Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Wakuu, naombeni msaada wa kesi na sheria zinazohusu talaka (divorce) na mgawanyo wa mali za ndoa (division of matrimonial properties) hasa kwenye kesi zinazohusu mgawanyo wa Mali ikiwa mwanandoa mmoja aliondoka na Mali kabla hajapetition 4 divorce na sasa anadai mgawanyo. Na ndoa ni ya kiislamu.

Asanteni sana

Cc Petro Mselewa, Dragoon, soskeneth na wengine wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu naombeni msaada WA kesi na sheria zinazohusu talaka(divorce) na mgawanyo WA Mali za ndoa(division of matrimonial properties) hasa kwenye kesi zinazo husu mgawanyo WA Mali ikiwa mwanandoa mmoja aliondoka na Mali kabla hajapetition 4 divorce na sasa anadai mgawanyo ... Nb ndoabni ya kiislamu.asanteni sana<br />Cc Petro Mselewa,Dragoon, Soskeneth na...... Na wengine wote<br /><br />Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, angalia hizi kesi, japo nimetoa kwa uchache pamoja na Article fupi iliyochambua masuala ya division of matrimonial properties. Kwa reported cases ukiachana na ile ya Bi Hawa Mohamed angalia pia:

Samwel Olung'a Igogo and two others v. Social Action Trust Fund and others [2005] TLR 343
Charles sio Manoo Kasare and another v. Apolina wlo Manoo Kasare [2003] TRL 425
Amina Taratibu Mhonde v. Selemani Ahmedi Mtalika [2000] TRL 56
Samweli Moyo v. Mary Cassian Kayombo [1999] TRL 197
Juma Rahisi Nanyanje v. Shekhe Farisi [1999] TRL 29
 

Attachments

  • Hindu-Christiam marriage.pdf
    590.5 KB · Views: 249
  • division 6.docx
    27.3 KB · Views: 170
  • division 1.pdf
    236.6 KB · Views: 129
  • division 2.pdf
    256.7 KB · Views: 122
  • division 3.pdf
    47.7 KB · Views: 389
  • division 4.pdf
    1.2 MB · Views: 117
  • division 5.pdf
    10.4 MB · Views: 205
  • article division.pdf
    185.8 KB · Views: 807
Mkuu Victoire, kwanza yategemea namna ya ndoa iliyofungwa baina yenu.Kama ni ya kiislam,kwa mfano,watoto wa nje ya ndoa hawawezi kurithi. Kama ni ndoa ya kimila,yategemea mila za kabila lenu husika. Kama ni ndoa ya Bomani, yategemea na makubaliano yenu katika ndoa yenu.Hii ni kwakuwa,kifungu cha 58 cha Sheria ya Ndoa kinaruhusu uwepo wa Makubaliano juu ya umiliki wa mali za ndoa.Umiliki ndio unaelekeza urithi hapo baadaye.

Nataka nieleweke kuwa, kama mali ni binafsi kama inavyoruhusiwa chini ya vifungu vya 56 na 57,urithi waweza kufuata sheria,mila au Wosia.Lakini,kama ni mali ya pamoja watoto wa nje ya ndoa (kwa ndoa za bomani na za kikristo) hurithi kutokana na matakwa ya wanandoa tu na si vinginevyo.
Sasa mfano wanandoa ni wakristo. Mme amepoteza maisha na hajaacha wosia wowote juu ya Mali hizo. Na watoto wa nje wamejitokeza wanataka Mali. Hyu mjane c ana haki ya kuwanyima hata mia?
 
Sasa mfano wanandoa ni wakristo. Mme amepoteza maisha na hajaacha wosia wowote juu ya Mali hizo. Na watoto wa nje wamejitokeza wanataka Mali. Hyu mjane c ana haki ya kuwanyima hata mia?
Mkuu, mjane au ndugu yeyote hana haki ya kugawa au kunyima mirathi. Msimamizi wa Mirathi huteuliwa na Mahakama baada ya taratibu za kisheria kufuatwa. Mabishano ya nani ni mrithi na arithi nini yatamalizwa mahakamani.
 
Mkuu, mjane au ndugu yeyote hana haki ya kugawa au kunyima mirathi. Msimamizi wa Mirathi huteuliwa na Mahakama baada ya taratibu za kisheria kufuatwa. Mabishano ya nani ni mrithi na arithi nini yatamalizwa mahakamani.
Aisee!!!! Lakin kwa uonavyo wewe kisheria hao watoto ambao hawajawah kuonekana nyumbani kwa marehem hta siku moja wanafaa kupata Mali yoyote???
 
Ni jinsi ipi ndoa inakuwa halali kisheria mkipitisha miezi mitatu mnaishi tuu? Naisikiasikia lakini sina elimu kuhusu hili
 
ni jinsi ipi ndoa inakuwa halali kisheria mkipitisha miezi mitatu mnaishi tuu?naisikiasikia lakini cna elimu kuhusu hili
Hiyo inaitwa presumption of marriage yaani dhana ya ndoa.Mnatakiwa kuishi miaka miwili mfululizo kama mke na mume .Asiwepo mwenye ndoa nyingine kati yenu,jamii inayowazunguka iwatambue kama mke na mume.Kinyume na hapo hakuna ndoa.
 
okk,maana kuna kesi watu wameishi miezi mitano mwanamme kamfukuza hawara yake na kipigo juu.hawara anataka wagawane mali
 
okk,maana kuna kesi watu wameishi miezi mitano mwanamme kamfukuza hawara yake na kipigo juu.hawara anataka wagawane mali
Hakuna ndoa hapo,hiyo inaitwa cohabitation ,aina mojawapo ya uchumba.Kama kuna vijizawadi labda bi dada alimpatia kwa ahadi fulani fulani aweza kumrudishia ila hakuna cha kugawana,sheria ya ndoa haitambui hayo.Hata Diamond na Zari bado hawana ndoa maana hawajakaa miaka miwili mfululizo.Zari muda mwingi yuko South Africa na Jamaa yuko madale.
 
Back
Top Bottom