Janie_Kelvin
Member
- Jun 5, 2022
- 33
- 51
Sehemu ya kwanza
Katikati ya msitu mnene, giza zito likiwa limetanda kila kona ya msitu huo alionekana kijana akikimbia huku jasho likimtoka ni dhahiri alikuwa amekimbia kwa muda mrefu sana na alikuwa na hofu iliyopitiliza huku nyuma sauti tofauti tofauti zikimfuata kadri alivyokuwa akizidi kukimbia ili kujiokoa na jambo hilo.
“Harry! Harry! Haaaarry! Hahahahahahah” Sauti hiyo ilizidi kumsogelea huku vicheko tofauti vikichukua nafasi ya kumuogopesha zaidi na zaidi.
“Harry!! Harry! Harry!. Hapo alisimama kisha akafumba macho yake kisha akageuka nyuma taratibu na kuyafumbua macho yake tena.
“Ni ndoto mbaya? Harry!”
Harry alipofumbua macho alimuona mama yake ameketi pembeni yake huku akimtizama kwa umakini.
“Mama!”
“Nimekuita muda mrefu Harry inaonekana ulikuwa ukiota tena ndoto mbaya ona jasho linakutoka”
“Ni kweli mama it’s bad dream” Alimsimulia mama yake jinsi alivyoota ndoto hiyo mbaya huku bado akionesha hofu sana usoni.
“Pole! Muombe Mungu akuondolee ndoto mbaya mwanangu Sawaa?”
“Sawa mama”
“Sasa leo nafasi ipo ya kutosha kesho kanisani na unajua kabisa wiki ijayo it’s your 20th birthday so twende leo tukafanye shopping ya mahitaji yote nataka siku yako iwe ya kipekee sana”
“But mama……”
Kabla hajamaliza kuongea tayari alishamziba mdomo ili asiendelee kuongea.
“Najua Harry lakini look kwa miaka karibia mitano your daddy hakuwahi kusherehekea kuzaliwa kwako huoni hii ni nafasi nzuri kufurahi tukiwa pamoja na baba yako?”
“Nakuelewa unachomaanisha mama kwakuwa umependekeza hivyo I have to accept that”
“Yes! Good boy that’s why I love you, haya inuka kajiandae then twende”
“Okay mom”
Aliinuka na kuelekea bafuni ili ajiandae na hapo mama yake alimuacha ajiandae na yeye alishuka chini kuendelea na kazi nyingne alifanya kila kitu yeye mwenyewe hakuhitaji mdada wa kazi kumsaidia kwani kazi zake hazikumfanya kuwa bize kiasi cha kushindwa kufanya shughuli za nyumbani kama mama.
Maisha yao yalikuwa ya kifahari sana kutokana na kuwa na pesa, pesa kwao haikuwa tatizo kabisa waliweza kusafiri kwenda nchi yoyote waliyotaka.
Mr Maurice Hilary na Bi Hannah Mollel ndio wazazi halisi wa kijana Harry, mtoto wa kwanza na wa pekee kwenye familia hiyo, walimiliki kampuni za madini na mafuta pamoja na miradi midogo midogo mbalimbali nyumba za kifahari.
Miaka takribani kumi walikuwa nje ya nchi walizunguka nchi tofauti tofauti karibia saba tokea Harry ana miaka mitano hali hiyo iliwafanya kuwa na uzungu fulani kwenye maisha yao hivyo kwa upande mwingine waliishi kama wazungu.
Baada ya kurudi nchini ilipita miaka mitatu Harry alipendekeza apate chuo hapa Tanzania asome japo wazazi wake hawakupenda asome ndani ya nchi ila kwa sababu alikuwa mtoto wao wa pekee waliheshimu ombi lake kwa muda huo ndipo alipoanza masomo yake ya chuo kikuu akiwa kijana mdogo kabisa kutokana na kuwa kijana mwenye akili nyingi ya kuchanganua vitu tofauti.
Sasa zilikuwa zimebaki siku chache kuifikia siku ya kuzaliwa kwa kijana Harry alitarajia kutimiza miaka ishirini tokea kuzaliwa kwake, na walipanga kufanya tafrija ili kumpongeza mtoto wao wa pekee.
“Hubby! Bado unafikiria kuhusu ndoto uliyoota? Kwanini hutaki kuniambia nini umeota? Ila hata Harry ameota ndoto mbaya sana” Aliongea Bi Hannah akimwambia mume wake.
“No mke wangu sio ndoto mbaya hata hivyo siwazi kuhusu ndoto, nafikiria nimepata safari ya ghafla ya kikazi”
“Mmh lini?” Aliuliza kwa kuhamaki
“This time Hannah! But I want to spend much more time with my family, si unajua next week ni birthday ya Harry sitaki kumdisappoint”
“So what is your plan?”
“I want to send the representatives”
“But are you comfortable?”
“Yes love I’m very okay, na nina furaha sana kwasababu tutakuwa pamoja kwenye Harry’s 20th birthday”
Bi Hannah aliishia tu kutoa tabasamu na kuendelea kuandaa kifungua kinywa kisha waondoke.
“Am…. Nilisahau tutatumia ile BMW honey!”
“It’s okay hamna shida hata mkichukua yote mimi nitakodi taxi” Aliongea kiutani Mr Hilary na kumfanya mke wake acheke.
“Kitakuwa kituko cha siku hahahah magari matano yote tutajigawaje?”
“Hahahah……..Nahitaji kwenda kuweka mambo Sawa ili tuweze kuwa pamoja wiki ijayo”
“Sawaa hamna shida”
Muda huo ndio Harry alikuwa akishuka kutoka juu ili ajumuike na wazazi wake kupata kifungua kinywa, hakuwa sawa kama siku zote kutokana na mawazo aliyokuwa nayo juu ya ndoto aliyoota.
“Daddy!!! Good morning”
“Good morning my boy are you okay?”
“Yes Daddy I’m okay”
“Usiwaze sana kijana wangu hiyo ni ndoto tu japo sio nzuri just pray hard” Aliongea huku akimpiga Piga begani.
Wakati wakiendelea kupata kifungua kinywa simu ya Mr Maurice iliita naye alisita kidogo kuipokea baada ya kuona mke wake amehamishia umakini wote kwake.
“Excuse me!! Sitaki kuwakosesha breakfast” Aliinuka na kwenda pembeni kidogo ili aongee na simu.
“Eeh!! Ha..hallo!..”
“Najua! Najua lakini sio kwa vishindo hivyo jamani ingekuwa vyema kama tukienda taratibu Eeh mambo gani haya jamani”
“Sa..sawaaa Hamna shida nimeelewa vizuri kiongozi, Sawaa” Alisikika Mr Maurice akiongea na haikujulikana anaongea na nani kwenye hiyo simu.
Alivyomaliza aligeuka ili arejee mezani macho yake yalikutana na mke wake ambaye alikuwa amekishika kiuno chake.
“Hubby ni nani huyo mbona ni kama una wasiwasi sana?”
“Usijali mke wangu ni mambo tu ya kazi na unakumbuka nilikuambia ilihitajika nisafiri? Nilikuwa najaribu kuweka mambo Sawaa”
“Really?”
“Yes! Wife twende tukaendelee na chai unajua mtoto atajisikia vibaya” Alimshika mkono mke wake na kurudi tena mezani lakini hawakumkuta kabisa Harry, waliishia kuangalia na tu , wakati wakijiuliza Harry yuko wapi walimuona akishuka kutoka juu akiwa tayari kwa safari.
“Mom mimi niko tayari”
“Chai mwanangu…”
“Nimeshiba mama”
Mr Maurice alimgeukia mke wake na kumwangalia kama kumpa ishara fulani naye akaitikia kisha akapandisha juu kwenda kuchukua funguo pamoja na vitu vyake muhimu vidogovidogo vya muhimu kwaajili ya kuondoka navyo.
“Son!! Najua unawaza kuhusu ndoto ni Sawa ila usiwaze sana keep praying hard, usiruhusu ikutawale sana”
“Daddy I understand the situation, naelewa vizuri sio kama nawaza sana kuhusu ndoto ila siko tu poa kwa leo worry out King”
“It’s okay, we nenda na mama nilitamani sana tungeenda wote ila nina majukumu”
“Usijali baba”
Bi Hannah alikuwa akishuka kutoka juu taratibu huku akiwaangalia baba na mwana wakiwa wanaongea.
“Hubby ungependa kuongozana nasi?”
“Nilitamani iwe hivyo ila nina majukumu mke wangu, mkaniwakilishe tu usisahau kuninunulia ile suti niipendayo”
“Hahah…. Umekumbuka hiko tu yaani sawa, Son let’s go”
Harry alimfuata mama yake na wote wakaondoka muda huo, Mr Maurice aliichukua simu na kupiga namba aliyoijua yeye na punde tu ilipokelewa na aliinekana akiongea kwa hasira sana kisha akakata simu na kuondoka, alitoka ndani na kuingia kwenye gari kisha akapiga moto na kutokomea.
Bi Hannah na Harry licha ya kuwa mwendoni kwa dakika karibia ishirini lakini hakuna aliyetoa neno lolote kulikuwa na ukimya wa ajabu ndipo Bi Hannah alipoamua kuuvunja ukimya.
“Harry! What’s up Son mbona kinyonge?”
“That house…… that house sometimes is full of drama, nashindwa kuelewa nini shida”
“Harry!…”
“Please Mom just… just stay calm”
Bi Hannah aliishia tu kumtizama mwanaye bila kutoa neno na alielewa kitu ambacho Harry alimaanisha.
ITAENDELEA….