Shida ni Mama Mkwe

the Villag Story

New Member
Feb 13, 2023
2
5
shida.png


MWANDISHI: INNOCENT


Tulianza mapenzi yetu tangu tukiwa secondary na hatukuishia hapo penzi letu lilifanikiwa kufika mpaka chuo kikuu pale mzumbe tawi la mkoa wa Mbeya mungu mwema na hatimae tukaoana.

Lakini kama ningevizingatia vijitabia flani vidogo vidogo alivonionesha mume wangu Terry enzi za uchmba wetu wallah nisingejaribu kuolewa nae. Wahenga walisema ni “kheri uwe na mume mbaya kuliko kuwa na mama mkwe mbaya.”. ulikua ni msemo ambao kamwe sijawahi uamini, lakini sasa unajidhihirisha ndani ya maisha yangu.

Naitwa Dorice ungana na mimi nikupe kisa changu kilichokithiri chungu, chuki, dharau, vituko vya mama mkwe wangu, twende pamoja.

Ni hivi tangu zamani mpenzi wangu ambae kwa sasa ni mume halali wa ndoa. Mapenzi yetu yalianza kama utani tukiwa secondary kwani tulikua hatupendani kabisa yani tulikua maadui wakubwa.

Na hii ni baada ya Terry kunishtaki kwa mwalimu eti mimi namuibia majibu yake tukiwa na kidato cha kwenza kwenye mtihani wetu wa kwanza kabisa. Lakini cha ajabu mwisho wa siku tulikua wapenzi na hatimae kuja kuoana, nikikumbuka mpaka nacheka mwenyewe.

Kwa nini nilianza kumpenda Terry ni kwamba cha kwanza alikua ni mzuri wa sura yani bonge la handsome, alikua mwenye akili sana, msafi, mrefu na sifa nyingine nyingi yani kiufupi ni mtu mwenye sifa ambazo ni ndoto kwa wanawake wengi.

Na mimi sio kwamba najisifia nilikua mrembo na mpaka sasa ni mrembo MashAlah, na enzi tunasoma tulikua tunachuana yani akiwa wa kwanza mimi wa pili aakiwa pili basi mimi wa kwanza. Tulimaliza secondary na kutegana kwa muda kidogo baada ya kwenda A-level.

Hatimae tulihitimu A-level na kuomba chuo kimoja na tulifanikiwa kwenda chuo cha mzumbe. Pale chuo tulikua moja kati couple’s bora kabisa yani tulipewa jina la utani couple gold na watu wetu wa karibu. Yani tulikua tunagandana kila sehemu kama ruba, kwa nini?

Ni kwamba Terry alikua ni mwenye wivu kupitiliza akiniona na mwanaume yoyote basi ilikua ugomvi, niliona kawaida kwani nilijua ni upendo tu. Hayawi hayawi yakawa na hatimae tukaoana na hapa ndo picha lilipoanzia.

Aisee kuna hii tabia moja ambayo inanikwaza sana toka tumeingia ndani ya ndoa. Ni hivi Terry ni “mama boy” nikimaanisha ni mtoto wa mama yani hana maamuzi kama mwanaume mpaka najiuliza hivi nimeolewa na yeye au nimeolewa na mama mkwe.

Kwake mama yake ndo kila kitu, “sawa hakuna ubaya lakini hii mh…mh hapana imezidi”. Kuna baadhi ya vitu inatakiwa aamue yeye kama mwanaume na kiongozi wa familia na sio kuamuliwa na mama yake,

“Hii kwa kweli nashindwa kuivumilia” twende pamoja na mimi ndugu msomaji.

Nikiwa nimekaa sebleni huku nimeshika simu yangu nikiendelea kusoma siulizi inaiyoitwa NDOA YA SHETANI, iliyoandikwa na INNOCENT katika page yake ya Facebook inayoitwa the village story(TVS), ghafra nikaskia mlango unagongwa kuashiria kuna mtu anapiga hodi.

Niliweka simu pembeni haraka nikainuka na kwenda kufungua na kujua aliepo nje ni nani.

Ile nafungua mlango tu, nilihisi joto kubwa ndani ya mwili, huku nikihisi kama nashindwa kupumua na yote haya ni taharuki niliyoipata ndani ya moyo wangu baada kuona aliyekua mlangoni ni…..

Tukutane sehemu ya pili wapendwa. ni mwandishi na member mpya humu naomba mnipokee.

nimawaleteeni simulizi hii nina uhakika mtaipenda.
 
SEHEMU YA 2

MWANDISHI: INNOCENT


ile nafungua mlango tu, nilihisi joto kubwa ndani ya mwili, huku nikihisi kama nashindwa kupumua na yote haya ni taharuki niliyoipata ndani ya moyo wangu baada kuona aliyekua mlangoni ni mama mkwe wangu.

Hakua peke yake aliyekua na mwanamke mwingine ambae hatukupishana sana kiumri alivalia viatu vya kamasai na gauni refu kwa kwa jicho la haraka nilijua tu “lazima huyu ni tetea wa shamba”

“Shi….shi..shikamoo mama”. Sikutaka makuu nilimsalimia huku nimepiga magoti, maana sikutaka kusikia “wanawake wa siku hizi hamna heshima unamsalimiaje mama mkwe wako huku umesimama” kama ilivo kawaida yake.

“Vizuri naona umeanza kujifunza adabu, mwanangu yupo wapi?” mama Terry aliniuliza kwa sauti ya shari huku akinipandishia macho juu mpaka chini.

“Bado yupo kazini mama, si unajua mara nyingi kazi zake anarudi usiku. Lakini kwa muda huu nadhani anakaribia. Niliongea huku nacheka kwa kicheko cha kujiradhimisha hakika ulikua usiku mgumu kwangu.

“Sio muda anarudi si ndio? Yani unaongea ongea tu. Kama unajua yupo njiani unafanya nini hapa? Kwa hiyo akifika atakunywa maji na kulala si ndio? Yani baada ya kumuandalia chakula mume wako kutwa upo tu kwenye mitandao.” Mama Terry.

“hapana mama tayari nimeshamuandalia chakula chake pendwa, wali nyama pamoja na maharage ya nazi. Wali ndo upo jikoni unakakamia mama, em ngoja niende nikaangalie”. Niligeuka haraka na kuanza kuelekea jikoni.

“Wewe unakwenda wapi em kuja hapa. Yani wewe mtoto mimi naogea na wewe alafu unaondoka kienyeji enyeji tu. Ama kweli mwanangu hana mke hapa, kwa hiyo mwanangu ndo amekua wa kula wali nyama siku hizi si ndio? Ndo maana mnakaa tu kama kaka na dada muda wote huu yani mwanangu amekua dhaifu mno”, mama Terry aliongea haraka kama mashine inayoendeshwa kwa umeme.

“Ndi…ndi…ndio mama”. Nilijikaza kujibu pamoja na kwamba gubu lilikua limenijaa shingoni, ila niliamua kujizuia tu.

“Ninachojua mwanangu hawezi lala bila ugali wa dona, nyama choma pamoja na mboga za majani pembeni bila kusahau mtindi ndo maana ulimkuta shupavu. Ila toka amekuoa wewe mmhh eeh mizimu ya kwetu naomba niokoleeni mwanangu” Mama Terry.

“Hapana mama akila chakula hiki ninachompikia huwa anakua na anafurahi zaidi, na ndio maana napenda kumuandalia zaidi.” Niliongea huku namuangalia kwa jicho la ghadhabu maana hasira zilikua zimenipanda mpaka mwisho.

“Eeeh…eeh… ama kweli maajabu hayotokuja kuisha hii dunia, kwa hiyo wewe ndo unamjua mwanangu sana kuliko mimi niliembeba miezi tisa tumboni mwangu? Yani miaka miaka isiyo na faida kazi kujaza tu choo hapa unajifanya mwanangu unamjuaa, we mtoto vipi wewe ebooo muone kule”, Mama Terry.

“Nisamehe mama”. Niliamua kukubali yaishe maana kwa upande wa maneno ni simuwezi kwa kweli. Ni ana maneno huyu mama yani nikiongea neno moja yeye kaongea maneno kumi, kungekua na fundi wa kushona midomo ningemshona zigi zaga wallah tena.

“ninyanyeee nyanya. Jisamehe mwenyewe yani namuonea huruma mwanangu kila siku analalamika kwangu kuwa wewe hujui kupika, mchafu, nyakula vyako havi ivi ndo mana anahara kutwa kwa uchafu wako.” Mama Terry.

“Kwanza hata chakula chako huko jikoni nina wasi wasi nacho” aliongeza kusema. Yani ndani ya muda mfupi Amani yangu ilipotea na kujihisi nipo kwenye ndoa ya shetani kama maria.

“Lakini mama, Terry hajawahi kuniambia hayo yote unayoyaongea hapa. Na pia hajawahi tilia shaka chakula changu, hayo unayoyasema ni mageni kwangu. Na kama ingekua hivo basi angeniambia mimi na sio wewe.” Niliongea kwa hasira huku machozi yanatoka nilitamani nimrukie mwilini kabisa.

“Eboo yani unanipandishia sauti mimi? Sasa kuanzia saizi huyu ndo atakua msaidizi wako, ndo atakua anampikia na kumfulia mume wako. Segito ebu beba hilo begi twende chumbani.” Aliongea mama Terry.

JE UNAPENDA KUENDELEA NA SEHEMU INAYOUFUATA BASI NIFOLLOW ILI UWE WA KWANZA KUONA KILA NINAPOWEKA SEHEMU MPYA.

AHSANTE,, ELIMIKA BURUDIKA.

Tukutane sehemu inayofuata.
 

Attachments

  • shida.png
    shida.png
    140.8 KB · Views: 37

Similar Discussions

Back
Top Bottom