Hoja kuu:
Kwenye uchumi wowote hupimwa kwa mfumko wa bei(inflation rate) wa bidhaa sokoni, mfumuko wa bei unapozidi zaidi ya 50% uchumi unakua hatarini.
Kwa hali ya nchi hivi Sasa ilivyo basi kwa nchi za wenzetu na watu walio serious na ustawi wa jamii na uchumi basi serikali kuu ilipaswa kuachia ngazi, aidha kwa rais kuvunja Baraza la mawaziri na kusuka upya ama Rais mwenyewe kujiuzulu.
Yaliwahi kutokea haya pale Uingereza pindi nchi ilipoyumba kiuchumi kwa mfumuko mkubwa wa bidhaa baada ya suala la BREXIT, hali iliyopelekea Waziri Mkuu Boris kujiuzulu na Mawaziri wakuu wawili wakajiuzulu ndani ya mwaka mmoja na nusu na ikapelekea Uingereza kua na Mawaziri wakuu watatu ndani ya miaka miwili.
Hapa kwetu kila kitu kwa sasa bei ghali, mfumuko wa bei ni maradufu,kuanzia daladala, mabasi ya mikoani, vifurushi vya simu (uhuni zaidi huku package zimepunguzwa unavhopata ila unalipia hela ile ile automatically ni mfumuko wa bei kwani unapata MB 500 kwa shs 1000 ilihali zamani ilikua unapata 1GB).
Tunapoongea hapa sasa hivi kununua sukari Tanzania hii ni anasa, bei ya sukari kilo moja unapata bia 3 na chenji inabaki, mfuko mmoja wa Cement kutoka Tsh. 13,000 mpaka Tsh. 17,000 mpaka 23,000 mikoa ya Kanda ya ziwa.
Serikali inatazama tu,waziri anasingizia mafuriko ya mvua,miaka yote mvua inanyesha na mfumuko mkubwa hivyo hakuna,kama sio wizi ni nini?!!
Mvua zinanyesha kila mahali, bado umeme ni wa mgao ilihali tunaambiwa mabwawa hayana maji- kama sio wizi ni nini? Yote haya ili watu wale hela za umma kupitia mitambo ya SONGAS, IPTL na mitambo ya gesi ndio maana umeme wa mabwawa ambayo 100% ni ya serikali wanahujumu kwani hakuna mabilioni ya kugawana.
Hali ya uchumi kwa Watanzania inahujumiwa na serikali? Kama Rais Samia hanufaiki na hafurahii haya kwa nini hatokezi kulisimammia?
Enzi za Magufuli Sukari iliadimika kwa wiki kama 2 na bei ikafika shs 4000-5000 na mara moja Magufuli alitoa tamkoa kua atafuta vibali vyote vya wauza sukari kama hawatoshusha bei, bei ilishuka na ikauzwa Tsh. 2800 mpaka alipoingia madarakani Rais Samia ambapo bei imekua maumivu kwa Watanzania.
Kuna watu wanasema Samia hana uchungu na Tanganyika, ndio maana hajali, kwani Zanzibar sukari kilo moja ni Tsh. 2000-2500 ilihali bara huku 5000-6000. Zanzibar hakuna mgao wa umeme, huku Tanganyika ambapo kunazalishwa umeme na kupeleka Zanzibar umeme mgao mtupu.
Rais Samia hafai kuongoza tena, anawaza uchaguzi tu na ya kubaki madarakani na ndio maana tumemsikia akitoa tamko Majeshi yajiandae.
Viongozi bora huwaza current and next generation, viongozi wabovu huwaza kufanya miradi ya corruption na how to rig next election!