Shibuda ampokea Kikwete Dodoma

Kama sivyo alikwenda kufanya nini kwenye kikao cha CCM? Je, alikwenda kukusanya habari juu ya kile CCM inachokifanya ili aje ku share na wenziwe?
Najiuliza haya maswali sipati jibu. Mwenye kufahamu habari za ndani ajaribu kutu habarisha juu ya mwenendo wa shibuda.
 
Kwanza tufahamu alimpokea wapi na Rais alikuwa na shughuli gani hapo. Kama safari ilikuwa ya Kiserikali ni sawa kabisa. Alimpokea kama Rais wa nchi. Mtu akishakuwa Rais, ni wa Watanzania wote bila kujali itikadi yake kwa maana hiyo Shibuda yuko sawa kampokea Rais. Labda kama Mhe. Rais angekuwa kwenye shughuli za kuimarisha chama chake ndio ingekuwa tatizo kwa Mhe. Shibuda kushiriki katika shughuli hiyo.

Ni shughuli za kuimarisha chama cha magamba na shibuda ni mojawao
 
Mukama anacheka nini kwenye hiyo picha? Kama ni kitu cha kuchekesha nilitegemea na Msekwa
angeshiriki.
 
BABA ZIMA KUJIPENDEKEZA KWA MWANAUME MWENZIo KAMA MWANAMKE haipendezi.
Una maana anatakiwa kujipendekeza kwa wanawake au una maana wanawake ndio wanajipendekeza kwa wanaume? Ongea differently hii mifano ya wanawake kwenye vitu vibaya is so yesterday!
 
Naomba niwatahadhali kitu kimoja kuwa, siasa za maswa ni ngumu sana kwa sasa na hasa ukizingatia mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea nchini.CCM kule maswa haina chake na hii ni kutokana na uwepo wa Shibuda kama mbunge wa CDM.Ikumbukwe pia kuwa ni Shibuda aliyesababisha Mzee BUKOYE kada wa CCM kuhamia CDM na ndiye alikuwa mmoja wa nguzo za wazee wa CCM maswa.Ukisikia mzee Bukoye maana yake ni siasa za Maswa.Shibuda lazima tumpe credit kwa kubadilisha siasa za Maswa, na leo hii huwezi kufikiria kuwa itatokea mgombea wa CCM kwangazi yoyote atashinda maswa hiyo sahau hataka kama atagombea yeye Shibuda hatashinda hiyo ndiyo Maswa ya leo.Kwa hiyo wale wanaofikiria kuwa shibuda anajipendekeza kwa JK na CCM wanapoteza muda bora wajadili mengine.

Tabia halisi za wasukuma:
Wasukuma wana tabia ya ukarimu na ubinadamu kwa kiwango kikubwa (isipokuwa fisadi che*****), kwa hali hiyo ndiyo maana ni kabila pekee lenye watani wengi hapa tz.Kule usukumani kuna ngoma za kienyeji za WAGALU na WAGIKA zinafanyika sana wakati wa mavuno, inapofika wakati wa ngoma mawasiliano kati ya haya makundi huwa yanakoma kwa muda hadi ngoma ziishe mara ngoma zikisha na mshindi kupatikana mahusiano huwa yanalejea kama kawaida na hata kukopesha na kuazimana vitu kunafanyika.
Nimalizie kwa kusema kwamba anachofanya Shibuda ni asili yake ndivyo wasukuma walivyo hawana adui, ila wakati wa majukumu ya kimaslahi hawana aibu ya kumuharibu au kumuua adui.Maswa kwa sasa ni ya CDM na shibuda anajua hilo msipoteze muda yeye na kikwete ni watani.
 
Siasa za kishamba hazitaisha nchi hii. Yaani wewe unadhani mtu kuwa upinzani basi asiwe na mahusiano au mawasiliano na mtu wa chama tawala? Siasa za wapi hizo? Unasemaje uhusiano wa Rais na Zitto au Mbowe na Lowassa? Ni vizuri mkajifunza kukomaa, siyo kudhani kwamba siasa ni vita. Mnaleta ushamba wa simba na yanga kwamba mchezaji akionekana na mchezaji au kiongozi wa timu pinzani basi anataka kuhongwa.
Pombo/mbopo!!nadhani wewe ni Pombe!!
 
Hapo ni mwenyekiti wa ccm kwani alienda kama kada na kiongozi wa ccm kulikoni shibuda kumpokea

Ikiwezekana waulizwe watu wa itifaki wa CCM, kwamba ilikuwaje Mhe. Shibuda kuwemo katika safu ya viongozi wakuu wa CCM waliopangwa kumpokea Mhe. Mwenyekiti wa Taifa wa CCM? Labda anajiandaa kurudi alikotoka. CDM walifanya kosa kubwa kumpokea wakati moyo wake ulikuwa bado katika mwili wa CCM. Yeye yaonekana hakufuata itikadi na sera za CDM bali ulaji wa pale mjengoni.
 
mbona tunasikia ya kuwa Mabere Marando ni wakili wa mafisadi? hilo nalo hulioni? Nalog off

Unajua humu watu wengi hawatafautishi Personals na issues zenye mshiko na maisha!! bora kama mtu anataka kutufurahisha lakini wengi wanaushabiki tuu bila hata kureason!! na very defensive!! nachukiaga sana!!

Hakuna ubaya mtu kua na urafiki na mtu mwingine!! na kama ni hivyo humundani wengi tupo tofauti na tunaheshimu pande zingine na aiwezekani watu wafikirie vile ambavyo kundi lingine la fikiri!!

Niliwahi safiri na shibuda kwenye flight moja na alikua anongea nikagundua jamaa kiasi furani muelewa na hataki kuburuzwa na hilo ndio wengi hawampendei!!
 
Ni mbaya kuwa vuguvugu, ni bora kuwa moto au baridi. Hii ya shibuda naweza kuifananisha na mtu aliyeoa lakini bado ana mapenzi na hawara(Demu wa zamani).na inafika mahali anashindwa kucontrol hisia zake juu ya Hawara.

AM sorry to use this example ila natafuta njia nzuri ya kuexpress mawazo yangu.
 
Mwone mishavu yake i njaa tu zinamsumbua!posho hazitoooshih anakwenda kujikosha kwa hao magambba!bola sheria ya ushoga ingepitishwa ili watu kama hawa wawe wazi kuliko kujifichaficha tu,wenzake wanahangaika na harakati kkama Lema na wakina lisu,slaa an mmbowe yeye anatafuta mabwana huko c.c.m,mi linanichefua ktk sehemu walizoharibu chadema ni kulipokea hili PUNGA,uharabuni wangekuwa wamesha ligadafi,cameroon mkubwa!
 
Sioni tatizo lolote kwani Kikwete sio rais wa ccm, cdm wala Tlp ni wa WaTZ wote , including Shibuda.
 
Ikiwezekana waulizwe watu wa itifaki wa CCM, kwamba ilikuwaje Mhe. Shibuda kuwemo katika safu ya viongozi wakuu wa CCM waliopangwa kumpokea Mhe. Mwenyekiti wa Taifa wa CCM? Labda anajiandaa kurudi alikotoka. CDM walifanya kosa kubwa kumpokea wakati moyo wake ulikuwa bado katika mwili wa CCM. Yeye yaonekana hakufuata itikadi na sera za CDM bali ulaji wa pale mjengoni.

Shibuda alikua anasubiri ndege ya serikali iliomleta Rais Dodoma,iwapeleke Dar kuunganisha ndege ya kwenda Marekani katika ziara ya kiserikali,walikuwepo Mh.Lucy Owenya,Zungu...labda yeye kaanza kufika kabla ya wenzie,Rais kamkuta shibuda waiting Lounge,hatujaona picha akimpokea toka kwenye ngazi za ndege
 
Back
Top Bottom