Shitambala bado aiota CHADEMA

Halafu leo anapinga maandamano?

shitambala.JPG
Mkuu njaa mbaya sana ukiendekeza, huyu aliendekeza njaa akapewa makombo sasa amebaki anawayawaya kwa aibu.
 
alizichanga karata zake vibaya alifikiri itakuwa kama wassira, lamwai, tambwe hiza na wengine, yeye kashikishwa mshiko habari ikaishia hapohapo,
 
Hatakaa awe na amani maisha yake yote kwa usaliti wake. Atapingaje habari za maandamano wakati yeye ndo alikuwa mstari wa mbele? Chitambala watakucheka watu!
 
Kumsikiliza "kilaka" ni sawa na kumsikiliza bwabwa akimsifia firauni wake!
 
Aliabika juzi siku alipo kuja Mbowe, alifanya mkutano atthe same time na kamanda Mbowe ktk kata ya Nzovwe ambayo Diwani wa CDM alipewa Tsh 7000000/= na kuachia kata sasa inasemekana yupo Dar.

Katika mkutano wake huo hukuna raia wa kawaida aliye spend muda wa kumsikiliza isipokuwa wa kijani na njano tu wengine wote wakahamia kwa Mh. MBOWE jambo lililo mfanya aahilishe mkutano wake
 
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Sambwee Shitambala, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mbeya, amekitaka Chadema kutambua kuwa siasa haiwezi kuendeshwa kwa namna ya maandamano,vurugu na uchochezi.

Amesema hayo jana wakati CCM kikizindua kampeni zake katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Majengo kwa ajili ya kumnadi mgombea wa nafasi hiyo, Samweli Mwamboma.

Shitambala alisema Chadema wamekuwa wakitumia maandamano yanayoambatana na vurugu wakidhani kuwa hiyo ndiyo njia mwafaka ya kukijenga chama chao bila kutambua kuwa Watanzani wanachotaka ni kuwa na chama ambacho kina mfumo mzuri utakaowawezesha kuwaletea maendeleo.

Alisema wananchi wa Mbeya wasikubali kuwapiga mawe viongozi na badala yake wapige kura kuwachagua viongozi waadilifu ambao wataweza kuwaletea maendeleo.

“CCM msipige mawe pigeni kura, CCM fanyeni maendeleo msifanye fujo, CCM jengeni hoja msifanye maandamano,” alisema Shitambala.

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, alisema wanachama wa CCM watembee kifua mbele kwani serikali yao iliyopo madarakani inafanya mambo mengi ya kuwaletea maendeleo.

Naye mgombea udiwani kata ya Majengo, Samweli Mwamboma, alisema akichaguliwa atahakikisha anashirikiana na wananchi wa kata hiyo katika kuwaletea maendeleo.

Ah!!! Kumbe ni huyu mnafiki...nina kazi na sina umeme nitasoma baadae...
 
kwa kawaida atajuta tu muda si mrefu!
anapenda vya bure huyo, alidhani amekuja kugawiwa ruzuku kumbe alikuwa amekuja kugombea
 
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, alisema wanachama wa CCM watembee kifua mbele kwani serikali yao iliyopo madarakani inafanya mambo mengi ya kuwaletea maendeleo.

Naye mgombea udiwani kata ya Majengo, Samweli Mwamboma, alisema akichaguliwa atahakikisha anashirikiana na wananchi wa kata hiyo katika kuwaletea maendeleo.

Kweli uchache wa akili za huyu mama ndio uliomfanya aibe mataulo hotelini...
Anasema 'wanachama wa CCM, serikali inafanya mengi kuwaletea maendeleo... ni lipi serikali imefanya la maendeleo kuwalenga wanachama wa CCM?
 
Shitambalaaaaaaaaaaaa!!! Asalam aleykhum! Upo? umeadimika kama milango ya pikipiki! DUh! Hiyo ndiyo Magamba bwana wanakutumia wakati wa kampeni tu kwisha kazi!
 
bado atachoka zaidi ya hapo alipo maana wanadanganyiwa kupewa uongozi wanahama lakini ukweli ni ndoto za mchana kweupe
 
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Sambwee Shitambala, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mbeya, amekitaka Chadema kutambua kuwa siasa haiwezi kuendeshwa kwa namna ya maandamano,vurugu na uchochezi.

Amesema hayo jana wakati CCM kikizindua kampeni zake katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Majengo kwa ajili ya kumnadi mgombea wa nafasi hiyo, Samweli Mwamboma.

Shitambala alisema Chadema wamekuwa wakitumia maandamano yanayoambatana na vurugu wakidhani kuwa hiyo ndiyo njia mwafaka ya kukijenga chama chao bila kutambua kuwa Watanzani wanachotaka ni kuwa na chama ambacho kina mfumo mzuri utakaowawezesha kuwaletea maendeleo.

Alisema wananchi wa Mbeya wasikubali kuwapiga mawe viongozi na badala yake wapige kura kuwachagua viongozi waadilifu ambao wataweza kuwaletea maendeleo.

"CCM msipige mawe pigeni kura, CCM fanyeni maendeleo msifanye fujo, CCM jengeni hoja msifanye maandamano," alisema Shitambala.

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, alisema wanachama wa CCM watembee kifua mbele kwani serikali yao iliyopo madarakani inafanya mambo mengi ya kuwaletea maendele.

Hapo kwenye red, mimi ndo huwa nashindwa kuwaelewa hawa CCM, hayo mambo mengi ndio yapi? Mbona hayatamkiki?
 
Maneno haya asemayo yeye kayagunua lini ? Maana kama kweli ni mtu makini angalikuwa anaongea kwa umakini .Huyo naye kasoma ?Kweli ukisha kuwa CCM basi akili zako zinaondoka.Huyu kazeeka mapema hivi ?Pole sana huyu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom