Sheikh Yahya: Mengi kuingia kwenye siasa, Kikwete Kushinda kwa Kishindo

Huyu jamaa alisema 2005 raisi lazima awe mwanamke. Ilipotokea JK akasema yeah utabiri umetimia si mnaona wenyewe JK ana haiba ya kike!!!!!!!!!


Huyu Sheikh alimdhalilisha sana Rais kwa kusema kuwa ana haiba ya kike.

Kama kweli katiba yetu inamlinda rais aliyemaliza muda wake hata kwa madudu aliyofanya bila kujali interest za taifa inakuwaje katiba hiyo haimlindi rais aliyeko madarakani kama akidhalilishwa personally namna hii?
 
Huyu jamaa alisema 2005 raisi lazima awe mwanamke. Ilipotokea JK akasema yeah utabiri umetimia si mnaona wenyewe JK ana haiba ya kike!!!!!!!!!

Bwaa haahhahhaaa mmeniacha hoi wazee kwa mabadiliko hayo ya papo kwa papo, lakini kuhusu hili la BWM linaweza kuwa kweli kwani anaweza kuwa amepata nyeti toka kwa mkulu wa nyumba kwani nijuavyo wanaukaribu wa kifamilia hawa
 
Kuna kitu kinaitwa uhuru wa kusema (freedom of speech). Ukimdhalilisha mtu kwa kutoa facts za uongo unaweza kushtakiwa kwa defamation, lakini sio kosa la jinai.

Mtikila anaonewa anapokamatwa kwa yale anayosema. Tuna uhuru wa kutoa maoni yetu kuhusu Rais. Kama naona ana haiba ya kike basi nina uhuru wa kusema hivyo. Si kosa (criminal or otherwise) kuwa na opinion yoyote.

We are free to have any and every opinion about the President. Kama kuna sheria inakataza hilo, basi sheria hiyo inakiuka haki za msingi za raia. There are such things as unconstitutional laws.
 
Sheikh Yahya Hussein:

Kuna tabiri ambazo naweza kumpa credit.

(a) Mwishoni mwa mwaka 2002 alisema kuwa Saadam Huessin atatolewa madarakani kwa nguvu mwezi Machi mwaka 2003. Ni kweli ilitokea hivyo

(b) Mwaka huo huo alisema kuwa kungetokea ajali ya chombo kikubwa sana cha anga; ni kweli Space Shuttle Columbia ilipasukia angani mwezi Januari mwaka huo wa 2003.


Lakini tabiri zake nyingi hazina ukweli.

(a) Wakati anasem Saddam atatolewa madarakani, alisema pia kuwa Osama bin Laden angeshikwa, kufariki au kuuwawa; lakini Bin Laden amekuwa anatoa kanda zake kila kukicha.

(b) Alisema kuwa rais wa Tanzania baada ya Mkapa angekuwa mwanamke. Sielewi kama huyu Kikwete (ambaye huko mitaani akina mama hawapumui) kweli ni mwanamke,

(c) Nadhani mwaka 1973 au 74 hivi alitabiri kuwa timu ya Yanga ingekuwa bingwa lakini ubingwa huo ulichukuliwa na Simba (au kinyume chake)

Kwani Osama bado yupo Hai?

Kuhsu Mkapa..alisema Rais atakuwa na haiba ya kiike..which means kupendwa.Na Jk alikuwa akipendawa sana na kila Mtu,hata zaidi ya wale wanaompinga zaidi ila zamani walikuwa wakimtetea.

Nmkumbuka Absalom Kibanda,Huyu alikuwa Shabiki nambari moja wa kikwete na sijui ilikuwaje akaanza kumchukia
 
Anasema wanajimu wapo toka binadamu alivyoumbwa. Hata Mamajusi walitabiri kuzaliwa kwa Yesu kupitia nyota. Mwaka 2009 ni mwaka wa Kimataifa wa unajimu . Means ni kitu kinakubalika . Na yeye ni mnajimu pekee East and Cetral Africa. Mnasemaje? Simfagilii ila je utabiri ni absolute truth au ni probability?
 
Hii ya mkapa siuoni ukweli zaidi ya kuendelea kutafuta ya kumuongelea hovyohovyo tu, lakini nimedokezwa na kuonyeshwa moja ya utabiri wake last year, alisema initial agreement ya zimbambwe ni sept 15 2008 na ilikuwa hivyo wakuu.

Wacha mzee azeeke taratibu kwa kamkate kake ambako kanapatikana kwa ridhaa huru kwake toka kwetu. Maana havunji nyumba za watu wala hauwi albino
 
Nadhani ni mtu mweledi na aliyebobea kwenye 'taaluma' yake. Mara kadhaa utabiri wake unakuwa astonishingly perfect. Binafsi alinishangaza sana mwaka 2005 alipoweza kutabiri BWM kuongoza kama rais kwa zaidi ya muda uliotarajiwa kisheria. Kwa bahati nzuri nilimsikia wakati akitoa utabiri huo (some months before 2005 election). Kwa wakati huo nilidhani pengine alikuwa akipiga debe tu la kisiasa ili katiba ibadilishwe na BWM agombee kwa kipindi cha tatu.

Ni kweli kuna tabiri nyingi tu anachemsha lakini nadhani pia si haki kum-discredit kabisa.
 
baadhi ya wahandishi wanataka kuingiza nchi hii kwenye mambo ambayo sio. Huu ni ushirikina mkubwa ambao unapandikizwa kwenye mioyo ya watanzania itafikia siku serikali na jamii kwa ujumla itakuwa haifanyi jambo hadi mnajimu aje aangalie. Hasara kubwa, siamini hata kimoja kati ya alivyosema na hata vikitokea si kwa kuwa yeye alisema bali ni mipango ya mungu.
 
Wakati fulani hawakuiva kabisa na Mwalimu kwa sababu ya utapelitapeli wake akakimbilia Kenya.Tunapowalaani waganga wanaosababisha mauaji ya ALBINO tunamwacha huyu anatamba kiasi hiki wenye akili timamu hawatuelewi.
 
Huyu ni Sangoma na wala masuala ya nchi hayawezi kuongozwa kwa unajimu na kubashiri.

Ndio hawa wanajimu kipindi cha vuguvugu la uchaguzi wa 2005 waliwahi mdanganya RPC wa Shinyanga kipindi hicho kuwa atamrithi IGP Mahita?
 
Niliwahi kusoma katika makala moja katika gazeti la rai enzi hizo ikimtuhuumu sheikh yahya kuwa ni usalama wa taifa,hivyo huwa anapewa hint ya what will happen in the next few days hili hata kama litatokea watu wasishituke hasa kama suala lenyewe ni la kushitua.Hivyo kuweni makini na utabiri wa sheikh yahya.Jamaa alitoa ushahidi aliosema unapatikana katika kitabu kiitwacho THE DARKNESS SIDE OF MWALIMU,binafsi sijawahi kukiona ingawa sijafanya juhudi ya kukitafuta.
 
Huyu mganga wa kienyeji nae aacha kuwadanga Watanzania. Imani za kipumbavu kama hizi ndio zinaendelezwa na vyombo vya habari na mwishowe tunakuta Maalbino wanauwa kwa upuuzi kama huu. Huu ni utabiri gani .. eti watu mashuhuri watakufa.. hali ya uchumi itakuwa mbaya.. mbona haya mambo hayahitaji hata utabiri? Huyu ni tapeli anayeganga mlo wake wa kila siku na hakuna cha utabiri wala nini... upuuzi mtupu...
Wizi Mtupu
 
Kikwete kushinda kwa kishindo 2010

Gloria Tesha

Daily News; Thursday, January 08, 2009 @21:15

Mtabiri maarufu nchini, Shehe Yahya Hussein, amemtabiria ushindi wa kishindo Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu mwakani na kwamba Serikali yake itakuwa ya Muungano wa Vyama vya Siasa.

Shehe Yahya amesema pia kuwa ushindi wa Kikwete utatokana na mwendelezo wake wa kufichua mafisadi na kuwafikisha katika vyombo vya sheria bila woga na kwamba katika uchaguzi huo, hakutakuwa na wizi wa kura, bali watu watashughulikia kutafuta fedha na mtandao wa mafuta.

Mtabiri huyo alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya utabiri wake kwa mwaka huu kwa waandishi wa habari. Kuhusu ushindi wa Kikwete na hali ya kisiasa kuelekea mwaka wa uchaguzi, alisema utabiri wa mwaka huu uliopewa baraka zote na Umoja wa Mataifa, kuwa mwaka wa kuongozwa na nyota duniani, unaonyesha kuwa kiongozi mwenye jina lenye herufi J na K nchini, ndiye anayeongoza nchi.

“Pamoja na kuwa na herufi hizo, pia mwenye bahati kuwa katika uongozi wa awamu ya pili, ya tatu na sasa ya nne, awe mwenye kichwa cha bapa, uso wa meza na rangi ya maji ya kunde … mwenye nyota hiyo ni Kikwete na hivyo namtabiria kuendelea kuongoza nchi 2010,” alisema Shehe Yahya.

Alisema pamoja na kuwa na nyota hiyo inayoonyesha ushindi, endapo ataacha kuwatetea wanyonge kwa kupingana na baadhi ya matakwa ya watu wa chama chake, atashindwa vibaya katika uchaguzi na akakionya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kiburi na kutambua kuwa hakitaongoza nchi peke yake mwaka huo.

Akifafanua kuhusu Serikali ya Muungano wa Vyama, alisema dalili zilizopo zinaonyesha Serikali ya Mseto na kuzitaja dalili hizo kuwa ni kampeni za kinyang’anyiro cha ubunge Mbeya Vijijini, ambako vyama vya upinzani vinaangushana na kuiunga mkono CCM.

Hata hivyo, alisisitiza hakutakuwa na wizi wa kura katika uchaguzi ujao na badala yake itaundwa Serikali ya Mseto na kwamba viongozi wakiwamo wabunge walioko madarakani watakaoendelea kufanya ufisadi na kutotenda haki kwa wanyonge, watashindwa vibaya katika uchaguzi huo.

“Mwaka huu vifo vya watu mashuhuri vitaongezeka sana na kutakuwa na kukwama kwa viongozi wapenda rushwa na wale watakaosema ukweli bungeni bila kuficha kitu, watachanua katika uongozi na maisha kifedha,” alisema.

Shehe huyo alimzungumzia pia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi, kuwa atajiunga na siasa mwakani na pia mgogoro wake na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, hauwezi kuendelea kwa kuwa herufi za majina yao ya pili ni M zikifuatiwa na herufi E na A ambazo kinajimu ni ndugu wa baba mmoja. Pia mnajimu huyo alimtabiria Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuwa kati ya sasa na Aprili mwaka huu, atapata kazi kubwa duniani ambayo itaiacha Dunia ikishangaa, hasa Watanzania.
 
baadhi ya wahandishi wanataka kuingiza nchi hii kwenye mambo ambayo sio. Huu ni ushirikina mkubwa ambao unapandikizwa kwenye mioyo ya watanzania itafikia siku serikali na jamii kwa ujumla itakuwa haifanyi jambo hadi mnajimu aje aangalie. Hasara kubwa, siamini hata kimoja kati ya alivyosema na hata vikitokea si kwa kuwa yeye alisema bali ni mipango ya mungu.

Nakubaliana na wewe mkuu Msasa, baada ya muda si mrefu watu wataanza kwenda Mlingotini, Sumbawanga mambo yasipokwenda kama ilivyotabiriwa.
Watanzania tujifunze kufanya kazi kwa bidii,unajimu haumpi mtu matarajio mazuri katika maisha.
 
Lakini ni Sheikh !!

"wajinga ndio waliwao...Sheikh mapepo huyu anawatapeli watu sana"




Sheikh maana yake ni Mzee ama wajaluo wanamwita Jaduong', nao wapare wanamwita Mghothi. Yaani mtu mzima ama mtu aliyekula chumvi nyingi.
 
Back
Top Bottom