Simulizi: Mapito (Sehemu ya 1)

miss nyanga

New Member
Dec 18, 2023
4
8
Nimekaa kwenye ofisi na siyo ofisi ndogo,ofisi kubwa sana,Tena ninaimiliki mwenyewe iliyosheheni furniture za thamani na kila kitu nilichokuwa nakitamani muda wote wa maisha yangu,ninayo Amani ya moyo na ninaona Nina kila kitu ambacho niliomba muda wote kwa Mungu wangu yaani kiufupi nimebarikiwa.

Basi nikasema niperuzi kidogo mtandaoni, ghafla nakutana na account ya Remmy (mme wangu wa zamani) kwanza nikashtuka ndo kazeeka Hivi,baada ya kuona picha zake basi akili yangu ikarudi nyuma miaka 9 iliyopita wakati tuko kwenye mahusiano ya uchumba alivokuwa ananijali na kunithamini ilhali Hana kitu chochote kipindi tunasoma,na niliona Dunia imeumbiwa mapenzi jamani na Wa kuyaenzi ni Mimi na yeye na sio wengine maana wengine wanadanganyana tu,Yaani Kuna point jamii inawachagua nyie muwe mfano wa kuigwa na Tulipewa majina ya Wapenzi waliokufa pamoja fyuu huo utoto hapana aisee,Tukipeana sabuni na mafuta na vocha basi hakuna kingine kwenye mapenzi tulichohitaji zaidi penzi letu lifike mbali tu,na hatimaye tuzeeke pamoja.

Basi miaka ikapita Mimi nikamaliza chuo na yeye akabaki na Nikapata kijikazi cha kujishikiza kusukuma muda na kujipatia hata maisha,na baada ya muda na yeye akamaliza tukiwa tuko vizuri zaidi ya jana japo kukwaruzana kupo lakini tulikuwa vizuri sana,Tukatembeleana na baadae akaamua kuniamishia sehemu alipo kutokana na mkataba wangu kuisha nikarudi nyumbani kwetu na yeye alikuwa anafanyia kazi mkoa huo huo basi tukawa karibu zaidi,nikawa naenda kwake sana na katika kwenda kujiachia kukahusika, baada ya muda nikahisi siko sawa mara leo mgongo mara kichwa yaani tafrani nikaamua kupima mkojo, nikajikuta Nina ujauzito nisioupanga na matumaini yangu nikimwambia atafurahi sana lakini nilivomuambia alinijibu Sawa nitalea hebu fikiria picha iliyokuja kichwani,nikaumia lile jibu fupi nikalia nmevuruga mipango yangu na nikajipa jibu hapa hakuna muoaji hapa, kitu kizitoo.

Kwetu ni wakali sana wazazi, wananiamini,najiheshimu Leo nizalie nyumbani Mimi big nooo,
Wakati namuelezea Niko kwake akasema tuhakikishe kipimo kikanunuliwa mimba Ipo na kutoa haiwezekani sababu siko tayari yeye pia hayuko tayari lakini hapo nimeshapata majibu alivokuwa kapoa kuwa hakuna muoaji kabisa lakini Sina jinsi sababu mimba sio ugonjwa, ujasiri wa ajabu nikajikubali haraka sana na nikafanya Siri nyumbani nilivofika nyumbani Niko na Siri yangu na hakunitafuta Hadi Mimi niwe namtafuta,mpenzi kapeperushwa na habari za mimba,

Zikapita siku mtu hata mkipanga kitu ni kawa mkali sana na hataki mazoea,baada ya muda nikasema takufa Mimi ikabidi nimueleze mama yangu na mama akamtafuta sababu walikuwa wanajua ni Rafiki yangu ikabidi amuite na kumuuliza na Kumbuka hapo baba hajui na alivoulizwa na mama akakubali kweli mimba ni yake na Atalea hasemi atanioa,mama akamwambia sawa Tupange Mimi na yeye inakuwaje akajibu sawa.

Siku mbili hapokei simu zangu ikabidi niende kwake na hapo kaanza mapicha picha yaani anawasiliana na wadada ambao ni wanawake zake nikasema liwalo na liwe napambania penzi langu,nikamuomba tuishi pamoja yaani mwenzenu mimba ya nyumbani Tena mtu niliyokuwa najiheshimu Leo nizalie nyumbani Tena niwape mzigo wazazi hapana mwenye mzigo hajafa na yupo na najua ni yeye Bora anikatae lakini nyumbani sikai,basi katika kumlazimisha akatafuta mshenga na akaenda naye nyumbani na nikatolewa posa na kuchumbiwa wakatajiwa tarehe ya kuja na wazee kupangiwa maali yaani naona kabisa jamaa Hana furaha na sio muoaji ila ninalazimisha tu.

Kabla ya kupangiwa maali baba aligundua Hali yangu na ikabidi aitwe akabidhiwe mke,Kumbuka moyoni Nina furahi sababu natamani kudeka na kuishi na mpenzi wangu kumbe najitafutia shida tu.

Wazee wake walikuja wakapangiwe maali nyumbani kwetu na taratibu zifuatwe na walifanikisha na Jambo likapita,Nilikaa na yule mwanaume ugomvi ndio ugomvi na akaanza kubadilika kila siku,yaani nikawa mtu wa huzuni tu na sikuwahi kusema nyumbani kiufupi nilijuta na sikuwa na msaada kwa muda ule nikavumilia na kuvumilia Tena.

Unaishi na mtu Hana muda na wewe,dada yangu alinipa mtaji nikaanza kuuza nguo na viatu vya kike ndio ikawa ahueni hata nikawa nanunua nguo lakini Ukweli Sijui hata nguo yake,Mda ukawa unasonga na mtu amebadilika jumla,nilienda kujisubiria uzazi kwetu na siku zilivofika Nikapata mtoto na ndo mwanzo wa mateso yangu.

Nakumbuka Nina siku tatu nitoke uzazi,alikuja na akaniambia ana habari Nzuri za kuniekeza nikafurahi nilichoelezwa.

Ntaendelea

nyanga

Screenshot_20240110-133348.jpg
 
MAPITO (Sehemu ya Pili)

Ilipoishia..

Nakumbuka Nina siku tatu Toka nitoke uzazi,alikuja na akaniambia ana habari Nzuri za kuniekeza nikafurahi nilichoelezwa...

Ananiambia unajua Kuna dada tulikuwa tunapendana Mimi naitikia tu eeh yaani hapo ninatamani nimpige hata mabanzi au hata nimrukie yaani ila nikasema moyoni jikaze mtoto wa kike usiye na thamani nikamsikiliza Tena kwa makini,nilikuwa nimelala ikabidi niinuke nikae kabisa kama napewa habari za kuletewa gari na upendo kumbe za mwanamke Tena mpenzi wake...

Nikakaa namsikiliza huku nimetengeneza tabasamu lainii la uongo kabisa,ananiuliza kwanza hautajisikia vibaya Mimi najibu ndio siwezi kabisa sababu napenda uwe na furaha na nakuamini mme wangu(Wakati siijui hata ndoa)

Basi akaendelea,huyo dada tulipotezana kabla sijaenda chuo na pia amenitafuta Leo nikiwa kazini anaulizia ahadi yangu ya kumuoa,Mimi najibu pole jamani ukamwambiaje,Yuko na ujasiri moyoni nasema lione bichwa hilo huku ninaumia,Akaniambia nikamwambia Mimi Kuna mtu nimezaa nae na naishi nae nmemuomba na msamaha,yaani amezaa na mtu ila hajaoa nikachekecha akili nikajuta sana,mabinti uchu wa kuolewa utatutesa sana!!
Nikamwambia pole muekekeze taratibu anajibu sawa kuwa na Amani Mimi ni wako nikawa namuitikia Kumbuka hapo Bado Niko kwa wazazi nasubirii uzazi,tumekaa hapo hapo huyo dada akampigia simu hawezi kupokea Mimi na kiherehere nikapokea na kumjibu amtafte baadae na akakata simu!
Nikamuomba aondoke Mimi nipumzike basi bila hiyana akaondoka zake.

Nimelala usiku simu inaita ninatafutwa na namba ngeni hapo mtoto kanisumbua nimechoka hatari,napokea akakata,nampgia hapokei kidogo sms inaingia naambiwa niache kujipendekeza kwa mme wake,mme Gani huyo,mtu aliyenipenda akanipenda na tukajiachia bila wasiwasi nikabeba na mimba nikaamini atakuwa mtu sahihi wa kunishika mkono Leo naambiwa niache mme wa mtu,Mimi nikamuuliza wewe nani nilitukanwa Yani simu ilijaa maneno ya dhiaka na mengine ninajua anaambiwa na huyo ninaemuita mume,ikabidi nimtishie kumshtaki ndio akawa mpole akakaa kimya,nikamtafta mme namuambia aje anajibu Yuko na kazi na akaniambia kama nadhida nitume sms jamani Afya ya Akili ni muhimu sana,nikatuma nikashitaki akajibu na wewe mtukane ila Hana kosa sababu ulimkuta!

Sasa akakata mguu nikiangalia nyumbani wananiulizia mtu hafiki nasema kabanwa na kazi,Badala ya kula supu naogopa kwa wazazi kuwatesa nasema supu siwezi Mimi nachemsha viazi mviringo naweka na Chinese ilete ladha ninakula ule mchuzi kana soup,na namshukuru Mungu hata nguo za mtoto ndugu walileta bag zima kwahiyo hata blankets,babyshow zile sikununua walininunulia dada zangu nikaletewa bila hivyo ingekuwa shida,akawa anaweza Kaa siku nne ndo anakuja Tena Hana muda ni dakika tu anaondoka,niliisha Mimi,nililia Mimi lakini wapi.

Siku moja amekuja ananiuliza vipi mbona umekonda alafu umekuwa mweusi Hivo,nikajibu mawazo tu Eti Anasema samahani kwa yaliyotokea Mimi sawa nataka nirudi nyumbani kwangu akajibu poa.

Baada ya muda nilirudi kwangu lakini nilifikia kwenye nyumba ngeni na kule kwa mwanzo tulihama,Tulipofika siku za mwanzo aliishi na Mimi vizuri lakini baada ya Muda picha likaanza,kitu kidogo anapanic na dharau juu,masimango ya kuambiwa nikivaa sipendezi na hapo Kumbuka Nina miez Mitatu ya uzazi nikaja gundua amempa mjukuu wa mwenye nyumba mimba na wameitoa na Binti anasumbua sana Anadai anaumwa akawa anapiga simu Hadi usiku,hapo Kumbuka Kuna huyo alihaidi ataniondoa Mimi atamuoa na Bado anadate na wanachuo Wawili,katika ule umri na changamoto ya uzazi Mimi nilipata tatizo la Afya ya Akili nikawa mda wote siko sawa yaani naweza ona kitu tu nikalia nikawa nachukia kila kitu yaani Ukweli nilijuta na akawa anawapa viburi wananitafuta naambiwa ana mpango wa kukuacha yaani ndo nazidi kuchanganyikiwa.

Naweza ona kitu nikamuuliza naishia kujibiwa shombo tu na nikisema niumie na nilie nitalia nitanyamaza ahangaiki na Mimi Wala!

Siku moja nikawa napiga picha Ile nimeweka simu najipiga full picture jamani alijua kunivunja moyo, ananiambia yaani Tumbo lote unapiga full huoni aibu dah,yaani umepoteza mvuto Mimi Sasa si kulia Huko yaani siku hiyo nilijichukia nikasema kumbe ndio maana hunipendi anajibu ndio sababu hata kuzaa na wewe bahati mbaya khee nikasema basi yaishe akatoka zake,nikampigia simu mama yangu nikamuuliza mama Nina Tumbo kubwa eti,mama ananijibu mbona limerudi kawaida nikasema mama ananipa moyo tu Sasa nikawa naogopa kuvaa nguo na hata kutoka nje yaani nikawa sijiamini Tena yaani akanipa depression kabisaa.

Maisha yakaendelea Akawa anae mpenzi Rasmi wa ndoto zake Mimi Niko ndani tu nje watu wanaona na kuwaelewa na penzi limenoga kinyama,siku hiyo mtoto kanisumbua usiku amelala usingizi ukakata niperuzi kwa simu nakutana kaweka status wamepiga miguu tu,pose la kukanyagana kabisa ahah,ameandika japo safari ngumu tutafika tu,khe nikasema kazi ipo af mda huo ni usiku na hayupo nyumbani,jamani sikulala nikamtafuta mpenzi wa Rafiki yake ndo kunipa mkanda mzima...

Yaani ni hivii....

Ntaendelea

Nyanga

Screenshot_20240110-150934~2.jpg
 
View attachment 2867565
Wanaume wangekuwa wanaelewa jinsi uzazi ulvyo mgumu. Kipindi Cha kutoka kujfungua n kgumu mnooo afya ya akili inakuwa dhaifu sana.. ninaelewa hik maana nimepitia ... Nyinyi wanaume mungu anawaona aisee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom