Tujikumbushe kidogo kauli za viongozi wa Simba

KJ07

JF-Expert Member
Dec 17, 2021
2,243
5,000
1:Try Again
"Tumedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakao kirudisha kikosi chetu kwenye ubora wa juu msimu ujao na hilo linawezekana kutokana na malengo tuliyokuwa nayo ya kuifanya Simba kuwa klabu kubwa Afrika"

Hii ilikuwa ni baada ya Young Africans Sports Club kufika fainali ya kombe la shirikisho msimu wa 2022/2023.

2:Try Again
"Juzi wakati nipo V.I.P Rais wa FIFA Gianni Infantino aligeuka na kuniambia timu yako inacheza vizuri kuliko timu zinazocheza hapa" Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC,

Hii ilikuwa baada ya kuishuhudia mechi ya Fainali AFL kati ya Mamelodi Sundowns na Wydad.

3:Murtaza Mangungu.
"Kama mnakumbuka mlichanga pesa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na pesa ile ilitumika kujenga ukuta wa uwanja wa Bunju na pesa nyingine zilitumika kuimarisha kambi ya Timu”

“Tujenge Simba imara kwa kizazi cha sasa na baadaye, tuendelee kushirikiana na naamini Mwenyezi Mungu atatutangulia”

Hii ni alipokuwa akitoa ripoti ya pesa za michango ya uwanja wa MO SIMBA ARENA BUNJU B.


4:Murtaza Mangungu.

“Niliwaahidi mashabiki wa Simba, msimu huu lazima tumfunge Yanga na tumemfunga tukafurahi wote. Kwenye hilo mashabiki hawanidai”.

Hii ilikuwa ni baada ya kuifunga yanga goli mbili kwa sifuri tarehe 16 april 2023.

5:Murtaza Mangungu.

“Hayo yanayosemwa na mimi nimeyasikia, nadhani kuna mapugufu kidogo kweye tafsiri ya maelezo ambayo yametolewa na wahusika. Mimi siwezi kuhusika kumjibia kwenye yale aliyoyasema kwa sababu mimi sio sehemu yake."

“Ninyi waandishi mnapenda kukimbilia kuwauliza watu mambo yaliyosemwa na watu wengine. Kama yeye ndiye aliyetoa hiyo kauli, sikutegema kama mimi ndiye nije studio kufafanua maelezo aliyoyatoa yeye, ilitakiwa ninyi mumuulize yeye. Simba haijawahi kuuzwa, haitokuja kuuzwa, Simba SC ipo."

“Kilichojitokeza ni uelewa wa watu wengi hata wanasimba wenyewe kuhusu mabadiliko yaliyofanyika ndani ya Simba."

"Mo Dewji ni mmoja wa watu waliojitolea sana kuisaidia Simba kwenye kipindi ambacho hakuwa sehemu ya Simba."

“Baada ya kujitoa sana, akatoa wazo kwamba tutengeneze mfumo ambao utasaidia watu kuwekeza ili klabu iwe ya ushindani zaidi."

"Ndipo tukaunda Simba Sports Club Company ambayo imegawanywa katika muundo wa share ya 51% kwa 49% ambayo iliwekwa na Serikali ili kuhakikisha kuwa wanachama wanakuwa majority shareholders."

"Simba imetoa mali zake na nguvu zake kuwekeza na mwekezaji ametoa pesa zake zikaunganishwa pamoja kutengeneza mtaji ili kuendesha klabu, huo ndiyo ukweli uliopo."

Hii ilikuwa ni baada ya Mo kuweka wazi ya kwamba Simba Sports Club ni mali yake.

Kauli ni nyingi.

Ntaziongezea kadri nitakavyozikunyanya katika vyanzo rasmi.
 

Attachments

  • mangungu-pic.jpg
    mangungu-pic.jpg
    254 KB · Views: 2
Weka basi na ile kauli ya kiongozi wa zamani Mh. Rage dhidi ya mashabiki na wanachama wa simba!

Au tunajikumbusha kauli za viongozi wa sasa pekee!!
 
Back
Top Bottom