Simba Kutumia Milioni 900 Kwenye Usajili

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
KLABU ya soka ya Simba imesema itatumia jumla ya Sh. Milioni 900 kuweza kusajili kikosi imara kitakachoiwakilisha timu hiyo katika Ligi Kuu na michuano mbalimbali ya Kimataifa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kasim Dewji alisema fedha hizo zipo katika bajeti yao ya usajili wa mwaka huu.

Dewji alisema mikakati ya kupata kiasi hicho cha fedha imeshafanyika na inaendelea kufanyika chini ya usimamizi maalum wa Kamati yake.

“Tunajitahidi kusajili kikosi imara ili tuweze kushiriki kikamilifu katika michuano ya kimataifa na kitaifa, ili ni jukumu letu sote ili kuhakikisha Simba inafanya vizuri,” alisema Dewji.

Simba inalazimika kufanya usajili wa maana ili kuweza kushiriki vyema msimu ujao wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika linaloandaliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

Source: http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2021510&&Cat=6
 
Simba hawana ubavu wakutumia mil.900 watatoa wapi hao? Mala ya mwish nilisikia wana mil.15 kwa ajili ya kusajili sasa sijui hizo zimetoka kwenye pango lao pale msimbazi au vp.
 
Hakuna timu yenye pesa hizo hapa nchini ingawa zingeweza kuwa nazo kama zingekuwa na uongozi madhubuti, Uongozi uliopo ni wa kuangalia matumbo yao na kutegemea wafadhili.

Mfano Simba na Yanga zingeweza kutengeneza pesa nyingi na kuwa mojawapo za timu kubwa Barani Afrika kama zitabinafsishwa na kuacha kuendelea kutegemea wanachama wanaochangia eti shs. ambazo nadhani ni kati ya 10,000 na 20,000 kwa mwaka. Sasa hapo kuna maendeleo kweli zaidi ya kutembeza bakuli kwa wafadhili?
 
KLABU ya soka ya Simba imesema itatumia jumla ya Sh. Milioni 900 kuweza kusajili kikosi imara kitakachoiwakilisha timu hiyo katika Ligi Kuu na michuano mbalimbali ya Kimataifa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kasim Dewji alisema fedha hizo zipo katika bajeti yao ya usajili wa mwaka huu.

Dewji alisema mikakati ya kupata kiasi hicho cha fedha imeshafanyika na inaendelea kufanyika chini ya usimamizi maalum wa Kamati yake.

“Tunajitahidi kusajili kikosi imara ili tuweze kushiriki kikamilifu katika michuano ya kimataifa na kitaifa, ili ni jukumu letu sote ili kuhakikisha Simba inafanya vizuri,” alisema Dewji.

Simba inalazimika kufanya usajili wa maana ili kuweza kushiriki vyema msimu ujao wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika linaloandaliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

Source: http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2021510&&Cat=6
Milioni 900 hela ya Zimbabwe au ya Tanzania? Timu imeshindwa kuajiri katibu mkuu inaweza kutumia mil 900 kufanya usajili? Ni vyema na ndugu zetu waandishi mkatusaidia kupunguza hizi habari zisizo na kichwa wala miguu!
 
I am a Simba fun, but this is a big hoax!!! where the hell can Dewji and his team acquire this much outlay?
 
Paukwa pakawa mwanangu mwanasiti na kiuno cha hariri, hadithi njoo uongo njoo na utamu kolea!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hakuna timu yenye pesa hizo hapa nchini ingawa zingeweza kuwa nazo kama zingekuwa na uongozi madhubuti, Uongozi uliopo ni wa kuangalia matumbo yao na kutegemea wafadhili.

Yanga aka KAGODA FC (Timu anayofadhili Fisadi Manji) wanazo. Mwaka jana walitumia close to that.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom