Tujikumbushe: Kikwete na uuzwaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) vs Rais Samia na kuuza Bandari zetu

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,101
2,344
Naona kosa alilofanya Rais wa awamu ya nne ndugu Jakaya M. Kikwete kuuza Shirika letu la Reli (TRC) Kwa wahindi na kubadilishwa kuwa Tanzania Railway Limited (TRL) analifanya tena Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuuza Bandari zetu Kwa waarabu wa Dubai..

Mtindo na ushawishi uliotumika kuaminisha watu kuwa tunakwenda kupata manufaa makubwa ya kiuchumi kwa kuwauzia wahindi TRC yetu ndiyo uleule unatumiwa na huyu mama na watu wake kuwaaminisha Watanganyika kuwa tunakwenda kupata manufaa haya au yale...

Wahindi walishindwa kuendesha TRC yetu na kwa kifupi kabisa ni kuwa, kwa serikali na bunge kuridhia mkataba ule ndiyo ukawa mwanzo wa mwisho wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), yaani TRC ikafa.

Kila tulichoambiwa kama manufaa ya kiuchumi ya uuzwaji ule wa TRC, kitambo kidogo tu ikadhihirika pasipo shaka kuwa kumbe kila tulichoambiwa lilikuwa ni uongo na hilo kumbe lilikuwa ni dili la ufisadi wa viongozi wa CCM na serikali akiwemo Rais Kikwete mwenyewe!

Ni mjinga gani anaweza kuuamini hiki kilichoelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kwa waziri wake wa ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kuwa kwa mkataba huu wa kuuzwa kwa bandari zetu, kwamba, tunakwenda kuongeza mapato ya bandari kutoka 37% hadi 67% kwenye pato la taifa..?
 
Na kwa TRC, kinara wa kuipigia promo kampuni ya RITES ya India kuichukua TRC alikuwa mzee wa vijisenti, Joka la makengeza. Eti "makosa tuliyofanya kuibinafsisha ATC kwa SAA hayatajirudia tena kwa TRC". Kumbe alishashikishwa kifunga uchumba.
 
Naona kosa alilofanya Rais wa awamu ya nne ndugu Jakaya M. Kikwete kuuza Shirika letu la Reli (TRC) Kwa wahindi na kubadilishwa kuwa Tanzania Railway Limited (TRL) analifanya tena Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuuza Bandari zetu Kwa waarabu wa Dubai..

Mtindo na ushawishi uliotumika kuaminisha watu kuwa tunakwenda kupata manufaa makubwa ya kiuchumi kwa kuwauzia wahindi TRC yetu ndiyo uleule unatumiwa na huyu mama na watu wake kuwaaminisha Watanganyika kuwa tunakwenda kupata manufaa haya au yale...

Wahindi walishindwa kuendesha TRC yetu na kwa kifupi kabisa ni kuwa, kwa serikali na bunge kuridhia mkataba ule ndiyo ukawa mwanzo wa mwisho wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), yaani TRC ikafa.

Kila tulichoambiwa kama manufaa ya kiuchumi ya uuzwaji ule wa TRC, kitambo kidogo tu ikadhihirika pasipo shaka kuwa kumbe kila tulichoambiwa lilikuwa ni uongo na hilo kumbe lilikuwa ni dili la ufisadi wa viongozi wa CCM na serikali akiwemo Rais Kikwete mwenyewe!

Ni mjinga gani anaweza kuuamini hiki kilichoelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kwa waziri wake wa ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kuwa kwa mkataba huu wa kuuzwa kwa bandari zetu, kwamba, tunakwenda kuongeza mapato ya bandari kutoka 37% hadi 67% kwenye pato la taifa..?
Mkataba wa Bandari,

Utaongezaje mapato ilhali TRA haitahusika kukusanya Kodi,

Wakati huo huo haionyeshi tutapata asilimia ngapi kama mgao!!
 
Back
Top Bottom