KLABU ya soka ya Simba imesema itatumia jumla ya Sh. Milioni 900 kuweza kusajili kikosi imara kitakachoiwakilisha timu hiyo katika Ligi Kuu na michuano mbalimbali ya Kimataifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kasim Dewji alisema fedha hizo zipo katika bajeti yao ya usajili wa mwaka huu.
Dewji alisema mikakati ya kupata kiasi hicho cha fedha imeshafanyika na inaendelea kufanyika chini ya usimamizi maalum wa Kamati yake.
Tunajitahidi kusajili kikosi imara ili tuweze kushiriki kikamilifu katika michuano ya kimataifa na kitaifa, ili ni jukumu letu sote ili kuhakikisha Simba inafanya vizuri, alisema Dewji.
Simba inalazimika kufanya usajili wa maana ili kuweza kushiriki vyema msimu ujao wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika linaloandaliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).
Source: http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2021510&&Cat=6