Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,154
- 10,416
Napenda sana kusoma vitabu, hali hii imenifanya nipende kuandika visa kadhaa ambavyo huwa ni vya kweli, Sina visa vya kutunga.simulizi zote zina ukweli kwa asilimia nyingi.lakini pia nitahadharishe , lugha zisizofaa huwa sipendi na kutukana siwezi, si kwamba siyajui matusi lakini huwa sioni faida yake.
Hii ni simulizi mpya ambayo inanihusu moja kwa moja, lengo likiwa ni moja tu burudani kwa wanajamvi,Code na vigezo vingine vimezingatiwa tiririka.........
SEHEMU YA KWANZA.
Kwa mara ya kwanza nilishiriki kampeni kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015,huku Mimi na washikaji zangu, tuliamua kujitosa kwenye zile kampeni baada ya mkubwa wetu wa kazi kutulazimisha tumuunge mkono kiongozi ambaye hakuna mtanzania yeyote aliwaza kuwa angekuwa Rais wa nchi, na kizuri zaidi hata yeye alikuwa anasema hakutegemea kuwa angeweza kuwa na cheo hicho cha juu.
Nikiwa karibu na nyumbani kwenye bar moja local nikiwa na konyagi ndogo na maji, simu yangu iliita nikaipokea,
Oyaa bob vipi uko wapi, aliongea yule jamaa yangu bila hata salamu.
Nipo home tu, vipi nambie bob, nilimjibu.
Oyaa jamaa naye kakatwa, huwezi amini amebaki (jina kapuni) pamoja na wanawake wawili, hebu niambie ni nani anaweza kushika kijiti? Jamaa yangu aliongea kwa mfumo wa swali Kisha akakata simu.
Nikapiga ili anipe data kamili akawa hapokei simu, licha ya kupiga mara kadhaa bado simu haikupokelewa,
Dah huyu mwafulani nilitegemea yeye ataweza kushika kijiti baada ya yule mwingine kukimbilia upande wa pili, kumbe naye kakatwa? nilijiuliza sana Kisha nikajikuta nacheka mwenyewe huku nikishindwa kuamini kama jamaa yetu kaingia top three.
Hata baada ya kuzama social network nilikuta kumechafuka , habari hiyohiyo, nikaamua kuachana na habari zile nikaendelea na nyagi zangu huku nikipokea simu kadhaa kwa watu mbalimbali zinazohusiana na ile habari mpya mjini.
Kesho nikiwa ofisini alikuja mkubwa wangu tukasalimiana , huku akionesha furaha ya moja kwa moja.
Dani eeh, nadhani umesikia ulichosikia , Sasa nakuomba wewe na wenzako mpo wengi inabidi tumsapoti mheshimiwa sawa . aliweka kituo.
Aaaaaaah Sasa boss Mimi na siasa wapi na wapi hapa nilipo hata sijui nipo chama gani cha siasa, halafu hata sijui naanzaje yaani, kifupi boss naona kama inaniwia vigumu , kama siasa ni kipaji basi nadhani kipaji hicho sina,. Niliongea huku nikijichekesha kwani nilikuwa naongea na mtu mkubwa sana kwangu.
Sikia Daniel Mimi nakujua mwanzo mwisho kuwa hujui kitu, kwani akina fulani wanajua nini? (aliwataja majina) lakini nishawaorodhesha!
Halafu najua Dani ni mtu wa kusahau wewe unajua fika Mimi nipoje na huyu mtu na pia hata wewe unamjua huyu mtu kwa kipindi kirefu sana aliongea huku akinikumbusha mambo mengi kiasi cha Mimi kutokuwa na pingamizi.
Sasa boss labda nikuulize, nitakuwa kwenye nafasi gani kwenye hii ishu maana nipo gizani. niliuliza
Ninachohitaji ni utayari wako tu, kuhusu cha kufanya utaelekezwa sawa. alinijibu Kisha akatoka.
Nilifikiria kwa muda Kisha nikaona moyo unapiga, niliwaza nitavyovaa mavazi ya ile rangi iwe kapelo , fulana na vingine nikajikuta sipendi kama nini ili sikuwa na namna.
Ikawa imebaki siku ya nani atapitishwa ili tuingie kwenye ule mpango, nakumbuka nikiwa home nilikuwa mubashara nikiangalia Television ya taifa kwa lazima kwani huko ndiko taarifa zote zilipatikana , nikawa active kwenye mitandao ya kijamii lengo nisiwe gizani , yaani nikiulizwa chochote iwe rahisi kujibu.
lakini nililazimika kujitengenezea TV ya chumbani maana nilishakuwa kero
Kwa familia lakini hata mke wangu alishtuka kidogo akauliza.
Mwenzetu si kawaida yako kufuatilia siasa zaidi ya taarifa ya habari ya kawaida, halafu watu sijui mkoje Kuna channel huwa unasema huipendi lakini nakuona kutwa huitoi vipi? aliuliza mke wangu.
Lakini sikumwambia chochote zaidi ya kusema nimeamua tu, labda ndiyo mwanzo wa kuijua siasa kwani hata hao wanasiasa hawakuanza tu.
My wife aliniamini na hakuwahi kuniuliza chochote tena, basi Mimi na washikaji zangu tulikutana maeneo fulani tukakaa na kujadili kiundani kuhusu kazi ya kutoa sapoti iliyopo mbele yetu, hakuna aliyekuwa anajua chochote tukajikuta tunacheeeeka, tukijua tushaingia cha kike mbaya zaidi nani angepinga maamuzi ya boss? Tukapiga maji yetu tukaagana.
Baada ya masiku kadhaa nilikuwa home nimetulia huku nikifuatilia kwa umakini yanayoendelea Dodoma,huku marafiki zangu wakiwadai wameenda kwenye tukio labda kwakuwa walikuwa na ile hamu lakini Mimi sikuipenda ile hali basi tu.
Mwamba akapita freshi huku nikistuka kumuona mgombea mwenza mwanamke kwa mara ya kwanza kwenye nchi yetu.
Baada ya lile zoezi niliingia mtaani kama kawaida nione sura watu wamelipokeaje, kumbuka upande wa pili Nako alisimama mgombea mwenye nguvu hivyo Mimi nikawa nashindwa kujua Nini kitajiri.
Baada ya siku tatu tuliitwa na boss wetu akatuambia kuwa zoezi ndiyo litaanza rasmi hivyo kwa kipindi chote cha kampeni tutakuwa kwenye msafara kila atakakokuwa mgombea na sisi tutakuwepo, jasho lilinitiririka sana tu , tena mno. huku nikishangaa wenzangu hawana wasiwasi kabisa ndiyo kwanza wanafurahia.
Mimi nadhani tumekubaliana na niwashukuru nyote kwa kuweza kukubali kushirikiana katika hili, japo nisiwafiche, namuona kama Daniel tunamlazimisha hivi, eeh eti Dani upo sawa? Kumbuka hata Dodoma hukuwepo, sijakulaumu kwakuwa kazi yenu ilikuwa bado ila kwasasa unatakiwa utuweke wazi kama utakuwa na sisi ama la! aliongea boss huku akinitazama bila kupepesa macho.
Hapana boss Mimi nipo na wewe na nitakuwa na wewe bega kwa bega tuliagana huku tukipewa baadhi ya taratibu tukaagana, lakini bado ule moyo sikuwa nao , ikabidi nimpigie simu baada ya kufika nyumbani.
Samahani boss kwani Kuna ulazima wowote wa kuvaa sare za chama? niliuliza swali ambalo ni kama niliropoka tu.
Alicheka sana Kisha akaniambia,
Sisi hatupo kwenye chama Dani sisi tupo kwenye kumsapoti mheshimiwa, kwani kuvaa hizo nguo ndiyo nini, unaweza kuvaa na ukawa moyo upo kwingine, na pia umesahau kama majukumu yetu yapo tofauti, halafu Dani sijui huwa upoje , hebu punguza pombe bwana, inawezekana Kila tunachojadili huwa hauko makini nacho. alikata simu huku nikigundua dizaini kama kachukia hivi.
Kesho asubuhi alinipigia simu na kuniambia kuwa, amekaa na kufikiria amegundua kuwa Mimi sipo pamoja na wao hivyo niendelee na majukumu ya kiofisi kama kawaida. licha ya kumbembeleza lakini ilishindikana, nikaamua kwenda ofisini kwake.
Ananiachaje kwenye huu mpango Sasa, haiwezekani.
Itaendelea.....................