Shirika la Reli (TRC) ndio limegoma kabisa kulipa kiinua mgongo "mkono wa kwa heri" kwa wastaafu wake?

Mangi wa Rombo

Senior Member
Sep 25, 2014
172
104
Habari!

Nimekutana na mzee mmoja mstaafu wa shirika la reli (TRC) ambaye alistaafu rasmi mwaka 2020. Huyu mzee wakati ana staafu alikuja kwangu kunikopa hela, hakikuwa kiasi kikubwa sana, na alihaidi kukirejesha pindi tu atakapolipewa pesa zake za kiinua mgongo ama "mkono wa kwa heri" kama wanavoita wenyewe wafanyakazi wa shirika la reli.

Kwa kweli yule mzee alistaafu lakini pesa pekee aliyoipata ilikuwa ni kutoka NSSF tu tena baada ya kufuatilia sana manake hata michango yake TRC walikuwa hawapeleki hivyo ilimpasa kufuatilia sana! Miaka 37 ya kazi yule mzee aliambulia Mil 21 tu. He was so depressed, mimi deni langu nilim samehe!

Anyway, nimekutana nae jana, ndipo akanipa update.

Kwa mujibu wa mkataba wa wafanyakazi na shirika walio nao, mtumishi anaye staafu kwa mujibu wa sheria ana haki ya kulipwa kile wanaita mkono wa kwa heri!

Ndani ya mkataba huo wanatkiwa walipwe:

1. Gharama ya usafiri kurudishwa mkoa alipo sajili kama nyumbani kutoka kwenye kituo chake cha mwisho

2. Cement na Mabati (sikumbuki mangapi) converted into cash.

3. Hela ya Kiinua mgongo ambayo ni sawa na mshahara wa mwisho wa mfanyakazi x idadi ya miaka (mf: kama mshahara wa mwisho wa mfanyakazi ni 100,000 na mamefanya kazi kwa miaka 30 bhasi atalipa 100,000 x 30 = 3,000,000

Cha kushangaza uongozi wa TRC unalipa kipengele namba 1 & 2 vizuri, icho namba tatu, huu ni mwaka wa saba sasa, hakuna mstaafu anayelipwa.

Kwa kweli wastaafu wa TRC wana hali mbaya mtaani, huwezi amini kama mtu amelitumikia shirika kwa miaka 30 ni aibu!l.

Anasema wameshaenda mahakamani na wameshinda kesi mara 2, lakini uongozi wa TRC umekuwa ukikata rufaa kila mara. Mkurugenzi wa shirika hili ndiye kinara wa kuwa nyonya wastaafu, yeye ndio anaye ongoza kupinga wazee hawa wasilipwe! Alipoingia tu, wakati wa mwendazake akatoa oda ya kusitisha malipo hayo!

Kupitia jukwaa hili, naomba serikali ichunguze ukweli kuhusu hili, najua Mama Samia ni msikivu na ana mapenzi makubwa kwa watumishi, kama ni kweli wazee hawa wana haki, nakuomba uingilie kati! Miaka 30 ya huduma kumuacha bila kitu sio sawa.
 
Back
Top Bottom