halafu hata kusema mwanangu shika na wewe watoto wakaishi unaleta ugumu, hapa lazima uongeze hata fifty (elfu hamsini)yaani nilinde kibingwa mwanao Basi, hapo unazo hela si unipe, na usinichukulie unaniweza, ulitaka kuniingiza kwenye matatizo kule nyumbani kwa mzungu hivi kwa mfano tungewekwa lockup, pale penyewe muda wote nilikuwa naomba MUNGU. anisaidie nisiingie kwenye matatizo, Sasa chagua moja unipe kwa hiyari au nichukue kwa lazima . aliongea yule dereva huku nikigundua pepo la dhuluma na tamaa limeshamuingia.

Kwanza nilicheka maana niligundua mwili mkubwa aliokuwa nao unamdanganya, anajua Mimi ni wale wanaume mdebwedo, ikabidi nikaze zaidi, wewe una tamaa na laiti ungeomba kwa adabu huenda kweli ningekuongeza hiyo pesa japo ni nje ya makubaliano, lakini kwa staili yako hapana.niliongea huku nisijue ameshapanic.

Ghafla akanirushia ngumi ambapo niliikwepa huku nikimpiga robber takatifu, hakujua Mimi mwenyewe nimezaliwa kwenye mlo mmoja kwa siku hivyo Kila shilingi kwangu Ina thamani,na nikigundua licha ya kazi yake ya udereva Bajaj ni jambazi pia , wakati huo naona analitaka begi, tulivutana mashati sana tu, mara nikishangaa kuona watu wanatuamulia nisijue wamefika saa ngapi,

Jamani hebu achaneni hamjui ni kosa kisheria kupigana hadharani, nikamwachia huku nikishangaa kundi kubwa la watu wake kwa waume limetokea wapi tena, lakini jamaa alitoka akaingia kwenye bajaji na kutokomea huku nikishindwa kujua ni mtu wa aina gani mbona mwanzo tulikuwa tunapiga stori safi tu huku akionekana ni mstaarabu tena aliyesoma?

Licha ya watu kutaka kujua ilikuwaje, sikujieleza chochote maana sikuona ulazima wowote watu wajue , kwakuwa nipo salama na hela zangu zipo salama, nikaingia mitini huku nikigundua kiatu changu soli yake inaachia kutokana na purukushani na yule jamaa, dah kweli maisha yamekuwa magumu yaani watu wanatafuta pesa kinguvu hivi loh. Ningekuwa mdebwedo angeondoka na hela zangu zote mpuuzi yule.

Nilifika nyumbani nikaoga nikajicheki kwenye kioo kama Kuna sehemu nimevimba au Kuna alama nikakuta nipo freshi maana ile ngumi ya jamaa ingenikuta ningeenda chini na hela zangu angechukua.

Kisha nikaja mezani kula huku wife akiwa bize sana na wageni fulani pale nje, nikamuita.

Hivi mke wangu yule dereva wa bajaji wa kipindi kile aliendaga wapi maana nimepiga simu asubuhi hakupatikana halafu sijamuona siku nyingi sana maana nilihitaji aje hapa anichukue ile asubuhi.niliuliza

Yule aliacha kazi ya Bajaj tangu mwaka jana, kwasasa ni mwalimu wa sekondari, alijibu mke wangu.

Hee kumbe yule kijana alikuwa mwenye taaluma yake, Sasa mbona alikuwa rafu sana, nywele, nguo anaweza akavaa hata wiki nzima haifuliwi japo nilimpendea kitu kimoja hakuwa na tamaa na hilo lilifanya awe na wateja sana tu. nilifafanua.

Sasa huo urafu unaosema ukimuona
Sasa hivi huwezi kuamini yaani , amekuwa mtanashati sana, labda ni kwa aina ya kazi aliyokuwa nayo . alijibu mke wangu.

Sasa leo nilikuwa na mishe fulani hivi ambapo niliacha gari kwa makusudi na nikaamua kutafuta Bajaj, ila sikwenda kijiweni wanapopaki bali nilisimamisha Bajaj ya jamaa mmoja
aliyekuwa ananipita , tukakubaliana safi kabisa lakini baadaye amekuja kunigeuka anataka kunipora eti, yaani Leo mke wangu sijui ingekuwaje,? likiweka kituo

Heee mume wangu na wewe, hebu achana na bajaji bwana , ah unaona unavyotaka kuhatarisha maisha yako? lakini Ina maana mtu huyo alitaka kukupora mchana huu ? Kweli mume wangu.
aliongea mke wangu akiona ni habari isiyoingia akilini.

Ndiyo, shangaa wewe mke wangu yaani vyuma vimekaza ,
Mzee kashikilia Sasa watu wanashindwa namna ya kujinasua kwenye hii hali mwisho wa siku wanaingia kwenye tamaa. wewe umpore mtu mchana.

Nilitoka ili jumamosi ile nikabadilishane mawazo na wananzengo huku siku hiyo wallet ikiwa si haba maana kitu ambacho Daniel huwa siwezi ni kujibanabana wakati hela ninayo hapa huwa siwezi kwakweli. nikatafuta sehemu yenye vibe isiyo Kaa kiswahili ili nianze kupiga vyombo.

Kabla hata sijatulia vizuri kwenye kiti, simu iliita mpigaji akiwa ni Jastini, sikuamini kama ni yeye, Wala sikupokea kwa haraka, nilitaka nijue kwanini aliamua kuondoka bila kuaga wiki nzima Mimi Sina Raha kama Sheikh aliyewekewa kipande cha nyama ya nguruwe chini ya uvungu wa kitanda chake.kanitesa sana huyu jamaa

Akapiga tena kwa mara nyingine, nikaipokea ile simu.

Itaendelea..............................
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Nikiwa chumbani kwangu peke yangu nilitoa ule mfuko wa madini Kisha nikaangalia huku moyo ukienda mbio sana maana nilishanusa harufu ya kutapeliwa ingawa Imani bado nilikuwa nayo.

Dah unaweza kujikuta umeshauzwa hivihivi na pesa niliyotoa siyo haba ikiwa itapoteaaaa, mmmmh ama kweli huwezi kuwa mjanja kwa kila kitu lazima kuna mahali utakwama tu,
niseme tu kuwa siku nzima nilikosa furaha si kwa kuuziwa madini bali ni kuonana na yule afande, mbaya zaidi anaonesha ana yake moyoni.
lakini nilijitahidi nikajizuia ili familia yangu isigundue chochote.

Siku inayofuata nilikuwa kazini asubuhi na mapema, niliingia ofisini nikawasha PC nikaanza kuangalia michoro fulani fulani ya ughaibuni huko kwani nilivutiwa na kitu fulani nikiwa nyumbani hivyo nikapanga nilifika jambo la kwanza litakuwa ni hilo, baada ya kumaliza nilifanya mambo yangu mengine Kisha nikaona ni muda wa kwenda site maana serikali yenyewe ilikaa vibaya mambo ya kukaa ofisini huku Ukiwa kwenye magroup ya mitandao ukichat yanaweza kukugharimu.

Kaka Dani vipi leo hatujaonana eti, aliuliza Da Vero.

Ni kweli mambo vipi dada kwema? Nilimsabahi.!!

Mimi mzima , vipi mbona unawasha gari unatoka nini bro,? aliuliza

Yes, ila narudi Sasa hivi nataka nikajionee mwenyewe huko maana unakuta vyombo vinaharibika hujui, na pia wahusika hawakuambii na hawaleti ripoti, Sasa siku mambo yakiharibika unalaumiwa ilhali hujui chochote, na si unajua serikali yenyewe ilivyokaa Sasa hivi hatupaswi kukaa vibaya.
nilimjibu kisha tukaagana.

Nilifika site nilizunguka huku nikigundua kila kitu kipo sawa tu, na hata hivyo nilifurahi namna Viongozi wa pale wanavyoendesha mambo nikajikuta narahisishiwa vitu vingi. ikabidi nivue reflector Kisha nikaelekea ofisini huku foleni nayo ikiwa ni changamoto

nikiwa kwenye gari niliwaza , mbona Jastini hanipigii, na alisema ikifika asubuhi atanipigia ili tujue tunafanyaje, hajapiga.
Halafu hadi muda huu hajapiga kwanini? Baridi fulani lilianza kuninyemelea huku nikianza kuamini hisia zangu japo bado nilikuwa na Imani naye sana. na nilipojaribu
Kumpigia simu haikuwa hewani, hili likaniongezea hofu zaidi.

Nilifika ofisini moja kwa moja kwenye ofisini ya dada Vero,

Bro Dani huyooo, siamini kama ni wewe siku hizi unajituma sana tofauti na mwanzo ulikuwa na kiburi sana, au ulikuwa ugeni wa suti! Maana ukiambiwa uende site ulikuwa unachukia sana unaenda basi tu. aliongea Vero huku tukigonga mikono na kucheka.

Wakati mwingine lazima ukubali kuwa unatumwa, nafsi isipokubali ndiyo yale unakuta mtu unanuna, kumbe ni majukumu yako unapaswa utimize.sasa dada Mimi Nina tatizo kidogo maana wewe ndiye Kila kitu na pia Kuna kitu nimewaza nikaona nikushirikishe my sister, kwanza unajua mambo mengi kuliko Mimi na pia umenipita hata umri hivyo najua utanipa mwanga fulani. nilianza kwa kumsifia.

Dani nikutahadharishe, kama ni masuala ya kupigana sijui kutukanana naomba usiniambie, nakujua wewe,
Mambo yaliyotokea kwenye bar au club usiniambie hayo ni matokeo ya starehe zako, kama ni mengine sema! aliongea huku akikaza uso. akionesha hatanii.

Siyo hayo dadaa, Iko hivi .....
Nikaanza kumsimulia kuhusu biashara ya Mimi na Jastini na pia nikimuhusisha na yule afande huku nikiunganisha dots kadhaa nikiona Kuna harufu ya kupigwa (kudhulumiwa)

Hahahaha malipo ni hapa hapa Duniani, na kwanza Dani biashara ya madini umeianza lini jamani , na Hawa watu wanaojifanya Wana madini wamekuwa wengi, juzikati Kuna watu wamekuja hadi nyumbani eti wanamwambia Mr Wana dhahabu, Mr akawagomea kuwa hizo si biashara zake na hazijui kiufupi Sasa na wewe Dani ukaingia kichwakichwa, wewe Rubi unaijua lakiniii? yaani hata sijui nikisaidieje.hapa kwakuwa unasema mmoja unamjua ni mshikaji wako, wewe mtafute ukiona humuelewi mripoti polisi hii ndiyo njia rahisi usije ukawaza visasi utaharibu maisha yako bro.
aliweka kituo dada Vero.

Nikarudi ofisini kwangu nikazugazuga ili tu ufike muda wa kwenda nyumbani ili nikapumzike.
Ila Jastini, jamaa yangu, msiri wangu, kweli anaweza akaweza kunidhulumu , halafu kama ndiyo aliwaza kunidhulumu mbona hela yenyewe siyo nyingi, atafanyia nini , dah, niliwaza huku nikipiga tena simu majibu yakawa ni yaleyale, nikapiga ishara ya msalaba kama ishara ya kumshirikisha MUNGU kwa linalonikabili.

Nikiwa nyumbani nilifikia chumbani nikatoa yale madini nikaanza kuyachungulia kwa umakini nikitazama kwa umakini sana,
Nikaamua kutoa simu ili niingie google Nikaona kuna utofauti mkubwa kwanza ile Rubi nayoona kwenye simu ilikuwa inang'aa sana.

Moyo ukaanza kunienda mbio sana nilitamani kumuita wife nimshirikishe
lakini ishu ilikaa vibaya sana na pia nikaona atanidharau kuwa sipo makini Hadi nadhulumiwa, hivyo heshima yangu kama mume itashuka. nikaamua kuugulia moyoni.

************************************

Tangu jana nakuona mnyonge sana vipi, mbona kama haupo sawa Kuna Nini mume wangu? aliuliza.

Hapana kawaida tu ni uchovu wa kazi tu si unajua tena, malengo hayatimii, ndoto zangu nyingi bado , hivyo ni vitu nakuwa nawaza sana.
nilidanganya

Mmmmh sawa, mimi natoka kidogo naenda hapo nyuma kuna ndugu yangu huyo mke wa afande kajifungua tangu majuzi hivyo nimesikia wamerudi ngoja nikamuone. aliaga.

My wife giza linaingia kwanini usiende kesho? halafu hawa watu urafiki umeanza nao lini?
niliuliza nikiwa sipendi.

Unajua baba Jack kama nikikufuatisha Kila unachoongea Mimi nitakosa hata majirani wa kushirikiana nao, mwanamke wa watu hana shida na mtu mpole , mtaratibu na napatana naye vizuri halafu wewe unakuja na mawazo tofauti, mwenzangu huwa sikuelewi
Ujue sijui unataka niishi maisha gani, siyo hivyo mume wangu . alijibu kisha akatoka nje.

Mke wa afande, mke wa afande, Hawa jamaa wamenikalia kushoto kweli yaani, na kipindi kile huyu jamaa anaulizia kiwanja hiki ningejua ni polisi ningemwambia wenyewe hawauzi. sijui nitafute eneo lingine nijenge ili nihame hapa? niliwaza kijinga mambo mengi huku Kila nikisikia neno afande nikiwaza madini ambayo Sina uhakika kama ni halali .

Kesho yake nikiwa kazini dada Vero alinifuata nilipo,

Jana nikiwa nyumbani nimekumbuka kitu niliwahi kusikia kuwa Kuna mzungu mmoja huwa ananunua madini kama uliyonayo , Sasa nikawaza kwanini usiende huko kama ni feki au ni halisi mbivu na mbichi zitajulikana, ni maeneo ya fulani huko kwa washua wewe ukifika ulizia kwa McDonald Miller almaarifu Mr Miller,utaambiwa alipo nahisi kapanga apartment maeneo niliyokutajia, suala muhimu je una Documents zozote zinazohusiana na madini usije ukaingia matatizoni zaidi ndugu yangu. alishauri dada Vero.

Niliwaza sana huku nikigundua mlima ninaopanda ni mrefu sana,hata baada ya kufika nyumbani Jastini aliyeniingiza kwenye mchongo huo bado akawa hapatikani kwenye simu.
nikaona Mimi Kwa huyo mzungu nitafika tu.sitajali nini wala nini.

Itaendelea.....................
Ushapigwa na kitu kizito
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA

Habari yako Jax, mbona umenifanyia hivyo unanikabidhi vitu halafu unapotea ,simu zako hazipatikani ndugu, vipi ilikuwaje tena? nikipokea simu kwa lawama.

Aaaaaaah Dani hata salamu?
Hutaki hata kujua nilikuwa na matatizo gani? lakini Mimi sijali vipi mnaendeleaje huko town?
Labda nikwambie tu kuwa baada ya yule afande kupokea ile hela, alinituma nifuate mzigo mwingine mkoani ambako kiukweli simu kupatikana ni shida sana huku machimbo. ila kwasasa nipo kwenye gari narudi nikiwa na grams kadhaa za rubi, kwahiyo naomba nisamehe Kwa kuwa nje ya muda ila nakuja ili tupeleke ule mzigo kwa bosi. aliweka kituo.

Sawa ila Mimi mzigo nimeuza Tena Leo hii hii , ukweli nilipata wasiwasi nikijua labda umenizunguka kwa kunipa vitu fake, nikaamua kwenda kujiridhisha kwa wanaofahamu ili nitue ule mzigo maana wiki nzima sina raha na wewe ambaye ni tumaini langu hupokei simu. nilimwambia ukweli.

Daniiiii kwanini uliwaza hivyo?
Mimi nikidhulumu, tangu lini kwanza, lakini si mbaya tusiongee mengi, hayo madini umeuza wapi na bei gani?
Lakini na Mimi nasimama wapi, nakua sehemu gani? akimaanisha anataka hela.

Wewe fika kwanza mengine tutaongea zaidi. nilijibu kifupi.

Ilaaa Dani hata kabla sijafika nikwambie tu ukweli umefanya vibaya kwa kufanya biashara hii pasipo kunishirikisha, na hii ishu jua kuwa huwa kunakuwa na umoja, watu au kundi mkipanga jambo basi linakuwa moja, Sasa kitendo cha wewe kuuza bila uwepo wanguuu, umefanya fault kubwa sana.
aliweka kituo huku akikata simu.

Huyu jamaa vipi yaani hajaniaga,
Hajatoa taarifa yeyote, halafu ananilaumu?
Huyu siyo mzima, na kuanzia leo haya akija sitaki anihusishe kwenye mambo yake ya kiuwendawazimu.
Madini, madini Mimi maisha yangu yanategemea madini?
Huyu chizi nini kwanza ngoja, tutaelewana tu.

Nilikata maji kisawasawa Kisha nikawasha chombo na kurudi nyumbani huku nikiwa makini sana na barabara maana ya MUNGU mengi.
Nilifika nyumbani huku nikiwa ovyo sana, ni wakati ambao mke wangu huwa hataki kukaribiana na mimi, huwa hapendi kabisa.

***************************************

Siku inayofuata nikiwa kazini nilijihisi nipo vyema kuliko siku zote sikuwa na wasiwasi wala stress yeyote, pia ni siku ambayo sikuwa na majukumu mengi sana, nikawa nipo tu nikiiwaza biashara ya madini.

Ah ingawa mambo yalikuwa ovyo hadi kumpata yule mzungu, lakini mbona kama ni biashara nzuri, yaani fasta tu nilipata hela mara mbili ya hela niliyowekeza, hivi ningekuwa nimeweka mzigo wa mkubwa sasahivi si ningekuwa vyema?

Hii ishu sipaswi kuiacha ni lazima niifanye nitahakikisha nafanya utafiti mwanzo mwisho, kisha nitajua mbivu na mbichi hii kazi ya kutegemea mshahara Kisha ufanye starehe ni ngumu. niliwaza huku nikijilaumu kuwekeza pesa kidogo, nikawa nishasahau adha niliyoipata .

Lakini kabla ya yote nampigia simu Jax nijue kama karudi ama la.
Nikapiga.

Oyaa nambie mwanangu wapi hiyo Ina maana hujarudi?
na kama umerudi uko wapi? niliuliza maswali mfululizo.

Nipo karibu na hotel ya (akitaja jina)
Nilijua muda wa wewe kutoka job bado ndiyo maana sijahangaika kukutafuta,. alijibu kiufupi

Basi ningoje nakuja hapohapo, agiza vinywaji nakuja, nilimjibu huku nikifungasha vilivyo vyangu na kutoka nje nikiamrisha mlinzi afungue geti, nikatoka huku nikiona kama ile hotel ipo mbali kwa siku hiyo.

Baada ya kufika nilishangaa kuona mshikaji wangu, mwanangu, na rafiki yangu amezongwa na maaskari huku akiwa analeta ugumu fulani kuondoka. nilijishauri mara mbili mbili kusogea pale, sasa dah huyu naye mbona ni mtihani?
Nikawa na akili tofauti, nimkimbie au nisogee tu nijue ana shida gani?
akili ikaniambia ni vyema nikae mbali kwanza maana mshikaji wangu namjua na mbanga zake za hapa mjini.

Nikatafuta sehemu nikajificha mahali
Kwenye kona Kisha nikazima simu,huku nikiona tukio zima linavyoenda.

Wewe fala sikia hela zako, jina lako visikufanye uvunje sheria kisa umaarufu wako, hebu inuka bwana, usitake tulazimishane.
ni jamaa mmoja akiwa anamtaka jamaa yangu ainuke.

Hela? umaarufu?
Mbona mnampa vyeo vikubwa sana, huyu ni boya mmoja tu asiye kuwa na lolote mjini, ni mtu mjanja mjanja anayedhani anaweza kufanya chochote halafu mamlaka zisijue, ni kweli alikuwa na pesa kipindi fulani lakini pesa zisizo za halali huwa hazidumu hata mara Moja. ni jamaa mwingine alifafanua.

Wakati huo watu wengi wakiwa wameshasogea eneo la tukio, na Kila mtu akiongea yake huku wale jamaa niliogundua kuwa ni askari wakiondoka na jamaa yangu kinguvu sana.

Kisha kwa huzuni na huruma nilitoka nje huku nikiiona defender ikiondoka huku jamaa wakimpiga baada ya kuwa aliwasumbua wakati wa kupanda gari,nilirudi ndani ya ile hotel huku nikiwa najifanya simjui Jax ikabidi nimuulize yule muhudumu.

Kwani yule jamaa kafanyaje na ana kosa gani? Mbona kabebwa kama vile ana tuhuma nzito kwani Kuna nini? niliuliza.

Eeeeeh we baba kwanza nakusikiliza una shida gani habari za watu achana nazo , umbeya tu mwanaume mzima.
alinizodoa yule dada.

Basi sorry sister naomba nipatie menu ili nichague nikitakacho, samahani Kwa kuwa nje ya mada.
nilijifanya kuomba msamaha.

Angalia kwenye hiyo TV hapo karibu yako Kila Chakula kipo na bei utaziona, na pia usijali kuhusu yule jamaa,
Ila kwa habari za chini chini ni kwamba yule ni tapeli.
alimdhulumu mtu eti atamletea madini lakini amekuwa akimzungusha tu huku hela akiwa ameshakula siku nyingi.
Lakini pia nasikia aliwekewa mtego na askari siku nyingi sana bila yeye kujua na amekuwa akishirikiana naye muda mrefu sana na huyo afande hadi pale alipojulikana kuwa anafanya biashara za magendo. alifafanua yule dada.

Sasa wewe umejuaje yote hayo wakati tukio lenyewe limetokea muda mfupi? niliuliza.

(Kwanza akacheka)
Huyu habari zake zinajulikana siku nyingi haswa kwakuwa hii ni hotel yake pendwa watu wengi tulijua atakuja tu,japo takribani wiki nzima hatukumuona. aliongea yule demu huku akikazana kama kuna menu nimeipenda nimwambie alete.
Nikampa buku tano na kumwambia kuwa sihitaji chochote ila Kuna mtu nilikuwa namtafuta ila simuoni.
nikasepa.

Ni askari gani kamchoma mwanangu, au ni yule fala Hussein? Lakini mbona kama wameshibana sana anawezaje kumfanyia unyama huu?

Dah mbona mtihani?
Ukisikia rafiki wa kweli ni kwenye shida na raha ndiyo leo. lakini Jax atakuwa kapelekwa kituo gani cha polisi?
Halafu mimi kwenda hukooooo , mmmmh nisije kuunganishwa kwenye matukio mwisho wa siku naangukia sehemu mbaya.

Niliwaza huku huruma ikiniingia nilitamani kujua Jax alipo ili nifanye utaratibu wa dhamana, lakini yupo kituo gani?
Ila kengele ya hatari ililia nikijua muda wote naweza kuwa mmoja wapo, kwani yule afande Hussein nilihisi alikuwa ni mtu anayempeleleza rafiki yangu Jax, hivyo huenda hata Mimi natafutwa maana ananijua tangu tulipouziana madini.

Niliendesha gari kwa tahadhari kiasi cha kuogopa kufika hata kwangu nikijua manyamwera wasije kuwa wametangulia kuweka mtego.

Nilipaki gari mbali kidogo Kisha nikatembea kwa miguu Hadi nyumbani na kulikaribia geti huku nikiwa makini kuangalia kulia na kushoto, lakini sikugundua chochote.
Nikagonga mlango mdogo huku ukifungiliwa kwa tahadhari.

Vipi wewe za hapa kwema?
Nilimsalimia kijana wangu wa pale home.

Safi kaka,vipi mbona kwa miguu kwema kaka? aliuliza.

Usijali, vipi Kuna mtu au mgeni yeyote alikuja hapa? niliuliza.

Hapana, walikuja tu wale wanachama wa mama na pia wameondoka , siyo muda pia hata mama kawasindikiza siyo muda. alijibu huku nikipata ahueni.

nilifuata gari Kisha nikaaingiza ndani huku nikitoa maagizo kutomfungulia mgeni asiyefahamika.
Huku ile biashara ya madini licha ya kufurahi baada ya kuuza na kuwa mzigo nishatua.
Lakini nikaona bado Kuna msala mzito kwenye ile biashara. nikijua Jax akibanwa mbavu sana anaweza kunitaja. hakika ilikuwa Moja ya siku mbaya zaidi.

Inaitwa Harakati za maisha, maisha lazima yaendelee , je itakuwaje? sehemu ijayo ina majibu.

Itaendelea.......................
 
Tunaomba muendelezo Leo tumeshakuwa mateja sasa

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA KUMI NA NANE

Niliamka saa kumi alfajiri nikatoka kuelekea nyumbani kwa Jastini lengo la kuwahi mapema ilikuwa ili nisiharibu ratiba za kwenda kazini.

Nilifika nikamuamsha mke wa Jax,

Kuna nini shemu mbona usiku hivi, usiku wenyewe sijalala , sijapata usingizi kabisa yaani.aliongea huku akijifuta machoni

Kwanini ukose usingizi Shemu.
niliuliza.

mambo anayonifanyia ndugu yako basi tu, juzi nilikwambia namna tunavyoishi, na ukweli kwasasa naondoka, japo nawaza wanangu wakija na kushindwa kumkuta mama yao hili nalo linanipa mawazo. ila ndugu yako hafai sijui ni mwanaume wa aina gani, umri wake na mambo anayofanya haviendani.
Napoongea hapa hajalala humu ndani , najua yupo kwa Malaya zake tu. Tangu afike huko alikokuwa namuona yupo busy tu, hataki kunipa hata muda wa robo saa nizungumze naye.

Kule dukani hakuna chochote nachouza na Jana sijafungua kutokana na kuona napoteza muda tu, nina madeni kibao kwenye vikundi vyetu , hata wewe ulivyonigongea muda huu nilijua ni wanakikundi wamefika hakika naumia shemu naumia mno. Leo siendi dukani na sina senti tano ya kula hata msaidizi wetu wa hapa nilishamruhusu siku nyingi sikuwa na cha kumlipa . aliongea yule mke wa Jax huku huruma ikiniingia vilivyo.

Sikutaka nimwambie kuhusu mumewe kuwa yupo mahabusu japo lengo la kwenda hapo ilikuwa kupeleka taarifa ile, ila aliyonieleza nikaona yanatosha ningemuongezea maumivu zaidi.

Basi shemu mimi nilipita tu niongee na jamaa mambo fulani Sasa kama hayupo basi ngoja niwahi kazini. niliaga huku nikiacha kumi moja maana sikuwa na namna.

Shemu kwanza nakushukuru sana, na pia naomba basi ongea na mwanaume mwenzio pengine atakuelewa , naumia, naumia sana.
alilalamika yule mwanamke.

niliwaza kwenda kwenye ile hotel ya Jana nikaona bado ni asubuhi sana, nikaelekea kazini huku nikikumbuka kitu, nilitaka nijue yule afande Hussein yupo kituo gani na hili nilikuwa nasahau mara nyingi. Lengo nijue maana nilihisi yeye huenda Kuna mchezo kamfanyia jamaa yangu.

Nikapiga simu kwa mke wa Jax lakini haikupokelewa licha ya kupiga mara kadhaa asubuhi ile nikiwa nazugazuga kupambazuke niende ofisini.

Harakati za Justini zikawa zinaenda vibaya sana maana Kila alichofanya kilienda kombo, nikaanza kuiwaza ajira yangu huku akili yangu ikiniambia hata kama nitamiliki biashara kubwa kiasi gani, lakini sitaacha kuajiriwa.
Maana Kuna muda unaweza kudhalilika hivi hivi.hata nilipwe mshahara mdogo kiasi gani bado nitakuwa kwenye ajira.

Nilifika ofisini huku nikikuta kuna ratiba mpya .

Daniel leo bwana unatakiwa kwenda sehemu (akitaja jina)
Tena imekuwa vizuri leo umewahi sana nasikia, yaani kwa despline hiyo unaweza kuorodheshwa kwenye watu watakaopanda daraja, tatizo nyinyi mmekariri kuwa Elimu kubwa ndiyo itakufanya upande cheo la hasha.

Nadhani hadi saa kumi na mbili utakuwa umesharudi, japo ripoti utaleta hata kesho, dereva yupo nje anakungoja . aliweka kituo huku nikiingia ofisini kwangu nikaswitch off baadhi ya vifaa.

Dah nilitegemea nitatumia nafasi hii kwenda kupeleleza habari za mshikaji wangu lakini huku nilikotupwa dah, sawa lakini ndiyo kazi zetu hizi hawakwambii mapema wanashtukiza tu, na ukihoji unatishiwa kuwa utapunguzwa.
Tukang'oa nanga huku dereva wangu akiwa mwenye furaha sana.uso wake ulionesha kitu.

Mimi hizi route za mbali nazipendea kitu kimoja tu Kuna vijichenji kibao unapata halafu unaendesha gari kwa raha yaani mjini unajibanabana mara foleni mara hiki. lakini huku burudani sana. aliongea yule dogo huku nikicheka kimoyomoyo maana anayoniambia hata sikujua maana yake nini.

Wakati huo mimi nilikuwa na mawazo kibao, nikaamua kuegama nitafute usingizi kinguvu japo usingizi ni kitu huja automatically.

Masaa mawili tayari tulikuwa eneo la tukio huku nikigundua dereva wa siku hiyo alikuwa na hamu na zile gari, na bado alikuwa ana hamu na safari za mbali hivyo mwendo wake ukawa siyo wa kawaida.

Oyaa kwani wewe unaitwa nani maana una drive kama upo kwenye mashindano mdogo wangu, huu si mwendo Kuna ajali zinaepukika. hakujibu akabaki kuchekacheka tu.

Yaliyonipeleka niliyakamilisha kisha nikageuza huku safari hii dereva kichaa licha ya kuambiwa apunguze mwendo lakini wapi, ni mwenye kujisahau kila saa .

Umesema una leseni daraja gani?
Na umesoma Chuo gani maana umeiva hadi umepitiliza, nilitania kisha akacheka.

Wapi itakuwa bro unadhani zaidi ya NIT,japo nilianza kuyajua magari nikiwa mtaani, ndiko nilikojifunzia
nikiwa naendesha magari makubwa, lakini pia ni operator wa mashine mbalimbali, na Mimi mbona nakufahamu ila wewe umenisahau kipindi kile ulikuja ukafumua D6 yote na kuirudishia huku ukikosa vijana wa kukusaidia ikabidi Mimi nijitolee huku
Ukiwa unanipa shilingi elfu mbili Kila siku jioni hakika ulinisaidia sana kwa kipindi kile. Mimi naitwa Saidi au Side.alijitambulisha.

Dah nimekukumbuka dogo, Sasa huku umefikaje kuwa dereva mkubwa? niliuliza.

Ndiyo maana nikasema wewe umenisahau, wewe ndiye ulinishauri kuwa Mimi ni dereva mzuri halafu umri wangu mdogo kwanini nisifanye mpango niende NIT ili nipate cheti?
aliweka kituo

Sawa nimekumbuka kwahiyo umenizidi Mimi siyo.niliuliza hasa baada ya kuona leseni yake Ina daraja kubwa kunizidi, dah hongera sana mdogo wangu maana kuufanyia kazi ushauri wa mtu ni dhahiri ulikuwa na Nia. nilimjibu.

Lakini na wewe hongera bro sikuwahi kufikiria kuwa siku moja nitakuwa dereva wako, kwanza ulifikaje huku maana Mimi najua wewe ni fundi?
aliuliza.

Yeah hata sasa mimi ni fundi japo nasimamia mafundi, ila kitu kikiwa kigumu basi navaa mavazi ya kazi. nilimjibu huku akionesha kufurahi kukutana na mimi ikabidi tubadilishane na namba kabisa maana ni mmoja wa madogo niliwakubali sana tangu zamani nidhamu, heshima na hata uvumilivu nikikumbuka kazi ilinielemea huko porini huku nikikosa msaidizi, watu wote dau nililotangaza waliona dogo wakaishia kunitukana wakidai Mimi napata pesa nyingi kwanini wao niwakadirie?
Ndipo alipojitokeza kijana mmoja ambaye alikubali kufanya kazi na Mimi kwa malipo ya buku mbili per day , huku nikigundua ni mchapakazi na anaelekezeka nikamshauri akasome .

Japokuwa nilikuwa namtania tu nikijua hatathubutu lakini dogo alifanya kweli, hatimaye ni mmoja wa madereva kwenye taasisi yetu ambapo sikujua aliingia lini.ila nilimpongeza sana.

Sasa hapa nipeleke nyumbani,nataka ukapajue na pia kesho asubuhi utanifuata sawa. nilimwambia.

Ah hiyo haina neno bro kuwa na amani wewe tena, aliongea huku akishika njia ya kuelekea home, nilifanya hivyo ili kujipa uzito maana majirani nao walizidi dharau maana wakikuona unaendesha gari mwenyewe wanakuchukulia poa. ila mara Moja moja ukiletwa na gari nyumbani angalau respect inakuwepo.

Nilifika home huku nikimtambulisha yule kijana Kisha akaondoka.

Mume wangu Kuna watu wawili walikuja na gari ndogo mida ya asubuhi, walisema niwaelekeze ofisini kwako nikasita nikaona si vema, ila wakaacha namba wamesema ukifika tu uwapigie. aliongea wife kisha akatoa kikaratasi fulani na kunipa kisha nikapiga kwa pupa huku nikiwa na wasiwasi fulani nilihisi kuna jambo halipo sawa.

Daniel naongea, mliacha namba kwa mke wangu, nilijitambulisha.

Unahitajika kituo cha polisi maeneo ya (akitaja jina) umeitwa kirafiki na Kwa heshima, kukaidi kwako ni kutafuta matatizo yasiyo ya lazima.

Fasta nilimpigia yule dogo ageuze gari anipeleke huku nikijua kwa kwenda na gari ile kutaniongezea uzito fulani, dogo hakuwa mbali akarudi Kisha nikaenda hiyo sehemu.

Itaendelea..........
 
Hapo ndo patamu 😁😁afande Chuse utamkoma kwa mkewe Mama Hanifa
 
SEHEMU YA KUMI NA TISA

Sasa bro wapi tunaelekea halafu mbona kama haupo sawa? aliuliza dereva wangu au mdogo wangu Side.

Twende kituo cha polisi cha (nikitaja jina) kuna watu nasikia walikuja kuniulizia asubuhi kwahiyo naenda kuitika wito wao.

Baada ya dakika kadhaa japo foleni nayo ilikuwa kikwazo pale Ubungo nilitamani gari ingeruka, huku kuna muda nikitamani nitembee kwa miguu, hatimaye tukafika kituo cha polisi tajwa.

Niliingia ndani kituoni, na kuwakuta askari wawili wakiwa pale Kaunda , mapokezi. nikawasalimia.

Nimekuta ujumbe nyumbani kuwa naitwa, hivyo nimekuja. nilijieleza huku nikiambiwa niketi.

Dah uliambiwa uje saa ngapi maana, hapa watu tumebadilishana na waliokuwepo asubuhi wamemaliza zamu, kwani unaitwa nani? aliuliza yule askari wa kike aliyevalia shuka la kimasai kwasababu ya baridi wakati huo,
Naitwa Daniel (nilitaja full name)

Aaaah kumbe ni wewe, niliachiwa maelezo kuwa ukifika nimpe afande (akimtaja jina)ngoja nimpigie simu, ila upo chini ya ulinzi na zunguka huku nyuma , aliongea yule askari huku akimuita askari fulani hivi mwenye silaha ili anilinde kisha yule mwanamke akatoka nje huku akibonyeza simu .

Alitumia muda mwingi sana, karibu saa nzima Kisha akarudi akiwa na askari wengine wawili, wakamwambia yule kijana aondoke aliyekuwa ananilinda ili eti nisikimbie.
Kukawa na jumla ya askari watatu wanaume wawili mwanamke mmoja

Ndiyo huyu, wakawa wanaulizana yule mwanamke akasema ndiye kwa mujibu wa maelezo aliyopewa kwenye simu.

Oyaa lile gari pale nje umekuja nalo wewe, aliuliza afande mmoja mnene, ambaye nilisikia akiitwa Big.

Yeah nimekuja nalo Mimi.
nilijibu kifupi.Kisha wakaangaliana kwa muda.

Ok sawa madini yako wapi, maana mmedhulumu weeeeeee, Hadi mmechoka,afande Hussein anatumiwa rubi na mkewe nyinyi mnanunua kwa bei rahisi na kuuza huku mkila Bata mjini , ila hiyo siyo kesi , kesi ni kwamba afande Hussein aliwauzia grams hamsini za Rubi japo mlimdhulumu grams mbili si neno. Ila mlimzunguka na kumtapeli hela kiasi cha million mbili nzima. Mwisho wa siku jamaa yako hapatikani wiki nzima, na pia ana madeni kibao hapa mjini huku mastermind ukiwa ni wewe. aliweka kituo yule afande wa kike.

Tena hili jamaa nasikia linapenda sana wake za watu, taarifa tunazo madam, hata wewe hapa unaweza Kuta keshakutamani. aliongea afande Big na kufanya wenzake wacheke.

Japo hata mimi nilicheka kimoyomoyo kuonekana nimemtamani yule afande, hapana Daniel napenda pisi kali jamani.

Weeeee amtake nani, kwahiyo kutumwatumwa na watu na hilo gari la watu ndiyo chambo ya kunipata mimi kwanza nashindwa kuelewa ni Mfanyakazi wa wapi huyu anafuga ndevu hivi, huu si uchafu huu. aliongea yule afande wa kike huku akinigusa kwenye kidevu na peni. hakika ilikuwa dharau ya aina yake.

Kutokana na haiba yangu ya upole huwa sipendi kujibizana nilikuwa mpole sana, Mimi kitu ambacho huwa nakiweza ni ngumi tu hilo MUNGU anisaidie sana , siwezi kubishana kwa maneno ila huwa nashangaa kibao kimenitoka tu.

Wewe chizi hebu njoo huku kwanza fala mwenzio tumemuhamisha hapa yupo central, shida yetu ni m2 tu, hivi nyinyi ni wajanja kushinda watu, au ndiyo mnajifunza utapeli siyo.

Hapana afande hata sijui nini kinaendelea mmeongea sana lakini kiukweli nipo njia panda ni vyema mkaniambia jambo lililo straight angalau nitakuwa najua nipo kwenye zone ipi.nilivunja ukimya.

Tapeli mwenzio yupo central na wewe tulitaka ukae ndani lakini kwakuwa afande Hussein kasema wewe hukuwepo hivyo tunakuruhusu uende mpuuzi wewe , yaani huyu ndiyo Daniel mbona ni boya mmoja tu sisi tukajua ni mtu wa maana.
waliongea wale maafande Kisha nikatoka na kupanda kwenye gari yangu muda huo ni saa nne za usiku.

Bro mbona umetumia muda mwingi vipi kulikuwa na nini umenipa wasiwasi ujue
aliongea yule dogo huku akiingia barabara kuu.

Ah Kuna vitu nilikuwa nahojiwa lakini freshi tu, sikutaka dogo ajue maana Kila mtu ana namna yake ya kufikiri na kupokea jambo, hivyo anaweza kuamini kuwa labda Mimi ni tapeli. Niliwaza kumuwekea dhamana Jax lakini ikawa ngumu kwasababu Mimi mwenye Kuna namna nahusishwa na ule msala.halafu lingine ilikuwa ni usiku sana hivyo isingewezekana.

Asubuhi dogo alinifuata huku niligundua bado ana hamu na gari ndiyo maana saa kumi na mbili tu akawa amekuja , madereva wengine Hadi uwalazimishe saa nyingine wanataka mpokezane kuendesha.

Siku hiyo nilipanga kwenda kumuwekea dhamana Jax, hivyo nikapiga suti yangu matata huku nikinyonga Tai, licha ya kuwa joto lilinisumbua lakini nilivumilia ili nitimize azma yangu.

Baada ya kuwa kazi zimepungua nilitafuta kisingizio ili nitoke, nikapewa gari ili ni match wadhifa wangu.
Saa tano kamili nilikuwa kwenye ile central, ila nilishangaa kumuona jax akiwa anatoka ameongozana na wanawake wawili na mwanaume mwingine mmoja ambao wote sikuwatambua ila nikahisi ni ndugu zake.

Pole sana mwanangu dah, huo ndiyo uanaume, matatizo tumeumbiwa binadamu. nilimwambia hivyo mara tu baada ya kusalimiana.

Wewe achana na mimi Dani, tena usijisimbue kwa lolote fanya habari zako tu kwani hapa kakuelekeza nani? nipo huru , nipo uraiani MUNGU kanipigania. aliongea Jax nikimuona ana hasira za wazi kwangu hata ndugu zake walimshangaa.

Hebu ingia kwenye gari tuongee Jastini, Mimi na wewe tumetoka mbali na najua unajisikia vibaya sana ila usihukumu kabla ni vyema tukaongea najua hasira yako Iko angle ipi. niliongea kwa sauti yenye utulivu.

Dada na ndugu zangu wote nawaombeni muende tu nyumbani Mimi naongozana na huyu na ndiye Dani ambaye nimetoka kuwaambia habari zake. Jax aliagana na ndugu zake.

Tukiwa kwenye gari Jax alikuwa akitabasamu kwa hasira huku akionesha kachukia sana Kisha akavunja ukimya,

Ina maana Dani hukupata hata chembe ya taarifa kuwa Mimi nipo ndani , na juzi nilikuita pale hotelini Ina maana hukupata taarifa yeyote?

(Huku akicheka)
Tuache hayo , kwani ndugu zangu wamenitafuta wamenipata ,
Yaani Ukiwa kwenye hili gari basi unajiona kama nani Dani ,
Halafu jamaa ukamu***** mke wake.

Dani mbona una utoto sana? Nilishindwa hata kukutetea siku ile kwani niliona Kuna ukweli ndani yake, huwafikirii wenzio?
Hivi kama wewe yule mkeo mama *****watu wakaishi naye hujawaza ni maumivu gani utapata?
Usichopenda kufanyiwa usiwafanyie wenzako..............

Kabla hajamalizia sentensi yake nilimkatisha,

Halafu sijui nikuweke kwenye kundi gani wee Jax yaani nilitegemea tuongee unawezaje kulipa hela za watu ulizodhulumu unaongea mambo ambayo hayana msingi wala huna ushahidi nayo? nilihamaki huku nikipaki gari pembeni tuongee vizuri.

Ahaaa kumbe umeshindwa kunidhamini kwa wakati, umeenda kunipeleleza, ndiyo maana nasema wewe ni mnafiki , yaani unajiona una heeeeela Dani,
Una hela gani bro,
Nikwambie tu ukweli pigo langu moja la Rubi au dhahabu nikiliotea. naagana na umasikini wewe hunipati hata mara Moja Dani nilikuwa na hela wakati huo wewe unaokota mizizi kwenye barabara za vumbi ilipopita excavator unajisahaulisha? aliongea kwa maudhi Jax.

Ni kweli ulikuwa na hela bro,
Lakini mla leo mla leo mla jana kala nini? cha muhimu tuzungumzie linalokikabili , una deni la million mbili kaka hiki ndiyo cha kujadili kwa sasa.
Usilete habari za eti nikiotea nini ama Nini? unadhani maisha ya Sasa yanataka kamari na hesabu za ndoto? niliongea huku nikishangaa.

Daniiiii hebu kwanza niache unazidi kunikera tu, million mbili ndiyo niiwazie mimi, unajua nilikuwa naikata siku moja tu, kweli wewe Dani masikini ndiyo maana Kila nikikutangazia fursa huwa unakuwa mgumu kitu cha laki tano Hadi umshirikishe mkeo, kwanza nashuka wewe nenda bwana. aliongea huku akishuka kwenye gari kibabe.

Hata Mimi nilikasirika nikatia gia, nikaishia.

Itaendelea..............................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom