TRC kusitisha safari mikoa 6 sababu ya mvua ni ushirikiano na wamiliki wa mabasi. Mvua hazikuwepo kipindi cha Hayati Magufuli?

TRAT

Member
Nov 29, 2022
41
117
Kuna tangazo la kusitishwa kwa safari za train ya abiria safari za Dar - Kigoma kupitia mikoa kadha ya kuelekea bara.

Sababu wanazotoa ni miundo mbinu kuharibiwa na mvua. Swali la kujiuliza ni mvua gani zilizonyesha kuzidi awamu ya miaka 6 ya Magufuli? Mbona hatukuona usimamishaji wa safari kipindi kile.

Hapa majuzi TRC imeifanyia ukarabati mikubwa reli hii ya zamani kulikoni tena safari hizi kusimama?

Sote tunajua kipindi hiki cha msimu wa kilimo abiria hupungua sana. Mabasi kwa sasa abiria wake wamepungua sana. Kitendo cha kusitisha safari hizi za traini ni kuyanusuru mabasi ya mikoani kutokosa abiria.

Ni wakati sasa Rais kufuatilia kama kweli miundo mbinu imeharibika au ni biashara ya wamiliki wa mabasi na maafisa wa juu wa TRC.
 
Kama athari za mvua kwenye miundombinu hiyo ya Reli itaathiri maisha ya binadamu kwa maana ya uwezekano wa ajali basi nakubaliana nao asilimia 100 ,hakuna spare ya maisha ya mtu.

Kama italazimishwa kufanya unavyotaka maana yake Kuna siku tutakuja hapa kuuliza 'mpaka ajali imetokea serikali hawakuona', tuacheni mchezo kwenye maisha ya watu
 
Back
Top Bottom