Sn2139
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 834
- 250
wana JF na wa-TZ wenzangu tuwe waangalifu, tofauti ya vyama haileti tofauti ya uraia na haki ya kukutana. Kikwete na Shibuda ni wa Tanzania na watakufa na kuzikwa Tanzania. Vilevile wote wawili ni viongozi wa kitaifa pamoja na ukweli kwamba wana majimbo yao, hivyo wanaweza wakakutana mahali popote pale ndani ya nchi yao.
Kuna uwezekano Shibuda alipokuwa CCM aliwahi kumpa Kikwete maoni au maonyo fulani fulani akayapuuza, hivyo si vibaya akienda kumkumbusha madhara ya kupuuza maoni yake ambayo yangeweza kukiokoa chama kisifike hapo kilipo hivi sasa. Kumbukeni Shibuda hakuichukia CCM bali alitofautiana na Katibu Mkuu wa chama wakati huo. Lakini vilevile si makosa akienda kumpa ushauri nasaha ili kunusuru nchi kuingia katika hali ya sintofahamu, kwa sababu madhara yake yatampata kila mtu akiwemo na yeye Mh Shibuda...
Sasa tuache speculations zitatufanya tupotoke. Tusianze kusema aah sasa Shibuda anataka kurudi CCM.. je tumejuwaje? Kusalimiana na mtu mnayetofautiana itikadi si vibaya na si haram, kesho na keshokutwa unaweza kumwona Shekh Mkuu akisalimiana na Karidinali Pengo, je tutasema Pengo anataka kuwa mu-Islam? Au Kakobe na Marasusa? au wa Upako na Mwingira...
Tuacheni speculations na tuendelee kubaki wa-Tanzania wenye tofauti ya makabila, dini, itikadi, elimu, maumbo ...lakini bado ni wamoja ndani ya Tanzania