Mapinduzi cup Milioni 100 bado ni ndogo kwa simba na Yanga, Waongeze dau lifike walau 300

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Kwa Yanga na Simba kila timu hapo ina sponsorships deals zenye kuingiza takribani bilioni 5 kila mwaka

Kombe la Ligi kuu bingwa anapewa milioni 500 lakini hio bado ni pesa ndogo, Malengo huwa ni kuvuta mpunga wa kimataifa, msimu wa mwaka jana pekee Simba kakunga bilioni 2 kasoro caf na bilioni 2 na nusu african cup, Yanga kakunja bilioni 2 na nusu kufikia fainali shirikisho.

Kombe la Fa nako mshindi ni milioni 150 lakini malengo huwa ni kukusanya mataji yanayotambulika na fifa na hata timu ikikosa nafasi ya caf mabingwa basi iweze kufuzu caf shirikisho waende kukunja dola ndefu.

Kombe la mapinduzi kuna milioni 100 mshindi wa kwanza na milioni 80 wa pili, hata itokee fainali wafike simba na yanga hizi ni pesa za kulipa mishahara ya mwezi moja tu kwa wachezaji wanaohesabika, hata hivyo kombe halina mchango wowote kwenye rekodi za fifa na haliipeleki timu kwenye michuano yoyote ya kukunja kitita kikubwa zaidi.

Dau lipande walau lifikie 300 Milioni,
 
Know the difference between competition league and tournament.

Hapo hela lazima zitofautiane mkuu.
 
Hivi wadhamini wa Simba na yanga ni katika mashindano yote ?sio kwamba sports pesa anaishia nbcpl tu ?
 
Timu zinaingiza mapato kupitia haki za matangazo pamoja na viingilio kwa sehemu kubwa hasa hasa kwa vilabu vikubwa kama Yanga na Simba.

Mfano; Kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mchezo wa Yanga au Simba utahitajika kuwalipa labda si chi ya Tshs. 10M. Pia viingilio vya michezo yao hata ukiweka Tshs. 3000 kwa kila atayeingia uwanjani, watu 10,000 ni sawa na Tshs. 30M. Ukiondoa kodi na gharama za wamiliki wa uwanja na timu walizocheza nazo utaona wanaweza kukunja si chini ya Tshs. 10M kwa kila mchezo.

Hitimisho, kwa haraka haraka Yanga na Simba hata wakitolewa ktk hatua za makundi wanaweza kuondoka na pesa si chini ya Tshs. 60M yaani ktk kila mchezo mmoja wanaweza kuingiza kiwango cha chini cha Tshs. 20M kupitia haki za kurusha michezo yao pamoja na viingilio vya mashabiki ndani ya michezo mitatu ya makundi.

Yanga/Simba wakicheza mechi 4 kwa mwezi wana uwezo wa ku-cover 75% ya gharama za uendeshaji wa timu kama mishahara, usafiri pamoja na hoteli bila kumtegemea mdhamini mkuu kupitia broadcasting rights, ticketing pamoja commercials. Pesa ya mdhamini mara nyingi sana hutumika kufanya usajiri ikienda kinyume chake maana yake timu ina uongozi mbovu.
 
Vilabu vya vikubwa vya soka havilengi ile pesa ya mshindi bali ni jumla ya package inayoambatana na mashindano husika. Bajeti ya Al Ahly kwa msimu huu ni zaidi ya $80M kwa timu ya mpira tu ila kwa ujumla na michezo mingine kama kikapu na mpira wa mikono ni $130M, winning prizes za CAF Champions league pamoja na ligi kuu ya kwao Misri havifiki hata robo ya bajeti yao.
 
Vilabu vya vikubwa vya soka havilengi ile pesa ya mshindi bali ni jumla ya package inayoambatana na mashindano husika. Bajeti ya Al Ahly kwa msimu huu ni zaidi ya $80M kwa timu ya mpira tu ila kwa ujumla na michezo mingine kama kikapu na mpira wa mikono ni $130M, winning prizes za CAF Champions league pamoja na ligi kuu ya kwao Misri havifiki hata robo ya bajeti yao.
Hawajui hili, kwa kuongeza, sio havifiki hata robo, ni havifiki hata 5% ya bajet yao,

Mshindi wa CAFCL analamba $2.5M, wakati yule wa ligi kuu ya Misri anapata $308k ambayo
 
Mleta mada hujui chochote mkuu,

Miaka mitatu nyuma kabla ya Azam na NBC hawajahusika na hii million 500 uliyoiongelea,

Kipindi hicho Vodacom almaarufu
VPL ilikuwa inampa mshindi million 80.

Swali la kujiuliza ,
ni je hii pesa inaweza kufidia gharama za msimu mzima?

Hapohapo tambua gharama za kuifuata Mbao fc kule Kanda ya ziwa Kuna gharama kubwa sana,

Mfano kuanzia Crew nzima ya timu ya Simba kuanzia wachezaji, viongozi na wadau wengine wa timu husika kutokana na umaarufu na ukubwa wake anahitaji hotel ya gharama yenye misosi ya gharama, n.k.

Lakini kumbuka mara nyingi mechi ikichezewa mkoani mapato ya uwanja huwa ni kichekesho tu si lolote si chochote. Labda mechi ichezwe Taifa angalau.
 
Back
Top Bottom