Benchikha hataki mzaha kwenye usajili dirisha hili dogo

franckkimm

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
440
852
Baada ya kukiangalia kikosi cha timu yake, Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha, ni kama ametoa angalizo kwa viongozi wa klabu hiyo kuwa makini wanapoenda sokoni kipindi cha dirisha dogo la usajili kulingana na aina ya wachezaji aliokuwa nao kwa sasa.

Kauli hiyo imekuja baada ya mchezo wa juzi uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya KMC FC.

Benchikha alisema ana kazi kubwa ya kufanya ndani ya kikosi chake ili kurudi katika ubora na kuendelea kupata ushindi katika michezo iliyopo mbele yao na kufikia malengo yao.

Alisema walicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi wakashindwa kuzitumia, lakini pia kulikosekana umakini katika safu yake ya ulinzi.

“Kwa sasa tutaendelea kukisuka kikosi katika michuano ya Mapinduzi pamoja na kufanyia kazi maboresho ya kikosi katika maingizo mapya, naamini tutarejesha makali yetu.

“Tuna kazi kubwa ya kufanya, tunahitaji kurudi katika hali ya kawaida na kupigamia mataji, timu inacheza vizuri, lakini kuna vitu vinakosekana ikiwamo kutumia nafasi tunazotengeneza, hilo ndilo jambo tunapaswa kulimaliza,” alisema kocha huyo.

Aliongeza kuwa wanaelekea kipindi cha mapumziko ambacho watakuwa makini katika maboresho ya kikosi kulingana na mahitaji ya timu lakini pia kutumia Kombe la Mapinduzi kuandaa kikosi imara.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, pia alikiri timu yao inahitaji mabadiliko makubwa kwa kusajili wachezaji wazuri wenye uchu wa mafanikio.

“Lazima tukiri kuwa kikosi chetu kinahitaji mabadiliko makubwa mawili, kwanza ni kuongeza wachezaji wenye ubora, uchu na kiu ya mafanikio.

“Pili ni wachezaji waliopo kuongeze ubora wao wa upambanaji. Huwezi kufanikiwa kwa kuwa na matokeo ya panda shuka, timu kubwa yenye malengo ya ubingwa lazima iwe na mwendelezo wa kupata matokeo mazuri,” alisema Ahmed.

Aliongeza kuwa wana miezi miwili ya kufanya mabadiliko hayo mawili makuu ambayo ameona ni tatizo ambalo linawakwamisha mpaka sasa.

Hata hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili ni kwamba, majina yanayotajwa kuwamo mezani mwa uongozi wa klabu hiyo ni Alves Ngakosso Oko, Hardest Malonga, Moise Gbai, Mohammad Alzabbad, Abdoulaye Djire, Abdul Aziz Issah, Derrick Fordjour, Ibrahim Seck na Jonathan Alukwu.

Credit://sokaleo
 
Benchikha ni kocha mjanja mjanja asiye na uwezo, kombe super cup 2022 alishinda na ya Rs berkane dume ilioyoundwa na Ibenge yeye akaiparamia kwenye mechi ya super cup lakini baada ya hapo alitimuliwa baada ya mechi sita tu za ligi, akaenda usma Alger napo aka fluke nakushinda kombe la shirikisho na super cup na usma aliyoikuta ina ubora mkubwa, lakini katika ligi timu ilikuwa inasuasua kiasi cha kushika nafasi za chini kabisa napo akaleta kiburi wakamla kichwa, sehemu zote alizopita nyingi hakudumu msimu mzima ni either atimuliwe au akimbie, hata hapa simba naona anakwenda kuwaharibia makolo, sababu nikama uongozi wa mbumbumbu fc na mashabiki wao wanamuogopa na kumuona kama mfalme juha, lakini ukweli nikwamba ni kocha wakawaida anahitaji timu iliyojengeka haswa ili uwezo wake uonekane, hana tofauti na jose mourinho na ndio maana anakimbia kimbia hovyo na hata hapo umbumbumbuni atakimbia
 
Tukiachana na yote.....hata kocha angekuwa guadiola Bado Simba inahitaji usajili makini (sio Bora usajili ) hii iko wazi kabisa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Benchikha ni kocha mjanja mjanja asiye na uwezo, kombe super cup 2022 alishinda na ya Rs berkane dume ilioyoundwa na Ibenge yeye akaiparamia kwenye mechi ya super cup lakini baada ya hapo alitimuliwa baada ya mechi sita tu za ligi, akaenda usma Alger napo aka fluke nakushinda kombe la shirikisho na super cup na usma aliyoikuta ina ubora mkubwa, lakini katika ligi timu ilikuwa inasuasua kiasi cha kushika nafasi za chini kabisa napo akaleta kiburi wakamla kichwa, sehemu zote alizopita nyingi hakudumu msimu mzima ni either atimuliwe au akimbie, hata hapa simba naona anakwenda kuwaharibia makolo, sababu nikama uongozi wa mbumbumbu fc na mashabiki wao wanamuogopa na kumuona kama mfalme juha, lakini ukweli nikwamba ni kocha wakawaida anahitaji timu iliyojengeka haswa ili uwezo wake uonekane, hana tofauti na jose mourinho na ndio maana anakimbia kimbia hovyo na hata hapo umbumbumbuni atakimbia
Au sio
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom