Shinyanga kuna tatizo gani

njugilo

Member
Feb 8, 2010
58
26
Members ,mie mwenzenu sielewi labda kwa kupitia hapa naweza nikapata kuelewa.Mkoa wa Shinyanga nadhani ni mkoa wenye madini kwa kipindi kirefu sana lakini mbona hapaeleweki ? Maisha ya wenyeji ni duni ,je nanyi pia mmeliona hili,kitu cha ajabu ni kwamba hata kituo cha mabasi yaingiayo na yatokayo mikoani ni vumbi kwa nyakati zote yaani mchana na usiku,hata ukiingia kituoni taa za hapokituoni nyakati za usiku ni hafifu ,je madini yanamsaidia nani hapa Shinyanga ? Je serikali ya mkoa ipo kimaslahi binafsi au ndio utaratibu waliojiwekea kuishi kimasikini ndani ya madini.Nifumbueni nipate elewa.
 
Hilo si tatizo la shinyanga tu...bali la karibu mikoa yote ya nchi hii. Au umesahu ndo sababu twaitwa nchi maskini. Raslimali kibao ila unufaikaji hakuna.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hilo si tatizo la shinyanga tu...bali la karibu mikoa yote ya nchi hii. Au umesahu ndo sababu twaitwa nchi maskini. Raslimali kibao ila unufaikaji hakuna.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
muulize ngeleja anajua sana,pia nanyi mnatakiwa kubadilika kwani huwa mnatuangusha sana kipindi cha uchaguzi mnajifanya mna mbwembwe nyingi za kuvaa matisheti ya ccm na nyimbo nyingi za ushereheshaji za kisukuma,badilikeni msaidiwe.Ni hayo tu kwa leo.
 
Back
Top Bottom