Sura yangu imesagika na kusawajika kwa kichapo cha mama mkwe

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
4,684
10,170
Mimi ni mtoto pekee katika familia ya kitajiri.

Tangu nilipoolewa, nimekuwa nikiishi kwa furaha na mume wangu kwenye ndoa yetu takatifu ya kikatoliki. Sikuwahi kupata changamoto yoyote.

Furaha yangu ilibadilika na kugeuka machungu baada ya mume wangu kwenda masomoni nchini Uingereza kisha mama mkwe wangu kuhamia hapa nyumbani kwa amri ya mume wangu.

Leo nimerudi kutoka sokoni mama mkwe akanidaka, akanikwida, akanibamiza ngumi ya katafunua kwenye kidevu changu, nikapepesuka na kudondokea chogo. Alinitifua ngumi ya uhakika.

Mama mkwe wangu ni mwanajeshi mstaafu, ndio huyo nimemuweka kwenye DP yangu.

Ananishutumu nilitoka kwenda kufanya umalaya nje na kugawa tamu ya mwanawe kwa watu wengine.

Aliponitifua katafunua ya kidevu, akanirukia kwa juu akanikanyaga teke la kisigino, nilipiga yowe nikaanza kubwatuka hovyo kwa maumivu. Ama hakika mama mkwe ana unyayo mkali sana!

Uso wangu wote umesawajika, nimevurugika, sura yangu imeumuka, komwe limetoka nundu kwa juu kama upembe wa faru fausta.

Sijui nifanyeje jamani, nateseka, nahangaika kwenye ndoa yangu!
 
Mimi ni mtoto pekee katika familia ya kitajiri.

Tangu nilipoolewa, nimekuwa nikiishi kwa furaha na mume wangu kwenye ndoa yetu takatifu ya kikatoliki. Sikuwahi kupata changamoto yoyote.

Sijui nifanyeje jamani, nateseka, nahangaika kwenye ndoa yangu!
Pole sana BICHWA KOMWE - rafiki yangu Itabidi uanze mafunzo ya Judo na Karate pale kariakoo karibu na msikiti wa Mtoro wanafundisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom