Simulizi: Bodaboda wa Mke wangu

Apr 19, 2023
77
123
Kulikuwa na kijana mmoja aliitwa Prince, alikuwa ni bodaboda aliyekuwa jirani yetu, tulikuwa tunamwamini na hata kumpa baadhi ya mizigo yetu ya msingi atupelekee mahali tulipotaka ifike.

IMG_7833.jpg

Huu ni utaratibu wa kawaida kwa familia zetu za mjini. Kwa sababu tulimuamini, mke wangu alikuwa akimtumia sana katika safari zake, mimi kiuhalisia sikuwa nikimtumia maana mm sio mtu wa kukaa nyumbani, niko bize na kazi zangu, nilimtumia tu pale ambapo labda niko nyumbani na nahitaji kufikisha mzigo fulani mahali na mke wangu ndiye aliyekuwa akinisuggestia kuwa tumpigie Prince apeleke, ndo maana mimi nilikuwa nikimuona kama bodaboda wa mke wangu.

Basi mke wangu yeye katika safari zake zote kila alipotaka kwenda, ni kumpigia prince aje ampeleke. Karibia safari zote za mke wangu Prince alikuwa akizijua, na mimi binafsi sikuwa na wasiwasi na prince kwa sababu hiyo ni biashara kama biashara nyingine na mtu hufanya biashara na anayemuamini. Hata baada ya kuja hizi Bolt na Ubber ambazo mtu akifanya request gharama zinakuwa chini kuliko gharama za bodaboda wa kawaida, lakini bado mke wangu yeye aliendelea kumtumia Prince kwenye safari zake ijapokuwa nilimshauri hilo, pia haikuwa shida kwangu maana niliona sio mbaya as long as prince ni mtu tunamuamini.

Sasa ikafika hatua prince akawa family friend, akawa anakuja nyumbani kama siku za mechi hivii, anakuja kuangalia mechi za Ulaya tunafurahi maisha yanaendelea na mambo mengine madogo madogo tunapiga tu story kawaida.

Basi ilitokea hiyo siku moja nimesafiri nimeenda mkoani, Nipo huko usiku mida ya saa nne hivi, nilikuwa hotelini ambapo nilikuwa nimefikia na ilikuwa ni safari ya kikazi, Basi nikapokea simu kutoka kwa dada mfanyakazi wa pale nyumbani, akaniambia kaka kuna vurugu hapa ndani, Prince anagombana na dada (mke wangu) nikawa namuuliza shida ni nini?

Alikata simu maana hata kunipigia alikuwa anaongea kiuogauoga. Napiga tena akawa hapokei. Niliwaza ni nini kinachoendelea huko nikawa sielewi. Ugomvi wa mke wangu na Prince umeanzia wapi? Na Prince anatafuta nini hapo nyumbani usiku wote huo? Niliwaza sana nafanya nini nikawa sielewi.

Nilimpigia mke wangu na yeye akawa hapokei simu kabisaa, nikampigia huyo huyo Prince na yeye akawa hapokei simu. Niliwaza sanaaa, lakini sipati majibu nifanyeje. Nilimpigia rafiki yangu Amoni anisaidie kufika nyumbani aangalie kuna nini kinachoendelea.

Amoni mara ya kwanza hakupokea, nikaelewa ni kwa sababu ni usiku sana, yawezekana amelala. Baadaye nikampigia tena, akapokea namuuliza kama yupo kwake ananiambia yupo club, halafu sasa hiyo club ni mbali na nyumbani, nikamwambia atoke nje sehemu iliyotulia tuongee mara moja akasema sawa. Nasubiria atoke nje anipigie jamaa hapigi, nikasubiria sanaa Ikabidi nimpigie tena, hapokei, nampigia mara ya pili ndo akapokea akaniambia anatoka nisubirie mara moja.

Basi ndo akawa ametoka akanipigia, kumbe ameshalewa hadi kulewa ndo sababu ya usumbufu wote. Nikamuuliza kwani uko nani akanitajia washkaji wengine aliokuwa nao nikamwambia anipe fulani niongee naye, akaingia ndani na kumcheki akamtoa nje ndo nikaongea naye, bahati nzuri yeye alikuwa hajalewa na nililijua hilo ndo maana nikamwambia nipe fulani, basi huyo jamaa nikamueleza kinachoendelea, nikamuomba anisaidie kufika nyumbani haraka kuangalia usalama maana hapa nimeshajaribu kila namna. Nimecheki hadi jirani yangu mmoja hivii naona ameshalala.

Jamaa akasema sawa sawa ngoja tuelekee huko. Alimchukua Amoni na pombe zake wakaenda nyumbani kwangu njiani akawa anamueleza Amoni kinachoendelea. Sasa walienda wakafika kwangu wakakuta kuko kimya, watu wote wamelala Ikabidi wagonge mlango.

Waligonga na kugonga lakini wapi, hakuna mtu anafungua mlango wakajaribu kuita lakini wapi kuko kimya, sasa wasiwasi wao ukawa ni hawaelewi kuna watu humo ndani au hakuna mtu, walimuita sana mke wangu lakini hakuna anayeitika humo ndani, waliogopa hata kunieleza kinachoendelea ila ilibidi tu wanipigie na kuniambia kuwa waligonga mpaka kidogo wavunje mlango lakini hakuna hata mmoja anayetingishika.

Sasa hawaelewi kuna nini kinachoendelea niliwaambia, sasa fanyeni hivii, muibukieni Prince. Nendeni kwake, mfikieni mjue nini kinachoendelea Walienda kwa Prince walifika kwake wakagonga mlango ukafunguliwa, unafunguliwa anatoka rafiki yake Prince wakamuuliza prince yuko wapi, Akawajibu Prince tangu alipoondoka hapa saa mbili hajarudi mpaka saivi. Wakamuuliza kama hakuna mahali anahisi atakuwepo, akasema hapana, maana yule ni bodaboda anaweza kuwa mahali popote kulingana na wateja wake.

Wakamwambia basi fanya hivii, mpigie simu Jamaa akampigia simu Prince, simu ikaita lakini haipokelewi. Akapiga tena haipokelewi, alipopiga mara ya tatu simu ikawa haipatikani, ikiwa na maana Prince amezima simu. Walichokaa, wakanipigia simu kunielezea yote hayo ambayo yametokea, nilichoka pia. Wakati huo mke wangu naye simu haipatikani tena, dada wa kazi yeye hapokei.

Nini kinachoendelea hapa? Mke wangu na dada wa kazi wako wapi? Zile zilikuwa ni vurugu za nini? Prince na yeye kaenda wapi? Maswali yote haya nilijiuliza bila kuwa na majibu yake, marafiki zangu waliniomba niwaruhusu wakapumzike kwanza, kesho asubuhi na mapema wataamka na hilo iIlikuwa ngumu kuwaruhusu waende kwao kupumzika, lakini hata nikiwakatalia, wabaki waendelee kufanya nini maana huo ulikuwa ni usiku wa saa saba tayari.

Usikose sehemu ya pili ya story hii maana hayo maswali ambayo uko nayo moyoni mwako yatajibiwa yote. Baki na mimi hapa hapa.
 
Kulikuwa na kijana mmoja aliitwa Prince, alikuwa ni bodaboda aliyekuwa jirani yetu, tulikuwa tunamwamini na hata kumpa baadhi ya mizigo yetu ya msingi atupelekee mahali tulipotaka ifike
View attachment 2608995







Huu ni utaratibu wa kawaida kwa familia zetu za mjini. Kwa sababu tulimuamini, mke wangu alikuwa akimtumia sana katika safari zake, mimi kiuhalisia sikuwa nikimtumia maana mm sio mtu wa kukaa nyumbani, niko bize na kazi zangu, nilimtumia tu pale ambapo labda niko nyumbani

na nahitaji kufikisha mzigo fulani mahali na mke wangu ndiye aliyekuwa akinisuggestia kuwa tumpigie Prince apeleke, ndo maana mimi nilikuwa nikimuona kama bodaboda wa mke wangu.
Basi mke wangu yeye katika safari zake zote kila alipotaka kwenda, ni kumpigia prince aje

ampeleke.
Karibia safari zote za mke wangu Prince alikuwa akizijua, na mimi binafsi sikuwa na wasiwasi na prince kwa sababu hiyo ni biashara kama biashara nyingine na mtu hufanya biashara na anayemuamini.
Hata baada ya kuja hizi Bolt na Ubber ambazo mtu akifanya request

gharama zinakuwa chini kuliko gharama za bodaboda wa kawaida, lakini bado mke wangu yeye aliendelea kumtumia Prince kwenye safari zake ijapokuwa nilimshauri hilo, pia haikuwa shida kwangu maana niliona sio mbaya as long as prince ni mtu tunamuamini

Sasa ikafika hatua prince akawa family friend, akawa anakuja nyumbani kama siku za mechi hivii, anakuja kuangalia mechi za Ulaya tunafurahi maisha yanaendelea na mambo mengine madogo madogo tunapiga tu story kawaida.

Basi ilitokea hiyo siku moja nimesafiri nimeenda mkoani,
Nipo huko usiku mida ya saa nne hivi, nilikuwa hotelini ambapo nilikuwa nimefikia na ilikuwa ni safari ya kikazi,
Basi nikapokea simu kutoka kwa dada mfanyakazi wa pale nyumbani, akaniambia kaka

kuna vurugu hapa ndani, Prince anagombana na dada (mke wangu) nikawa namuuliza shida ni nini?!
Alikata simu maana hata kunipigia alikuwa anaongea kiuogauoga.
Napiga tena akawa hapokei
Niliwaza ni nini kinachoendelea huko nikawa sielewi. Ugomvi wa mke wangu na Prince umeanzia

wapi? Na Prince anatafuta nini hapo nyumbani usiku wote huo?!
Niliwaza sana nafanya nini nikawa sielewi.
Nilimpigia mke wangu na yeye akawa hapokei simu kabisaa, nikampigia huyo huyo Prince na yeye akawa hapokei simu.
Niliwaza sanaaa, lakini sipati majibu nifanyeje

Nilimpigia rafiki yangu Amoni anisaidie kufika nyumbani aangalie kuna nini kinachoendelea.
Amoni mara ya kwanza hakupokea, nikaelewa ni kwa sababu ni usiku sana, yawezekana amelala.
Baadaye nikampigia tena, akapokea namuuliza kama yupo kwake ananiambia yupo club, halafu

sasa hiyo club ni mbali na nyumbani, nikamwambia atoke nje sehemu iliyotulia tuongee mara moja.
Akasema sawa
Nasubiria atoke nje anipigie jamaa hapigi, nikasubiria sanaa
Ikabidi nimpigie tena, hapokei, nampigia mara ya pili ndo akapokea akaniambia anatoka nisubirie mara moja

Basi ndo akawa ametoka akanipigia, kumbe ameshalewa hadi kulewa ndo sababu ya usumbufu wote
Nikamuuliza kwani uko nani akanitajia washkaji wengine aliokuwa nao nikamwambia anipe fulani niongee naye, akaingia ndani na kumcheki akamtoa nje ndo nikaongea naye, bahati nzuri yeye

alikuwa hajalewa na nililijua hilo ndo maana nikamwambia nipe fulani, basi huyo jamaa nikamueleza kinachoendelea, nikamuomba anisaidie kufika nyumbani haraka kuangalia usalama maana hapa nimeshajaribu kila namna,
Nimecheki hadi jirani yangu mmoja hivii naona ameshalala

Jamaa akasema sawa sawa ngoja tuelekee huko, Alimchukua Amoni na pombe zake wakaenda nyumbani kwangu njiani akawa anamueleza Amoni kinachoendelea,
Sasa walienda wakafika kwangu wakakuta kuko kimya, watu wote wamelala
Ikabidi wagonge mlango

Waligonga na kugonga lakini wapi, hakuna mtu anafungua mlango
Wakajaribu kuita lakini wapi kuko kimya, sasa wasiwasi wao ukawa ni hawaelewi kuna watu humo ndani au hakuna mtu, walimuita sana mke wangu lakini hakuna anayeitika humo ndani, waliogopa hata kunieleza kinachoendelea

ila ilibidi tu wanipigie na kuniambia kuwa waligonga mpaka kidogo wavunje mlango lakini hakuna hata mmoja anayetingishika.
Sasa hawaelewi kuna nini kinachoendelea

Niliwaambia, sasa fanyeni hivii, muibukieni Prince. Nendeni kwake, mfikieni mjue nini kinachoendelea Walienda kwa Prince walifika kwake wakagonga mlango ukafunguliwa, unafunguliwa anatoka rafiki yake Prince
Wakamuuliza prince yuko wapi, Akawajibu Prince tangu alipoondoka hapa

saa mbili hajarudi mpaka saivi, Wakamuuliza kama hakuna mahali anahisi atakuwepo, akasema hapana, maana yule ni
bodaboda anaweza kuwa mahali popote kulingana na wateja wake.
Wakamwambia basi fanya hivii, mpigie simu Jamaa akampigia simu Prince, simu ikaita lakini

haipokelewi.
Akapiga tena haipokelewi,
Alipopiga mara ya tatu simu ikawa haipatikani, ikiwa na maana Prince amezima simu
Walichokaa, wakanipigia simu kunielezea yote hayo ambayo yametokea, nilichoka piaa
Wakati huo mke wangu naye simu haipatikani tena, dada wa kazi yeye hapokei

Nini kinachoendelea hapaaa?
Mke wangu na dada wa kazi wako wapi?! Zile zilikuwa ni vurugu za nini?!
Prince na yeye kaenda wapi?!
Maswali yote haya nilijiuliza bila kuwa na majibu yake, marafiki zangu waliniomba niwaruhusu wakapumzike kwanza, kesho asubuhi na mapema wataamka

na hilo. Ilikuwa ngumu kuwaruhusu waende kwao kupumzika, lakini hata nikiwakatalia, wabaki waendelee kufanya nini maana huo ulikuwa ni usiku wa saa saba tayari

Usikose sehemu ya pili ya story hii
Maana hayo maswali ambayo uko nayo moyoni mwako yatajibiwa yote.
Baki na mimi hapa hapaa
unganisha ya pili mkuu hawa itaendelea wanatuzingua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom