Siku yangu ya kwanza kuingia ofisi za kubeti kwa bahati mbaya

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,109
22,562
Salaam, Shalom!

Siku moja nilitoka nyumbani kwangu nilipanga kwenda mjini kununua baadhi ya mahitaji muhimu ya vifaa vya umeme,

Niliondoka nyumbani majira ya saa tisa hivi, baada ya nusu saa, nilifika mjini, Sasa Pana duka la vifaa vya umeme kubwa nililokuwa nikitumia kununua mahitaji yangu hapo mjini muda mrefu uliopita, nikiwa natembea nikasema, niende duka lile nikapate mahitaji yangu na kuokoa muda.

Nikapaki gari yangu pembeni kidogo ya sehemu lilipokuwapo duka lile, Nilishuka na kutembea kulikaribia duka lile.

Kilichonishangaza, nikakuta mazingira tofauti kabisa, nje Kuna huduma za chakula watu walionekana wanakula na kunywa Kwa furaha.

Nilikuta duka lile limeongezeka ukubwa na kuongewza urefu, nje alikaa afisa wa ulinzi smart, palifungwa camera za USALAMA, ofisi ilinakshiwa kisasa zaidi. Ndani palikuwa na wazungu kadhaa na wafanyakazi waliovalia mavazi nadhifu.

Nikavutiwa kuingia ndani ya ofisi hiyo kujua nini kinaendelea humo, pia nilitaka kujua muuza electronics alihamia wapi,

Kuingia ndani ya ofisi hiyo, nikakuta watu wenye Rika mbalimbali watanashati, wengi walikuwa vijana na wanawake Wachache,

Mle ndani palikuwa na utulivu wa kutosha, AC Kila Kona, kila mtu alikuwa ameshika kalamu na karatasi na alionekana kumakinika na kusoma kilicho kwenye karatasi,

Nikawaza hiki ni nini watu Hawa wanafanya, niliwaza, yaezakuwa wanafanya labda mtihani hivi, niliwaheshimu sana, nilipoona hali Ile, nami nikalazimika kusogea pembeni alipokuwa askari yule wa USALAMA na kuuliza watu wale wanafanya nini, na ofisi Ile inajishughulisha na nini,

Mlinzi yule alinijibu kuwa pale ni ofisi za BETTING, watu wanachukua mikeka kutabiri timu za mpira wa miguu.

Sura yangu ilifura ghafula, nilitoka haraka ndani ya ofisi Ile nikijilaumu kupoteza muda wangu kuingia ofisi ya ulaghai Kwa nguvukazi yetu ya Taifa inayowateka vijana kuamini kuwa maisha yaezapatikana Kwa Bahati nasibu.

OMBI: Atokee kiongozi mmoja mkorofi aina ya Magu, afute Ujinga huu unaopoteza nguvu KAZI ya Taifa.

Haiwezekani mchina anapokea coin Kwa wanafunzi wa shule za msingi mtaani Ili wabet, Taifa tunalipeleka wapi?

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿.

Amen.
 
Sasa ndio ukatupiga na picha ukapost...

images (8).jpeg
 
Sasa ndio ukatupiga na picha ukapost...

View attachment 2936167
Ama Kweli Dunia inapinduka,

Waliokimbia shule saiz wako makini wameshika pen na paper kutabiri hatma ya maisha Yao,

Yaani bodaboda anakwepa kugongwa na magari barabarani, akipata pesa anaenda ipekeka betting Kwa mzungu👀

IPO siku atainuka mtawala mkorofi mwenye maono tutajuta.
 
Biashara ya boda ilivyo ngumu,

Mtu akipata elfu kumi, anabeti elfu Tano.

It's not fair!!
Not fair indeed.....
Inasikitisha sanaa jamani..hivi hawa ndo watakua na familia na kuziendesha kweli? Mungu aingilie kati...no wonder vijana wanapenda mashangazi wapate mserereko wa kimaisha..maana kwa hali hii ndo maana tabia hatarishi zimeongezeka..
 
Wake wa wanaume wenye kubeti wamehangaika vya kutosha kushauri lakini wapi,

Unawezajaje kufanya betting kuwa sehemu ya kipato Cha kuendesha family,

Mume bila Aibu anamwomba mke pesa ya vikoba akabet, Ili airudishe na faida akila mkeka.

Umagharibi utafukarisha Afrika.

Bad enough, pesa wanazochuma wamiliki wa betting zinaenda Ulayaaaaaa..
 
Salaam, Shalom!

Siku moja nilitoka nyumbani kwangu nilipanga kwenda mjini kununua baadhi ya mahitaji muhimu ya vifaa vya umeme,

Niliondoka nyumbani majira ya saa tisa hivi, baada ya nusu saa, nilifika mjini, Sasa Pana duka la vifaa vya umeme kubwa nililokuwa nikitumia kununua mahitaji yangu hapo mjini muda mrefu uliopita, nikiwa natembea nikasema, niende duka lile nikapate mahitaji yangu na kuokoa muda.

Nikapaki gari yangu pembeni kidogo ya sehemu lilipokuwapo duka lile, Nilishuka na kutembea kulikaribia duka lile.

Kilichonishangaza, nikakuta mazingira tofauti kabisa, nje Kuna huduma za chakula watu walionekana wanakula na kunywa Kwa furaha.

Nilikuta duka lile limeongezeka ukubwa na kuongewza urefu, nje alikaa afisa wa ulinzi smart, palifungwa camera za USALAMA, ofisi ilinakshiwa kisasa zaidi. Ndani palikuwa na wazungu kadhaa na wafanyakazi waliovalia mavazi nadhifu.

Nikavutiwa kuingia ndani ya ofisi hiyo kujua nini kinaendelea humo, pia nilitaka kujua muuza electronics alihamia wapi,

Kuingia ndani ya ofisi hiyo, nikakuta watu wenye Rika mbalimbali watanashati, wengi walikuwa vijana na wanawake Wachache,

Mle ndani palikuwa na utulivu wa kutosha, AC Kila Kona, kila mtu alikuwa ameshika kalamu na karatasi na alionekana kumakinika na kusoma kilicho kwenye karatasi,

Nikawaza hiki ni nini watu Hawa wanafanya, niliwaza, yaezakuwa wanafanya labda mtihani hivi, niliwaheshimu sana, nilipoona hali Ile, nami nikalazimika kusogea pembeni alipokuwa askari yule wa USALAMA na kuuliza watu wale wanafanya nini, na ofisi Ile inajishughulisha na nini,

Mlinzi yule alinijibu kuwa pale ni ofisi za BETTING, watu wanachukua mikeka kutabiri timu za mpira wa miguu.

Sura yangu ilifura ghafula, nilitoka haraka ndani ya ofisi Ile nikijilaumu kupoteza muda wangu kuingia ofisi ya ulaghai Kwa nguvukazi yetu ya Taifa inayowateka vijana kuamini kuwa maisha yaezapatikana Kwa Bahati nasibu.

OMBI: Atokee kiongozi mmoja mkorofi aina ya Magu, afute Ujinga huu unaopoteza nguvu KAZI ya Taifa.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿.

Amen.
Nani azifute wakati wanakusanya kodi tena nyingi si kidogo.
Magu alifunga hadi bereau lakini si kampuni za kubet
 
Magufuli alishindwa kuifuta kamari licha ya kupewa ombi na yule sheikh.
Samia akipewa hili ombi surely atafuta kamari ndani ya siku moja .
Aliweza kufuta/kuzuia mitandao ya porno mara tu alipopata ombi.
Sema kizazi cha nyoka hakisikii kinawasha VPN kupata PORNO.
Akifunga kampuni za betting ataokoa mabilioni ya fedha kila siku.
Nguvu kazi ya taifa inaharibika, uchumi wa Taifa unaibwa na wageni kwa njia ya kamari
 
Wake wa wanaume wenye kubeti wamehangaika vya kutosha kushauri lakini wapi,

Unawezajaje kufanya betting kuwa sehemu ya kipato Cha kuendesha family,

Mume bila Aibu anamwoba mke pesa ya vikoba akabet, Ili airudishe na faida akila mkeka.

Umagharibi utafukarisha Afrika.

Bad enough, pesa wanazochuma zinaenda Ulayaaaaaa..
Hata magharibi watu wenye uraibu wa kucheza michezo hiyo si kwamba wanawachukulia poa.
 
Back
Top Bottom