Sheikh Yahya: Mengi kuingia kwenye siasa, Kikwete Kushinda kwa Kishindo

...opportunists tu hao, binaadamu wote wanauwezo wa kutabiri.
 
Mkuu YY,

Huwa SINA imani kabisa na ubashiri, siamini kama ubashiri wa Sheikh ni sahihi........

....Lakini otherwise, ya utabiri ni waste of time kumsikiliza ingawa pia hamlazimishi mtu kumsikiliza....

....
Nilitegemea mjadala kama huu wote tunaoitakia mema nchi hii tungeungana kukataa mambo ya uaguzi,uchawi,utambuzi wa nyota nk, lakini hata wale wachangiaji wazuri kwenye mada zingine ambazo wakati mwingine ni za kipuuzi kabisa wako mbele kutoa maoni, watu km invisible,masatu,field marshal,kibunango na wengine, hawa ni wanafiki wakubwa! Hakuna hata chembe ya kulitakia taifa hili mema, ni wanafiki tu
Mkuu katika maandishi niliyonukuu hapo juu nani mnafiki? Nadhani unatakiwa kusoma kilichoandikwa na yeyote unayemwita mnafiki kabla ya kumhukumu hivyo.

Unafiki mkubwa ungekuwa pale ambapo tungejifanya hatujui huyu mzee kaamua kujitangaza kwa kutoa Press Conference na kuongelea kile anachopenda kimtangaze zaidi kwa watanzania walio wengi wenye kuamini masuala ya Ubashiri ambao kwangu KAMWE sina imani nao.

Hukututendea haki, nadhani uende mbali zaidi useme magazeti ya Tanzania yote ni wanafiki na watanzania wote walioangalia Taarifa za habari pia wanafiki pamoja na wote waliochangia mada hii iwe wanapinga ama wanaafiki ni wanafiki (ambapo nawe utakuwa mmoja wetu!).

Anyway, hatuwezi kulingana mitizamo "Mpiga kura wa kweli".

Invisible
 
Sheikh Yahya Hussein:

Kuna tabiri ambazo naweza kumpa credit.

(a) Mwishoni mwa mwaka 2002 alisema kuwa Saadam Huessin atatolewa madarakani kwa nguvu mwezi Machi mwaka 2003. Ni kweli ilitokea hivyo

(b) Mwaka huo huo alisema kuwa kungetokea ajali ya chombo kikubwa sana cha anga; ni kweli Space Shuttle Columbia ilipasukia angani mwezi Januari mwaka huo wa 2003.

Lakini tabiri zake nyingi hazina ukweli.

(a) Wakati anasem Saddam atatolewa madarakani, alisema pia kuwa Osama bin Laden angeshikwa, kufariki au kuuwawa; lakini Bin Laden amekuwa anatoa kanda zake kila kukicha.

(b) Alisema kuwa rais wa Tanzania baada ya Mkapa angekuwa mwanamke. Sielewi kama huyu Kikwete (ambaye huko mitaani akina mama hawapumui) kweli ni mwanamke,

(c) Nadhani mwaka 1973 au 74 hivi alitabiri kuwa timu ya Yanga ingekuwa bingwa lakini ubingwa huo ulichukuliwa na Simba (au kinyume chake)

Mkuu ,
umeniacha sina mbavu!
utabiri mwingine bwana!
 
Kama angekuwa mtabiri mzuri angeweza kutabiri kuhusu meli iliyozama ziwa Victoria miaka michache iliyopita na kuweza kulifanya taifa kuwa katika hali ya hadhari (niliambiwa na mtaalamu mmoja kuwa tahadhari ni kitenzi) na hivyo kuondokana na janga la kitaifa liliokotea.

Angeweza pia kutabiri kuhusu ajali zinazoua ndugu zetu kila kukicha hapa nchini. Kuna mambo mengi tu ambayo angeweza kutabiri na kutufanya kuwa makini katika kukabiliana na matatizo yanayotukumba katika nchi yetu.

Nasema hivi kwa vile naamini mtabiri ni mjumbe wa Mungu, ambaye huwa anatoa ujumbe fulani ili uwasaidie watu waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha katika jamii wanayoishi. Mbona hatuoni hilo lilitendeka kupitia mtabiri huyu anayepewa sifa za bure?

Nami naungana na wale wanaohoji utabiri wake. Na tukiendekeza watu wa namna hii tunakuwa 'misled' na nchi yetu itanedelea kuwategemea wapotoshaji wa hali halisi ya maisha ya watu.
 
pia atabiri lini wapalestina watakuja wawashinde waisrael. aguse huko tuone, yeye si anajifanya mtabiri?aguse hata kwenye mboni ya jicho la Mungu huko kama hataokota makombo jalalani na kutembea bila nguo.
 
Huu ni uwongo mtupu! na wizi mtupu! Huyu jamaa Sheikh Y anauhusiano wa namna fulani na familia ya JK.akijua ana-interest ktk familia hiyo ndiyo maana anampigia debe.Si anajua upepo ni mgumu kwa huyo muheshimiwa.Is propaganda to make him clean and beuty, slowly the poison will enter the mind of Tanzanians, to think that we don't have another choice.
Mpaka kieleweke. watafuteni masheikh,wachungaji,mapadri na kadhalika sisi tunasema TUMECHOSHWA NAYE. we need a strategic person to lead towards developments.
 
Hivi hapa tatizo liko wapi jamani?..
Huyu ni Mtabiri na wapo dunia nzima hata ddunia ya kwanza wapo watu kama hawa na sioni tatizo ni lipi..
Hata ktk elimu tunao madaktari ambao wanakupa diagonosis hii ukienda Hospital kumwona daktari mwingine wanakwambai tofauti!..Dini zetu zenyewe zina tabiri na dalili ya dunia kwisha na kila siku wahubiri huja na kutuambia kuwa dunia inakwisha kesho mara kesho kutwa!.. Ni maswala ya Utabiri tu hayana matusi ndani yake..

Huyu mtu katabiri alofikiria ktk ujuzi wa kazi yake hukubaliani naye huna haja ya kuvimba mishipa ya kichwa kwani huu ni Utabiri tu..Kweli kuna kila dalili Kikwete kushunda tena kwa kishindo, Mengi anaweza kuingia siasa kwani kuna kipingamizi?.. zaidi nini hasa! Ni kitu gani hasa kilichowafanya mfikie hata kutovumilia..
 
JF kila kitu udini... Aaah! mi nachoka kabisaa...! Watu wanafikia hata kupoteza hikma na busara zao...! Kaaziii... kweli kweli!
 
Ikumbukwe marehemu mwandishi Ali Nabwa alishawahi kuonya watanzania kuhusu ubashiri wa Shk.Yahya.

Anajenga hoja kuwa jamaa natumiwa na serikali toka enzi za nyerere kwa namna mbali mbali.

Nitaeleza chache, mfano serikali inataka ku-assassinate kiongozi wa serikali mwenye cheo cha uwaziri basi jamaa atatabiri kutokea kwa ajari itakayo muua waziri, watu wa usalama wataanda ajali deki na kumuua waziri na sisi wananchi hatutastuka sana maana tulishaandaliwa kisaikolojia.

Pia hutumika sana kipindi uchaguzi unakaribia kwa mfano CCM inataka kumsimamisha mgombea fulani sasa haina uhakika jinsi wananchi watamchukuliaje, basi huyu jamaa ataropoka na kuanza kutoa utabiri kuhusu huyu mgombea na sisi tutaanza kuropoka mitaani na usalama watakusanya data jinsi gani mgombea huyo atapokelewa hata kabla ya kuchaguliwa.

Naweza kueleza mengi ila mfano mzuri ni kwenye kitabu cha THE DARK SIDE OF NYERERE, mwandishi anaeleza jinsi alivyokimbilia Kenya na kukutana na Sheikh Yahya ambae alimkaribisha chumbani kwake na kujikuta akipoteza documents zake muhimu chumbani kwa Sheikh Yahya katika mazingira ya kutatanisha na documents hizo alizikuja kuziona tena Dar es Salaam zikiwa mikononi mwa Usalama wa Taifa baada ya kukamatwa na kurejeshwa nchini.

Mweye masikio na......
 
Mimi ninatabiri hivi:

-Hakuna mfanyabiashara atakayeingia tena kwenye siasa kuanzia sasa;
-wasiotaka serikali ya mseto Zanzibar watafagiliwa pembeni;
-nchi itakumbwa na njaa kwa sababu waziri wa kilimo hana habari na kinachoendelea mipakani ambayo mahindi ya Tanzania sasa yanauzwa Sudan na wajanja kutoka Kenya;
-Serikali itaingia ubia na nchi fulani kuagiza na kuhifadhi mafuta ya peteroli nchini;
-Balance sheet na Income statement na Sources and Uses of Funds za benki kuu, Hazina, Vyuo Vikuu, wizara na mashirka mbalimbali yatakuwa yakichapishwa kila miezi mitatu ili kutoruhusu fisadi kufanya kazi zao wakati wengine tumelala;
-ATC itafufuliwa ikiongozwa na vijana wajasiliamali na wataanza biashara kwa kuleta mizigo toka Dubai, China, India na Marekani kusini.
-Gati ya mafuta itajengwa Pemba na Wazanzibari tutakuwa tunaagiza mafuta moja kwa moja kwa kupitia shirika jipya la peteroli Zanzibar;
-Mawaziri wakuu wote wa zamani na wote waliokuwa na nyadhifa za uwaziri, ukatibu mkuu, wakuu wa mikoa na wilaya wastaafu na walimu wastaafu, madaktari wastaafu, madereva wastaafu, wakulima na wafugaji wenye umri mkubwa wataundiwa Baraza la Wazee la Taifa au Bunge la Ushirikishwaji wanajamii na wanataaluma;
-Mrahaba toka wachimbaji dhahabu na madini utaongezwa na kuwezesha Watanzania kusomesha bure watoto wao toka Chekechea hadi Chuo Kikuu!

Haya tuone ya Sheikh Yahaya (hivi Quran inaruhusu sheikh kutabiri kweli, mimi kafiri sina neno nikitabiri hata hivyo!).
 
Hivi hapa tatizo liko wapi jamani?..
Huyu ni Mtabiri na wapo dunia nzima hata ddunia ya kwanza wapo watu kama hawa na sioni tatizo ni lipi..
Hata ktk elimu tunao madaktari ambao wanakupa diagonosis hii ukienda Hospital kumwona daktari mwingine wanakwambai tofauti!..Dini zetu zenyewe zina tabiri na dalili ya dunia kwisha na kila siku wahubiri huja na kutuambia kuwa dunia inakwisha kesho mara kesho kutwa!.. Ni maswala ya Utabiri tu hayana matusi ndani yake..

Huyu mtu katabiri alofikiria ktk ujuzi wa kazi yake hukubaliani naye huna haja ya kuvimba mishipa ya kichwa kwani huu ni Utabiri tu..Kweli kuna kila dalili Kikwete kushunda tena kwa kishindo, Mengi anaweza kuingia siasa kwani kuna kipingamizi?.. zaidi nini hasa! Ni kitu gani hasa kilichowafanya mfikie hata kutovumilia..

we si ndo walewale wanaosapoti uchawi na upiga ramli na uganga kama wa kutabiri? hapo unajionyesha picha yako halisi ilivyo. siajabu wewe ndio mmojawapo wa vigogo wanaosapiti uchawi, kama wale wanaonunua viungo vya albino. si ajabu hata hapo unapoandika umekalia hirizi. watu kama wewe kuna siku mmetengewa, mtajibu kila kitu mlichofanya. ukae ukijua ya kuwa, mtu anayesapoti kosa, ameshiriki kosa. unatakiwa kujua ya kwamba, Mungu anakataza vyote hivyo, na wewe unatakiwa kuvikataa lasivyo utaadhibiwa na Mungu. kazi kwako na uchaguzi ni wako.
 
JF kila kitu udini... Aaah! mi nachoka kabisaa...! Watu wanafikia hata kupoteza hikma na busara zao...! Kaaziii... kweli kweli!

Dini ndio inayokufanya hata wewe uiishi leo. kwa maovu yanayofanyika tz, Mungu angeshatuadhibu muda mwingi kama hakungekuwa na watu wadini wanaoomba na kulia kwaajili ya rehema kwa tz kila siku. hivyo dini ni muhimu sana hapa. wewe unadharau dini, ndio maana unaona kama kuongelea mambo haya kwa mlengo wa haki ya Mungu ni kupotea. jirekebishe.
 
Back
Top Bottom